Jan 25, 2018
Mbinu Itakayokufanya Ukue Kibiashara Ili Upate Faida Ni Hii...
U hali gani mpenzi
msomaji wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO bila shaka u mzima
na unaendela vyema na majukumu yako ya kila siku, naomba nichukue wasaa huu
nikukaribishe siku ya leo ili tuweze kujifunza kwa pamoja mbinu moja ya
muhimu ambayo itakufanya ujiongee thamani na wateja kwa ujumla katika biashara
unayofanya.
Nimekuletea mbinu hii
moja muhimu kwa sababu nimegundua ya kwamba ni mbinu ambayo imekuwa
ikiwasaidia wafanyabiashara wengi wakubwa kwa wadogo, ambao wamekuwa
wakiiitumia mbinu hiyo.
Naomba pia niwe muwazi
kwako kama endapo mbinu hiyo haitukusaidia endapo utaamua katika biashara
yako naomba tuwasiliane nipo tayari kurudisha kiwango cha Mega bites(Mb)
zako ambazo utatumia kusoma makala hii.
Pasipo kupoteza muda
mbinu hiyo ni kutoa ofa kwa wateja wako au ‘promotion’ kama wengi
wanavyopenda kuita.
Kanuni hii kwa
mfanyabishara mdogo anaweza akasema labda kanuni hii hamhusu ila ukweli ni
kwamba kanuni hii ni nzuri sana kwa mfanyabishara mdogo na mfanyabishara mkubwa
pia, hii ni kwa sababu mbinu hii ina mashiko sana katika kuikuza biashara yako.
Hata ukifanya
uchunguzi wako usio rasmi utagundua makampuni yaliyo mengi yana ushindani
mkubwa katika jambo hili la utoaji wa ofa, yaani wengi wao wamekuwa
wakiishinda kuleta ofa mbalimbali mpya zitakazowavutia wateja wa zamani
na wateja wapya.
Na katika ofa hizo
huendana na maneno mazuri yenye kuleta hamasa za kumvutia mteja, wapo
ambao utawasikia wanasema ya kwamba jaza ujazwe, wapo wengine ambao husema onja
msimumuko, wapo wengine husema jipimie, wapo wengine husema usipoelewa
utarudishiwa ada yako na maneno mengine kama hayo.
Yupo mfanyabishara
mwingine nimewahi kukumbana na bango dukani kwake lenye maneno yanasomeka
hivi “ ofa ofa piga picha mbili kwa bei ya moja” mwisho
wa kunukuu. Kwa maneno kama haya unadhani mteja hawezi kwenda kweli? Naomba
majibu ya swali hilo uyaweke ‘password.’
Hivyo haijalishi ni
biashara ndogo au kubwa ni vyema kuna wakati uweze kutoa ofa kwa wateja
wako na katika kutoa ofa hii ni lazima uzingatie ya kwamba ni lazima iwe ofa
ambayo haitakuletea maumivu makubwa katika biashara yako, bali iwe ni ofa
ambayo itakuongezea faida kwani siku zote ikumbukwe utoaji wa ofa katika
biashara huleta faida.
Mwisho nisikuchoshe
kwa maneno mengi, kwani maneno mengi hayavunji mfupa bali nikwambie ya kwamba
biashara ili iweze kwenda vizuri inahitaji pia ni ofa na ofa huleta faida na wateja kemkem. Hivyo walau kwa mwaka ukiweka ofa moja katika biashara
yako basi itapendeza zaidi.
Ndimi: Benson chonya
0757909942
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.