Jan 18, 2018
Hamasa Nne Za Ushindi Wa Mafanikio Yako.
Mbali na malengo unayojiwekea, maisha ya
mafanikio yanahitaji sana pia hamasa na msukumo utakaokusaidia wewe kuweza
kusonga mbele kila siku. Pasipo kuwa na msukumo au mhemuko huo hakuna hatua
kubwa utakazoweza kuchukua.
Ndio maana ni muhimu kuwa na hamasa au kitu
kinachokufanya uchukue hatua kila siku. Kwa sababu hiyo ndiyo maana kila siku
unajifunza hapa ili kupata maarifa ya kukusaidia kusonga mbele na hamasa pia.
Kama nilivyosema Unatakiwa ujifunze
kila siku na kupitia kujifunza ndio unajikuta unahamasika pia kuchukua hatua. Leo kupitia makala haya naomaba tujifunza
hamasa nne muhimu za kukusaidia kukupa mafanikio maishani mwako.
HAMASA
YA 1, Muda wa mafanikio.
Jipe
muda wa kufanikiwa kwa kuamua kutumia muda wako vizuri. Ukijipa muda wa
kufanikiwa halafu wakati huo huo ukawa mvumilivu
na king’ang’anizi utafanikiwa.
Kitu
kimojawapo kinachokufanya ushindwe kufanikiwa ni kwa wewe kushindwa kujipa muda
wa kufanikiwa na kuamua kukata tamaa mapema.
Tumia
muda wako vizuri kwa kila dakika unayoipata muda huo utakupa mafanikio yako,
kuliko kuupoteza bila sababu za msingi.
Kama
nilivyosema, jenga uvumilivu na amua kuwa king’ang’anizi ili kujipa muda
wako sahihi wa mafanikio.
HAMASA
YA 2, Kuwa mtu wa muhimu.
Amua
kuwa mtu wa muhimu, amua kuwa mtu wa thamani. Kwa jinsi unavyoendelea kuwa mtu
wa muhimu na mtu wa thamani hivyo ndivyo ambavyo utazidi kupata mafanikio
katika dunia hii.
Mafanikio
uliyonayo yanatoa picha ni kwa jinsi gani ambavyo wewe thamani yako ilivyo.
Kama una mafanikio kidogo basi ujue kabisa hata thamani unayoitoa na umuhimu
wako ni kidogo pia bado.
Hivyo
unapaswa kubadilika mara moja na kujua thamani bora ambayo utakuwa unatoa hiyo
ndio itakayokuwa inakupa na sio vinginevyo. Anza leo kukuza thamani na umuhimu
wako ili uvune mafanikio yako.
HAMASA
YA 3, Juhudi na mafanikio.
Kama
hutaki kuweka juhudi kubwa kwa kile unachokifanya, basi jiandae kupata matokeo
sawa sawa na juhudi zako hizo unazoziweka. Huwezi kupata matokeo kinyume na
juhudi unazoziweka hata siku moja, ni lazima utapata matokeo yanayoendana na
juhudi zako hizo unazoziweka.
Kwa
hiyo ni swala la wewe kuangalia, unaweka juhudi za aina gani kwenye kile
unachokifanya. Juhudi zako hizo ndizo zitakazoamua zikupe matokeo ya aina gani.
Kama unaweka juhudi kubwa utapata matokeo makubwa, kama unaweka juhudi kidogo basi
utapata matokeo kidogo, kusiwe na mtu wa kumlaumu tena kwako.
HAMASA
YA 4, Matokeo ya juhudi zako.
Mafanikio
uliyonayo mpaka sasa, ni matokeo ya juhudi na nguvu zako ulizojitoa ndizo
zilizokufikisha mpaka hapo sasa ulipo. Mafanikio hayo uliyonayo, hujayapata kwa
bahati mbaya ni matokeo ya kujitoa kwako kwa namna fulani hivi.
Pasipo
kuangalia una mafanikio ya aina gani, lakini ni matokeo ya kujitoa kwako. Kama
ulijitoa kidogo basi tunaona mafanikio yako ni kidogo pia, kama umejitoa kwa
nguvu zote na juhudi zote basi ni wazi tunaona mafanikio makubwa pia.
Ni
nini unachotakiwa kufanya kama huridhishwi na mafanikio yako? hakuna kingine
zaidi ni kuongeza ile nguvu ya kujitoa. Endelea kujitoa zaidi na zaidi, endelea
kutafuta maarifa zaidi, endelea kuongeza juhudi utapata mafanikio makubwa.
Hakuna
ambaye anayeongeza juhudi na kuamua kujifunza halafu akaangushwa. Mtu huyo
hayupo. Chukua hatua leo ya kuendelea kuweka juhudi za ziada kwa kila
ukifanyacho ili juhudi hizo zikufikishe kwenye mafanikio uyatakayo.
Fanyia kaza haya, na chukua hatua sahihi za kuweza kufikia ndoto yako.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.