Aug 31, 2016
Kama Unajiambia Na Kufikiri Hivi Kila Wakati, Huwezi Tena Kufanikiwa.
Mara nyingi katika maisha yetu kama tuna kawaida ya kujiambia
maneno au kauli za aina fulani, ni lazima tutajihisi kwa namna ile
tunavyojiambia sisi mwenyewe. Kumbuka kujiambia huku huwa tunafanya kati yetu
binafsi kila siku na kila wakati vichwani mwetu ambapo mazungumzo huwa
yanaendelea huko, ambayo mara nyingi ni siri zetu.
Kama ikatokea tuna kawaida ya kujiambia maneno au kauli za aina
fulani, ni lazima tutajihisi kwa namna tunavyojiambia. Hivyo, wakati mwingine
kujiamini au kutokujiamini kwetu ni matokeo ya yale yanayoenda vichwani mwetu,
yaani tunajiambia nini kuhusu sisi wenyewe. Kwa kujiambia kwa namna fulani,
hisia, hali na mazingira yetu yatakuwa hivyohivyo.
Naomba nikufundishe jambo moja ambalo ni muhimu sana kwako
kulijua. Kama kweli unataka kujiamini, ni lazima uanze kujichunguza namna au
jinsi unavojiambia wewe mwenyewe. Kujichunguza huku maana yake ni kutambua,
kufahamu na kujua kwamba, huwa kuna mazungumzo ambayo unayaendesha kichwani
mwako kuhusu wewe mwenyewe.
Kumbuka kwamba, kile ambacho huwa tunajiambia, yaani yale
mazungumzo tunayoyafanya vichwani mwetu, ambapo mara nyingi ni kujilaumu,
kujishusha, kujikatisha tamaa na mengine ya aina hiyo, yanakuwa yana nguvu sana
kwetu. Kwa nini? Ni kwa sababu, tunapojiambia mambo hayo inakuwa sawa kabisa na
tunavyowaambia watu wengine.
Kasi ya kuzungumza, lafudhi na hata sauti tunayoitengeneza huko
kichwani, havina tofauti sana na wakati tunapokuwa tunamwambia mtu mwingine kwa
sauti tu ya kawaida ya mdomo. Ndiyo maana yanakuwa yana nguvu ya kutuathiri.
Inakuwa ni kama kweli kabisa, ingawa ni ukweli kwamba hayo yote tunakuwa
tumeyazungumzia vichwani mwetu.
Hivyo, tunapojiambia huko kichwani, ‘mimi ni bwege tu siwezi kufanikiwa’ au ‘mtu mbaya kama mimi nani atanipenda!’ ama ‘nitakufa
maskini tu, si nimetoka familia maskini hata hivyo’, ni wazi hayo
yatakufanya ujitoe thamani na kutokujiamini. Yanakuwa ni maneno ya kukuumiza
wewe ni sawa kabisa na kama vile unaambiwa na watu wengine.
Mbaya zaidi pia ni kwa sababu ni sisi wenyewe, tunaojiambia mara
nyingi tena na tena na athari zinakuwa kubwa zaidi kwetu kutokana na msisitizo
tunaouweka bila hata kujua. Kama nilivyosema awali, unapaswa kujua kwamba
unafikiri. Ukishajua, itakuwa rahisi sana kwako kujiuliza kama yale unayojiambia
kuhusu wewe mwenyewe ndiyo unayotaka au hapana.
Kama siyo unayotaka, kwa kadri unavyojiambia ndiyo utakavyokuwa
unazidi kupata hisia usizozitaka. Kama ukianza kutambua kwamba huwa unafikiri,
itakuwa ni rahisi sana kwako kuweza kubaini kuwa, huwa unajiambia nini juu yako
mwenyewe ambacho kinaweza kukusaidia au kukuumiza na kuharibu maisha yako
kabisa.
Kama unataka kujiondoa na janga la kujitia katika kutokujiamini,
inabidi uchukue kalamu na karatasi, ujaribu kuandika kile usichokipenda ambacho
huwa unajiambia kuhusu wewe, mara kwa mara au kile unachojiambia katika mazingira
fulani. Kwa kujua kile unachojiambiwa mara kwa mara ambacho hukipendi,
itakusaidia kuwa makini nacho na pengine kukiepuka kabisa katika fikra
zako.
Kwa mfano, huwa inatokea ukajiambia, ‘achia hapo usije ukaadhirika
wewe’, au labda ‘usifanye tena si umeona ulivyoshindwa safari ile ‘, ama ‘ni
kawaida yangu kukosea nimezoea’ ama ‘siwezi kumudu kwa sababu ni bwege basi’.
Kumbuka kwamba, maneno hayo ni mabaya na kamwe hayawezi kukusaidia
kujiamini na kupata unachokihitaji. Ni maneno yenye nguvu sana ya kuweza
kuingiza hisia usizozitaka ndani kabisa ya mfumo wako wa kufikiri. Kumbuka,
siyo wakati huu, bali hata wakati mwingine, ukikutana na mazingira
yanayokufanya ujiambie hivyo, utajihisi hovyo hivyohivyo.
Kwa kuyaandika na kuyaelewa na kuelewa ni wakati gani na kwenye
mazingira gani huwa unajiambia maneno hayo, inaweza kuwa rahisi kwako kuanza
polepole kudhibiti mazungumzo hayo hayaendayo kichwani mwako. Ukifanya hivyo,
polepole, utaanza kujiamini.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO.
IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,
Aug 30, 2016
Mambo Ambayo Watu Wenye Mafanikio Huyafanya Sana ‘Wikiendi’.
Kimsingi,
ipo tofauti kubwa sana kati ya watu waliofanikiwa na watu ambao hawajafanikiwa,
husani katika suala zima la matumizi ya siku za mapumziko hasa wikiendi.
Mara
nyingi watu waliofanikiwa huzitumia wikendi zao kwa manufaa zaidi ukilinganisha
na wale ambao hawajafanikiwa. Kutokana na matumizi haya ya muda huo wa
mapumziko ndio wakati mwingine huweza kuleta utofauti hata wa mafanikio.
Hebu
tuangalie watu wenye mafanikio huzitumiaje ‘wikiendi’
zao;-
1. Kuamka asubuhi na mapema.
Mara
nyingi watu wenye mafanikio, ratiba yao ya kuamka ipo pale pale bila kujali
kwwamba ni siku ya kawaida au ‘wikiendi’. Siku zote hujitahidi sana kuweza
kuamka asubuhi na mapema.
Hufanya
hivi kwa sababu wanatambua muda ni wathamani sana. Hivyo, hawako tayari
kupoteza muda kwa chochote zaidi ya kuamka mapema na kuanza kuwekeza kwenye
muda huo ili uwape faida.
2. Kujisomea.
Kati
ya kitu amabacho watu wenye mafanikio huhakikisha wanakifanya wikiendi ni
kujisomea. Kupitia kujisomea huko hujifunza mambo mengi ambayo yanawasaidia
katika kukua kimafanikio na kupambana na changamoto za maisha.
3. Kutafakari juu ya maisha.
Watu
wenye mafanikio katika wikiendi zao hawaishii kujisomea tu, bali wakati
mwingine kutafakari sana juu ya maisha yao. Hutumia muda huo kujiuliza wapi
walipotoka, wapi walipo na wapi wanapokwenda. Maswali hayo huwasidia kupiga
hatua nyingine kubwa ya kusonga mbele.
4. Kufurahia maisha na familia.
Pia
wikiendi kwa watu wenye mafanikio huzitumia sana kuwa pamoja na familia zao. Ni
wakati ambao hupenda kucheza na kwenda maeneo tofauti na nyumbani kama ‘beach’ au mbuga za wanyama, kufurahia
maisha na familia zao.
5.
Kuweka mipango sawa ya wiki lijalo.
Mara nyingi watu wenye mafanikio huzitumia
wikiendi zao, kwa kupanga mipango mipya ya wiki lijalo. Hapa hukaa chini na
kujiuliza ni mikakati gani ambayo wataichukua ili kufanya wiki lijalo liwe bora
na la manufaa zaidi.
6. Kufunga
mawasiliano yasiyo ya muhimu.
Hiyo haitoshi watu wenye mafanikio ‘wikiendi’ zao huwa hawapendi sana kuwa
na masiliano mengi kama ilivyo siku za kawaida. Kama ni simu wakati mwingine
huzifunga au huwa hawapendi kuwasiliana sana na wengine katika kipidi hiki
kifupi cha mapumziko.
7.
Kutoa shukrani.
Shukrani ni jambo lingine la pekee ambalo watu
wenye mafanikio hulifanya kwenye siku za mapumzikio. Ni kipindi ambacho huweza
kuishukuru jamii kwa kwa namna tofauti mfano kutoa zawadi au kutembelea
wagonjwa na mengineyo.
Kwa kifupi hayo ndiyo mambo machache ambayo
watu wengi wenye mafanikio huyafanya sana katika siku zao za mapumziko ya wiki.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Aug 29, 2016
Kama Unataka Kufanikiwa Ni lazima Uongozwe Na Jambo Hili Kwanza.
Kisaikolojia kila binadamu anaongozwa na nafsi mbili ambazo ni
hisia na Hoja .
Hisia ni hali ya utabiri isiyokuwa na uhakika wa jambo. Huenda
ikawa na ukweli au uongo. Mara nyingi hisia hutawaliwa na tamaa ya macho au
mwili. Hoja ni uhalisia wa jambo au mambo yanayoonekana kwa macho. Ni mambo
yenye uhalisia kimtazamo. Mtu yeyote anayeongozwa na hoja hufanikiwa kwa 100%
lakini mtu anayeongozwa na hisia au tamaa ni kama mcheza kamari, anaweza kupata
au kuliwa au kushindwa kabisa.
Hisia kama tulivyoona ni tabia ya kimaumbile aliyonayo mtu. Kila
mtu ana tamaa ya kupata mafanikio katika maisha yake. Hiyo ni hisia haina hoja
ya msingi katika kuleta mafanikio. Mafanikio ili yapatikane lazima iwepo hoja
ya msingi itakayo tawala katika maneno na vitendo vya mtu katika maisha
ya mtu. Kivipi kuwe na hoja za msingi?
Ukitaka mafanikio lazima ujenge hoja za msingi na zenye
mashiko. Ni lazima uwe tayari kuizishinda hisia za matamanio katika maisha.
Uamue kuifanya akili yako iongozwe na hoja badala ya kuongozwa na hisia.
HOJA ZA MSINGI ZITAKUSAIDIA KUFANIKIWA. |
Hoja humfanya mtu kuwa na uhakika wa kile anachokifanya. Kuwa na
‘data’ sahihi za kile anachofanya.
Humfanya mtu kufanya kila kitu kwa ufanisi MKUBWA.
Hoja humfanya mtu kujiamini na kuthamini kile anachofanya. Hoja
humpa heshima na kumfanya athaminike na jamii kutokana na kufanya vitu sahihi
na vyenye tija kwa jamii.
Hisia au tamaa humfanya mtu kufanya maamuzi yanayompelekea
kujuta baadae katika maisha take.
Hisia zikimtawala mtu hufanya vitu vya aibu na kumdhalilisha katika
jamii kama kuiba, kubaka, kulawiti, kusema uongo kwa manufaa binafsi, kula mali
ya haramu bila Hofu. Hisia zikimtawala mtu hukosa kujiamini na kujiona mwenye
mapungufu na kukosa ujasiri.
Katika kumalizia somo letu naomba kutoa angalizo kuwa kabla ya
kufanya maamuzi katika jambo lolote unalohitaji kufanya kwanza jiulize
unayotaka kufanya je, yanaongozwa na hisia au hoja? Kama yanaongozwa na hisia
au tamaa kamwe usifanye jambo hilo na kama jambo hilo linaongozwa na hoja
hakika lifanye maana litakufaa katika maisha yako.
Naomba tuishie hapa kwa leo tukutane muda ujao kwa ajili ya
kujifunza zaidi na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza kwa kina.
Tupo pamoja,
Shariff H. Kisuda (Mzee wa Nyundo)
Simu; 0715 079 993,
Aug 19, 2016
Hatua Muhimu Za Kukusaidia Kutoka Kwenye Madeni.
Wapo
watu wengi ambao huwa hawafikiri sana kwamba, kujiingiza kwenye madeni mengi ni
kitu cha hatari. Watu hawa huja kugundua kwamba wapo kwenye hatari hiyo mara baada
ya madeni hayo kuwalemea sababu ya wingi wake.
Kutokana
na madeni hayo kuwa mengi, na kushindwa kuyalipa, hapo sasa ndio majuto na
kilio huanza kutanda. Na wengi huanza kujilaumu kwa nini walikopa mikopo mingi,
mikopo ambayo kama inawatesa kwa sasa, kutokana na kushindwa kuilipa.
Najua
umeshawahi kukutana na watu ambao wana mizigo mingi na mikubwa ya madeni. Inawezakana
watu hawa walikuwa jirani zako, ndugu au pengine hata wewe mwenyewe. Je,
ulishawahi kujiuliza inapokutokea hali kama hii ni kitu gani unachotakiwa
kufanya?
Leo
kupitia makala haya, twende kwa pamoja kujifunza hatua muhimu za kukusaidia
kutoka kwenye madeni.
1. Weka mipango imara.
Hatua
ya kwanza itakayokusaidia kutoka kwenye madeni yako, ni kule kuamua kuweka
mipango imara ya kukutoa kwenye madeni yako uliyonayo. Utaweza kulifanikisha
hili vizuri, ikiwa utakaa chini na kupitia kiwango cha pesa unachotumia,
ukilinganisha na kile kinachoingia.
Weka mipango imara ya kutoka kwenye deni ulilonalo. |
Kwa
mfano, inawezekana kabisa upo kwenye madeni kwa sababu unatumia pesa nyingi
hovyo. Kwa hali hiyo hukupelekea matumizi yazidi kipato na kukufanya kukopa. Hivyo,
hakuna namna nyingine zaidi ya kuweka mipango imara ya kubana matumizi na
kuweza kuondokana na madeni.
2. Tafuta chanzo kingine cha pesa.
Njia
nyingine nzuri ya kuweza kuondokana na madeni uliyonayo ni kutafuta chanzo
kingine cha pesa. Acha kung’ang’ania kuwa na chanzo kimoja cha pesa, hiyo
inaweza ikawa ni hatari sana kwako katika harakati za kujikwamua kutoka kwenye
madeni.
Kwa
mfano, kama umeajiriwa tafuta namna yoyote ile uwekeze kwenye hiyo biashara. Halikadhalika,
kama umejiajri kwa kufanya biashara yako mwenyewe, jitahidi baada ya muda uwe
na biashara nyingine. Kwa kufanya hivi itakusaidia kuweza kutoka kwenye madeni.
3. Punguza matumizi yasiyo ya lazima.
Mbali
na kuweka mipango imara na kutafuta chanzo kingine cha pesa, pia unaweza kutoka
kwenye deni ulilonalo kwa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Wengi wetu mara
nyingi huwa ni watu wa matumizi mengi pasipo kutarajia.
Unawezaje
kutoka kwenye matumizi yasiyo ya lazima? Kwanza, unaweza kuepuka matumizi
yasiyo ya lazima kwa kuepuka kununua vitu visivyo vya lazima sana kwako. Pili, ni kuwa makini na
kila pesa inayotoka kwa kuiwekea kumbukumbu. Kwa hatua hiyo, inaweza kuwa msaada
kwako kukutoa kwenye madeni.
4. Anza kulipa madeni makubwa.
Kama
madeni uliyonayo ni mengi, ni vizuri kuya orodhesha madeni yako na kuanza
kuyalipa madeni yale makubwa. Kwa kuchukua hatua hiyo utajikuta mahali, umeweza
kuuotoa mzigo wa madeni ambao ulikuwa unakusumbua kwa muda mrefu.
Kwa
kuhitimisha makala haya, naomba niseme hivi; mikopo ni mizuri ikiwa itatumia
vizuri kwa malengo maalumu. Endapo utaitumia vibaya inaweza ikawa ni mzigo
mkubwa na kugeuka kuwa deni.
Kama
mkopo uliouchukua umekuwa deni, tafadhari hizo ni baadhi ya hatua ambazo unaweza
kuzitumia kutoka kwenye madeni uliyonayo. Lililo kubwa kwako, fanyia kazi hicho
ulichojifunza na chukua hatua.
Nikutakie
siku njema na kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
Chukua hatua sitahiki za
kubadili maisha yako na endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com
kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Blog;
dirayamafanikio.blogspot.com
Aug 18, 2016
Mawazo Muhimu Unayotakiwa Kuwa Nayo Ili Kukuza Biashara Yako.
Biashara
shaka naongea na wewe katika siku hii ya leo ukiwa kwenye biashara yako au
pengine ukitarajia kuanza biashara hivi punde. Kama uko kwenye biashara,
pengine naongea na wewe ukiwa kwenye harakati za kutafuta wazo bora litakalo kusaidia
kukuza biashara yako na kuwa ya mafanikio makubwa.
Kama
uko kwenye hali ya kutafuta wazo bora litakalokusaidia kukuza biashara kwa
kusoma makala haya itakusaidia sana. Ieleweke kwamba kuanzisha biashara na kuikuza
biashara hadi ukaiona inaleta matunda ni vitu viwili tofauti. Wengi hujitahidi
sana kuanzisha biashara lakini linapokuja suala la kukuza, hushindwa kwa sababu ya kukosa mawazo muhimu.
Kwa
namna yoyote ile, mfanyabiashara anahitaji kuwa na mawazo muhimu yatakayomsaidia
kukuza biashara yake wakati wote. Haijalishi
udogo au ukubwa wa biashara husika, lakini mawazo bora ni nguzo muhimu ya
kuifanya biashara ikaendelea mbele na kutoa mafanikio makubwa.
Leo
kupitia makala haya hebu tuangalie mambo gani muhimu unayatakiwa kuwa nayo ili
kukuza biashara yako.
1. Tanua soko lako.
Biashara
yako itaweza kukua ikiwa utakuwa una wazo la kutanua soko lako kila wakati. Kwa
mfano, kama umekuwa ukiuza bidhaa zako ndani ya mtaa mmoja, ni vyema ukafikiri
namna ya kuzipeleka na mtaa wa pili. Kwa wazo hilo litakusaidia sana kukuza biashara yako kwa viwango vya juu.
Jenga mtandao wa kukuza biashara yako. |
2. Pata maarifa ya biashara.
Kila
wakati inabidi ujifunze kuunoa ubongo wako na kujifunza sana juu ya biashara
unayoifanya. Maarifa ni muhimu sana katika kuikuza biashara yako, vinginevyo
biashara hiyo ni lazima itadondoka. Hivyo, unatakiwa kujisomea vitabu au kuhudhuria
semina mbalimbali za kibiashara ili kufanikisha hilo.
3. Toa huduma za ziada.
Unaweza
ukaifanya biashara yako ikakuwa na kuwa ya mafanikio ikiwa utajifunza kutoa
huduma za ziada. Kwa mfano, unaweza ukawapa wateja wako zawadi ndogo ndogo kila
wanaponunua bidhaa. Hilo litawasaidia kuwavuta na kujikuta ukikuza biashara
yako siku hadi siku.
4. Tengeneza mtandao wa kibiashara.
Huwezi
ukasema unakuza biashara yako na kusahau kukuza mtandao wako wa kibiashara. Ni lazima
kujitengenezea ‘netwek’ na
wafanyabiashara wenzako ya kukusaidia kukufanikisha. Hilo litakusaidia katika
kutatua changamoto na wakati mwingine hata kukuza bidhaa kwa urahisi.
5. Boresha bidhaa zako.
Mwisho,
ili uweze kukuza biashara yako, kwa vyovyote vile unalazimika kuboresha bidhaa
zako. Kila bidhaa unayoitoa ni lazima iwe ya viwango vya juu. Kwa hali hiyo
itapelekea utapata wateja wengi kila kukicha
na kusababisha biashara yako kuweza kukua.
Ikumbukwe
kwamba kutanua soko, kupata maarifa ya kibiashara, kutoa huduma za ziada, kutengeneza
mtandao na kuboresha bidhaa kila wakati, ni moja ya mawazo muhimu ambayo
unatakiwa kuwa nayo kila siku ili kukuza biashara yako.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku. Ila hakikisha unawashirikisha wengine waweze kujifunza zaidi.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Aug 17, 2016
Vitu Ambavyo Wengi Hujutia Sana Wanapofika Uzeeni.
Naamini
wote tunajua tunazaliwa, tunakua na ipo siku tutakuja fikia uzeeni. Hivyo kila
mtu kwa kujua hilo, hujitahidi sana kuishi maisha ambayo hatakuja kuyajutia kwa
hapo baadae akifika uzeeni. Kwa kifupi, kila mtu anapenda uzee wake uwe mzuri
ambao hauna lawama.
Hakuna
ambaye anapenda aje achekwe na watoto au wajukuu zake eti kwa kutotimiza
majukumu fulani. Kila mtu anapenda watoto au wajukuu zake wamsifie kwamba kweli
babu enzi za ujana wako ulifanya makubwa.
Hilo ndilo kila mtu analolitamani litokee katika uzee wake.
Lakini
hata hivyo kwa wengi waliofikia uzeeni kile wanachokitamani kiwe, huwa
hawakipata kwa sababu kadhaa. Hujikuta wakiishi maisha ya kujuta sana. Majuto
hayo hutokana hasa na mambo ambayo waliyafanya wakiwa vijana na kupelekea
pengine maisha yao kuwa magumu.
Sitaki
uwe miongoni mwa watu ambao wakifika uzeeni uje ujute kwa kulia sana. Leo
nanawa mikono kwa kukuonyesha vitu vya msingi ambavyo wengi huvijutia sana kila
wanapofika uzeeni. Sasa basi, vitu hivyo ambavyo wengi huvijutia sana hasa
wanapofikia uzeeni ni kama hivi vifuatavyo;-.
1.
“Kwa nini nilipoteza muda sana?”
Kati
ya jambo la wazi ambalo wengi waliofikia uzeeni wanalojutia ni kule kupoteza
muda. Huwa ni watu wa mawazo sana kutokana na lawama ambazo wanazipata kutoka
kwa jamii, watoto au wajukuu zao.
Mara
nyingi lawama hizi huelekezwa ni kwa nini maisha yao yako hivyo. Maswali kama
babu ulikuwa wapi wakati wnzako wanawekeza huulizwa sana. kwa hali kama hiyo
suala la kupoteza muda hujutiwa sana na wengi wakiwa uzeeni.
Wengi hujuta sana kwa kupoteza muda wao. |
2.
“Kwa nini sikuwekeza mapema?”
Si
kupoteza muda tu ambapo wengi wanapofikia uzeeni hujutia. Ila wakati mwingine
wanajuta kwa nini hawakuwekeza mapema wakati wa ujana wao. Hujiuliza maswali
mengi kwa nini hawakununua mashamba, hawakujenga nyumba, au kwanini hawakufanya
uwekezaji wa maana?
Hayo
yote huibuka mara baada ya kujiona wao wapo mikono mitupu na hawana nguvu tena.
Kilio, sononeko na majuto yanakuwa makubwa sana, hali ambayo inaweza kupelekea
kupata magonjwa yasiyotarajiwa kama shinikizo la damu.
3.
“Kwa nini sikuishi kwa kufuata ndoto zangu?”
Hili
pia huwa ni jambo linaloleta majuto hasa kwa wengi wanaopofikia uzeeni. Kitu
ambacho hujiuliza kila wakati kwa nini waliishi maisha ya kutimiza ndoto za
watu wengine, badala ya kukaa chini na kutimiza ndoto zao. Hapa huwaza sana je,
kipindi hicho walikuwa wamerogwa.
Hapa
walio fikia uzeeni hujiona wana hatia na makosa makubwa sana ambayo waliyafanya
wakiwa ujanani. Ukweli wote huo wanakuja kuujua baada ya kugundua kumbe hakuna
hata kitu cha maana walichokifanikisha duniani zaidi ya kufanikisha ndoto za wengine
na kusahau za kwao.
4.
“ Kwa nini sikuwasaidia wengi kutimiza ndoto zao?”
Pia
hufika mahali wale waliofikia uzeeni hutambua kwamba upo umuhimu mkubwa sana wa
kuisaidia jamii, hata kwa kidogo walichonacho. Lakini kila wakiangalia hakuna
msaada wa maana walioutoa. Hapo sasa ndipo huanza kuumia na kuwaza mengi.
Kiuhalisia,
huwa ni kipindi kigumu sana. Hapo ndipo unapoona wanajaribu kutoa angalau
msaada lakini inakuwa inashindikana kwa sababu pengine hawakujiweka vizuri
kiuchumi. Majuto ya kutokuwasaidia wengine huwaumiza sana pia.
5.
“Kwa nini sikujituma sana? ”
Wapo
wengine ambao hujita na kujilaumu kwa sababu ya kuona kwamba walitakiwa
kujituma sana hadi kufanikiwa. Sasa wanaona hawajafanikiwa na wanajua wazi hilo
ni kosa lao. Kila wakati wanapata shida na kujiuliza kwa nini hawakujituma sana
ili kujenga maisha mazuri zaidi.
Ikiwa
kweli una kiu kubwa ya kutaka uzee wako uonekana wa maana, basi unalazimika
kujituma sana kwenye kila jambo unalolifanya. Ikiwa hutajituma na kuweka
misingi imara wakati ukijana, sahau kuwana mafanikio uzeeni na zaidi utalamikiwa
na kujutia uzee wako wako wote.
6.
“ Kwa nini sikuishi na familia yangu kwa upendo?”
Haya
ni majuto huwa yapo wale wazee ambao kila wakikumbuka waliishi na familia kwa
migogoro mibgi sana. pi hali hiyo ilipelekea hata kutengana na kujikuta
wakiziacha familia zao zikiteseka.
Sasa
inapofika kipindi chha uzeeni hujikuta wakijuta na kujilaumu ni kwanini hayo
yote yalitokea. Ni kwa nini hawakuweza kuaysuluhisha mapema na kusababisha
mgogoro ambao unawasumbua hapo wakiwa uzeeni.
Kwa
kawaida unapokuwa kuwa kijana unaweza ukafanya makosa mengi na ukayachukulia
kawaida. Lakini inapofika uzeeni ndio unaanza kuelewa kwa nini ulikosea kufanya
hivyo.
Maisha
yako yapo mkononi mwako, kama bado una nguvu, jifunze kuwajibika ili baadae
usije ukajuta kwenye maisha yako ya uzeeni. Ukiangalia kwa ufupi hayo ndio
baadhi ya mambo ambayo wengi hujutia wakifikia uzeeni mwao.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani
Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Aug 16, 2016
Mambo Ya Kuzingatia, Ili Kuifanya Akili Yako Ifanye Kazi Kwa Ufasaha Na Mafanikio Makubwa.
Naamini katika maisha, huwa inafika mahali
kila mtu anatamani akili yake ifanye kazi vizuri na imletee mafanikio makubwa.
Lakini hata hivyo, pamoja na matamanio hayo wengi bado huwa hawajui wafanye
nini au wachukue hatua zipi ili kuweza kuipa akili nguvu zaidi kila siku na
kufanya kazi kwa ufasaha.
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, baada ya kufanya
utafiti kwa muda, walikuja kukaa chini na kuweka vigezo ambavyo kwa mtu akiviafuta
basi ni ni lazima akili yake iweze kufanya kazi vizuri zaidi na kwa mafanikio.
Moja ya vigezo walivyoviweka kama unataka akili yako ifanye kazi vizuri ni kama
hivi vifuatavyo:-
1. Chakula bora.
Ili akili yako iweze kufanya kazi vizuri sana,
inahitaji kwa kiasi kikubwa chakula bora, chenye virutubisho muhimu. Kwa mfano,
tafiti nyingi zilizofanywa kitaalamu zinaonyesha vyakula vya jamii ya samaki ni
muhimu sana katika kuipa akili yako afya ya kufanya kazi vizuri.
Hata hivyo utafiti huo haukuishia hapo tu,
unazidi kufafanua mara nyingi, watoto wanao tumia vyakula jamii ya samaki sana
huwa pia wana uwezekano wa kufanya vizuri hata darasani. Hivyo unaona, chakula
bora ni muhimu sana katika kuipa akili yako nguvu ya kufanya kazi vizuri.
2. Mazoezi.
Kati ya kitu rahisi ambacho hakiwezi
kukugharimu sana lakini ikiwa utakifanyia kazi na kitaifanya akili yako ifanye
kazi vizuri, ni mazoezi. Mazoezi yana uwezo mkubwa sana wa kuipa akili yako
nguvu kuliko. Wengi wanaofanya mazoezi, akili zao zipo vizuri.
Unaweza ukachukua jukumu leo la kuifanya akili
yako ikafanya kazi vizuri kwa kuamua kufanya mazoezi. Pengine unaanza kuwaza
unaanzia wapi? Kama ni hivyo usipate shida. Dakika 20 kwa siku iwe jioni au asubuhi
zinakutosha kabisa kuifanya akili yako ikawa na afya bora.
3. Fanya kazi za kujitolea.
Si kila wakati kazi unayofanya ni lazima ikupe
malipo. Kuna wakati kubali kujitolea kufanya kazi za jamii tena bure.
Unapofanya kazi kama hizi kikawaida kunakufanya ujisiie vizuri na mwisho wa
siku akili yako nayo inaanza kufunguka na kufanya kazi vyema hivyo hivyo.
Naona unashangaa katika hili, sikiliza. Wewe
ni matokeo ya jamii uliyopo. Kwa mujibu wa kanuni za maumbile ili uweze
kufanikiwa ni lazima uirudishie jamii yako kitu fulani kama shukrani. Sasa
mojawapo ya vitu hivyo, ndio kazi kama hizi angalau mara moja moja. Ukifanya hivyo
ujue kabisa akili itaanza kufanya kazi vyema.
4. Pata usingizi wa kutosha.
Pia usingizi wa kutosha kimetajwa kama ni
kigezo kimojawapo cha kuifanya akili yako kufanya kazi vizuri. Inasemakana
akili yako ili iweze kufanya kazi vizuri angalau unatakiwa kupata usingizi
usiopungua angalau saa nane kwa siku.
Najua hili unalijua vizuri, lakini je huwa
unalizingatia? Kama huwa ulizingatia sana, kuanzia sasa litilie mkazo na kuhakikisha
lazima akili yako inapumzika na kuipa nguvu ya kufanya kazi vizuri upya kwa
siku inayofuata. Ukifanya hivyo ni lazima akili yako ifanya kazi kwa ufasaha,
utake au sitake.
5. Jisomee kila siku.
Chakula bora peke yake hakitoshi kuipa akili
yako nguvu ya kufanya kazi kwa ufasaha. Kitu cha ziada ambacho kingine unatakiwa
kukiongeza ni kujisomea. Akili inayojisomea inakuwa ina nguvu sana ya kufikiria
na kufanya mambo kwa ubora.
Najua hili la kujisomea ni shida kwa wengi,
lakini hakuna namna nyingine ya kuifanya akili yako ikawa ina nguvu ya kuteda
kwa ubora, zaidi ya kujisomea. Unapojisomea unakuwa unaufikirisha ubngo na kuupa
changamoto na mwisho wa siku unajikuta umefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa kumalizia makala haya, tambua hayo ndiyo
mmbo ya msingi ambayo yamezungumzwa na wataalamu kwamba yanaweza kuipa akili yako
nguvu ya kufanya kazi kwa ufasaha.
Chukua
hatua sitahiki za kubadili maisha yako na endelea kujifunza kupitia DIRA YA
MAFANIKIO kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Aug 15, 2016
Mambo Mawili Ya Kuzingatia Sana Ili Kufanikiwa
Kitu kimojawapo kikubwa kinachotofautisha watu wanaofanikiwa na
wale wanaoshindwa kwenye maisha ni MATENDO ama ACTION kama wenye lugha zao
wanavyopenda kuita.
Haijalishi unajua nini, haijalishi unasema nini wala haijalishi
una uelewa mkubwa kiasi gani! Hivyo vyote unavyojua na kusema, kama huchukui
hatua ni sawa na kelele na havitaweza kukusaidia katika safari yako ya
mafanikio.
Mafanikio ya kweli kwenye maisha yako siku zote yanakuja,
ikiwa utajua kile unachotaka na kuchukua hatua za kuelekea kwenye mafanikio
yako kila siku. Hapa ndipo mafanikio yako yanapoanzia.
Bila kuchukua hatua, halafu ukasema eti unatafuta mafanikio,
hiyo itakuwa ni sawa na kujidanganya mwenyewe mchana kweupee.
Kitu cha kufanya na kukumbuka kila siku ikiwa unataka kufanikiwa
na kujitofautisha na wale walioshindwa ni KUCHUKUA HATUA KILA SIKU, HATA KAMA
NI KIDOGO bila kusahau kujua kile unachotaka.
Ukijua kile unachotaka na kuamua kuchukua hatua, hapo
utakuwa upo kwenye njia sahihi ya kukamata mafanikio yako. Mambo mengine ya
kukusaidia kufanikiwa kama kufanya kwa ubora, nidhamu binafsi au uvumilivu
yatakuja yenyewe, lakini ikiwa utajua unachokitaka na kuchukua hatua.
Haya ni mambo mawili muhimu sana ambayo ukiyazingatia ni lazima
ufanikiwe. Hata kama uliwahi kuitwa huwezi kufanikiwa tena, kilaza au eti una
uwezo mdogo, Lakini ukizingatia kujua kile unachokitaka na kuchukua hatua,
mafanikio ni yako.
Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi. Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Nakutakia kila la kheri,
Imani Ngwangwalu.
Aug 10, 2016
Hii Ndiyo Dozi Sahihi Ya Maisha Yako Ya Mafanikio.
Mara
kadhaa unatakuwa umekuwa shahidi kwa namna moja ama nyinyine kwa kuona ya
kwamba mtu akiumwa ni lazima atafute matibabu ili aweze kupona ugonjwa ambao unamsumbua.
Hivyo
hivyo mtu huyo akipewa dawa anatakiwa
kuzitumia katika utaratibu ambao unaeleweka ili aweze kupona, utaratibu huo
ndio ambao huitwa dozi, dozi hiyo lazima mtu aifuate ili aweze kupona na endapo
atatumia kinyume na alivyoelekezwa na
mtalamu upo uwezakano mkubwa kuweza hudhurika zaidi au kupoteza maisha.
Kama
ilivyo kwa mgonjwa ili aweze kupona na kuimarika vizuri katika afya yake hana
budi mgonjwa huyo kuweza kufuata
utaratibu wa kutumia dozi ili aweze kupona.
Hata
kwenye safari yako ya mafanikio ndivyo ilivyo, unahitaji kupata dozi, dozi
ambayo ina misingi na utaratibu wake wa kuitumia. Wengi wetu tunamani kupata
mafanikio kwa haraka zaidi, huku tukisahau ya kwamba mafanikio ni hatua kwa
maana ya kwamba ni lazima tumalize dozi ndipo tupate mafanikio hayo.
Hivyo
nakusihi uweze kufuatana nami ili uweze kujua namna ya kuweza kupata dozi ya
mafanikio yako, pia suala si kupata dozi tu, bali uzitumie katika maisha yako, na si
kuzitumia tu bali uzitumie ili upone
ugonjwa wa dhiki, shida na taabu za
kimaisha ili uweze kupata mafanikio yako.
Vile
vile nisisitize kwa kusema ya kwamba ili uweze kufika ambapo unataka ya kwenda
kwa maana ya kupata mafanikio huna budi ya kuamini na kuwa mvumilivu na mbunifu
wa hali ya juu sana.
Ifuatayo ndiyo dozi sahihi ya safari
yako ya mafanikio.
1. Angalia matumizi yako ya muda
katika kutekeleza malengo yako.
Ipo
haja leo ya kujua mambo ambayo yatakusaidia kuweza kutimiza malengo yako. Watu
wengi huwa tunakosea sana hasa katika kujali na kuzingatia muda wa kutekeza
mambo yetu.
Kwa
mfano watu wengi licha ya kuwa na malengo huwa hatuweki ni kwa muda gani ndoto
yako itakuwa imekamilika. Mfano ili uweze kufanikiwa na kutimiza malengo yako,
kwa mfano unataka kuwa mfanyabiashara fulani ni lazima ujue ni muda gani utakuwa umetiza jambo lako. Hii ni muhimu sana
kuzingatia.
Hata
hivyo kuwa na maono ya muda (time limit)kwa kila jambo lako itakusaidia kuweza
kujua ni kwa namna gani utakuwa umetiza lengo lako. Hivyo nakusihi kwa kila jambo lako ambalo unatamani kulifanya
kwa hapo baadae ni lazima uwe umelipanga ni baada ya muda gani lengo hilo litakuwa limekamilika. Pia mara
kadhaa endelea kukumbuka msemo ule mtamu wenye kukutia hamasa ya kwamba ni
‘muda ni mali’ hivyo huna budi kulizingatia hilo.
2.
Jifunze kutoka kwa watu walifanikiwa
huku na wewe ukitumia njia ambazo ni za tofauti.
Mara
kadhaa tumekuwa ni watu kulamika sana hasa pale ambapo tumefeli kwenye jambo
fulani. Kulalamika huku mara kadhaa nimegundua ni kwa sababu kuu moja ya kwamba tumejifunza kwa watu ambao wamefeli.
Lakini
kufanya hivi mara kadhaa hutupa picha ya kwamba hata sisi hatuwezi hii ni
kutokana mtu fulani alifeli. Kufeli kwa mtu
mwingine katika jambo lake kwa asilimia kadhaa hutengeneza hofu ndani
yetu, hofu hiyo ni ile hofu ambayo utajiona ya kwamba hauwezi.
Hata
hivyo kama unataka kupata mafanikio jambo la kuzingatia ni kwamba unatakiwa
kupata ushauri kwa watu sahihi ambao wamekwisha fanikiwa kufanya hivi
inakusaidia kwani wao wana taarifa sahihi kuhusiana na jambo hilo.
Kwa
mfano unataka kufanya biashara ya kuuza chipsi ukiomba ushauri kwa mtu ambaye
anauza mkaa, muuza mkaa huyo atakwambia biashara hiyo ina hasara sana, lakini
sababu hizo sio za kweli kwa sababu hana taarifa sahihi, hivyo kama unataka
kuuza chipsi ni lazima uweze kumfuata mtu ambaye amefanikiwa katika biashara
hiyo kwani mtu huyo anazo taarifa kamili juu ya biashara hiyo.
Hivyo
nakusihi ili uweze kupata mafanikio huna budi kuayazingatia hayo kwa hali ya
juu sana, hasa katika suala la utekelezaji, kufanya hivyo kutukufanya uweze
kuwa mshindi wa maisha yako. Endelea kufuatana nami katika safu hii kila
wakati.
“Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra
sahihi” kwa kuendelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ndimi; afisa mipango Benson Chonya
Blogu;
dirayamafanikio.plogspot.com
Email;
bensonchonya23@gmail.com
Aug 9, 2016
Kinachowaathiri Wafanyabiashara Wengi Na Kufanya Biashara Hizo Kufa Ni Hiki.
Siku
zote kumbuka ya kwamba biashara ni mchakato, ninapozungumzia mchakato ni maana
ya kwamba kuna kupanda na kushuka. Hapa nikiwa na maana ya kwamba kuanzisha
biahara ni rahisi sana, ila endapo biashara hiyo ikifa kurudi tena katika
kufanya biashara hiyo huwa ni vigumu sana.
Zipo
baadhi ya sababu ambazo zinawafanya wafanyabiahara wengi wayumbe sana hasa
katika biashara ambayo wanayofanya, najua wakati unaendele kusoma makala haya
bado unashangaa ya kwamba nazungunza na nani?
Usishangae
nazungumza na wewe, huenda ukawa unafanya biashara au haufanyi. Nazungumza na
wewe ili uweze kuepukana na mambo ambayo yanafanya au yatafanya biashara yako
ife.
Zifuatazo ndizo sababu ambazo zinawawathri
wafanyabiashara wengi.
1. Kukosekana kwa elimu ya jinsi ya
kukabiliana na ushindani katika soko.
Zipo
biashara ambazo zinakuwa au ambazo tayari zimekwisha kua ambazo mara nyingi
huwa zinateteleka kwa namna moja ama nyingine hasa linapokuja suala la
ushindani wa bidhaa au huduma katika soko.
Wafanyabiashara
walio wengi huwa wanakuwa na mtazamo mmoja tu. Mtazamo huwa ndio ambao unakuwa
unawaathari kwa asilimia kubwa sana. Mtazamo huo huwa katika suala la mfanano wa
utoaji wa huduma.
Kwa
mfano unakuta bidhaa ambayo utanunua mahali fulani, ubora na wingi wa bidhaa
vinafanana na mfanyabiashara/wafanyabiahara wengine. Kufanya hivi kunafanya
kuwepo kwa kutoeleweka ni nani mmiliki au mwazilishi au huduma imenunuliwa kwa
nani!
Hivyo
ifike mahali kila mmoja wetu ambaye anafanya biashara kuwe na utofauti kati
mfanyabiashara mmoja na mwingine, maana kufanya hivyo kutakutofautisha katika
kutambulisha huduma au bidhaa kwa mteja.
Vilevile
huna budi kuwa na utofauti na wengine kwa kuwa mbunifu katika biashara. Katika
ulimwengu huu wa dunia ambayo inaenda kasi kuliko neno lenyewe huna budi
kutumia teknolojia katika kujifunza kufanya biashara tofauti na watu wafanyavyo
sasa.
Hata
hivyo siri ya mafanikio ya kibiashara iliyojificha ni kwamba huna haja ya
kuongeza mtaji mkubwa katika biashara ila inakupasa kuweza kuongeza thamani
katika biadhaa au huduma.
Kwa Mfano badala ya kuuza samaki ambao wateja
wamezoea kwa shilingi elfu moja unaweza ukatumia teknolojia ya kuwakausha
samaki, na kufunga katika vifungashio vizuri na kuuza samaki yule yule ambaye
ulikuwa unamuuza kwa shilingi elfu moja na wewe ukaja ukamuuza kwa shilingi
elfu tano.
Kufanya
hivyo ndipo ninapozungumzia katika biashara yeyote ambayo unaifanya, fikiri kwa
umakini sana na kwa jinsi gani unaweza ukaongeza thamani ya bidhaa au huduma
kama ulivyoona kwa mfano wa biashara ya samaki hapo juu.
2. Kuwa na mtazamo hasi juu ya watu
wanaokuzunguka kibiashara.
Biashara
nyingi huwa hazikuwi au hufa kabisa hii ni kutokana na kuwa na mtazamo hasi juu
ya mambo ambayo tunayafanya katika kibiashara. Watu wengi hususani watu ambao wanafanya
biashara huwa ni ubinafsi sana.
Ubinafsi
huu ndio ambao unazidi kujenga uhasama kwa asilimia kubwa hasa kwa
wafanyabiashara wengine ambao wanakuzunguka. Ubinafsi huo ni kama ufutao.
Kwa
mfano unaweza ukaenda sehemu fulani kununua bidhaa za jumla ila ghafla unakuta
mtu huyo hana bidhaa fulani ila anajua kwamba jirani yake bidhaa hiyo anayo kutokana
na ubinafsi wa kibiashara mfanyabiashira huyo hawezi kumuelekekeza mteja bidhaa
hiyo atapata wapi? Zaidi ya kumwambia kaishiwa.
Au mfanyabiashara huyo hawezi kwenda kumfuatia
mteja bidhaa au huduma kwa jirani yake. Sasa kwa staili kama hiyo tutafanikiwa
kweli? Hivyo wito wangu kwako ni kwamba ni lazima uwe na ushirikiano wa kutosha
baina yako na wafanyabishara wengine ambao wanaokuzunguka.
Kufanya
hivyo kutafanya kukuza biashara yako hasa katika ongezeko kubwa la wateja. Watu
wengi hufanya hivi huku wakiamini ya kwamba kufanya hivi ni kuibiwa wateja wako
ila ukweli ni kwamba kufanya hivyo ni
kuongeza makuzi ya kibiashara na kuongeza wateja kwa ujumla.
“Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra
sahihi” kwa kuendelea kujifunza kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ndimi;
benson chonya
Email; bensonchonya23@gamail.com
0757909924
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)