Jan 16, 2018
Umaskini Utazidi Kukunyemelea Sana Kama Una Tabia Hizi Za Pesa.
Kushindwa katika
maisha hakuji kwa bahati mbaya bali kuna kuja kutokana na tabia zetu ambazo
tunazo kila siku kwenye maisha yetu. Tabia hizo kiuhalisia zinaturudisha nyuma
sana kimafanikio kama tunazikumbatia.
Kupitia makala haya ya
leo nataka nikukumbushe baadhi ya tabia chache tu, na kama tabia hizo
utazikumbatia uwe na uhakika unazidi kuukaribisha umaskini ukunyemelee kwenye
maisha yako na kukupoteza kabisa.
Inatakiwa kuwa makini
sana na tabia hizi ambazo zinaweza zikaingilia uhuru wako wa kifedha na kuweza
pengine kukuharibia karibu kila kitu kwenye maisha na kukuacha ukiwa mtupu
hauna kitu. Tabia hizi ni zipi, twende pamoja tuweze kujifunza;-
Tabia 1: Matumizi yako ni makubwa sana.
Kama una matumizi
makubwa kwa namna yoyote ile huwezi kukwepa kuishiwa. Inatakiwa matumizi yako
uweze kuyabana kiasi cha kwamba yapate nafasi ya kukupa pesa ya ziada. Ni vizuri
kuwa na daftari la kumbukumbu litakalokusaidia kutunza kumbukumbu zako za
matumizi ili kimatumizi usikengeuke kwa kutumia sana pesa zako hovyo.
Tabia 2: Pesa nyingi unatumia kwenye usafiri.
Iwe matumizi ya nauli za
kawaida au matumizi ya gari lako binafsi ila kama pesa zako nyingi unazitumia
hovyo kwenye usafiri tu, basi jiandae kuanguka pia kiuchumi. Haiwezekani ikawa
karibu muda wako wote ni wewe wa kusafiri tu, halafu ukategemea mambo yako
yakaenda sawa. Kuwa makini na matumizi ya pesa unazotumia kwenye usafiri,
vinginevyo umaskini unakufuata.
Tabia
3: Unazungukwa na marafiki wabovu.
Marafiki zako wanaokuzunguka
ikiwa tabia zao ni mbaya juu ya matumizi ya pesa, basi hata wewe utakuwa ni
miongoni mwao. Haitawezekana kwako wewe uweze kukwepa kiunzi hicho hata siku
moja ni lazima utakuwa kama rafiki zako tu na sio vinginevyo. Kukwepa hilo
unatakiwa kuchagua marafiki makini zaidi kwenye matumizi ya pesa.
Tabia
4: Huweki akiba.
Pengine nikuulize
unafikiri, ni kitu gani ambacho kitatokea ikiwa wewe kila aina ya pesa kwako unayoipata
unaamua kuitumia. Jibu ni rahisi sana hapo ni utaendelea kushiwa na mwisho wa
siku unaukaribisha mwenyewe umaskini. Usijaribu kujiingiza kwenye mtego huu,
pesa yoyote unayoipata iwekee akiba hata kama ni kidogo sana, wewe weka akiba.
Tabia 5: Unatawaliwa na matumizi ya starehe.
Hapa utakuta badala ya
mtu kuwaza maendeleo, lakini kila pesa unayoipata wewe unawaza ni kwa namna
gani utakavyoweza kuifanyia matumizi tena matumizi ya starehe. Hakuna mafanikio
yanayokuja kwa nama hiyo kwa kutafuta vitu vya starehe peke yake. Kama uko ‘siriazi’ na kutafuta pesa itafute, la
sivyo tabia hii itakuachia janga kubwa sana la umaskini.
Kufikia hapo nikwambie
hivi tu, kama utaendekeza tabia hizo umaskini utazidi kukunyemelea sana na
kutaka kukupoteza kabisa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.