Jan 30, 2018
Vitu Vya Kufanyia Kazi Sana Katika Maisha Yako Ya Mafanikio.
Yapo mambo mengi sana ya kufanyia kazi katika safari ya
mafanikio ili uweze kupiga hatua. Kwa bahati nzuri sana mambo hayo tumekuwa tukijifunza
hapa DIRA YA MAFANIKIO karibu kila
siku, naamini hilo unalijua vyema.
Leo hii kupitia makala haya, tumekuandalia vitu
vingine vya msingi vya kufanyia kazi sana katika safari yako ya maisha ya
mafanikio. Soma kwa makini na kutendea kazi, na maisha yako utayabadili ikiwa utachukua hatua.
1. Njia ya mafanikio ni njia ambayo ina changamoto nyingi sana
katikati yake. Pale tu unapoanza safari yako ya mafanikio kwa chochote kile
unachotaka kukifanya elewa mbele yako kuna changamoto tayari zinakusubiri. Huwezi
kukwepa changamoto.
2. Ikiwa utakosa nidhamu
kwenye maisha yako, basi dunia itakuonyesha jinsi nidhamu inavyotakiwa iwe.
Utapewa adhabu kulingana na kukosa kwako huko nidhamu. Matokeo yoyote
utakayoyapata maishani kwa sababu ya kukosa nidhamu usilaumu.
3. Jiruhusu mwenyewe katika
siku hii ya leo uishi kwa kutoa thamani yote uliyonayo. Usiishi nusu nusu kwa
kuwaza mambo ya jana au juzi. Usiishi nusu nusu kwa kufikiria kwamba kesho
itakuwaje, ishi leo kwa siku nzima kama ilivyo ili kupata matokeo bora.
4. Kila mafanikio ambayo
umeyapata, ni matokeo ya kwamba kuna vitu ambavyo ulivifanya na vikakupa
mafanikio hayo. Kwa kujua hilo, endelea kufanya vitu hivyo, endelea kuchukua hatua
ili upate mafanikio mengine zaidi na zaidi tena.
5. Maisha yako yanaishia
wapi au yatafika wapi, inategemea sana na vitu viwili ambavyo ni mtazamo na
jinsi unavyochukulia mambo. Mtazamo wako na jinsi unavyochukulia mambo ndivyo
vinavyoamua maisha yako yaweje.
6. Chochote unachokizingatia
kwenye maisha, kitu hicho kinakua. Kama unasahau kuzingatia kile kinachokupa
matokeo ya kubadili maisha yako, hiyo itakuwa ni kazi bure hata kama ungekua
unatunza muda vizuri sana. Anza leo kuzingatia sana kile kinachobadili matokeo
ya maisha yako na utafika mbali kimafanikio.
8. Miaka kumi ijayo kuanzia
leo ikifika, haitajali ulivaa kwa sasa kiatu cha aina gani au ulivaa nguo za
mtindo upi zilizotoka au ulitembelea sana maeneo yapi au uliangalia ‘movie’ ipi
nzuri kwako. Miaka hiyo kumi ijayo itajali na itakuja na matokeo ya
ulichowekeza leo, bila kujali uliwekeza kitu cha aina gani.
9. Usijaribu kuangalia nyuma
kwenye maisha yako na kuchunguza yale maeneo kila wakati uliyokwama na kujiona
huwezi kitu. Ni vyema kuangalia maeneo uliyofanya vizuri na kuedelea
kujiboresha na hadi kuweza kufanikiwa zaidi ya hapo.
10. Moja ya tabia ambayo
unatakiwa kuiendeleza ndani mwako na katika maisha yako kwa ujumla, ni kwa wewe
kutokuruhusu, kuwahukumu watu wengine. Usiumize kichwa chako sana kuwahukumu
watu wengine, utapotea. Waache waishi maisha yao. Kuwahukumu watu mara kwa mara
inaweza hata ikakuletea msongo wa mawazo.
11. Kila mtu unayekutana
naye kuna vitu vitatu ambavyo anavyo ndani yake;-
Kuna kitu anachokipenda.
Kuna kitu anachokiogopa.
Kuna kitu ambacho
amekipoteza.
12. Watu wengi katika maisha
hawasikilizi ili kuelewa, bali wanasikiliza ili kukimbilia kujibu. Kuwa msikivu
mzuri unapoongea na watu wengine, hiyo itakusaidia sana kudumisha mawasiliano
yako na kwa bora kabisa.
13. Katika hii dunia, hakuna
kitu ambacho kinaitwa ulinzi bali kuna fursa. Kama unafanya kazi na kutegemea
sana ulinzi au ‘security’ kama wengi
wanavyodai unajipoteza. Tafuta fursa za kukusaidia kufanikiwa na si kutafuta
ulinzi.
14. Siri ya kuweza kusonga mbele kwa chochote
kile unachokifanya ni kuanza. Usijidanganye sana kama unapiga hatua mbele kama
hujaanza. Ni muhimu sana kuanza, kwani unapoanza unajenga ‘momentum’ ya kukusaidia kuweza kusonga mbele zaidi kila siku
kuliko usingeanza kabisa.
15. Kupata utajiri ni zaidi
ya mawazo na mipango uliyonayo. Ili uwe tajiri ni lazima uwe na akili ya
kitajiri/rich mindset na sio mawazo na mipango peke yake. Mawazo mazuri na
mipingo mizuri haiwezi kukusaidia kama una ‘poor
mind set.’
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.