Jan 5, 2018
Mambo 10 Unayotakiwa Kuyazingatia Na Kuyasimamia Mwaka 2018.
Yapo
mambo mengi sana ya msingi ambayo unapaswa kuyazingatia kila siku katika safari
yako ya mafanikio. Kwa bahati nzuri mambo hayo tumekuwa tukiyaeleza sana hapa DIRA YA MAFANIKIO karibu kila siku.
Katika
mwaka 2018 kitu cha muhimu au mambo muhimu ambayo unatakiwa kuyazingatia na
kutembea nayo ni kama haya yafuatayo;-
1. Unapofika
wakati tayari umeshaamua kufanya kitu fulani, anza kukifanya kitu hicho mara
moja, acha kuchelewa sana. Kwa mwanzo
hata kama unaona mambo ni magumu na hayaeleweki, ukilazimisha kuanza, mwisho wa
siku mambo hayo kadri unavyoyafanya utazidi kupata uzoefu na kujikuta ukizidi
kusonga mbele kimafanikio.
2. Kuwa
na mawazo bora sio ndio mafanikio tayari bali ni njia ya kukufikisha kwenye
mafanikio ikiwa utachukua hatua sahihi. Hivyo acha kujisifu una mawazo bora na
kujiona umefanikiwa tayari, wazo bora ni sawa na barabara inayokuongoza kwenye
safari yako. Mawazo bora ukiongeza na vitendo ndio sawa na MAFANIKIO.
3. Kuwa
makini sana na yale yanayoitwa matumizi ya hovyo na madogo madogo. Matumizi
hayo madogo madogo ndiyo yanayopelekea wewe kupoteza pesa nyigi sana ambazo kwa
baadae zingeweza kukusaidia.
4. Kuna
wakati unaweza ukawa ni chanzo cha kushindwa kwako kwa sababu ya kushindwa tu
kuweka juhudi zinazotakiwa kwa kile unachokifanya. Ili kufanikiwa unatakiwa
kuweka juhudi kubwa sana zitakazokusaidia kuweza kufanikiwa.
5.
Kufikia mafanikio makubwa, inakutaka na wewe uwe mtu wa tofauti. Inatakiwa
kufanya vitu vya tofauti na kuishi kwa tofauti, hapo utaweza kumudu kutatua
matatizo makubwa ya watu na wewe ukawa mshindi katika maisha yako.
Haiatawezekanai kufanikiwa na kufika juu kabisa, kama utaendelea kubakia kama
ulivyo.
6. Inawezekana
umefanya kosa wewe au kosa hilo limefanywa na mtu mwingine. Lakini kama ni kosa
tayari limeshafanyika. Kama kuna kosa tayari umeshalifanya haina haja ya kujuta
sana, unatakiwa kuachana na kosa hilo na kuamua kusonga mbele. Nguvu zako
elekeza mbele kwa ajili ya kesho na achana na kufikiri kosa ambalo limeshatokea
na huwezi kurudi nyuma tena kulirekebisha.
7.
Upo ulazima wa wewe kufanya mambo ambayo wakati mwingine unafikiri huwezi
kufanya. Unapofanya mambo hayo yanakupa ukomavu mkubwa wa kuweza kufanya mambo
mengine zaidi na zaidi. Kama hauko tyari kufanya mambo amabayo kuna wakati
unafikiri huwezi kuyafanya, kupiga kwako hatua, kitakuwa ni kutakuwa kwa tabu.
8. Tenga
jumapili moja kila wiki, halafu tafuta muda ambapo kila jioni unakuwa unakaa
angalau saa moja na kuanza kutafakari juu ya maisha yako wapi unapotoka na wapi
unapokwenda na kisha kupanga mipango ya wiki linalofuata. Tabia hii ukiisimamia
kiuhakika, itakufanya upige hatua sana.
9.
Kaa karibu na watu ambao utaamua kujifunza vitu kutoka kwao. Usikae na watu
ambao wanaweza kukuzamisha kimaisha, watu hao ni hatari sana kwenye maisha yako
kimafanikio na ni rahisi kukurudisha nyuma.
10.
Usiende kitandani kulala ukiwa na kazi yoyote ya kufanya au kuna jambo la kina
la kulifikiria. Kitandani pako pafanye iwe ndio sehemu ya wewe kwenda
kupumzika, ukienda kulala, na ulale kweli kama mtoto mdogo mdogo.
Naamini
kwa kujifunza mambo hayo, itakusaidia sana kuweza kupiga hatua na kuweza
kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwenye safari yako ya mafanikio.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.