google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

May 11, 2018

Acha Kufanya Mambo Haya…Yatakupotezea Mafanikio Yako.

No comments :
Ili kufanikiwa, unatakiwa ujiulize sana swali hili, kile unachikifanya sasa kina uwezo wa kukusaidia kufanikisha ndoto zako? Kama kitu hicho unachokifanya sasa hakina uwezo wa kukusaidia kufikia ndoto zako, unatakiwa ukibadili mara moja au kuachana nacho.
Inawezekana unanishangaa au nimekuchanganya kidogo, lakini narudia kama kitu unachokifanya hakikusaidii achana nacho. Usije ukajifanya huelewi au unajifanya huoni, jiulize kwanini ufanye kitu ambacho hakikusaidii kutimiza ndoto zako?
Utakuwa ni upotevu mkubwa sana wa muda kwako na rasilimali, kama unafanya kitu ambacho hakikusaidii kufanikiwa kwako. Unatakiwa uishi kwa malengo juu ya ndoto zako, kwa kufanya kila kitu chenye mchango wa kukufikisha kwenye ndoto zako.
Najua kubadilisha kitu hicho pengine unachokifanya inaweza kuwa ni ngumu sana kwako, lakini jiulize kama kitu hicho hakikusaidii kukufikisha kwenye ndoto zako cha nini kuking’ang’ania? Hata uking’ang’ania hakitakufikisha kule utakapo.

Kama utakuwa mbishi iwe kwa kujua au kutokujua na ukaendelea kufanya kitu ambacho hakikusaidii kukufikisha kwenye ndoto zako, basi ujue wewe utakuwa ni sawa na mtu anayeng’angania kupanda gari ambalo halimfikishi kwenye safari yake.
Ili kufanikisha ndoto zako inakutaka sana wewe uwe mtu ambae wakati wowote uwe tayari kubadili mwelekeo wa kile unachokifanya kama unaona hakikusaidii. Ukiwa hujui kubadili mwelekeo haraka ujue kabisa utaingia ‘vichakani’ kwenye kushindwa.
Sifa mojawapo ya kufikia mafanikio ni kwa wewe kuwa makini na kutambua mapema kwamba hiki nikifanyacho kinanisaidia kufanikiwa au hakinisaidii kufanikiwa. Haijalishi kitu hicho ni biashara au kazi uifanyao, lakini kama hakikusaidii unatakiwa kukibadili tu.
Zoezi mojawapo ambalo unaweza ukalifanya wewe kimya kimya ni kwa wewe kujiuliza kila wakati je, kitu hiki ninachokifanya kinanisaidia kunifikisha kwenye ndoto zangu, kama unaona hakikusaidii unaachana nacho mara moja.
Hapa yaani unakuwa kama dereva wa gari ambae hajui njia aiendeayo. Dereva huyo kila atakapokuwa anapita ni lazima  atajiuliza njia hii ni kweli itanisaidia kunifikisha? Kila dereva huyu anapoona njia hiyo inampeleka porini anakuwa mwepesi sana kuibadili.
Hiki ndicho kitu ambacho hata wewe unatakiwa ukiweke akilini mwako na kukifanyia kazi. Hutakiwi kuishi kiholela tu ilimradi unaishi, kila shughuli au kazi unayoifanya ifanye iwe ina mchango wa kukusaidia kufikia ndoto zako hata kama ni kwa kidogo sana.
Kitu cha kujifunza leo, unatakiwa uwelewe hivi kubadili mwelekeo kwa kile ukifanyacho au kuachana nacho sio jambo baya kama jambo hilo halikufikishi kwenye ndoto zako. Fanya mambo ya kukusaidia kufanikiwa na ndoto zako zitatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Kama pia unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia rafiki kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,






No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.