May 31, 2016
Misingi Mitano (5) Unayotakiwa Kuifahamu, Ili Kujihakikishia Kipato Cha Kudumu.
Kati
ya kitu ambacho kinatafutwa sana na wengi katika hii dunia ni pesa. pesa hiyo
imeanza kutafutwa toka enzi za mababu na mababu mpaka leo. Juhudi za kutafuta
pesa hadi kuipata zimekuwa ni kubwa sana kila kukicha. Kutokana na matokeo ya
juhudi hizo, hiyo yote imekuwa ikitudhirishia au kutuonyesha kwamba kumbe pesa
ni sehemu ya maisha yetu, tena maisha ya kila siku.
Lakini
pamoja na juhudi kubwa za kuitafuta pesa hiyo bado lipo kundi kubwa la watu
ambao wamejikuta wakiikosa pesa hiyo. Harakati zote za kuamka asubuhi na mapema
na hata kuchelewa kulala kwa sababu ya pesa zimekuwa ni kama kazi bure kwa
sababu hawaipati. Watu hawa wamekuwa wakipishana na pesa karibu kila siku,utafikiri
wao wanalaana na pesa hiyo hadi washindwe kuipata.
Hebu
jaribu kuangalia kwenye eneo unaloishi jinsi pilika pilika za kutafuta pesa
zilivyo nyingi. Lakini cha kushangaza pamoja na juhudi na pilika pilika hizo
bado ni wachache wanaoipata pesa na kuwahakikishia kipato cha kudumu. Wengi
wamekuwa wakitafuta sana pesa na kuishia maumivu na mateso ya kutokuipata. Sina
shaka hali hii unaijua vizuri ya wengi kuendelea kukosa pesa ingawa wanaitafuta
sana.
Kutokana
na mazingira haya wapo ambao huanza kuamini wamelogwa. Na wengine pia huanza
kuamini wana mikosi au laana. Je, kitu cha kujiuliza hizo ndizo huwa sababu
halisi za wao kukosa pesa? Ukifatilia kimsingi, hizo sio sababu halisi za wao
kukosa pesa, bali sababu hizo hutumika kama kisingizio. Watu hao kitu
wasichokijua mara nyingi hushindwa kuwa na kipato cha kudumu kwa sababu ya
kukosa misingi ya kuwaongoza.
Ndio.
Naona unashangaa, inawezekana hata wewe ukawa kwenye wimbi la kutokuwa na
kipato cha kudumu kwa sabau ya kukosa misingi ya kukuwezesha kuwa na kipato
hicho. Kama unafikiria natania, kwa nini huna kipato cha uhakika na kudumu
mpaka sasa? Nafikiri sasa, utakubaliana nami kwa kile ninachosema. Je, unajua
misingi hiyo ni ipi unayotakiwa kuwa nyo ili kujihakikishia kipato cha kudumu?
1.
Bajeti.
Hatua
ya kwanza itayokuhakikishia wewe uwe na kupata cha kudumu ni kujijengea
utaratibu wa kuwa na bajeti yako. Bajeti hiyo itakuongoza kujua pesa yako
inatoka wapi na pesa yako inaenda wapi. Lakini
si hivyo tu, unapokuwa na bajeti inakusaidia pia kujua ni lini na wapi
uweze kuwekeza pesa yako. Hivyo ni njia mojawapo muhimu sana ya kukuhakishia
kipato cha kudumu kwenye biashara na maisha yako kwa ujumla.
Pesa unayopata hata kama ni kidogo, wekeza. |
2.
Kuwekeza.
Njia
nyingine bora ya kukupa kipato cha kudumu ni kuifanya pesa yako ikuzalishie.
Hakuna namna nyingine ya kuweza kuifanya pesa yako ikuzalishie zaidi ya kuweza.
Kama una kitega uchumi kimoja, ongeza na kingine cha pili, cha tatu na
kuendelea. Watu wenye mafanikio wana vipato vya kudumu kwa sababu wamewekeza
katika maeneo mengi. Halikadhlika, nawe unatakiwa kufanya hivyo ili kuwa na kipato
cha kudumu.
3.
Kuweka akiba.
Kati
ya kitu cha msingi katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa ni
kujiwekea akiba. Kwa kiasi chochote cha pesa unachokipata, jifunze kuweka
akiba. Akiba hiyo itakusaidia katika kuwekeza kwenye miradi mingine mingi baadae,
lakini si hivyo tu pia ni njia mojawapo ya kukutengenezea kipato cha kudumu.
Kama inatokea umeishiwa ni rahisi kuweza kuchukua pesa kwenye akiba yako kuliko
kukopa kopa hovyo.
4.
Kulipa madeni mapema.
Ni
vyema ukajua mapema ili kujiweka salama katika safari yako ya mafanikio,
jifunze kulipa madeni mapema. Unapokuwa unalipa madeni mapema inakusaidia sana
kutokukuvurugia mambo yako mengi. Kama una mkopo benk au sehemu nyingine, lipa
mapema ili uanze kuwa huru kutafuta pesa zako mwenyewe ambazo zitakupa uhuru
mkubwa wa kimafanikio. Kama unadaiwa
kila wakati si rahisi sana kuendelea na kuwa na kipato cha uhakika.
5.
Kuwa mjasiriamali mpambanaji.
Hautaweza
kuwa huru kipesa na kujijengea kipato cha kudumu, kama leo hii hutaweza kuamua
kuwa mjasiriamali mpambanaji. Amua kuwa mjasiriamali mpambanji unayetaka kutengeneza
matokeo na sio mjasiriamali wa kulalamika kila siku. Hakuna mafanikio
yanayoweza kuja au kupatikaa kwa kulalamika. Kama kuna changamoto zitatue na utafika
mbali kimafanikio kipesa.
Kabla
ya kuweka kalamu yangu chini, naomba utambue kwamba kama hutojiwekea misingi
hiyo imara ya kipesa, suala la kupata pesa na kuwa na kipato cha kudumu
litakusumbua sana. Usishangae ukawa mtu wa kufukuza pesa siku zote za maisha
yako bila mafanikio. Zingatia hili sana na chukua hatua.
Ansante
kwa kunifatilia na pia washirikishe wengine waweze kujifunza kupitia mtandao
wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 04 80 35,
May 30, 2016
Usipokuwa Makini Na Mambo Haya, Yatakuzuia Sana Kufanikiwa.
Ni matumaini ya tulio wengi ni kupata mafanikio
kwa kila mambo ambayo tunayafanya, na ukichunguza kwa umakini mara nyingi
huwa hutapati kile ambacho tukitamani huku changamoto zikiwa nyingi kuliko
mafanikio yenyewe. Huku wengine wakiamua hata kutumia njia zisizo rasmi katika
kusaka mafanikio hayo na yote hufanyika kwa sababu ya tamaa iliyoko ndani ya
mtu katika kutekeleza malengo yake. Na ukiendelea kufanya uchunguzi huo utakuja
kugundua kuwa idadi kubwa ya watu hao huenda wasipate mafanikio hayo na
kupoteza fedha nyingi zaidi ya kile wanachokitafuta.
Kwa kuwa mimi huwa naamini sana katika kufanya
utafiti. Niliendelea kufanya utafiti ili kujua sababu zingine na vikwazo
ambavyo mara kadhaa vimekuwa chanzo cha watu wengi kutokufanikiwa zaidi.
Nakusihi ufuatane nami kwa kujifunza kupitia Makala haya mwanzo hadi mwisho.
Vifuatavyo ndivyo vikazo ambavyo vinasababisha
watu wengi kutokufanikiwa.
1. Kutokujua pesa inafanya matumizi yapi.
Mara nyingi nimekuwa nikieleza kuhusu pesa, Pesa kwa sababu ndizo tunazozitafuta ili kupata mafanikio. Ila mambo yetu huwa hayawi kama tunavyotaka hii ni kutokana na kutokujua jinsi ya matumizi sahihi ya pesa kwa maneno mengine naweza sema kuwa hatuna nidhamu ya pesa. Kwa kuwa na maana hatujui pesa tunazopita zinatakiwa kutumika kwa utaratibu, ukitaka kubaini juu ya ukweli huu tofauti na daftari za kumbumbuku za biashara yako je una daftari inayohusu mapato na matumizi yanayohusu maisha yako binafsi na familia kwa ujumla?
Mara nyingi nimekuwa nikieleza kuhusu pesa, Pesa kwa sababu ndizo tunazozitafuta ili kupata mafanikio. Ila mambo yetu huwa hayawi kama tunavyotaka hii ni kutokana na kutokujua jinsi ya matumizi sahihi ya pesa kwa maneno mengine naweza sema kuwa hatuna nidhamu ya pesa. Kwa kuwa na maana hatujui pesa tunazopita zinatakiwa kutumika kwa utaratibu, ukitaka kubaini juu ya ukweli huu tofauti na daftari za kumbumbuku za biashara yako je una daftari inayohusu mapato na matumizi yanayohusu maisha yako binafsi na familia kwa ujumla?
Kama haupo katika misingi hiyo anza sasa kuwa
na daftari ambalo utajaza kila kitu kinachohusiana na matumizi yako ya
kifedha na familia kwa ujumla. Pia kama una amini katika kujifunza
kama mimi soma kitabu cha "rich dad,
poor dad" kilichoandikwa na Robert Kayosaki ambacho kitakupa mwangaza
zaidi juu matumizi sahihi ya kifedha.
Ipe thamani elmu yako itakufanikisha. |
2. Kutoipa thamani elimu yako.
Hapa ndipo ambapo kunatufanya tuwe maskini
zaidi. Mara nyingi mtu anashindwa kufanya kitu fulani kwa sababu hana elimu.
Siwezi kulaumu sana maana tumeshakuta mifumo ambayo inatuambia msomi ni yule
mwenye elimu ya chuo kikuu kwa maana shahada( degree) . Na kwa kuwa mifumo hiyo
ndiyo ambayo tumeikuta na tumekuwa tukiamini hivyo. Na kwa kuwa imani ina nguvu
basi tunajikuta wengi tunaamini hivyo. Na wale ambao kwa namna moja au nyingine
hawana elimu hiyo ya chuo kikuu hujikuta wanafanya mambo ambayo siyo rasmi kama
vile wizi, ukahaba na mengineyo mengi hii ni kwa sababu waliaminishwa ya kwamba
elimu ni ufunguo wa maisha na kwa kuwa wao hawana elimu hiyo hujikuta wanafanya
mambo ambayo sio ya kisomi.
Tatizo kubwa ambalo linasabisha yote hayo ni
kutoipa thamani elimu iliyo nayo kwamba unaweza kufanya mapinduzi makubwa ya
kimafanikio. Mtu anashindwa kufanya jambo fulani eti kwa kisingizio cha elimu
aliyonayo. Mtu utamsikia si unajua niliishia darasa la saba au sikubahatika
kumaliza elimu ya sekondari. Maneno hayo ni sumu kuliko ilivyo sumu ya panya
katika swala zima la kimafanikio.
Hebu tuangalie watu wawili ambao ni uhakika
unawafahamu sana. Yule tajiri ambaye ameamua kuilisha Tanzania kwa vyakula na
vinywaji na kuuza ving'amuzi je elimu yake ni ipi? Haya yule msanii anayetuwakilisha vizuri hasa
katika kuitambulisha vizuri nchi yetu kimataifa je na yeye elimu yake ni kiasi
gani? Usinipe majibu ila nikuombe uweze kufuatilia kwa umakini juu ya elimu zao
ili kujua kwa undani ili kuipa thamani ya elimu uliyo nayo uone ni jinsi gani
elimu hiyo uliyonayo inaweza kufanya mabadiliko makubwa ya kimafanikio binafsi
na jamii kwa ujumla.
Niweke nukta kwa kusema mafanikio makubwa
yanakuja kama utaamini kile ulichonacho.
Nikutakie siku njema na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza.
Imeandikwa na afisa mipango; Benson chonya.
E-mail; bensonchonya23@gmail.com
Imeandikwa na afisa mipango; Benson chonya.
E-mail; bensonchonya23@gmail.com
May 27, 2016
Aina Nne (4) Za Hofu Zinazokukwamisha Kufikia Malengo Yako.
Kila mmoja wetu bila shaka anaifahamu hofu aliyonayo. Zipo hofu zile ni za
kawaida ambazo zipo ndani ya mtu na kila mmoja anayo. Kwa mfano mtoto akiwa
peke yake mahali penye giza ni lazima aogope, pia ipo mifano mingine mingi kama
hiyo.
Lakini leo nataka tujadili aina zingine za hofu ambazo zinatengenezwa na watu
wengine katika jamii zetu, pia zipo aina nyingine za hofu ambazo
tunazitengeneza sisi wenyewe kutokana na vile tunavyoona mambo ambayo yanatuzunguka.
Hofu hizi ndizo zinazotuzuia kuwa na maisha mengine ya utofauti. Mwisho wa siku
tunajikuta ni watu wa kuishi maisha ya vilevile kila wakati. Hata hivyo katika
hali hiyo huenda ukawa unalaumu sana ukisema labda unashindwa kufanikiwa zaidi
kwa sababu una changamoto ya pesa au sababu wewe ni yatima, mjane au umezaliwa
katika familia maskini.
Inawezekana ya kwamba unaona ya kwamba Sababu hizo zina uzito
sana na zimechangia wewe kuwa hapo ulipo. Ila ukweli ni kwamba moja ya chanzo
kikubwa kilichosababisha wewe kuwa katika hali ya chini ni HOFU iliyopo ndani
yako ambayo umeitengeza mwenyewe.
Zifuatazo ndizo aina za hofu zinazotufanya tushindwe kufikia
malengo yetu.
1) Hofu ya kukoselewa.
Watu wengi wamebaki na maisha yale yale ya kila siku kwa sababu ya hofu hii ya kokosolewa. Watu wengi wamekata tamaa ya kuendelea kufanya jambo fulani kwa sababu ya kuna watu waliwakosoa kwa jambo ambalo walikuwa wanafanya. Kwa mfano kuna baadhi ya watu wana kipaji cha kuimba na katika hilo wapo wengine hupeleka nyimbo zao stesheni mbalimbali za radio na pindi wanapoambiwa kuwa nyimbo zao ni mbaya huwa wanakata tamaa na hiyo ndiyo hofu ya kukosolewa.
Watu wengi wamebaki na maisha yale yale ya kila siku kwa sababu ya hofu hii ya kokosolewa. Watu wengi wamekata tamaa ya kuendelea kufanya jambo fulani kwa sababu ya kuna watu waliwakosoa kwa jambo ambalo walikuwa wanafanya. Kwa mfano kuna baadhi ya watu wana kipaji cha kuimba na katika hilo wapo wengine hupeleka nyimbo zao stesheni mbalimbali za radio na pindi wanapoambiwa kuwa nyimbo zao ni mbaya huwa wanakata tamaa na hiyo ndiyo hofu ya kukosolewa.
Vivyo hivyo hata katika biashara watu wamekuwa wakiambiwa na watu wengine
wamekuwa ya kwamba huwezi kufanya hivyo na kwa kuwa mtu anakuwa ana hofu hiyo
ya kukosolewa ana amini na mwisho wa siku anaacha kufanya jambo fulani. Pia ikumbwe
ya kwamba hii ndiyo sumu kubwa ambayo inaua ndoto za watu wengi sana. Ila
kumbuka aina hii ya hofu ndiyo yenye mafanikio makubwa sana mbeleni.
Ondoa hofu ya kukosolewa, utafanikiwa. |
2) Hofu ya kuzeeka na kufa.
Kuna baadhi ya watu wanataka mafanikio ya muda mfupi huku wakiwa na imani kubwa ndani yao kwamba Mafanikio ya muda wa kusaka mafanikio kwa muda mrefu haiwezekani kwa sababu inawezekana wakafariki au wakazeka. Mtu unamwambia matokeo ya jambo hili ni baada ya miaka ishirini kwa kuwa mtu huyo ana hofu atamsikia nikifa je?
Kuna baadhi ya watu wanataka mafanikio ya muda mfupi huku wakiwa na imani kubwa ndani yao kwamba Mafanikio ya muda wa kusaka mafanikio kwa muda mrefu haiwezekani kwa sababu inawezekana wakafariki au wakazeka. Mtu unamwambia matokeo ya jambo hili ni baada ya miaka ishirini kwa kuwa mtu huyo ana hofu atamsikia nikifa je?
Mwingine anapoelezwa jambo hilo utamsikia anasema aaah nitakuwa
nimezeeka. Kwa mifano hiyo utakuwa umegundua hofu hizo ni kwa jinsi gani
umekuwa unahairisha kufanya mambo fulani ya kimafanikio huku ukihofia aina hizo
za hofu. Ili kuondokana na hali hiyo daima kumbuka ishi kama utakufa kesho ila
jifunze vitu vingi kama utaishi milele.
3) Hofu ya kushindwa.
Aina ya hofu hii imekuwa inatatesa wengi. Kimsingi ni kwamba kabla ya kuamua
kufanya jambo fulani akili yako imekuwa inawaza juu ya jambo hilo. Ila kutokana
na kuamua kwako kila ukiwaza juu ya utekelezaji wa jambo hilo unapata majibu mbalimbali
ambayo yanakwambia hutaweza. Na kwakuwa unaona ya kwamba utekelezaji wake ni
mgumu unaanza kuwaza kwamba jambo hilo ni gumu kwako.
Hivyo unaachana na kufanya jambo hilo. Pia wapo baadhi ya
watu wao huamini ya kwamba wao ni wa kushindwa tu kwa kuwa kila mara kadhaa
wamekuwa wanafeli sana. Wito wangu kwako ni kwamba achana mara moja na hofu ya
kushindwa amini wewe ni zaidi ya mshindi katika jambo lako.
4) Hofu ya kuwasaidia
wengine.
Tupo baadhi ya watu tumekuwa ni watu wa binafsi sana katika kuwasaidia wengine.
Tumekuwa ni watu wakutofundisha watu wengine, huku tukiamini ya kwamba kufanya
hivyo ni tutaibiwa mawazo yetu na sababu nyingine kama hizo, huku tukiamini
kufanya hivyo ni kuwanufaisha wengine na kuzidi kuamini ya kwamba watatuzidi
kiutalaamu. Ila nikwambie kumsaidia mwingine ni jambo jema sana pia kumbuka
kuwa wewe ni origino hata akifanya hawezi kuwa kama wewe. Hivyo ni wakati wako
muafaka wa kuua aina hiyo ya hofu na kuwasaidia wengine.
Tunakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Imeandikwa na afisa mipango; Benson chonya.
Email; bensonchonya23@gmail.com
Email; bensonchonya23@gmail.com
May 26, 2016
Tunaposhindwa Kulinda Tunachokipenda Huvuna Maumivu.
Wazazi
wana nafasi gani kwenye kutuamulia maisha yetu ya uhusiano? Jibu la swali hilo
linategemea mambo mengi. Mojawapo ya mambo hayo ni malezi yetu, na namna
tulivyopata nafasi ya kukua kiufahamu nje ya malezi. Lakini ukweli ni kwamba,
wazazi wana nafasi ya ushauri tu, kuhusu maisha yetu ya uhusiano. Lakini kwa
bahati mbaya, wazazi wengi hujipa nafasi kubwa na mamlaka zaidi na watoto wengi
huwaruhusu wazazi wao kuchukua nafasi hiyo.
Hebu
tuchukulie kwa mfano mzazi ambaye anamkatalia mtoto wake wa kiume asimuoe binti
aliye nyumba ya tatu kwa sababu ya kuona tu binti yule ni mfanyakazi wa ndani. Kwa
tafsiri ya haraka haraka mzazi huyu anakuwa amemwona binti yule kama nusu mtu
na asiyefaa kitu. Naye mtoto wa kiume pengine kwa kusikiliza ushauri wa mzazi
anaweza kukubali lakini baadae inaweza ikawa majuto kwake ikiwa ataoa mwanamke
ambaye atamtesa ingawa kiuhalisia anakuwa ametoka familia tajiri.
Lakini
pia huwa inatokea sana kwa wazazi wanapoona mtoto wao awe wa kike au kiume
akiwa amependana na mtu ‘choka mbaya
kimaisha’ kwa wengi huwa sio rahisi kukubali mahusiano hayo na kujikuta
kuweka vizuizi vingi sana kwa watoto ili wasiweze kuoana. Hapa watoto wasipokuwa
makini hujikuta wamekubali walichoelezwa na wazazi wao na matokeo yake hujikuta
kwa pande zote mbili kujuta kutokana na kujiingiza kwenye mahusiano yasiyo
sahihi.
Linda unachokipenda, kisipotee. |
Hali
kama hizi zipo sana katika jamii zetu. Kuna wengi ambao ndoa zao zinaingiliwa
sana na wazazi au hata ndugu zetu na pengine tu hata marafiki zetu na kujikuta
hata kukosa uhuru. Hali kama hii inapokutokea na ukajikuta umekosa uhuru wa
kuonyesha ukakamavu wa kuonyesha kile unachotaka kwenye mahusiano au ndoa yako
utaumia sana. Utahisi dunia sio sehemu salama kwako kwa sababu ya kuhisi kama
ndugu wanakuonea kila wakati. Kama hili limewahi kukutokea pole sana.
Naamini
umeshawahi kusikia mikasa kama hii ya kuingiliwa kwenye mahusiano. Wengi wetu
mara nyingi tunafundishwa namna ya kuishi na wake au waume zetu, kama tuendelee
kuwa nao au tuwaache. Huwa tunawasikiliza wazazi, ndugu au marafiki na kuvunja
uhusiano. Baadaye, kwa maumivu makubwa tunakuja kubaini makosa tuliyoyafanya. Tunajaribu
kuunga palipokatika. Huwa inawezekana, ingawa mara nyingi haiwezekani tena.
Unaweza
ukasambaratishwa kwenye mahusiano au ndoa yako na ndugu zako pasipo kujua na
matokeo yake kuleta majuto makubwa sana. Na majuto hayo unaweza ukaendelea
kuamini pengine ungedumu kwenye uhusiano wako wa mwanzo ungekuwa upo salama
kimafanikio na kindoa pia. Lakini ulipo ‘moto’
umewaka kutokana na kwamba upo sehemu ambayo siyo sahihi. Ni kitu ambacho
kina uwezo wa kukuuma sana siku zote na ukajikuta umeharibu kila kitu ikiwa
pamoja na mafanikio sababu ya uhusiano.
Kumbuka
kwamba, wewe ndiye unayetakiwa kusema na kuamini kwamba, umempenda fulani. Wewe
ndiye unayetakiwa kulinda uhusiano wako kwa msimamo wa hali ya juu. Wengine wanakuwa
wana uhuru wa kutoa maoni kuhusu penzi au mpenzi wako, lakini hawana ruhusa au
nafasi ya kuamua kuhusu hatma ya penzi lako. Ikiwa kwa namna moja au nyingine
utashindwa kulinda kikamilifu kile unachokipenda, elewa utavuna maumivu tena
makubwa sana.
Tunakutakia
mafanikio mema katika ndoa na maisha. Pia endelea kujifunza kupitia mtandao
wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048 035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
May 25, 2016
Tabia Tatu (3) Muhimu Unazotakiwa Kuziendeleza, Ili Kufanikiwa.
Mafanikio
ni matokeo ya tabia nzuri ambazo unaziendeleza katika maisha yako karibu kila
siku. Tabia hizi chanya ama unazoziendeleza na kuzifanya kuwa zako, ndizo zinazokupa mafanikio. Hivyo, kwa mtu
yeyote anayesaka mafanikio ni lazima kwake kuendeleza tabia bora za kimafanikio
ili kufanikiwa.
Watu
wenye mafanikio wanatambua ukweli huu kuwa mafanikio ni tabia. Na kutokana na
kuujua ukweli huu unaowapa mafanikio, huamua kufanyia kazi ukweli huu karibu
kila siku. Lakini kwa kusoma makala haya, utajua tabia tatu muhimu unazotakiwa
kuziendeleza ili kufanikiwa. Ni tabia ambazo watu wenye mafanikio huzitumia pia
kufanikiwa.
1.
Tabia ya utendaji.
Haijalishi
una mipango au malengo mazuri vipi, kama hakuna utendaji hiyo itakuwa ni sawa
na kazi bure. Kuwa mtendaji wa jambo ulilolipanga, ni njia mojawapo bora ya
kukupeleka kwenye mafanikio. Mara nyingi wengi huwa wanashindwa kufanikiwa kwa
sababu ya kuwa waongeaji sana kwenye mambo yao.
Mbinu
nzuri ya kufanikiwa kwenye mambo yako ni kujifunnza kuwa mtendaji. Wakati
wengine wanapiga mdomo kwamba watafanya jambo hili kesho au mwezi ujao, wewe
tafuta namna ya kulifanya hata kwa kidogo. Watu wote wenye mafanikio ni
watendaji. Ukijifunza kuiendeleza tabia hii, uwe na uhakika utafanikiwa.
2.
Tabia ya kuanza na kidogo ulichonacho.
Mbali
na kuwa mtendaji pia, unatakiwa kujifunza kuanza na kile kidogo ulichonacho.
Acha kusubiri sana mpaka kila kitu kikamilike, anza na kile ulichonacho. Hata
kama kitu hicho unakiona ni kidogo anza nacho hicho, baada ya muda fulani
kitakuwa kikubwa. Jambo la kuzingatia hapa unapoaza na kidogo ni kuhakikisha
unanidhamu ya kutosha na kukitunza.
Kwa
mfano inawezekana ukawa unataka kuanza biashara ya mtaji wa milioni tano na
wewe una milioni moja mkononi, acha kusubiri sana. Unaweza ukaanza na pesa yako
hiyo kwa kufanya biashara ndogo ndogo na ukajikuta unakuza mtaji wako hadi pale
unapotaka kufika. Kuanza na kidogo ulichonacho ni mbinu mojawapo nzuri ya
kukufanikisha.
3.
Tabia ya uzingativu.
Ili
uweze kufanikiwa ni muhimu sana kuweka nguvu za uzingativu kwa kile
unachofanya. Kama nguvu zako utakuwa unazipeleka na kuamua kuzingatia kila
jambo ni wazi hutaweza kufanikiwa. Siri ya mafanikio yako ipo kwenye kuzingatia
mambo machache, ikiwezekana jambo moja lenye kukupa mafanikio makubwa.
Katika
maisha yako, unaweza ukajikuta upo kwenye wakati mgumu pengine hufanikiwi kwa
sababu ya kukosa uzingativu. Wengi huwa wanajikuta hawafanikiwi kwenye maisha
kwa sababu hii. Utakuta ni watu wa kujaribu kutaka karibu kila kitu, matokeo
yake kunakuwa hakuna kitu kikubwa walichokifanikisha.
Kwa
kumalizia makala haya, nifupishe kwa kusema hivi, tabia ya utendaji, kuanza na
kidogo ulichonacho na uzingativu ni moja ya tabia muhimu ambazo unatakiwa
kuzizingatia kila wakati ili uweze kufanikiwa.
Tunakutakia
kila la kheri katika safari ya mafanikio yako na endelea kuweka nguvu katika
kujifunza kupia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
May 24, 2016
Athari Za Kuwa Na Mipango Mingi Kwa Wakati Mmoja.
Moja ya
changamoto kubwa ya kushindwa kufanikiwa ni kutokujua unataka nini katika Maisha
yako. Huenda ukawa haujanielewa ngoja nikueleweshe, ni hivi unakuta mtu anaona
maisha hayaendi vizuri mwisho wa siku ukimuuliza mtu huyo anataka kufanya nini,
bila shaka kwa kuwa mtu huyo hajui kile anachokitaka atakwambia kazi yeyote ile
mimi nafanya.
Ukiangalia juu ya kauli hiyo ni sawa, mtu huyo
huenda akawa sawa hii ni kutokana na hali yake aliyonayo. Lakini katika kununi
ya kimafanikio hakuna majibu ya kusema unataka kufanya chochote kile. Ila ni
lazima ujue unataka kufanya nini. Moja ya majonzi ya watu waliofeli kimaisha ni
kwamba walichanganya vitu vingi kwa wakati mmoja.
Tujifunze
kitu kupitia hadithi ifuatavyo.
Hapo
zamani za kale kulikuwepo na mfugaji fulani katika kijiji fulani. Na mfugaji
huyo alijipatia umaarufu mkubwa sana kijinini hapo hii ni kutokana
alivyobobea katika shughuli hiyo, na kutokana na umaarufu huo aliweza kulinda
heshima ya jina lake na kuongeza idadi kubwa ya mifugo.
Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo na mifugo ilivyozidi kuongezeka miaka na miaka, hata hivyo kama ilivyo kwa jongoo kuwa na miguu mingi bila macho ni sawa na bure hivyo ndivyo ilivyotokea kwa mfugaji huyo kutokana na ufugaji hakutaka hata siku moja kumuuza hata mnyama mmoja kwa sababu aliweka malengo yake ya muda mrefu na kuamini ipo siku atakuja kuwa na pesa nyingi na kuwa tajiri mkubwa zaidi kijijini hapo.
Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo na mifugo ilivyozidi kuongezeka miaka na miaka, hata hivyo kama ilivyo kwa jongoo kuwa na miguu mingi bila macho ni sawa na bure hivyo ndivyo ilivyotokea kwa mfugaji huyo kutokana na ufugaji hakutaka hata siku moja kumuuza hata mnyama mmoja kwa sababu aliweka malengo yake ya muda mrefu na kuamini ipo siku atakuja kuwa na pesa nyingi na kuwa tajiri mkubwa zaidi kijijini hapo.
Acha kuwa na tamaa na mipango mingi, itakukwamisha. |
Hata
hivyo kutokana imani hiyo aliyokuwa nayo furaha na umarufu uligeuka kilio na
majonzi hasa pale ulipo ingia ugonjwa wa bonde la ufa (Rift valley) kijijini
hapo. Ugonjwa huo uliweza kuangamiza idadi kubwa ya wanyama aliowamiliki mpaka
akabakiwa na ng'ombe mmoja.
Mfugaji
alinung'unika sana lakini alimbidi akubaline na hali hiyo ambayo imetokea.
Hivyo akaamua kumuhudumia yule ng'ombe kama mtoto wake kwani kila
alichokihitaji ng'ombe yule alikipata kutoka kwa mfugaji huyo. Hayo ndiyo
yalikuwa maisha ya mfugaji na ng'ombe yalivyokuwa.
Siku moja
alfajiri mfugaji aliamua kwenda na ng'ombe wake sehemu ambayo ng'ombe yule alikunywa
maji kama ilivyokuwa ratiba ya mfugaji yule kila siku. Wakati wanaelekea katika
eneo hilo ghafla mbele aliona kiatu, kiatu ambacho kilikuwa ni kizuri sana,
aliamua kukichukua kiatu kile na kukiangalia na kuona kinamtosha vizuri baadae
ilishangaa mbona kiatu kizuri kiasi kilikuwepo pale barabarani wakati
anajiuliza hayo aling'aza macho yake huku na huko lakini hakuona kiatu kingine
cha mguu mwingine.
Kwa kuwa hakuona kiatu kingine aliamua kuachana na kiatu kile na kuondoka na ng'ombe wake. Mfugaji aliendelea na safari yake kwa mwendo mrefu sana lakini kadri alivyozidi kwenda ghafla alikutana na kiatu kingine cha mguu mwingine ambacho kinafanana na kile alichokiacha awali. Mfugaji alifurahi sana hivyo alimua akiache kiatu kile cha pili pamoja na ng'ombe mahali pale na kurudi kwa kasi sana kwenda kuchukua kiatu kingine.
Kwa kuwa hakuona kiatu kingine aliamua kuachana na kiatu kile na kuondoka na ng'ombe wake. Mfugaji aliendelea na safari yake kwa mwendo mrefu sana lakini kadri alivyozidi kwenda ghafla alikutana na kiatu kingine cha mguu mwingine ambacho kinafanana na kile alichokiacha awali. Mfugaji alifurahi sana hivyo alimua akiache kiatu kile cha pili pamoja na ng'ombe mahali pale na kurudi kwa kasi sana kwenda kuchukua kiatu kingine.
Lakini
cha ajabu kilichomkuta ni kwamba baada ya kwenda mahali pale kilipokuwepo kiatu
cha mwanzo hakukiona kiatu kile, alijaribu kukitafuta sana kiatu kile lakini
hakukipata hivyo aliamua kurudi mwanzo ambako aliamuacha ng'ombe na kiatu cha
pili lakini cha kushanganza ni kwamba hata huko hakumkuta ng'ombe wala kiatu
kile. Mfugaji alilia sana kwa sababu alimpoteza ng'ombe wake ambaye alibaki
mmoja na aliyempenda sana. Mwisho wa siku alikosa vyote.
TAFSIRI
YA HADITHI HII NI NINI?
Tafsiri
ya hadithi hii ni kwamba watu wengi ni wazuri wa kimawazo na kuchangamkia fursa
mbalimbali ila changamoto kubwa inakuja hasa pale ambapo unataka mafanikio ya
haraka hivyo unajikuta unaingia katika sakata la kuchanganya mambo mengi kwa
wakati mmoja. Mwisho wa siku unajikuta unafanya kitu hiki unaacha mara unafanya
kitu kingene kama alivyofanya mfugaji na mwisho wa siku akajikuta anakosa yote.
Hivyo ni wakati muafaka leo wa kujua unataka kufanya nini na kukimalisha na sio
kuwa na maisha yakutaka mambo mengi kwa pupa pupa na mwisho kukosa vyote. Kuwa
mtu chanya ili kupata mafanikio ya kweli.
Nukuu ya
Leo inasema; Ukijua kilichomo ndani yako wewe ni tajiri.
Mwandishi
ni afisa mipango ;Benson chonya.
Facebook; Benson chonya
Simu; 0757-909942
E-mail: bensonchonya23@gmail.com
Facebook; Benson chonya
Simu; 0757-909942
E-mail: bensonchonya23@gmail.com
May 23, 2016
Mambo Ya Msingi Kuhusu Mafanikio Unayotakiwa Kuyajua.
Ili uweze
kufanikiwa kwa jambo lolote, ni lazima uwe na msingi imara wa jambo hilo kwanza.
Pasipo kuwa na misingi imara utasumbuka sana katika kufikia mafanikio kwa kile
unachokifanya. Lakini hiyo haitoshi unatakiwa pia kulielewa kwa mapana zaidi
jambo unalolifanya ili likufanikishe. Hata kwenye maisha yako binafsi, huwezi kufanikiwa
kama hujui mafanikio ni nini kwako au yanataka nini.
Wengi
kwa sababu ya kutokujua hili hujikuta wakisaka mafanikio kwa muda mrefu na
kuambulia patupu. Kama unataka kufanikiwa kweli, kuanzia leo anza safari yako
ya mafanikio kwa kuyapata mtazamo chanya wa kitofauti. Ni lazima ujue mambo ya
msingi yanayohusu mafanikio ili uweze kufaniwa na kuwa mtu wa tofauti. Acha kun’gang’ania
kukaa kwenye umaskini, toka hapo na uufuate utajiri.
Karibu
sana na twende pamoja kujifunza mambo ya msingi yanayohusu mafanikio.
Mafanikio
ni hatua.
Hakuna
ambaye amewahi kulala na kuamka asubuhi akiwa tajiri. Hakuna ambaye aliyeweka
juhudi kubwa kwa muda mfupi halafu akawa tajiri. Hakuna mafanikio ambayo
yanapatikana kwa muda mfupi. mafanikio yote unayoyajua wewe yanatengenezwa kwa
hatua. Ndio, mafanikio ni matokeo ya kupiga hatua kwa hatua kila siku.
Usitishike
na kuona mafanikio makubwa ya watu ukafikiri walianzia hapo walipo. Kama
unawaza hivyo, unajidanganya. Mafanikio yao yalijengwa kidogo kidogo, siku kwa
siku na hata miaka. Ikiwa unataka kufika huko waliko acha kukurupuka. Jipange
na anza kuelekea kwenye mafanikio yako hatua kwa hatua. Baada ya miaka michache
utakuwa mbali sana.
Mafanikio ni hatua kwa hatua, usikate tamaa. |
Mafanikio
ni kujitoa.
Siku
zote mafanikio ni kujitoa tena kwa moyo wote. Hakuna mafanikio ambayo unaweza
ukayapata kama haupo tayari kujitoa. Iwe unataka au hutaki ni lazima ujitoe na
kukubali kupoteza baadhi ya vitu ili uweze kufanikiwa. Upo wakati ambapo ni
lazima utapoteza marafiki, muda wako, pesa kwa ajili ya mafanikio.
Yanapotokea hayo yote usijali sana, kwani kumbuka kama nilivyosema mafanikio yanahitaji kujitoa. Kwa wale rafiki zangu ambao wanataka
mafanikio lakini wakati huo huo hawako tayari kupoteza baadhi ya vitu ili kufanikiwa,
huwa sio rahisi kwao kufanikiwa. Ili kufanikiwa unahitaji kujitoa mhanga kwa mambo mengi
sana ikiwemo pamoja na kuwa mgumu kwenye mambo yako. Bila kujitoa kikamilifu
mafanikio utayasikia kwa wengine.
Soma; Tabia Zinazoua Ndoto Na Mafanikio Ya Wengi.
Soma; Tabia Zinazoua Ndoto Na Mafanikio Ya Wengi.
Mafanikio
ni uchaguzi.
Kila
siku katika maisha yetu huwa tuna chaguzi nyingi ambazo tunazifanya. Kwa mfano
huwa ni watu wa kuchagua chakula tunachokula. Huwa ni watu wa kuchagua mavazi, njia
na mambo chungu nzima yanayofanana na hayo. Halikadhalika, na mafanikio
unayoyatafuta nayo ni uchaguzi. Ni lazima uchague kufanikiwa ili ufanikiwe bila
kufanya hivyo, hutafanikiwa.
Kwa
bahati mbaya wengi huwa hatuna uchaguzi na maisha ya kimafanikio tunayoyataka.
Kwa mfano nikuulize wewe, umeshawahi kujiuliza unataka kufanikiwa kwa viwango
vipi? Usitoe macho tu, ulishawahi kujiuliza hivyo? Kama huwa unajiambia nataka
tu kufanikiwa, lakini hujui kwa viwango vipi ni sawa na kama hujafanya uchaguzi
kabisa. Fanya uchaguzi sahihi wa kufanikiwa kwako na ujue unataka kufika wapi
na kwa muda upi?
Mafanikio
ni kuona fursa.
Ili
ufanikiwe ni lazima utumie kila aina ya fursa inayokuja mikononi mwako vizuri.
Lakini hiyo haitoshi, kama huna uwezo wa kuona fursa za kukusaidia kufanikiwa
pia hutaweza kufanikiwa. Ni muhimu sana kuzijua fursa ambazo unatakiwa uzitumie
ili kufanikiwa. Bila kufanya hivyo utahangaika sana kutafuta mafanikio bila
kuambulia kitu.
Watu
wanaopata mafanikio mazuri kwenye maisha yao, siku zote wanatumia fursa. Ni
jambo ambalo kwa sasa unatakiwa kulijua na kulizingatia vizuri sana kichwani
mwako kwamba mafanikio pia huwa yanakuja kwa kuona na kutumia fursa vizuri. Ikiwa utakuwa unaona na kutumia
fursa vizuri kila wakati, uwe na uhakika hakuna wa kukuzuia kufanikiwa.
Soma; Mambo 7 Ya Kujifunza Kutoka Kwa Bilionea Bill Gates.
Soma; Mambo 7 Ya Kujifunza Kutoka Kwa Bilionea Bill Gates.
Mafanikio
ni kutatua matatizo.
Katika
safari ya mafanikio wakati mwingine inakuwa ni safari yenye kila aina ya
vizuizi. Na wakati mwingine kutokana na vizuizi hivi hutufanya tuumie na hata
kulia. Sasa ili uweze kufanikiwa unapaswa kutambua pia mafanikio wakati mwingine
ni ule uwezo wa kutatua matatizo. Kwa kadri unavyotatua matatizo ndivyo ambavyo
unajikuta unazidi kufanikiwa.
Kama
unafikiri natania mafanikio sio kutatua fursa, kuanzia leo anza kutatatua
matatizo yaliyo katika kijiji chako au eneo unaloishi. Kwa kutatua matatizo hayo
utajikuta ukijipatia pesa kwa wingi sana. Hiyo yote inadhihirisha kwamba
mafanikio ni kutatua matatizo. Jifunze juu ya hili na tatua matatizo muhimu
kwenye jamii na hakika utafanikiwa.
Mafanikio
ni kufanya kazi kwa bidii.
Hakuna
ubishi wowote ili uweze kufanikiwa ni lazima ufanye kazi kwa bidii. Kama ulikuwa
huna mtazamo huu mwanzoni unalazimika kuwa nao na kujua kwamba mafanikio ni
kufanya kazi kwa bidii zote. Hakuna lelemama katika kutafuta mafanikio. Unatakiwa
kujituma sana tena sana kila siku ili ufanikiwe. Vinginevyo usipozingatia hili
hutaweza kufanikiwa.
Kwa
kuhitimisha makala hii, nifupishe kwa kusema mafanikio ni hatua, mafanikio ni
kujitoa, mafanikio ni uchaguzi, mafanikio ni fursa, mafanikio ni kutatua
matatizo ya jamii na mafanikio pia ni kufanya kazi kwa bidii. Kwa kujua mambo
haya yatakusaidia sana kujiwekea mtazamo tofauti juu ya mafanikio ambao utakupa
msukumo mkubwa wa kuweza kusonga mbele na kufanikiwa.
Ansante
kwa kuwa nami na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 04 80 35,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
May 20, 2016
Mfumo Bora Utakao Badili Maisha na Biashara Yako.
Kila
utayekutana leo endapo utamuuliza unapenda nini katika maisha yako? Jibu ambalo
atakupa bila shaka litakuwa linahusiana na masuala ya mafanikio na endapo
utakutana na mtu ambaye majibu yake yatakuwa ni kinyume na
mafanikio ni lazima utabaki unamshangaa huyu mwenzangu vipi? .
Bila shaka idadi ya
watu wengi ni kuona kila mmoja anapata mafanikio ila tatizo ni pale linapokuja
suala zima unapataje Mafanikio hayo. Tulio wengi ni wazuri wa kunuia (kusema )
kuliko kujua tunapaje Mafanikio hayo.
Leo niamua kuwaza kwa sauti hata wewe mwenzangu usikie nilichokiwaza ili uweze kupata mafanikio hayo na sio kuishia kusema nataka kile bila hata kujua utakipata vipi.
Zifuatazo ndizo mbinu zitakazobadili mfumo wa Maisha yako;
1. Usijadili vitu kwa macho.
Katika safari ya kuelekea au kupata mafanikio hakuhitaji kuvitazama tu vitu bali ni lazima ufanye uchunguzi wa kutosha. Huwa nakumbuka sana wakati tunasoma shule hasa somo la hesabu wengi wetu tulikuwa tukiyatazama maswali tulikuwa tunasema haya yameisha kwa maana ya kwamba uhakika wa kupata majibu ya maswali hayo upo wazi, lakini kinyume chache baada ya kusema hivyo tulikuwa tunakosa na kufeli somo hilo kwa sababu tulikuwa wazuri sana wakuona na kusema kuliko kutenda.
Leo niamua kuwaza kwa sauti hata wewe mwenzangu usikie nilichokiwaza ili uweze kupata mafanikio hayo na sio kuishia kusema nataka kile bila hata kujua utakipata vipi.
Zifuatazo ndizo mbinu zitakazobadili mfumo wa Maisha yako;
1. Usijadili vitu kwa macho.
Katika safari ya kuelekea au kupata mafanikio hakuhitaji kuvitazama tu vitu bali ni lazima ufanye uchunguzi wa kutosha. Huwa nakumbuka sana wakati tunasoma shule hasa somo la hesabu wengi wetu tulikuwa tukiyatazama maswali tulikuwa tunasema haya yameisha kwa maana ya kwamba uhakika wa kupata majibu ya maswali hayo upo wazi, lakini kinyume chache baada ya kusema hivyo tulikuwa tunakosa na kufeli somo hilo kwa sababu tulikuwa wazuri sana wakuona na kusema kuliko kutenda.
Jaza kichwa chako mawazo chanya. |
Mfano huu
ndivyo unavyoendelea mpaka leo hii kwa watu wanaotaka kupata mafanikio. Wengi
wao hutumia macho tu na kujipa majibu kwamba watafanikiwa. Kwa mfano mtu
anataka kufungua biashara mahali fulani kwa kuwa anatumia macho peke yake
katika kuona, anaona wafanyabiahara wengine wanafanikiwa na yeye kwa kutumia
uzoefu wake wa kuona tu hujikuta na yeye kaanza biashara mara moja.
Lakini inapotokea pale mtu huyo ambapo biashara hiyo haitakwenda vizuri utamsikia mtu huyo anasema karogwa ila ukweli hakuna atakayekuwa amekuroga zaidi ya kujiroga mwenyewe. Pia daima kumbuka kuona peke yake haitoshi bali uchunguzi wa kina huhitajika kwa jambo ambalo unataka kulifanya.
2. Kujaza kichwa chako mawazo chanya.
Mawazo chanya ni mawazo yatakayokufanya uweze kutoka hatua moja hadi nyingine ya kimafanikio. Swali dogo la kujiuliza kabla siku mpya haijaisha, je huwa unajiuliza ni mawazo gani chanya ambayo umewaza kutwa nzima? Na umeyachukulia hatua kwa kiasi gani? Na kama umechukulia hatua yana uwezo gani wa kubadili maisha na kinyume chake ni vipi.
Nikumbushe tu ya kwamba moja ya sifa ya watu wenye mawazo chanya kwa kile ambacho anakiwaza hukiandika katika kumbukumbu huku utekelezaji ukisubiri kuanza mara moja. Mawazo chanya ndiyo ambayo humbadilisha mtu siku zote na mawazo hasi ndiyo ambayo yamekuwa yakiwafanya watu waishi mawazo ya umaskini kila siku.
Mara nyingi mtu huanza kuwaza maamuzi mazuri ila namna ya kutekeza ndiyo huja mawazo hasi ya utekelezaji, Kwa mfano mtu anawaza kuwa mfanyabiashara mkubwa wa maduka ya nguo ndio hayo ni mawazo chanya lakini mawazo ya utekelezaji jambo hilo yanakuja mawazo mabaya kama vile tumia njia za kishirikiana hapo utafanikiwa. Baada ya hapo kwa kuwa mtu huyo baadala ya yeye kuiongoza akili yake ila yeye anaongozwa na akili yake mwisho wa siku anaingia katika kutekeza jambo lake kwa njia zisiso rasmi na mwisho wa siku anakuwa maskini maisha yake . Badili mtazamo na waza chanya ama hakika utafanikiwa.
Nukuu ya leo inasema ; Hakuna Binadamu aliyeletwa duniani kuzurura.
Imeandikwa na Afisa Mipango; Benson Chonya.
Simu ;0757-909942
E-mail: bensonchonya23@gmail com
May 19, 2016
Kupinduana Kwenye Ndoa Hutokea Sana.
Unapoishi
nyumbani na ndugu yako, jamaa yako na hata mtumishi wa kike, ni vizuri
ukajitahidi kulinda ndoa yako. Kumbuka kwamba, wanaume hawajali sana hisia, bali
hujali zaidi mwili. Kama ukimwachia jamaa yako, ndugu yako au rafiki yako
kumzoea sana mumeo, jua tu kwamba, inawezekana unajitengenezea maumivu makubwa
sana hapo baadae.
Tafiti
zinathibitisha sasa kwamba, mwanamume anapohisi kuwa mwanamke fulani
anamwonesha kwamba, yeye ni mwanaume kwelikweli, anapoonesha kwamba, anatambua
uwepo wake na mchango wake katika familia, mwanaume huanza kumpenda, bila
kujali sura au hadhi.
Kama
ndugu yako ni mjuaji wa mambo haya, anaweza kumwonyesha mumeo kwamba, anaamini
kuwa ni mwanamume kwelikweli. Hii hufanyika kwa kumsifu, kutokupingana naye,
kumpongeza mara kwa mara na kumwosha kwamba, anaamini katika yeye.
Hata
wale watumishi wa ndani, wanaochukuliwa na wanaume za watu hawafanyi hivyo kwa
sababu, ati hao watumishi ni wazuri sana wa sura au wanajua sana mapenzi,
hapana.
Kuwa makini na ndoa yako. |
Wanaume
huwachukua kwa sababu, wake au wapenzi wa wanaume hao, wameshindwa wajibu wao,
wameshindwa kujua kwamba, wanaume hutazama uhusiano kwa jicho tofauti.
Lakini,
iwe ndugu zetu au jamaa zetu na hata watumishi majumbani mwetu, bado na wao ni
binadamu, wana udhaifu. Kwa udhaifu wao, pamoja na udhaifu wa wanaume au
wapenzi wetu, wanaweza kutusaliti. Kwa hiyo ni juu yetu kulinda ndoa zetu, ili
udhaifu huo usiwe chanzo cha kuvunjika kwa matumaini na matarajio yetu ya
kujenga familia.
Kuna
mambo mawili makubwa hapa. Kwanza, inawezekana tumejiachia sana kama wanawake
na kusahau kuwa wanaume huvutiwa na mambo gani. Kwa hali hiyo, tunawaacha wale
waliokaribu nao kuwafanyia yale wanayohitaji na kuchukua nafasi zetu..
Lakini
pili, ni udhaifu wa kibinadamu na zaidi kwa wanaume, linapokuja suala la mwili.
Kwa udhaifu huo, inabidi tuwasaidie kuwalinda ili wasishawishiwe kiurahisi. Lakini,
ndugu zetu wa kike au watumishi tunaoishi nao, inabidi tuwakague vizuri na
kuacha kuwaamini kupita kiasi kwa wanaume au wapenzi wetu.
Ni
hatari sana kwa mwanamke kwa mfano, kumwambia au kumruhusu mumewe aende sehemu
za starehe na rafiki yake wa kike au na ndugu yake wa kike, ati kwa sababu
anamwamini rafiki huyo au mumewe. Kumbuka, suala hapa siyo kuaminika, bali
ukweli wa kiimaumbile pia. Chunga ndoa yako, ilinde sana, kwani siyo dhambi
kufanya hivyo.
Nakutakia
siku njema na Baraka katika ndoa yako.
Makala
hii imeandaliwa na Devotha Kauki. Unaweza kuwasiliana na mwandishi kwa
dvkauki@gmail.com
May 18, 2016
Kweli Nne (4) Kuhusu Mafanikio, Ambazo Hutakiwi Kuzisahau.
Ili
uweze kufanikiwa ni lazima uzijue kweli zenye uwezo wa kukupa mafanikio.
Haijalishi unafanya nini, ukizijua kweli, kanuni au mbinu zinazotoa mafanikio
ni lazima ufanikiwe. Hivyo haitajalisha una historia gani au unatoka katika
taifa ama familia gani kufanikiwa kwako kutakuwa ni lazima ukielewa kweli au
kanuni hizo. Mara nyingi watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu ya
kushindwa kuzijua kweli hizo.
Sipendi
uwe miongoni mwao ukashindwa kufanikiwa kwa sababu ya kutokujua mafanikio
yanataka nini. Kwa kusoma makala haya, nitakushirikisha kweli ambazo unatakiwa
kuzijua ili uweze kufanikiwa. Ni kweli ambazo zinatumiwa na wengi ikiwemo mpaka
na watu wenye mafanikio makubwa. Hakuna ubishi ukijua kweli hizi na kuzifanyia
kazi, nafasi ya kufanikiwa kwako itakuwa ni kubwa. Je, kweli hizo ni zipi?
1. Maisha yako yanakutegemea
kwa asilimia zote.
Ukitaka
kufanikiwa kwa viwango vikubwa, elewa kabisa kwamba maisha yako yanakutegemea
wewe kwa asilimia zote. Acha kutegemea kitu au chochote kilicho nje ya maisha
yako, wewe ndiye unayewajibika katika maisha yako kwa asilimia zote. Hata
inapotokea pengine umekosea acha kusukumia makosa hayo kwa wengine, jifunze
kutambua wewe ndiye chanzo.
Kwa
kuwa umeshajua maisha yako yanakutegemea wewe, acha kubeba visingizio
vinavyokuzuia kufanikiwa. Sahau juu ya habari ya wazazi wako eti kwamba ooh
hawakuweza kukusomesha, sahau kila kitu. Wajibu wa maisha yako, unao wewe.
Tenda kazi zako kwa nguvu zote huku ukiamini mtu pekee wa kubadilisha maisha
yako ni wewe. Huu ni ukweli ambao kamwe hupaswi kuusahau kwenye maisha ya
mafanikio.
Wewe ni mshindi. |
2. Mawazo yako ni kila kitu.
Mawazo
uliyonayo ndiyo yanayaoamua maisha yako yawe vipi. Upo hapo kimaisha ni kwa
sababu ya mawazo ambayo ulikuwa nayo siku za nyuma. Kwa hiyo, sisi ni matokeo
ya fikra au mawazo tuliyonayo. Mawazo yetu ndiyo yaliyotufikisha hapa na sio
kitu kingine. Hivyo kwa kujua hili ni muhimu sana kuwa makini na kile
unachokiwaza kwa sababu utakivuna, haijalishi kiwe kibaya au kizuri.
Kila
siku jifunze kufikiri mawazo chanya. Fikiria yale mambo ambayo unataka
yakutokee. Acha kufikiria yale usiyataka utayapata. Mawazo yako
hayatakudanganya, utavuna kile unachofikiria. Kumbuka kama nilivyoanza kwa
kusema, upo hivyo kwa sababu ya mawazo uliyonayo. Kwa kulijua hili, itakusaidia
kuwa makini na kile unachokiwaza.
3.
Una uwezo mkubwa wa kupata chochote, ukiamua.
Kweli
nyingine ambayo hutakiwi kuisahau katika maisha yako ni kwamba, una uwezo wa
kupata chochote ikiwa utaamua. Kama utaamua kuwa na mafanikio makubwa,
utayapata. Kama utaamua kuwa mwanamziki, mwandishi au kitu kingine chochote,
unauwezo wa kukipata pia. Kitu cha msingi ili kukipata hicho unachokitaka ni
lazima ujitoe kwanza.
Hakuna
ajali kwenye mafanikio. Upo hivyo pia kwa sababu ya maamuzi yako uliyoyafanya.
Kama kuna kitu chochote unachokitaka, fanya maamuzi na kisha chukua hatua. Uwezo wa kufanikisha
chochote katika maisha yako, unao.
4.
Una nguvu kubwa zilizo ndani yako.
Fanya
kazi kwa ubora na juhudi zako zote huku ukiamini nguvu kubwa ambazo unazo ndani
yako. Unao uwezo mkubwa wa kufanikisha jambo lolote ulio ndani yako. Lakini kwa
bahati wengi wetu ni watu wa kutumia nguvu zilizo chini ya viwango vyetu. Ukijua
uwezo ulionao na ukaamua kuutumia, utafanikiwa sana. Huu ni moja ya ukweli
unaotakiwa kuujua kuhusu mafanikio na kukubali kutumia.
Utafika
kwenye mafanikio makubwa ikiwa utaamua kuzitumia kweli hizo, kukusaidia
kufanikiwa.
Tunakutakia
siku njema na endelea kujifunza kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila
siku.
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
May 17, 2016
Njia Tano (5) Bora Za Kukuza Biashara Yako.
Moja ya changamoto
kubwa inayowakumba wafanyabiashara walio wengi ni kutokujua kiundani juu ya
biashara zao. Kutokana na changamoto hiyo ya kutokujua kiundani biashara zao, wafanyabiashara
hao walio wengi hujikuta biashara zao huwa haziwi za muda mrefu na hata pale
zinapokuwa za muda mrefu huwa hazikui.
Naamini kwa kuwa lengo lako ni kukuza biashara, ni vyema kwa kupitia makala haya, ukafahamu pia baadhi ya mambo muhimu yatakayokusaidia kukuza hata biashara yako. Nakusihi ufuatane nami mwanzo hadi mwisho ili kuweza kuona biashara yako inakuwa na maisha marefu na yenye kukua siku hadi siku.
Naamini kwa kuwa lengo lako ni kukuza biashara, ni vyema kwa kupitia makala haya, ukafahamu pia baadhi ya mambo muhimu yatakayokusaidia kukuza hata biashara yako. Nakusihi ufuatane nami mwanzo hadi mwisho ili kuweza kuona biashara yako inakuwa na maisha marefu na yenye kukua siku hadi siku.
1. Ongeza maarifa kwa kujifunza.
Kama kweli unahitaji mafanikio zaidi ya kiabiashara ni vyema ukawa ni mtu wa kujifunza kuhusiana na biashara yako. Ni lazima ujifunze mbinu mbalimbali ambazo wanazitumia wafanyabiashara wengine kufanikiwa. Kujifunza huku kukupe muda muafaka wakugundua pale ambapo wafanyabiashara wengine wanashndwa. Baada ya kujua wanashindwa wapi kwako ifanye kama fursa ya kuboresha biashara yako. Kufanya hivyo kutakufanya uongeze wateja kwani utakuwa mbunifu zaidi.
Acha kuridhika na hali uliyonayo. |
2. Badili tabia
zako.
Moja ya chachu nzuri ya kukufanya ukue kibiashara ni lazima uweze kujua vizuri tabia yako. Inawezekana wewe unajiona upo sawa ila kumbe sivyo unavyofikiri. Hata hivyo ili kuweza kujua ni ipi tabia yako ni vyema ukafanya uchunguzi ili kujua watu wanakuzungumziaje wewe? Kufanya hivyo kutasaidia kwa sababu watu wengine ndio wana picha kamili juu ya wewe na biashara kwa ujumla. Pia ili kuweza kufanikiwa ni lazima uweze kubadili tabia uliyonayo ya uvivu na ongeze juhudi za kiutendaji katika kufanya kazi.
3. Tenga muda wa kufikiri kuhusu biashahara yako.
Moja ya mbinu ya kuweza kukuza biashara yako ni kuweka muda kwa ajiri ya kujua biashara yako inakwenda vipi. Biashara zilizo nyingi huwa hazina maisha marefu kwa sababu wahusika hawa na muda wa kutosha kuhusu kufikiri jinsi gani biashara inakwenda bali walio wengi hutazama faida tu. Kufanya hivyo tambua biashara yako hatakuwa na Maisha marefu ni vema ukawa mzuri kujua utendaji wako wa kibiashara na changamoto zake na jinsi ya kutatua.
4. Tambua mchango wako wa watu wengine.
Ukitaka kufanikiwa zaidi ni vyema ukajua ni kwa jinsi unavyojenga mahusiano mazuri pamoja na wafanyabiashara wengine na wateja wako pia. Mchango mzuri uliona nao utakufanya uongeze wateja wengine. Kwa mfano unauza biashara fulani ghafla ukaishwa bidhaa fulani harafu mteja akaja kuuliza bidhaa hiyo, usimwambia mteja huyo kwamba kama huna bidhaa hiyo mwambie ngoja nikakuchukulie kwenye stoo. Na kwa kuwa wewe huna bidhaa hiyo nenda kwa jirani yako nenda ukanunue na uje kumpa mteja huyo. Kufanya hiyo kutakufanya uweze kujenga mahusino na wafanyabiashara nyingine pia njia ya kuongeza wateja na kufanikiwa zaidi.
5. Usiridhike na hali uliyonayo.
Kuwa mfanyabiashara mkubwà ni lazima kuwa katika imani ambayo inatamani kufanikiwa zaidi. Maana yangu hata kama wewe unajiona tayari umefanikiwa wewe jione bado una kiu ya kufanikiwa zaidi. Kama wasemavyo kwamba pesa haitoshi basi hata wewe una deni la kufanikiwa zaidi. Moja ya kufeli kwa biashara ni pale mtu anapoona amepata mafanikio na yeye anaridhika . Kuridika ni adui wa mafanikio. Kuridhika ndiko kunako turudisha nyuma watu wengi sana. Pia nikumbushe ya kwamba kufeli sio kushindwa ni sehemu ya mafanikio.
Haya ndiyo mambo kadhaa unayoweza kuzingatia ili kuweza kukuza biashara yako. Chukua hatua mapema za kubadili maisha yako.
Moja ya chachu nzuri ya kukufanya ukue kibiashara ni lazima uweze kujua vizuri tabia yako. Inawezekana wewe unajiona upo sawa ila kumbe sivyo unavyofikiri. Hata hivyo ili kuweza kujua ni ipi tabia yako ni vyema ukafanya uchunguzi ili kujua watu wanakuzungumziaje wewe? Kufanya hivyo kutasaidia kwa sababu watu wengine ndio wana picha kamili juu ya wewe na biashara kwa ujumla. Pia ili kuweza kufanikiwa ni lazima uweze kubadili tabia uliyonayo ya uvivu na ongeze juhudi za kiutendaji katika kufanya kazi.
3. Tenga muda wa kufikiri kuhusu biashahara yako.
Moja ya mbinu ya kuweza kukuza biashara yako ni kuweka muda kwa ajiri ya kujua biashara yako inakwenda vipi. Biashara zilizo nyingi huwa hazina maisha marefu kwa sababu wahusika hawa na muda wa kutosha kuhusu kufikiri jinsi gani biashara inakwenda bali walio wengi hutazama faida tu. Kufanya hivyo tambua biashara yako hatakuwa na Maisha marefu ni vema ukawa mzuri kujua utendaji wako wa kibiashara na changamoto zake na jinsi ya kutatua.
4. Tambua mchango wako wa watu wengine.
Ukitaka kufanikiwa zaidi ni vyema ukajua ni kwa jinsi unavyojenga mahusiano mazuri pamoja na wafanyabiashara wengine na wateja wako pia. Mchango mzuri uliona nao utakufanya uongeze wateja wengine. Kwa mfano unauza biashara fulani ghafla ukaishwa bidhaa fulani harafu mteja akaja kuuliza bidhaa hiyo, usimwambia mteja huyo kwamba kama huna bidhaa hiyo mwambie ngoja nikakuchukulie kwenye stoo. Na kwa kuwa wewe huna bidhaa hiyo nenda kwa jirani yako nenda ukanunue na uje kumpa mteja huyo. Kufanya hiyo kutakufanya uweze kujenga mahusino na wafanyabiashara nyingine pia njia ya kuongeza wateja na kufanikiwa zaidi.
5. Usiridhike na hali uliyonayo.
Kuwa mfanyabiashara mkubwà ni lazima kuwa katika imani ambayo inatamani kufanikiwa zaidi. Maana yangu hata kama wewe unajiona tayari umefanikiwa wewe jione bado una kiu ya kufanikiwa zaidi. Kama wasemavyo kwamba pesa haitoshi basi hata wewe una deni la kufanikiwa zaidi. Moja ya kufeli kwa biashara ni pale mtu anapoona amepata mafanikio na yeye anaridhika . Kuridika ni adui wa mafanikio. Kuridhika ndiko kunako turudisha nyuma watu wengi sana. Pia nikumbushe ya kwamba kufeli sio kushindwa ni sehemu ya mafanikio.
Haya ndiyo mambo kadhaa unayoweza kuzingatia ili kuweza kukuza biashara yako. Chukua hatua mapema za kubadili maisha yako.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)