Jan 17, 2018
Achana Na Hadithi Zote Za Uongo, Njia Halisi Ya Mafanikio Yako Iko Hivi.
Ili uweze
kufika mahali fulani, kwa kawaida ipo njia ambayo inatumika ili iweze
kukufikisha kule. Kwa mfano, kama upo Dodoma na unataka kwenda Kigoma ipo njia
ambayo inatumika kuweza kukufikisha Kigoma na usizuiliwe na mtu kufika huko.
Hata
katika safari yako ya mafanikio, ipo pia njia ambayo unatakiwa uifate na njia hiyo
ikusaidie kukufikisha kule kwenye kilele cha mafanikio unako taka kufika. Njia
hii ninayoiongelea ipo na ni kweli inakufikisha ukiamua iwe hivyo.
Lakini
kwa bahati mbaya sana njia hiyo ya kuelekea kwenye mafanikio yako, si njia
rafiki sana kwako, si njia ambayo imenyooka kama ulivyokuwa ukidanganywa au
ukijidanganya wewe mwenyewe kipindi cha nyuma.
Njia
hii ambayo unatakiwa kuifata hadi ikifukishe kwenye mafanikio yako ni njia
ambayo ina mabonde, ni njia ambayo ina miinuko na pia ni njia ambayo ina miti
na milima ya kila aina ambayo hukutegemea kama itakuwa hivyo.
Kwa kuwa
najua umeamua kufata njia ya kukupeleka kwenye mafanikio yako, najua huwezi
kukwepa kuifata njia hiyo ninayokwambia hapa. Ni jukumu lako kufata njia hii
hadi iweze kukufikisha kule unakotaka kufika kimafanikio.
Ila kama
hupendi kufika kule unakotaka kufika kimafanikio, naomba nikupe ruksa tu,
unaweza ukaiacha njia hiyo na kuamua kufuata njia nyingine ambayo wewe mwenyewe
kwako unaweza ukaona labda inafaa.
Kikubwa
unachotakiwa kufanya ni kuwa mvumilivu na kukabiliana na kila hali unapokuwa
kwenye njia ya mafanikio. Ikiwa utaleta mchezo, utapata ajali na mwisho wake
utafika kati na hutaweza kufanikiwa.
Kwa
hiyo unatakiwa kuwa dereva mwangalifu, unatakiwa kuwa dereva mwangalifu
kuangalia vikwazo au vizuizi vyote ambavyo vinaweza vikakukwamisha na ukashindwa
kufika mwisho wa safari yako ya mafanikio.
Sina
shaka unajua kiuwazi kabisa dereva yeyote anapokuwa barabarani anatakiwa kuwa
makini sana, kama asipofanya hivyo ajali inaweza kumhusu. Hata wewe unapata
njia ya kuelekea mafankio yako unatakiwa umakini huo uwe mkubwa sana.
Naelewa
mpaka sasa umeshajua njia unayoifata inayokupeleka kwenye mafanikio yako si njia
rafiki sana kwako yaani wakati wowote unaweza ukagonga mwamba au ukaingia
shimoni kwa hiyo umakini unahitajika.
Nimekwambia
haya kukuonyesha njia ya mafanikio unayaoifata jinsi ilivyo. Kama ulikuwa una
hadithi zako kichwani kwamba njia unayoindea kwenye mafanikio ni njia
iliyonyooka kama mstari mnyoofu, hapana hapo ulijidanganya.
Kuna
mabonde na milima mingi sana au kwa lugha nyingine mafanikio hayapo kwenye
mstari mnyoofu kama ambavyo unaweza ukadhani au ukafikiria. Ni jukumu lako wewe
kuamua kukomaa na njia hiyo mpaka
kiweze kieleweka kwako.
Hata
hivyo kama itafika wakati unaona njia hiyo ni ngumu kwako pia uamuzi ni wako
kuamua kubaki pembeni na kuwaacha wengine wapite, huo ni uamuzi ambao unatakiwa
kuuamua ipasavyo.
Ikiwa
lakini utaamua kuchukua uamuzi wa kukaa pembeni na kuamua labda kutafuta njia
ya mkato, hapo napo ndio naona unakuwa unajipoteza zaidi, maana mwendo huo
unaweza ukawa ndiyo njia ndefu kuliko hata ile ya mwanzo ambayo ulikuwa
unatakiwa uifate.
Ni
nini ninachotakiwa kukwambia kupitia makala haya, ni kwamba unapaswa kuelewa
mafanikio sio rahisi na njia ya kuelekea kwenye mafanikio yako sio rahisi pia.
Kama njia ya kukufikisha kwenye mafanikio ingekuwa ni rahisi kila mtu angekuwa
tajiri.
Unachotakiwa
kufanya ni wewe kuwa mvumilvu, kuvumilia kila adha na ugumu unaokutana nao na
hadi kuona mafanikio yako yanatokea. Ikiwa utakuwa unaona unaonewa kwamba wewe
hukustahili kupata hayo unayokutana nayo utakosea.
Kila
siku tafuta kitu cha kujifunza wakati upo kwenye njia ya mafanikio yako hata
kama haieleweki, tafuta jinsi ya kuvuka vizuizi vyote na mwisho wa siku
utajikuta upo kwenye ngazi kubwa sana ya
mafanikio kwako.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.