Jan 1, 2018
Jinsi Unavyotakiwa Kuishi Katika Mwaka Huu Wa 2018 Ili Uweze Kufanikiwa Katika Maisha Yako.
Ndugu rafiki katika mafanikio, awali ya yote ni kutakie heri ya kuona mwaka
mpya. Lakini nitakuwa mchoyo wa wafadhira kama nitashindwa kumshukuru Mungu
ambaye ndiye kasababisha hayo yote yaweze kutokea.
Lengo la kukuandikia makala haya kwako ni kukumbusha
ya kwamba mwaka ndio huo umeanza, hivyo natamani sana na wewe mwenzangu
ufanikiwe katika maisha yako kama ambavyo mimi binafsi nimepiga hatua kwa
kiwango fulani.
Hivyo kwa kuweza ili uweze kupiga hatua hizo vyema ukayatazama mambo yale
ambayo yapo mbele yako katika mwako huu, kwani yaliyopita si ndwele tugange
yajayo, hajalishi ni mangapi umepitia kipindi cha nyuma.
Lakini pia katika mwaka huu wa 2018 unahitaji kuwa na marafiki wanakukosoa
kuliko wale wanakusifia tu. Marafiki wanakukosa watakupa mwanga na akili mpya
ya kufikiri na kuweza kutenda jambo fulani kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Jambo hilo ni la muhimu kwa sababu wakati mwingine ukikosa watu wanaokukosoa
kunakufanya ushindwe kuwa mbunifu katika mambo mbalimbali ambayo unayafanya
kwenye maisha yako ya kila siku.
Pia hiyo haitoshi kwa mwaka huu wa 2018 ili uwe wa
mafanikio, unalazimika sana kufanya haya ili yakusaidie kuweza kupiga hatua,
ikiwa utakwenda kinyume ujue kuna namna fulani hivi, utaweza kukwama.
1. Piga kazi sana. Hapa kama inawezekana ukajikana
kabisa jikane, ila chapa kazi hadi uweze kuona mafanikio yako yakitokea na kuwa
wazi. Kazi ndio msingi wa maendeleo yako hata kama mfukoni huna ktu kabisa.
2. Jifunze. Kubali kuifanya 2018 uwe mwaka wa
kujifunza kwako. jifunze kupitia vitabu, jifunze kupitia kwa wengine pia. Ukikwama
kujifunza utaendelea kushindwa kama ambavyo miaka mingine umekuwa ukishindwa
pia.
3. Jenga nidhamu kubwa. Kazana kwa mwaka huu,
kujenga nidhamu tena na tena kwenye kila eneo la maisha. Jenga nidhamu ya pesa.
jenga nidhamu itakayokusaidia kuweza kutimiza ndoto zako za kila siku.
4. Usipoteze muda. Jenga historia kwa 2018 usikubali
kupoteza muda wako tena. Kila unachokifanya, hakikisha unakifanya kwa mahesabu
ytakayoweza kukuokolea muda wako. Kama wewe utazidi kupoteza muda utakwama pia.
5. Kuza mahusiano bora na wengine. Hakuna mafanikio
yanayojengwa ukiwa peke yako. Jitahidi sana kukuza mahusiano bora ili yakupe mafanikio. Ukishirikiana
na wengine utaweza kufikia mafanikio yako.
6. Timiza lengo lako kubwa moja. Usikubali 2018
ikakupita bila kutimiza lengo lako moja kubwa. Hakikisha kuna lengo lako moja
kubwa unalitimiza, hata kama yapo mengi ila lengo lako moja kubwa litimize.
Ni matumaini yangu makubwa mapendekezo yangu utayafanyia kazi na
kuyatekeza.
Nikutakie siku kuu njema na sherekea kwa amani kubwa.
Ni wako katika mafanikio, Benson chonya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.