Jan 7, 2018
HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Maneno Hayana Mbawa, Lakini Yanaruka Umbali Mrefu Sana.
Karibu
rafiki, katika ukurasa huu wa hekima za maisha na mafanikio. Leo katika ukurasa
wetu wa hekima za maisha na mafanikio sitakuwa na mengi sana, zaidi
nikukaribishe ukaribie, tuweze kujifunza hekima za maisha na mafanikio kama
ambavyo ilivyotolewa na wahenga wetu. Andaa kalamu yako na karibu mkekani
tuweze kujifunza kwa pamoja;-
1.
Mafanikio na uvivu ni vitu ambavyo havikai pamoja.
Ni
hekima ambayo inatukumbusha kwamba uvivu na mafanikio ni vitu ambavyo haviwezi
kukaa sehemu moja hata iweje. Hekima hii inaonesha ili uweze kufanikiwa ni
unatakiwa uvivu kuweza kuuweka mbali bila ya kufanya hivyo, sahau kuweza
kupata mafanikio kwenye maisha yako.
Watu
wengi utakuta ni watu wakutafuta mafanikio, lakini wakati huo huo ni watu ambao
wanakuwa ni wavivu. Sasa maneno ya hekima za maisha ya mafanikio yanatukumbusha
kwa uwazi mafanikio na uvivu ni vitu ambavyo haviwezi kukaa pamoja hata siku
moja. Ni lazima uvivu ukae mbali mafanikio yatakuja.
2. Maneno hayana mbawa, lakini yanaruka
umbali mrefu sana.
Kuna
wakati unakuta habari inatoka hapa inaweza ikawa ya kweli au sio kwaeli, lakini
baada ya muda mfupi habari hio utaikuta imezagaa eneo kubwa sana. Hiyo yote
inaonyesha nini, kwamba maneno yana kasi kubwa ya kusambaa. Kasi yake ya maneno
inayosambaaa inafananishwa na mbawa.
Pamoja
na kwamba maneno hayana mbawa, lakini wahenga wanatukumbusha kwamba yanasambaa
sana kama vile yamevishwa mbawa. Hapa ndipo tunapotadharuishwa na wahenga wetu
kwamba ni muhimu kuwa makini sana na maneno yetu, vinginevyo habari zetu tutazikuta
mbali sana.
3. Huweze kujua ulichonacho kama ni
kizuri, mpaka umekipoteza.
Kwa
kawaida kila mtu anathamani kubwa sana, thamani ambayo anatakiwa ajidai nayo
kwa sabbu anayo. Lakini kwa bahati mbaya watu wengi hawajui thamani kubwa
walizonazo ndani mwao, mpaka thamani zile wanapoanza kuzipoteza ndio wanakuja
kukumbuka kwamba thamani hizo wanazo.
Kupitia
hekima na maisha na mafanikio, inatuonya na kutukumbusha ya kwamba, ni muhimu
kutambua sana thamani ya vile vitu tulivyonavyo. Haijalishi ni kazi au kitu
gani. Lakini ukishajua thamani ya ulichonacho na ukakitunza kwa ufasaha hiyo
itakusaidia hata kuweza kupata na vitu
vingine. Jua thamani ya ulichonacho na ikutunze.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.