Jan 13, 2018
Mbinu Za Masoko Kwa Wafugaji.
Habari rafiki, leo nimependa kuzungumzia swala la masoko
ya mazao ya ufugaji kama unavyojua tunafuga na mwisho wa siku lazima tuingize
mazao yetu sokoni, kumekuwa na changamoto kubwa kwa wafugaji wengi katika kupeleka
mazao yao ya mifugo sokoni.
Wengi wananipigia simu wananiambia wanamazao ya mifugo lakini
hawajui wapi watauza kuku wao wengine wananiambia wana mayai hawajui watawauzia
wapi hii imekuwa changamoto kubwa kwa wafugaji wengi.
Leo nimeona nije na mbinu au kanuni ambayo inanisaidia mimi na
huwa inawasaidia watu wengi pia katika kufanya biashara zao za kuku na mwisho
wa sikui na wamekuwa wanafurahi sana kwasababu soko ni kubwa na mafanikio ni
makubwa.
Wewe ambaye umeingia
katika uwekezaji huu wa kuku na umekuwa ukihangaika kupata wateja wa mazao yako
ya ufugaji karibu sana katika somo hili la leo uweze kujifunza na kufurahia
ufugaji wako.
MIGHAHAWA MIKUBWA NA
MIDOGO.
Hii ni sehemu nzuri sana ambapo unaweza kufanya biashara yako ya
mazao ya ufugaji (kuku na mayai), hawa ni watu ambao wanauhitaji mkubwa wa kuku
na mayai kwa ajili ya chakula cha biashara katika biashara zao.
Nimekuwa nikifanya nao biashara mara kwa mara sehemu hii na
wamekuwa wateja wangu wakubwa na bei zao ni nzuri sana, wao mara nyingi
wanapelekewa kuku na mayai na madalali sasa wewe kama mfugaji ukitembelea
sehemu hii utafanya biashara nzuri sana.
WAUZAJI WA SUPU.
Hawa utawakuta maeneo mengi ya mijini hasa maeneo ya stand, baa,
soko, hospital, utawakuta wanauza supu hawa niwateja wazuri sana wa kuku mimi
mwenyewe nishahidi mzuri sana wa hili.
Kwa mfano hapa nilipo kuna watu wamenizunguka wanafanya biashara
ya supu nashuhudia wakihangaika kutafuta kuku hadi wanaenda sokoni kutafuta
kuku, sasa huoni wewe unahangaika bure wakati soko unalala nalo nyumbani sasa
wewe endelea kulalamika sisi tunakuacha.
WATU WENYE MASHEREHE.
Eeeh! yaani hadi hapa utaniambia soko hakuna rafiki changamka
ufugaji wako ni Pesa yako, ulizia wapi kunasherehe mwezi huu katika mtaa wako
hata wilaya yako kawaambie mimi nitawauzia kuku mkihitaji utashangaa
watakavyochangamkia fursa, nenda kaonane nao utaniambia.
Nimekuwa nashuhudia watu wanaweka sherehe kuku wanapita kutafuta
mitaani na kwenye vibanda vya kuku ili wapate kuku kwanini wewe usiwarahisishie
kazi kwa kuwaambia utawapelekea kuku, endelea kushangaa na kufa njaa wakati
chakula unacho mimi sipooo!
FUNGUA VIBANDA VYA
KUUZA KUKU.
Nimekuwa nikishudia watu wengi wakihitaji kuku na hawajuwi wapi
watapata wananiambilia sehemu zenye vibanda vya kuuzia kuku ili kujipatia kuku,
cha kushangaza vibanda vingi havimilikiwi na wafugaji Bali vinamilikiwa na
wafanyabiasha.
Sasa wewe unaonaje ufungue kibanda chako na unakua unauza kuku
hapo, kiukweli sijui na wala siamini kama kunachangamoto katika soko la kuku
kwa maana naliona pana sana.
MADUKA YA MATUMIZI YA
NYUMBANI.
Hapa ni sehemu ambayo watu wengi huwa tunaenda kununua matumizi
mbalimbali ya nyumbani sehemu nyingi huwa kunakuwa na mayai wanauza wewe
unadhani wanafuga wao wenyewee! Hapana wananunua sasa unaonaje kama wewe ukiwa
mmoja ya watu wanaowapelekea mayai.
Sasa wewe kaa hivyo hivyo na kusema ufugaji hauna soko na ujihakikishie
kufeli kwenye ufugaji mimi sipo wewe baki ukilia peke yako mimi masoko ninayo
yakutoshaaa!
TUMIA KUNUNI HII ILI
UNASE WATEJA WA KUTOSHA
Nenda stationary katengeneza business card ambayo utaandika
taarifa zako muhimu na mazao ambayo unayo nyumbani kama vile (kuku na mayai)
baada ya kutengeneza kadi yako ya biashara nenda maeneo ya kazi mfano:
maofisini (bank, hospital, shuleni, na sehemu mbalimbali za ofisi).
Ukifika maeneo hayo zungumza nao kwa uchache kwa sababu wapo
maeneo ya kazi hawaweze kukaa kukusikiliza wewe hivyo unachotakiwa
kufanya wagawie kadi yako ya biashara na waambie wakutafute
nakuhakikishia utapokea wateja hadi utashangaa, naomba nikwambie unadhani
wafanyakazi wakiwa na shida na nyama au mayai nani atakuwa wakwanza kutafutwa
kama siyo wewe, sasa wewe shangaa watu tubebe wateja wako.
Hizi ni baadhi tu ya masoko kuna mengi sijayazungumzia fanyia
kazi hayo kama kuna sehemu utafeli karibu tuzungumze.
Ni Mimi rafiki
yako
Frank Mapunda,
Mawasiliano yangu ni
0758918243/0656918243
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.