May 24, 2018
Kama Unapata Pesa Halafu Zinapotea Kwa Haraka Sana, Soma Hapa.
Najua unawajua wale watu ambao wanaweka sana juhudi katika kile wakifanyacho, kama ni pesa wanapata kweli, lakini pamoja na kupata pesa hizo baada ya muda zile pesa na mafanikio yao halisi yanakuwa tena hayaonekani.
Hapa
ndipo wengi huanza kuwaza na kutafuta ni mchawi yupi aliyewaloga. Watu hawa
wanakuwa hawaamini kama kweli wanaweza wakapata pesa halafu mafanikio hakuna. Kinakuwa ni kitu kigumu
kutokuamini zile pesa zimekwenda wapi walizozipata.
Pamoja
na hayo, kwa kawaida kunakuwa ipo sababu inayopelekea hali hii kutokea sana. Ikumbukwe
hali hiyo inakuwa inatokea si kwa bahati
mbaya au si kwa sababu una mkosi wa aina fulani bali inatokea kwa sababu.
Sababu hii ni kwamba
watu hawa wanakuwa hawana mafanikio ndani yao, basi. Ipo hivi, huwezi kufanikiwa
kama ndani yako hujafanikiwa bado. Utaweka juhudi sana na kufanikiwa kwa muda,
lakini utaanguka tena kwa sababu ndani hujafanikiwa.
Siri ya kuweza kuweka
mafanikio ya kudumu kwenye maisha yako ni kwa wewe kuumba mafanikio ya kutosha
ndani yako. Ukiona hujaweka mafanikio ya kutosha ndani yako kufanikiwa kwa nje
ni ngumu pia kwako.
Ndio maana, kabla hujaanza
kulaumu kwa nje kwa nini huna mafanikio, jiulize na kujitazama mwenyewe kwa
ndani yako upya, je, yale mafanikio unayoyataka unayo na unayaona ndani yako
jinsi yalivyoumbika.
Kama ndani yako huoni kitu
halisia yaani kile unachokitaka na una malengo ya jumla, kufanikiwa kwa nje na
ukaweza kudumisha mafanikio hayo inakuwa ni ngumu sana kwako kuweza kutokea na ndio
maana unatakiwa kulifahamu hili vyema.
Kwa kifupi, unatakiwa uwe na
picha kamili ya kile unachokitaka ili ufanikiwe, na kama hauna picha hiyo wewe
sahau kupata mafanikio hayo hata kama ukipata pesa nyinggi leo uwe na uhakika
haziwezi kudumu sana, utazipoteza.
Elewa, kama unataka kujenga
mafanikio ya nje ya kudumu, anza kufanikiwa ndani yako kwanza na huku nje
utafanikiwa tu. Ukumbuke mafanikio yako ya nje yanategemea sana ndani yako
umefanikiwa kwa kiasi gani, hakuna uchawi katika hili, tafakari.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
pia wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji
vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM
PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya
KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI.
Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
May 23, 2018
Wewe Ni Mtawala Na Mfalme Wa Maisha Yako Kwa Namna Hii.
Kila unapoanza siku yako mpya, naomba uweke akilini hili na kutambua kwamba wewe ndiye unayatawala maisha yako kwa kila kitu. Hakuna ambacho wewe si chanzo cha kutawala. Wewe ndio unatawala na kuamua maisha yako yawe ya mafanikio au kushindwa.
Nikiongea
kwa mifano, angalia, wewe unatawala matendo yako. Hakuna mtu ambaye anaweza
akakuongoza, wewe ndiye unayeamua uchukue hatua hii au usiichukue kabisa na
uachane nayo ufate mambo mengine.
Wewe
ndiye unatawala akili yako. Hakuna anayeweza kukuamulia usome kitu fulani au uache. Hakuna anayekuamulia uangalie tv au usiangalie. Wewe ndiye mtawala wa akili
yako na akili hiyo inakuongoza kufanya yale uyatakayo.
Wewe
ndiye unatawala mtazamo wako. Kwa mtazamo wako ulionao, wewe ndio unaruhusu
sana uwe na mtazamo wa namna hiyo. Hakuna mtu ambaye anakuamuru uwe na mtazamo
wa aina fulani kama si wewe, mtazamo wako unabebwa na wewe.
Wewe
ndiye unatawala mwili wako, hakuna anayekuamulia ule nini au usile nini, hakuna
anayekuamulia ufanye zoezi la aina fulani au usifanye, hakuna anayekuamulia
uamke mapema au usiamke, mwili wako unautawala wewe na kwa kila kitu.
Wewe
ni mtawala wa mahusiano yako, mahusiano hayo yanaweza yakawa ya kimapenzi au ya
kawaida. Hakuna anayekuzuia kuwa na mahusiano na watu wengine. Uchaguzi wa nani
ujenge mahusiano naye nae, unabaki nao wewe binafsi.
Wewe
ni mtawala wa muda wako. Ni wewe ndio ambaye kila wakati unaamua muda wako
uutumie zaidi kwenye jambo gani. Pengine uutumie muda wako kwenye jambo
linalokupa mafanikio au uutumie kwenye jambo ambalo linakupa hasara.
Wewe
ndio mtawala wa hisia zako. Tunaona hisia kama wasiwasi au woga ni wewe ambaye
unaamua kuzibeba au kuzipoteza lakini wewe ni mtawala wa hayo mambo tena kwa
kiasi kikubwa sana na unatakiwa uelewe hivyo.
Wewe
ni mtawala wa matokeo ya maisha yako. Chochote kinachotokea kwenye maisha
yako, chanzo kikubwa ni wewe. Kwa hiyo hutakiwi kulaumu kitu, utawala huo unao
wewe na unatakiwa kuelewa hili kwa ufasaha na kufanyia kazi.
Ukiangalia
kwa makini utagunduia wewe ni mtawala wa kila kitu kwenye maisha yako. kama iko
hivyo kwa nini ulaumu wengine wamekuharibia maisha yako. Tambua ni sehemu ndogo sana ambayo imechangia
hao waharibiu maisha yako kama unavyofikiri.
Kuanzaia
leo elewa wewe ni mtawala wa maisha yako na kama iko hivyo kwako, unatakiwa
kukubali kuwajibika kwa sababu wewe ni mtawala wa maisha yako na chochote
kinachokutokea kwenye maisha yako kinakuhusu haswa.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
pia wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji
vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM
PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya
KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI.
Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
May 22, 2018
Hivi Ndivyo Watu Wanavyopenda Kushindwa Kwenye Maisha.
Unaweza
ukaona kama ni kitu cha ajabu au kama nimekosea vile kuandika kichwa cha habari
ya makala haya, lakini elewa sijakosea na ninachokimaanisha ndicho, lipo kundi
kubwa la watu linapenda kushindwa kwenye maisha.
Unashangaa,
ndio, kundi hili kubwa ndilo ambalo likiulizwa, lina mipango mizuri sana ya
kimafanikio, lakini maneno na vitendo vya kutaka maisha hayo haviko sawa. Kundi
hili kubwa ambalo labda na wewe upo, hujikuta likipenda kushindwa kufanikiwa
maishani.
Najua
unajiuliza kivipi? Hebu angalia kuna watu ambao muda wao muda mwingi sana ni kuangalia
Tv, utakuta zaidi ya saa tatu mtu amekaa anaangalia Tv, unategemea hapa nini
kitatokea kama si kuanguka tena vibaya kwenye maisha yake.
Ule
muda mwingi unaopotea kwenye kuangalia Tv, naamini ungetumuka kufanya kitu
kingine kama kutafuta maarifa ya aina fulani hivi, basi mtu huyo angekuwa yupo
mbali sana kimafanikio. Kwa bahati mbaya
muda huo unapotezwa mchana kweupe.
Si
Tv tu peke yake, ukiwaangalia watu wengi wanaishi maisha ambayo hayana maana
kabisa, ni watu wa kuishi maisha ya kuwadanganya na kuwapoteza kabisa kwa
kufanya vitu ambavyo haviwastaili. Ni watu ambao dhahiri wanajidanganya.
Kwa
kawaida unapofanya mambo yanayoenda kinyume
na mafanikio, hata kama unatamka mara ngapi kwamba wewe unataka
mafanikio hayo, hiyo haitaweza kukusaidia kitu. Ndio maana unatakiwa
usijidanganye kwenye maisha yako mwenyewe.
Unatakiwa
utafute vitu vya kufanya ambavyo vinakusaidia kukupa mafanikio. Hata hivyo kwa
bahati mbaya unaishi maisha ambayo kiuhalisia kwa maisha hayo hayakusogezi
mbele hata kidogo kuweza kufanikiwa sana sana yanakurudisha nyuma.
Watu
wengi inaonyesha wanajishughulisha na kazi ndogo ndogo ambazo haziwasaidii
kupiga hatua. Kazi hizo zinaweza zikawa kama kupiga stori, kudhurura na
kufatilia habari zizsizo na maana. Mafanikio hayawezi kuja kwa namna hiyo hata siku
moja.
Waangalie
watu waliofanikiwa, wamefanikiwa kwa sababu ya kuishi na tabia za kimafanikio.
Pia waangalie watu ambao wameshindwa nao pia wameshindwa kwa sababu ya kuishi na tabia zile za kushindwa.
Nimekwambia
hata uimbe wimbo mzuri vipi ambao unajisemea kwamba unataka maisha mazuri, ila
kama unaishi maisha yanayokurudisha nyuma utakwama tu. Hakuna muujiza katika
kukupa mafanikio yako. muujiza ni wewe.
Anza
kubadilika ishi tabia za watu wa mafanikio ili ufanikiwe. Ukiendeleza ubishi
nakwambia utakwama sana. Amua kujifunza, acha kudharau yale ambayo kuna watu
walipoteza muda wao kukusaidia wewe.
Kumbuka
matendo yako ya kila siku ambayo unayetenda kinyume na mafanikio ndio yanayotuonyesha
kwamba wewe unapenda sasa kushindwa. Hata kama hutaki kama unatenda kinyume na mafanikio,
ujue basi unapenda kushindwa kwenye maisha yako.
Ishi
kwa kujiamini, amua kusonga mbele kwa kuhakikisha kila unachokifanya, kiwe na
matokeo ya kukusogeza wewe mbele. Ukiona kitu hicho kikimbie na hakina maana ya
kuweza kukusaidia leo na hata kesho.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
pia wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji
vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM
PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya
KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI.
Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
May 21, 2018
Fanyia Kazi Mambo Haya 4, Yataleta Mabadiliko Na Mapinduzi Makubwa Ya Maisha Yako.
Hakuna muujiza wala ramli katika kufikia mafanikio yako. Mafanikio yanajengwa juu ya kanuni tena wakati mwingine kanuni hizo zinakuwa ndogo ndogo sana ambapo wakati mwingine zinapuuzwa lakini ndizo zijengazo mafanikio yako na ya mwingine.
Hakuna siri tena,
ukifanyia kazi mambo ya msingi katika mafanikio utafanikiwa moja kwa moja. Ukumbuke,
Yapo mambo mengi ya kufanyia kazi, lakini hapa kupitia makala haya nakupa
mambo manne tu, kama ukiyafanyia kazi yataleta mapinduzi ya maisha yako.
1. Tambua ulipo sasa
kimaisha na wapi unapokwenda.
Kitendo
cha kujua hapo ulipo kimaisha ni hatua nzuri ya kukufanya uchukue hatua za
ziada. Ila unatakiwa ujue, kujua hapo ulipo haitoshi, unatakiwa kujua ni wapi
unakwenda kimaisha baada ya miaka miwili au baada ya miaka mitano.
Ukijua
pale ulipo pengine upo kwenye hali mbaya sana, lakini na ikawa haujui ni wapi
unakwenda kwenye maisha yako nalo hilo ni tatizo kwako. Kama hujui unakokwenda
ni dalili tosha inaonyesha hautafanikiwa maana utafanya chochote ilimradi iwe
hivyo.
Jiulize
hapo ulipo una ndoto ya maisha yako. Je, una kitu ambacho unataka kukitimiza na
tayari umeshaanza kukichukulia hatua. Kama huna ndoto yoyote ya kimaisha niseme
kwa uwazi kwako hutaweza kufanikiwa.
Kutaka
kuishi maisha ya kimafanikio halafu huku ukiwa mweupe, ukiulizwa kile
unachokitaka kila kitu unajisemea na unakitaka huko ndiko kunaitwa kupotea. Ni lazima
ndoto yako iwe wazi, hata ukiulizwa usiku wa maneno ndoto yako ni ipi, unaisema
tu.
Kujua
ndoto yako peke yake haiwezi kukupa uhakika wa kufanikiwa, unatakiwa ujue pia
ni kipi utakifanya ili ndoto zako zitimie. Hapa ni lazima ujue kazi au shughuli ambayo utaifanya karibu kila siku ili ikusaidia kukusogeza kwenye ndoto zako.
Ukishajua
ni kipi ambacho unatakiwa kukifanya ili kuhakikisha ndoto yako inatimia, hapo
ndipo kitu hicho unatakiwa kukifatilia kila siku. Tafsiri yake ni hii, kushindwa
kufanya kitu hicho unajiweka kwenye wakati wa kukwamisha ndoto yako.
Asikudanganye
mtu mafanikio yako hayaji kwa mdomo tu au kwa kusema. Mafanikio yako yanakuja
kwa wewe kuchukua hatua tena hatua za kuweza kukusaidia kufanikiwa. Ukichukua hatua
utaweza kufanikiwa tena kwa kiasi kikubwa tu.
Ikiwa
utaendelea kusema tu kila wakati bila kutekeleza ni ngumu sana kuweza kufanikiwa
kwako. Kuchukua hatua mapema ndio mpango mzima na sahihi wa kukuwezesha wewe
kufanikiwa kwa kile ukifanyacho.
Fanyia
kazi mambo hayo kila siku na uwe na uhakika utaleta mabadiliko ya maisha yako
kila unapofanyia kazi mambo hayo, tena mabadiliko hayo utayaleta kwa kiasi
kikubwa sana mpaka unaweza ukafika wakati ukashangaa.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
pia wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
May 20, 2018
HEKIMA ZA MAISHA NA MAFANIKIO; Maneno Mabaya Yana Mwangwi Mkubwa Kuliko Maneno Mazuri.
Mbali na kanuni za kimafanikio ambazo tumekuwa tukijifunza mara kwa mara, lakini unapaswa kujua kwamba pia maisha ya mafanikio yametawaliwa sana na hekima. Hiyo yote inaonyesha hekima ni za msingi sana katika maisha yetu pia.
Hekima zinatufunza busara,
hekima zinatufunza namna ambavyo tunatakiwa kuishi na jamii inayotuzunguka na
hekima pia zinatusaidia kuweza kujifunza kanuni kwa ujumla za mafanikio
zilizopo kwenye maisha yetu.
Kwa mantiki hiyo, katika siku hii ya leo, nikukaribishe, tuweze kujifunza kwa pamoja baadhi ya hekima za
maisha na mafanikio. Ni kusudio langu utatoka na kitu cha kuweza kukusaidia na ambacho
utakifanyia kazi.
1. Shoka halikumbuki mti lililoukata, bali mti huo huikumbuka shoka ile.
1. Shoka halikumbuki mti lililoukata, bali mti huo huikumbuka shoka ile.
Katika hekima hii
inatuonyesha katika maisha, unaweza ukamfanyia mtu kitu ambacho kitagusa maisha
yake pasipo kujali kitu hicho ni kibaya au kizuri, lakini kumbukumbu inakuwa
inabaki sana kwa yule aliyeguswa na alichofanyiwa.
Ndio maana unaweza
ukamsaidia mtu usikumbuke, unaweza ukamfanyia mtu ubaya usikumbuke, lakini yule
aliyefanyiwa ubaya huo anakuwa anakumbuka sana. Hapa ukumbuke tunaaswa kuwa makini yale yanayogusa maisha ya wengine.
Jiulize ni mara ngapi au kuna
wakati uliwahi kumfanyia mtu kitu fulani ambacho kilimsaidia, utakuta muda
unakuwa umepita na wakati huo umesahau, lakini unapokutana na mtu yule anakukumbusha
na kukwambia unakumbuka ulinifanyia kitu hiki.
Mara nyingi wengi wetu
hubaki tukishangaa kwa kukumbushwa kitu kile. Kwa hiyo unaona hata ubaya
ukimfanyia mtu ni hivyo hivyo. Kwa wewe ukiyefanya ni rahisi kusahau lakini si
kwa ,mtu aliyefanyiwa ubaya huo hata kidogo hawezi sahau.
Hapa ndipo unaweza ukapata
picha kwa nini shoka halikumbuki mti liloukata na kwa nini mti uliokatwa
hulikumbuka shoka. Unaona mti unakumbuka shoka kwa sababu shoka liligusa
maisha ya mti huo kwa namna fulani.
2.
Maneno mabaya yana mwangwi mkubwa kuliko maneno mazuri.
Ni kawaida sana maneno mabaya
kuweza kuenea kwa haraka kuliko maneno mazuri. Unaweza ukafanya mengi mazuri
lakini ukikosea kidogo maneno hayo yatasambaa sana kuliko ambavyo hukutarajia
iwe hivyo.
Hapa kupitia hekima hii inatunaonyesha
wazi kwamba maneno mabaya yana mwangwi mkubwa kuliko maneno mazuri, hilo ni la ukweli na halina ubishi. Mwangwi wa
kitu kibaya unasikika zaidi kuliko mwangwi wa kitu kizuri.
Angalia kipindi ambacho
ulifanya ubaya, mwangwi wake ulisikika vipi na kipindi ambacho ulipofanya mazuri
mwangwi wake ulisikikaje pia. Hapo utagundua kipindi ambacho ulifanya mabaya
mwangwi wake ulionea sana.
Tahadhari kubwa unayopewa
hapa ni kuwa makini sana na maneno mabaya. Kwa tafsiri nyingine inaonyesha tenda
wema unavyoweza wewe ila uelewe maneno mabaya siku yakija kukuibukia yana
mwangi sana kuliko maneno mazuri.
Fanyia kazi hekima hizi
naamini kwa sehemu zitakuwa zimekusaidia kutoka hatua moja na kulekea hatua
nyingine ya maisha yako. Kila wakati hekima zinakupa busara, hekima zinakuza
uelewa wako kwa namna fulani.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
pia wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji
vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM
PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya
KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI.
Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
May 18, 2018
Kama Utakuwa Na Kitu Hiki, Kitakufanya Uwe Imara Na Mwenye Mafanikio Ya Kudumu.
Fikiria kama kila kitu unachokihitaji wewe ingekuwa unakipata kila wakati hata pasipo kuweka juhudi kubwa, pasipo changamoto, pasipo kukipigania kitu hicho sana na wala pasipo hata kuweka kazi kubwa yoyote ile inayohitajika, ila kitu hicho unakipata.
Najua kama itatokea hivi, wengi wangefurahi sana na kusema hiyo
itakuwa safi maana mambo yao yatakuwa yamewaendea sawa tena kwa uhakika. Lakini
nikwambie ikitokea hivyo kwako ujue unakwenda kuwa dhaifu sana na mafanikio
yako hayatadumu.
Nimekwambia utakwenda kuwa dhaifu na hautatengeneza mafanikio ya
kudumu nikiwa na maana hii, changomoto yoyote itakayotokea hata kama ni ndogo
kiasi gani hautaweza kukabilina nayo, kwa sababu mafanikio yako uliyapata
kiulaini.
Mafanikio yoyote unayoyapata kwa njia rahisi sana pasipo
kuyapigania uelewe hayana mizizi imara, hayana fundisho, hayana sehemu ambayo
yamekukomaza na ndio maana huwezi kiuhalisia kukua kimafanikio bila kupambana
kikamilifu.
Kama imetokea umepata mafanikio ya moja kwa moja pasipo kupitia
changamoto, unatakiwa kuwa makini sana, la sivyo unaweza kupoteza kila kitu.
Waangalie watu wanaopata bahati nasibu ni kitu gani kinawakuta baadae, wengi
hufilisika tena.
Hiyo yote kama nilivyosema,
inaonyesha huwezi kuwa na mafanikio imara na ya kudumu kama hujakutana
na upinzani au changamoto za kutosha. Kila unapokutana na changamoto hizo hilo
si swala la kuchukia bali ni kujifunza na kusonga mbele.
Maumivu unayokutana nayo wakati huu kwa sababu ya upinzani ama
changamoto, wewe yavumilie kwani ni
rafiki mkubwa sana wa mafanikio yako. Unaweza usione faida yake leo, lakini kesho
utakuja kugundua kile nisemacho na kina ukweli gani.
Tambua kama hujawahi kushindwa, kama hujakosea, kama hujakutana
na upinzani wa kutosha, halafu ukasema unataka mafanikio makubwa unajidanganya.
Hata ukipata mafanikio yataporomoka kwa sababu hakuna kitu kilichokukomaza.
Majasiri na mashujaa
katika maisha ni wale watu wote ambao wamepitia kwenye nyakati ngumu sana ambazo
hata hazieleweki. Nyakati hizi ngumu ndizo ambazo zilizowajenga na kuwapa
jeuri kubwa ya kuweza kufanikiwa.
Watu hawa ukiwaona wana nidhamu na ule uchungu wa maisha. Kuna
kitu ambacho unaona kinachemka ndani mwao yaani wana kiu na hamasa kubwa sana
ya kufanikiwa kwao. Yote hayo yanaletwa na upinzani ama changamoto
walizokutana nazo.
Huhitaji kujilaumu, huhitaji kujuta kila unapokutana na changamoto
kwani hapo ndipo nguvu kubwa ya mafanikio yako ya kudumu ilipo. Changamoto na
upinzani mwingi unakuja kama rafiki wa kukusaidia kukukomaza na kukupa
mafanikio ya kudumu.
Hata watu wengi katika maisha ni watu ambao hawapendi kusikia
sana hadithi za watu ambao walifanikiwa
moja kwa moja kwenye maisha. Hadithi za watu, ambao walifanikiwa moja kwa moja pasipo
kupitia changamoto hazina mvuto.
Kila mtu anapenda sana
kujifunza kwa watu ambao waliumia au watu ambao waliteseka juu ya changamoto
fulani hivi, lakini mwisho wa siku wakaja kufanikiwa. Hivyo elewa, mafanikio ya
moja kwa moja hayakupi nguvu na wala hayakukomazi .
Wewe hapo ulipo una nguvu kuliko unavyofikiri ya kukabiliana na
changamoto yoyote ile. Ukiona umeshindwa wewe umeamua tu. Na changamoto yoyote
unayokabiliana nayo ukiona umeishinda, tambua umepiga hatua fulani kubwa ya
kimaisha.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio kwa undani, karibu
kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO,
kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF
WINNER’S kwenda 0713 048 035,
hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Kama
wewe pia ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
May 17, 2018
Ili Ufanikiwe, Maisha Hayataki Wewe Uwe Na Kitu Hiki…
Kama una lengo la kujiongezea kipato, acha kuogopa kufanya kitu chochote. Kama kuna kitu fulani ambacho unatakiwa ukiuze, hebu uza kitu hicho. Acha kujisikia vibaya kwa sababu unauza kitu fulani eti ambacho hakina hadhi yako.
Maisha hayataki aibu, fanya kitu chochote cha
kukukiingizia kipato ilimradi kitu hicho kiwe halali na hakiwaumizi wengine.
Maisha ya kuona aibu kufanya jambo fulani yatakufanya uzidi kukosa pesa kila
kukicha.
Acha kuwa na
ndoto za kufanya mambo makubwa saana na halafu ukadharau kufanya hata vidogo
ambavyo huna. Kumbuka, jiwekee ndoto kubwa sana lakini anza na hapo ulipo, anza
na kidogo ulichonacho pasipo kujali ni kitu gani.
Hutaki kufanya kitu kwa sababu ya kuona aibu,
jiandae kufikia ndoto zako hutaweza kufanikiwa. Kwa nini uone aibu kwa kile
ambacho kinakupatia kipato? Shida yako iko wapi na hapo unatakiwa ujiulize.
Ukiona unaona aibu kwa kile unachotaka kukifanya
ujue kabisa hujaamua kujitoa kabisa kuweza kufanikiwa. Huna sababu ya kuendelea
kuona aibu, ni ukweli uliowazi wewe hapo huna kitu, sasa aibu ya nini?
Inawezekana zipo sababu ambazo zinakufanya uone
aibu, sanasana pengine labda umesoma kwa hiyo unaona ukiweka genge mtaani kwako
unakuwa ni mtu kama wa kujizalilisha yaani genge sio hadhi yako.
Naweza nikakubalia sawa, sasa kipi unachoweza
kufanya ambacho ni hadhi yako? hapo ulipo najua unaweza ukawa una tai vizuri
lakini unashindwa kutatua tatizo la shilingi elfu mbili tu, lakini na tai
yako shingoni. Sasa kwa hali hiyo aibu ya nini?
Hapo yaani inaonyesha unashindwa kutatua tatizo dogo
la shilingi elfu mbili na usomi wako. Jiulize tu mwenyewe je, ni akili kweli kuona
aibu kufanya kitu cha faida yako? Kipi bora uendelee kulala au uzunguke mtaani
na kuamua kufanya kitu cha faida.
Nikwambie tu, kwa sasa nyakati zimebadilika sana,
kuendelea kujishaua wakati maisha yanataka uyabadilishe huwezi kufanikiwa. Kama
unaendelea kupaka rangi kwenye maisha yako, nakwambia endelea kupaka rangi, kuna
watu wanajenga ujue na hawapaki rangi.
Mambo hayakusubiri ili yabadilike, ila wewe ndio
unatakiwa kuyabadilisha mambo hayo hatua kwa hatua. Huhitaji kufanya kitu
maalumu sana ili ufanikiwe, anza na kitu chochote tu, ambacho kinakuingizia
kipato bila kujali ni nini, ila kiwe halali.
Acha kusikiliza maneno ya watu, funga masikio na kuamua
kufanya jambo lolote mahali popote na eneo lolote, ilimradi jambo hilo liwe ni
la kukuingizia kipato. Tafakari kwa kina na fanya uamuzi wa busara wa kuacha
kuona aibu zisizo na msingi.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
May 16, 2018
Ukiwa Na Tabia Hii Moja Tu, Itakuzuia Sana Kufanikiwa Kwako.
Zipo tabia nyingi ambazo zina mchango mkubwa sana kwa anguko la maisha ya wengi. Na kwa bahati mbaya, wengi wanakuwa hawajui kama tabia hizo ndizo zinazowaangusha na hivyo hujikuta ni watu wa kurudia tabia zile zile kila wakati.
Matokeo
yake ya kutokujua tabia hizo, hupelekea wengi kuanguka kweli na kunakuwa hakuna
mafanikio yanayoonekana na mwisho watu hawa hujiuliza sana ni kitu gani
kilichotokea hadi maisha yao yakawa katika hali hiyo.
Leo kwa
kupitia makala haya tutajiffunza tabia moja tu ambayo kama ukiwa nayo
itakukwamisha sana kwenye safari yako ya mafanikio. Nasema hivyo kwa sababu,
kuna watu tayari wanayo matokeo mabovu yamewapata sababu ya tabia hizo.
Tabia
moja ambayo itakukwamisha sana na haitakusaidia kufanikiwa kama utakuwa nayo na
kuiendeleza ni ile tabia ya kuamua kuwa mtu wa kushangaa katika maisha.
Wapo watu ambao tabia zao ni kushangaa tu karibu kitu.
Kwa
mfano, Utakuta wao ni watu wa kushangaa na kuhamasika sana na miradi
wanayofanya watu wengine, ukija upande wao hakuna hata kitu kimoja wanachofanya
au hawachukui hatua kabisa.
Pia
utakuta ni watu wa kuingia kundi moja, wanashangaa kinachoendelea humo na
kutoka na kuingia tena kundi lingine wanashangaa wee na kutoka tena, pia bila
kuchukua hatua. Watu wenye tabia za namna hii kamwe ni watu wasiofanikiwa.
Dunia
ya sasa hivi ni ya mwendo kasi, watoto wa mtaani wanakwambia ‘hutakiwi
kuuza sura’, fanya kazi. Kama kuna fursa hata kama ni ndogo, itumie
ikusaidie kufanikiwa na acha kubaki tu kuwa mtu wa kushangaa. Kama ni kujifunza, jifunze kweli.
Uzuri
au ubaya wa maisha hakuna ubabaishaji, ukileta ubabaishaji wa aina yoyote ile,
utaumbuka tu na ni lazima utajibiwa na maisha kama vile wewe unavyobabaisha.
Badilika rafiki na achana na biashara ya kushangaa, kuwa mtendaji na aamua
kufanya kazi.
Jiulize
utashangaa hadi mwaka gani au hadi lini. Watu wanaoshangaa ni mara nyingi ni
watu ambao hawafanikiwi. Maisha yanataka uwe mtendaji zaidi na si kuishia
kushangaa ambako haukuwezi kukusaidia chochote.
Kama
ulikuwa una tabia ya kushangaa basi ndoto na mipango yako mingi sana itaweza
kukwama na hautaweza kufanikiwa. Wale wote wanaofanikiwa hawashangai bali wanaamua
kujifunza na kuamua kuchukua hatua za kusonga mbele.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
May 15, 2018
Njia Sahihi Ya Kupima Kama Unapiga Hatua Za Kimafanikio Au Upo Palepale.
Hapo ulipo unao uwezo wa kupima kama unapiga hatua au hupigi hatua kwa kile ambacho ukifanyacho. Ni rahisi sana kuanza kujiuliza hivi kwa hiki nikifanyacho mimi, napiga hatua au nimebaki pale pale nilipo tu.
Mara
nyingi ipo njia sahihi ambayo inaweza ikakusaidia wewe na mtu yeyote kujua kama
anapiga hatua ama hapigi hatua. Njia hii si nyingine bali ni kwa wewe kukaa nje ya mazoea
uliyoyazoea kila siku.
Ukiona
kila siku unafanya kitu hicho kwa namna hiyo hiyo yaani hubadilishi kitu na upo
kwenye mazoea yale yale si rahisi sana wewe kuweza kupiga hatua. Kama ukiona
kile unachokifanya na unakifanya nje ya mazoea ujue kuna kupiga hatua hapo.
Upo uwezekano
wa wewe ukawa bado hujanielewa kwa namna fulani hivi, lakini nitakupa mifano
zaidi ambayo itakusaidia kuweza kuelewa. Tambua hivi, ni jambo la hatari
kufanya mambo yako kwa hali ya mazoea kila siku, maana hutafanikiwa.
Niweke
labda wazi kwako nakurudia hivi, hutaweza kufanikiwa kama hauko nje ya mazoea
yako. Mazoea ni moja ya sumu kubwa sana inayokuzuia kufanikiwa. Ukiendelea
kufanya mambo yako na mazoea utashangaa unabaki palepale miaka nenda rudi.
Wanaobadilisha
maisha ni wale watu ambao wanaamua kwenda nje ya mazoea yao. Kwa tafsiri ya
haraka mazoea uliyonayo ndio yaliyokupa matokea uliyonayo. Hivyo kwa kuendelea
kuyang’angania utaendelea kupata matokeo yaleyale.
Hiyo
inamanisha kwamba, hata kama una malengo na mipango mizuri vipi, ila kama
unachukua hatua kwa mazoea, basi utaendelea kubaki pale pale karibu kila wakati
kwenye maisha yako na hautaona ukipiga hatua mbele ya kukusaidia kufanikiwa.
Hivyo,
kila wakati jaribu kufanya jambo jipya ambalo litakupa matokeo tofauti na yale ambayo
umekuwa ukiyapata. Kwa kufanya kwako jambo jipya kuna vitu vingi sana ambavyo
utajifunza na vitakubadilishia mtazamo wako kabisa.
Huhitaji
kusubiri kitu, anza kujua kama unafanikiwa au hufanikiwa kwa kujipa changamoto
ya kukaa nje ya mazoea yako. Hata kama kwako unaona inakuwa ngumu lakini
dhamiria kukaa nje ya mazoea uliyonayo kila wakati.
Unapaswa
kujua, kitakuwa ni kupimo sahihi kwako kama unapiga hatua au hupigi hatua za kimafanikio kwa kukaa nje ya mazoea
yako. Ukiona unafanya mambo yako na unaona kawaida ujue hakuna ulichobadili na
hapo kufanikiwa itakuwa shida pia.
Jitahidi
uwezavyo kama nilivyosema kaa nje ya mazoea yako, hiyo itakusaidia kukujengea
nidhamua na hata kukupa mafanikio ambayo hukuyatarajia kwa sababu ya nidhamu
yako. Hivi ndivyo unavyoweza kupima mwendelezo wa mafanikio yako.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
May 14, 2018
Usiruhusu Maisha Yako Yatawaliwe Na Mambo Haya Kabisa.
Ikiwa upo kwa ajili ya kutaka maisha ya mafanikio makubwa, yapo mambo ambayo hutakiwi kuyaruhusu kabisa yatawale maisha yako. Unapokuwa unaruhusu mambo haya yatawale maisha yako, hiyo inakuwa ni sawa na kuamua kuharibu maisha uliyonayo.
Ni
wajibu na jukumu lako kuyajua mambo haya ambayo tunakwenda kuyajadili na
kuyafanyia kazi. Je, mambo haya ni mambo gani ambayo hutakiwi kuyaruhusu
yatawale maisha yako? twende pamoja tujifunze;-
Mambo yaliyopita.
Kwenye
maisha yako usifanye kosa ukaruhusu maisha yako ya sasa au yajayo yakatawaliwa
na mambo ambayo yamepita. Mambo ambayo yamepita ni tayari yamepita pasipo
kujali yamekuumiza au hayajakuumiza.
Achana
na kila kitu cha nyuma ambacho tayari kimeshapita, kwani hata ukiendelea
kukibeba sana hakitakusaidia kitu zaidi utaendelea kuumia na kuharibu kesho
yako. iwe kuna makosa ulifanya, ulifanyiwa kitu kibaya na wengine, achana na
hiyo habari.
Kuendelea
kukumbuka mambo ambayo tayari yameshapita hiyo ni sawa na kuendelea kuyapa
nguvu mambo hayo. Kikubwa maisha yako anza kuyatengeneza hapo ulipo na mambo
yaliyopita usiruhusu yatawale maisha yako tena.
Maoni ya watu wengine juu yako.
Jambo
la pili, usiruhusu maisha yako yatawaliwe na maoni ya watu wengine. Watu wanaweza
wakawa na maoni juu ya maisha yako ambayo hayaendani kabisa na malengo yako, kwa
hiyo ikiwa utaamua kuyafata basi utakuwa unajipoteza wewe.
Ndio
maana kabla hujafanya kitu unatakiwa kujiuliza unakifanya kitu kwa sababu yako
au kwa sababu ya maoni ya wengine? Wapo watu ambao hawawezi kufanya kitu mpaka
wasikilize maoni ya wengine wanasema nini.
Umezaliwa
kwa sababu ya makusudi maalumu ambayo unatakiwa uyatimize. Sasa makusudi hayo huwezi kuyatimiza kama maisha
yako unayeendesha kwa kutumia maoni ya watu. Usijaribu kuishi kwa ajili ya
maoni ya wengine sana, utakwama.
Mawazo yako hasi.
Yapo
mawazo ambayo unayo na mawazo hayo yamekuwa yakikuzuai kwa muda mrefu sana
kuweza kufanikiwa. Pengine umekuwa na mawazo ya kusema kwamba siwezi kufanikiwa
kwa sababu hii au ile.
Ukiangalia
mawazo hayo hayana ukweli ila yamekuwa yakikuzuia kufanikwa kwa sababu
unavyojiwazia. Kama unajiwazia kwa ndani huwezi kufanikiwa kwa sababu umezaliwa kwenye ukoo haujiwezi au
kwa sababu huna bahati ni dhahiri hutaweza kufanikiwa.
Kwa
jinsi ilivyo, kama hakuna kinachokuzuia ndani yako kuweza kufanikiwa, basi na
hata nje hakuna kitu ambacho kitaweza kukuzuia kufanikkiwa hata iweje. Uamuzi
unabaki kwako, kutokuruhusu mawazo ya kutokufanikiwa yakutawale, basi.
Mahusiano.
Kati
ya kitu kimojawapo chenye nguvu sana katika maisha ni mahusianao. Ni hatari
sana kujihusisha na mahusiano na mtu yeyote eti kwa sababu huna mtu. Hiyo
nikiwa na maana unaingia kwenye mahusiano kwa sababu furaha pekee unaipata
huko.
Kama
wewe unaona mahusiano ndimo sehemu pekee ya kupata furaha na huwezi kupata
furaha mpaka uwe kwenye mahusiano basi utakuwa kwenye wakati mgumu sana maana
utakuwa unatawaliwa na mahusiano.
Ninachotaka
kusema hapa ni kwamba, unatakiwa uwe imara na kutengeneza furaha yako wewe mwenyewe
bila kujali upo kwenye mahusiano au la. Ni rahisi kuingia kwenye mahusiano mabovu
na kuharibu maisha ikiwa utakuwa na mahusiano ya hovyo.
Pesa.
Tunaposema
usiruhusu pesa itawale maisha yako tukiwa na maana hii, si kwamba pesa ni mbaya
au kwamba hutakiwi kuitafuta, hapana. Hapa kinacholengwa usije ukakubali ukafanya
maamuzi kwa sababu una pesa.
Unachotakiwa
kuelewa ni kwamba usiruhusu pesa, ikawa ndio inatawala maamuzi yako. Fanya
mambo yako si kwa sababu ya pesa. Ifanye pesa ibaki kwako kama kitu cha
kukusaidia na si kwa sababu una pesa kichwa kinaanza kuyumba hovyo hovyo.
Haya
ndio mambo ya msingi ambayo hutakiwi kuyaruhusu kabisa yatawale maisha yako. Unaporuhusu
mambo haya yakatawala maisha yako kuna namna ambayo unakuwa una haribu maisha
yako, kuwa makini na fanyia kazi.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)