Oct 31, 2016
Acha Kukata Tamaa, Mafanikio Yote Yanaanza Hivi…
Kama upo kwenye
safari ya mafanikio jifunze sana kutokuwa na dharau na kile kidogo ulichonacho.
Kama una kitu ambacho ni kidogo iwe pesa au uwezo fulani au kitu chochote
ambacho unaona ni kidogo kithamini sana kitu hicho.
Kitu nilichojifunza
katika safari ya kutafuta mafanikio ni kwamba, mafanikio mara nyingi huweza kuanza
kidogo kidogo sana mithili ya mbegu ya haladari. Kazi ya kukuza au kupapalia
kile kidogo ulichopewa ili kiwe kikubwa sasa hapo ndiyo inakuwa kazi yako.
Kwa mfano, kama ni
pesa huwezi kuanza na kuwa na pesa nyingi mara moja, katika maisha yako unaweza
ukaanza na pesa kidogo tu, lakini hizo pesa kidogo ukazifanya kama mbegu na
kuwekeza huku na huko na baadae kuwa pesa nyingi.
Kama ni gari,
nyumba, mtaji au maarifa fulani vyote hivyo huwa vinaanza kidogo kidogo na baadae
kuwa vitu vikubwa vya kushangaza. Chochote ambacho unacho hata kama ni kidogo
acha kukidharau hata kidogo zaidi kiheshimu.
Mafanikio yote makubwa, yanaanza kama mbegu. |
Tambua Hakuna
mafanikio ambayo yanaanza juu kabisa. Asili ya mafanikio yote makubwa yanaanza
kwa kuanzia chini. Hizo ndizo hatua za mafanikio. Wakati wote mafanikio yapo
kama hatua za mtoto mdogo ni lazima atambae kwanza kabla ya kutembea, na
mafanikio yapo vivyo hivyo.
Kwa hiyo kwa
kulijua hilo chochote ulichonacho hata kama ni kidogo vipi, mshukuru MUNGU
kwa hicho na kisha kifanye kiwe mbegu kwako ya kukusaidia kufanikiwa. Acha kuwa
na dharau na kidogo ulichonacho na kama ukiwa na dharau hutafika popote.
Kama una pesa
kidogo zitunze. Kama unafanya kazi unayolipwa mshara mdogo iheshimu kwanza kazi
hiyo, na halafu ile pesa kidogo unayoipata ifanye kuwa kama mbegu ya kukusaidia
kufanikiwa katika maisha yako kwa kuiwekeza.
Hapo ulipo hata
kidogo acha kuogopa kwa jinsi unavyoteseka na kusota kwa sababu ya kukosa pesa
au maisha magumu, ninachotaka kukwambia huo ni mwazo tu wa mafanikio yako.
Usikate tamaa endelea kupambana, Mungu yupo pamoja nawe.
Hakuna kitu ambacho
hakibadiliki hata maisha yako yanakwenda kubadilika ikiwa hutakubali kushindwa
na ukawa mtu wa kuchukua hatua. Siku zote kumbuka kuthamini kile kidogo
ulichonacho.
Kama unakumbuka katika
maandiko matakatifu wakati wana wa Israel wakiwa wamekosa tumaini na kuamini ni
lazima wafie katika bahari ya shamu, lakini Mungu aliwaokoa kupitia fimbo
aliyokuwa nayo mtumishi wake Mussa.
Hata wewe hapo
ulipo kipo kitu ambacho unacho hutakiwi
kukidharau. Kama Mussa angeizarau fimbo yake na kusema kwamba isingeweza kufanya
kitu basi wana wa Israel wangefia wote katika bahari ya shamu.
Kwa chochote
ulichonacho, chukua hatua. Kiheshimu hicho ulichonacho na kifanyie kazi. Kama unaona
unapata pesa kidogo sana, ziweke pesa hizo, acha kuzitumia hovyo na kusema haziwezi
kunisaidia kitu.
Hivyo, ili kufanikiwa ni
lazima utambue mafanikio yako huwa yanaanza kwa kidogo sana. Jukumu la kuyakuza
na kuyafanya yawe makubwa lipo mikononi mwako. Kama ni mbegu ya mafanikio tayari
unayo, acha kulaumu chochote zaidi, heshimu kidogo ulichonacho na utafanikiwa.
Endelea kujifunza
kupitia dirayamafikio.blogspot.com
Napenda pia
kukaribisha wewe rafiki yangu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifutia na jina
lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
Hakuna gharama na karibu sana.
Tunakutakia kila la
kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
Ni wako rafiki
katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
Oct 28, 2016
Jinsi Ya Kudumisha Afya Njema Na Kuishi Maisha Marefu.
Katika
hali ya kawaida, hakuna mtu ambaye ana uhakika mkubwa wa maisha yake kwamba ni
lazima afike kesho. Muda na dakika yoyote ile unaweza kuachana na mwili wako na ukafa. Swala
la kufika kesho au kutofika huwa mara nyingi linabaki mikononi mwa Mungu
mwenyewe.
Pamoja
na kwamba binadamu huyo hana uwezo wa kujua kesho yupo au hayupo, lakini upo
uwezo wa kutambua kama binadamu huyo ataishi maisha marefu au mafupi.
Inawezekana unaanza kujiuliza maswali hilo linawezekana vipi? Tulia usiwe na wasiwasi nitakwambia.
Kwa
mujibu wa wataalamu wa afya wanadai kwamba, ikiwa binadamu ataishi maisha yake
ya kawaida bila kupata changamoto
nyingine za nje yake kama kugongwa na gari au
namna yoyote ile ya kukatisha uhai wake upo uwezo wa kujua maisha yake
yataishia wapi.
Vyakula vyenye mafuta sana ni hatari kwa afya yako. |
Wataalamu
hao wanatuonyesha viashiria ambavyo vinaonyesha kama ukiishi hivyo ni lazima
uishi maisha marefu. Mambo hayo au viashiria hivyo walivyotoa, ni matokeo ya
utafiti yaliyofanywa hasa kwa watu walioishi miaka 100 na kuendelea.
Kwa
mfano utafiti huo ulionyesha, watu wanaokula vyakula vyenye mafuta kidogo, watu
hawa wao waliishi maisha ya muda mrefu. Mara nyingi ni kweli unapokula vyakula
vya mafuta kidogo hiyo inakusaidia sana katika swala zima la mwili wako
kutopata magonjwa hovyo.
Pia
utafiti huo uliendelea na kuonyesha kwamba, watu wanaokula vyakula vyenye wingi
wa protini pia afya zao ziliimarika zaidi na kupelekea kuwa na maisha marefu. Vyakula
hivyo ni kama samaki, dagaa, maharage,
nyama ana vinginevyo.
Hata
hivyo pia watu wanaofanya mazoezi kila siku nao pia walionyeshwa kwamba
wanauwezo wa kuishi maisha ya muda mrefu kutokana na mazoezi huweza kuimarisha
afya na kupunguza baadhi ya magonjwa na hali za kunenepeana hovyo.
Hivyo
utaona, vyakula visivyo na mafuta sana, vyakula vyenye protini na kufanya
mazoezi ni mambo ambayo yametajwa na wataalamu yanaweza kuboresha afya yako na
kupelekea kuwa na uwezekano mkubwa sana wa kuishi maisha marefu.
Kumbuka
siku zote, afya ni kitu cha muhimu sana katika maisha yako na safari yako ya
mafanikio kwa ujumla. Kama ukiwa huna afya njema hakuna utakachokifanikisha
kwenye hii dunia. Ni muhimu sana kutunza afya yako kwa ajili ya mafanikio yako.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Pia
napenda kukukaribisha rafiki kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza
pamoja. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO
YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com
Oct 27, 2016
Namna Ya Kutambua Shughuli Iliyokuleta Duniani.
Watu wengi huwa ni watu wa kujiuliza na kutaka kujua hasa ni
shughuli ipi iliyowaleta duniani. Mara nyingi wengi huwaza ‘ Sasa
nitajuaje kwamba, kazi hii ndiyo ambayo imenileta au nimekuja kuifanya hapa
duniani’? Ni kweli kila mtu duniani ameletwa au amekuja kwa ajili ya shughuli
ama kazi maalumu kwake ambayo ni lazima aitimize ili kuweza kufanikiwa kwa
viwango vya juu zaidi.
Tatizo kubwa linalooonekana kwa wengi wetu ni kutokujua hasa
shughuli iliyotuleta hapa duniani. Kwa kutokujua huko hupelekea wengi kuvamia
kazi ambazo sio zao na matokeo yake kushusha kiwango cha ufanisi. Kama unataka
kufikia kiwango kikubwa cha mafanikio ni muhimu kujua shughuli iliyokuleta
duniani. Swali la kujiuliza hapa utajuaje hasa shughuli iliyokuleta hapa
duniani?
1.Tambua ni kipi kimeikalia akili yako sana.
Hatua ya awali itakayokuwezesha kujua shughuli au kazi uifanyayo
ndiyo hasa unayotakiwa kuifanya, ambayo ndiyo itakayokupa ridhiko la moyo na
mafanikio, ni kuangalia kiwango chako cha kuipenda na kuridhika nayo. Lakini
pengine pia ni kupima au kujiuliza juu ya shughuli au kazi ambayo inaingia
akilini mwako mara kwa mara.
Siyo kuingia akilini kwa kufikiria kipato, hapana, bali kuingia
akilini ukitamani kuifanya. Wakati mwingine hata kuona kama vile wale
wanoifanya shughuli hiyo inayoitawala sana akili yako wamependelewa au kupata
bahati. Shughuli hii inayotawala akili yako kwa muda mrefu, mara nyingi huwa ndiyo shughuli iliyokuleta duniani.
Watu wanaofanya shughuli zilizowaleta duniani huwa wana mafanikio
mkubwa sana, hata kama shughuli hizo zinaonekana ni za watu duni, wasio na
kipato wala heshima katika jamii, lakini huweza kustawi kimapato na kuweza
kuishi kwa utulivu wa nafsi. Mtu anapofanya kile ambacho ndicho kilichomleta
duniani, kufanikiwa kwake ni lazima.
2. Tambua ‘hobi’ yako ni ipi.
Kuna wakati shughuli zilizotuleta hapa duniani ni yale mambo
ambayo sisi huwa tuyachukulia kirahisi na kuyafanya kwa urahisi kwa sababu ya
kujifurahisha. Utafiti mwingi kuhusiana na malengo yetu maishani, unaonyesha
kuwa, yale mambo tunayoyaita ‘hobi’ zinaweza zisiwe ‘hobi’ bali ndiyo shughuli
zetu za kutupa mafanikio ya kweli maishani.
Kwa mfano unaweza ukaona mtu ana kipaji kikubwa sana cha kuchora
na akawa anakitumia katika kujifurahisha tu, mwenyewe anaita ‘hobi’ wakati
ukweli ni kwamba, angeamua kuingia kwenye uchoraji kama shughuli kamili,
angefanikiwa sana. Wakati mwingine hata zile tunazoziona kama ‘hobi’ zisizo na
maana sana, wengine ni shughuli maalumu kwao na kubwa.
Kama unayo shughuli au jambo ambalo unalipenda sana na unalifanya
kama ‘hobi’, jaribu kulikagua. Inawezekana kabisa isiwe ‘hobi’ kama
unavyofikiri bali ndilo limefanya ukaletwa hapa duniani. Kumbuka hakuna
shughuli ndogo, ya kijinga au haina faida, bali inategemea wewe unayeifanya
unaifanya kwa sababu gani?
3. Kama haina umuhimu wa nje.
Kama mtu anaipenda shughuli ambayo ni wazi haijulikani wala
kufahamika kwa nje nap engine hata iikfahamika ni kwa kudharauliwa sana nab ado
mtu huyo akajivunia kuifanya shughuli hiyo, hii ni dalili nzuri ya mtu kuwa
kwenye shughuli iliyomleta hapa duniani.
Kuna watu ambao huficha shughuli zao, hawataki wengine wakajua
wanafanya shughuli gani. Huficha kwa sababu wanahisi aibu kwa kuamini kwamba
hizo shughuli zao ni zenye pengine kudhalilisha. Hawaoni kama wanastahili
kuzifanya, kwani kwao hizo ni shughuli za watu wa aina Fulani wa kiwango cha
chini.
Mtu anapogundua kuwa, anahisi aibu kutaja shughuli yake kwa sababu
anadhani ni shughuli duni, ni vizuri akaacha kufanya shughuli hiyo, kwani
anapoteza muda wake wa bure. Kudhani shughuli mtu aifanyayo ni dhalilisho, ni
dalili kubwa ya kwamba mtu huyoanafanya shughuli ambayo hakutakiwa kuigusa
maishani mwake.
4. Kutambua matatizo siyo hoja.
Kama kweli shughuli ambayo unaifanya ndiyo imekuleta hapa
duniani,ndiyo shughuli ambayo unatakiwa kuifanya, haeiwezi kuwa na matatizo.
Siyo kwamba ukifanya shughuli hiyo, huwezi au shughuli yenyewe haiwezi kukumbwa
na vikwazo, hapana. Bali yanapotokea matatizo hutakata tamaa na kusema ‘basi’.
Badala yake matatizo hayo yatakusukuma kusonga mbele na kukusaidia kujikita
zaidi kwenye shughuli hiyo.
Bila shaka umeshawahi kuona au kusikia juu ya watu ambao shughuli
fulani wazifanyazo zinakumbwa na matatizo, wengine wote wakajitoa, lakini wao
wakabaki peke yao na kuendelea nazo, kama kwamba hayo matatizo ndiyo waliokuwa
wanayasubiri. Biashara inakumbwa na matatizo ya aina fulani ambapo kuendelea
kwake ni kwa kubahatisha sana na wengi wazifunga biashara zao, lakini mwingine
anaendelea kama vile hakijatokea kitu. Kazini na mahali pengine hali kama hiyo
huweza kujitokeza pia.
Kama kweli shughuli unayoifanya ni yako kabisa haiwezi kutokea
hata mara moja ukaiacha kwa sababu ya matatizo. Hata kama utaiacha ni kwa muda
tu, kwani utajikuta unatafuta njia au mbinu ya kupata ufumbuzi wa matatizo
hayo. Matatizo hayawezi kukukatisha tamaa kama ambavyo yanaweza kumkatisha
tamaa mtu ambaye anaifanya shughuli hiyo kwa sababu za nje, ikiwemo kipato.
Huyu anayeifanya kwa sababu ya kipato, umaarufu au madaraka na sababu nyingine,
ndiye ambaye tatizo likitokea ni mwepesi kughairi na kubadili shughuli.
5. Kuwa na ridhiko la ubunifu au ugunduzi.
Kama kweli shughuli unayoifanya ndiyo ambayo ‘umeandikiwa’
kuifanya, utajikuta mara nyingi unakuwa mtundu nayo na kuvumbua au kugundua
mambo mapya. Hata kama mambo hayo mapya hayakupi faida inayogusika au ya moja
kwa moja kama ya kipato, bado uvumbuzi au ugunduzi huo utakufanya kuridhika zaidi
kuliko yule ambaye angepata pesa na kufurahia kuridhika tu kwa sababu ya pesa.
Wengi wanapobuni au kuvumbua vitu kwenye shughuli zao hukata
tamaa, kuvunjwa moyo, kuvunjwa nguvu na pengine kubadilisha shughuli zao hasa
wanapoona kwamba hakuna mtu aliyeonyesha kutambua ugunduzi wao na pengine
kuwapa zawadi au fedha. Ukiwa hivyo jua kabisa unafanya shughuli ambayo siyo
yako na ambayo haijakuleta duniani.
Kugundua na kuvumbua kinachozungumzwa hapa kunaweza kuonekana
kuwahusu watu wachache, wasomi au wenye taaluma maalumu, hapana. Mtu yoyote,
katika shughuli yoyote anaweza kugundua au kuvumbua jambo jipya na la manufaa
kwa shughuli yake, kwake mwenyewe na kwa wengine pia.
6. Nguvu ya wito.
Kuna wakati huwa tunajiuliza ni kwa nini baadhi ya watu ambao
wanauwezo mkubwa wa kubadili shughuli, bado wanang’ang’ania
shughuli ambazo zinaonekana kuwa hazina hata matumaini kidogo ya baadaye? Kwa
hapa ilifika mahali Fulani ambapo ualimu ulionekana kama vile kuufanya ni
kujitafutia umaskini na balaa kubwa kimaisha.
Lakini ni jambo linaloweza kuonekana kama la kushangaa kugundua
kuwa, kuna baadhi ya watu ambao wangeweza kufanya shughuli nyingine na
kufanikiwa sana kimapato, lakini wameamua kuwa walimu kwa furaha kubwa, wewe
mwenyewe ni shahidi umeshawahi kukutana na watu wa namna hiyo.
Hapa ndipo ambapo tunasema, mtu anafanya shughuli fulani kwa
sababu ya wito, siyo kwa sababu ya kitu kingine. Mtu anajua wazi kwamba,
shughuli aifanyayo inadharauliwa nap engine haina maslahi ya fedha, lakini yeye
anajisikia vizuri, anaona fahari na anafurahia kuifanya. Wito maana yake ni mtu
kufanya kile ambacho ndicho alichotakiwa kuja kukifanya hapa duniani, ambacho
kwa hali hiyo kimemkaa moyoni na akilini.
Kumbuka, hakuna aliyekuja hapa duniani kufanya tu shughuli ambayo
haimhusu, kila mtu ameletwa na shughuli yake. Kaa chini tafakari na utafute
shughuli iliyokuleta hapa duniani itakupa mafanikio makubwa sana.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,
Oct 26, 2016
Kipindi Muhimu Sana Cha Mafanikio Yako.
Njia
mojawapo kubwa ya uhakika ambayo ukiitumia ni lazima itakupa mafanikio ni
kusubiri. Hakuna kitu au mafanikio ambayo utashindwa kuyapata katika maisha
yako ,ikiwa utakuwa ni mtu wa kufanya kazi na kusubiri.
Wataalamu
mbalimbali wa mafanikio, akiwemo mwandishi wa vitabu wa kimarekani ndugu J.G
Holland amewahi kuthibitisha hili pia kwa kusema“Hakuna mafanikio makubwa duniani ambayo utayapata bila kufanya kazi kwa
bidii na kusubiri”.
Hiyo
ikiwa inaonyesha kuwa upo uhusiano mkubwa sana kati ya kile unachokitaka na
swala zima la uvumilivu wakati unasubiri kufanikisha jambo lako. Ni lazima
ufanye kazi na usubiri mchakato wa kufanikisha jambo lako hilo.
Hakuna
mafanikio ambayo unaweza kuyapata ‘chapuchapu’ na kuamua kukwepa njia hii.
Mchakato wa kusubiri na kuwa mvumulivu kwa kile unachokitaka, upo palepale. Watu
wote wenye mafanikio wanapitia njia hii kufanikiwa na sio kinyume cha hapo.
Vumilia mpaka utimize ndoto zako. |
Kwa
kawaida ile tu kujua kusubiri kitu ambacho una mhemko nacho au mchecheto mkubwa
kukipata ni siri au hatua kubwa sana ya kuweza kukusaidia kufanikiwa. Utulivu utakao
utengeneza wakati unasubiri, ndio utakusaidia ukae sana na kitu hicho tofauti
na ungekipata kwa upesi.
Elewa zipo namna nyingi za kusubiri kile unachokitaka kwenye maisha yako ili ukipate. Kwa mfano, kipo kipindi cha kusubiri wateja kuongezeka pale unapoanza biashara yako. Kipo
kipindi cha kusubiri miezi tisa mtoto, pale mama anapopata ujauzito. Kipo kipindi cha kusubiri kujibiwa majibu yako
pale unapoomba kazi.
Kuwa
na subira, ni kipindi muhimu sana cha mafanikio yako na pia ni kanuni ya asili. Kanuni hii inaweza
ikajitokeza katika yai. Kwa kawaida yai haliwezi kutoa kifaranga mpaka zifike
siku 21.
Si
hivyo pia tunaona kanuni hii inajitokeza pale unapoumia na kupata kidonda. Kwa mfano
tunaona, ukipata kidonda huwa hakiponi mara moja, upo muda wa kusubiri hadi
kidonda chako kipone. Na ndivyo kanuni hii inafanya kazi kwa misingi kama hiyo
kwa mambo mbalimbali.
Kwa
hiyo inapotokea umejiwekea malengo yako na kuanza kuyafanyia kazi, jifunze kuwa
na subira. Acha kuwa na haraka zisizo na msingi kuharakisha matokeo. Kama kila
wakati wewe ni mtu wa haraka haraka hutafika popote. Maisha yanakutaka sana uwe
mvumilivu na mtulivu ili kufanikisha makubwa.
Kipo
kipindi ambacho kinakulazimisha uwe na subira ili mambo yako yatimie. Hiki ni
kipindi au muda ambao unakujenga na kukufanya uweze kufanikiwa. Hichi ndicho
kipindi au wakati muhimu sana wa mafanikio yako. Ukishindwa kuvumilia hapa basi
utaharibu kila kitu.
Hebu
jaribu kufikiria ni wangapi ambao huwa hawana uvumilivu wa kusubiri mafanikio
yao, bila shaka ni wengi tu. Huwa kuna ugumu kwa watu wengi kuvumila kile wanachokitaka,
zaidi ya wengi hutafuta njia za mkato sana ambazo pia huwaangusha.
Kutokana
na kukosa subira, wengi hutaka mipango yao iende upesi sana. kwa mfano, vijana
wa miaka 22 wao hutamani kwa umri huo wawe wana gari, nyumba nzuri, mke mzuri,
miradi ya kutosha na watoto. Haa! Haa! Haa! kama hizo ni ndoto zako umepotea.
Huwezi
kufanikisha maisha yako kwa kwenda kinyume na kanuni za asili au kanuni za
mafanikio. Maisha yanakutaka ufuate kanuni ndogo ndogo ambazo zitakusaida
kupiga hatua kila siku. Mojawapo ya kanuni hizo ni kuwa na subira.
Kama
huna subira ya kutosha unataka mambo kwa upesi sana huwezi kufanikiwa. Anza leo
kwa kujenga msingi wa maisha yako kidogo kidogo. Anza leo kwa kuchapa kazi huku
ukiwa na subira na ndoto zako. Kumbuka ile kusubiria ndoto yako itimie, ni
kipindi muhimu sana cha mafanikio yako.
Endelea
kuwashirikisha wengine waweze kujifunza kupitia mtandao wako wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Pia
napenda kuchukua fursa hii kukaribisha wewe rafiki yangu, kwenye kundi la Whats App ili
uweze kujifunza pamoja nami kwa ukaribu zaidi. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO
YANGU, kisha ikifuatia na namba yako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
Oct 25, 2016
Sheria Ya Mafanikio; Nguvu Ya Umakini.
Katika mojawapo ya hatua za mwanadamu kujitambua,
kufahamu sheria hii ni mojawapo kati ya hatua za muhimu sana kwenye kufahamu
maajabu ya ulimwengu. Uelewa wa sheria hii ni faida kubwa sana hasa kwa
wanadamu wanaopenda kujifunza mengi na kuboresha maisha yao katika njia sahihi.
UMAKINI: Ni nguvu kani. Ni kama vile energy. Umakini unapelekea kukusanya ufahamu wako katika
sehemu moja na kupelekea nguvu zako kukusanyika na kuweka nguvu kubwa kwa
pamoja.
Mwalimu
mmoja wa ki-Asia aliwahi kusema kuwa “Umakini ni kama mwanga wa jua, unauona ni wa kawaida lakini
ukiweka lensi mbinuko unaukusanya mwanga ule na kuwasha moto.”
Ni sawa na umakini. Unaweza ukawa umeshawahi kuona
tamaduni za Ki-Asia mtu akiwa anajifunza wanasisitiza mtu kujifunza kwanza
kuuongoza umakini. Mfano Kung-Fu mtu ili aweze kutumia nguvu ya Chi anatakiwa
aweke umakini wake katika nguvu hiyo na attention yake yote iwe hapo ndipo
nguvu hiyo huamka.
Kile unachokizingatia sana, ndicho Unachokipata. |
Umakini una nguvu kubwa sana katika ulimwengu, ukijifunza
chochote kwa umakini unaweza kuwa na uwezo mkubwa sana. Mfano mzuri ni pale
unapoamua kujifunza kitu kama Piano na Guitar, ukiweka akili yako hapo kwenye
Piano utajikuta unaweza kupiga mzunguko ambao hata hukutegemea kama ungeweza
kutengeneza.
Hapo bado hatujaingia katika sheria hii kwa undani. Hapo nilikuwa najaribu kukuelekeza umakini ulivyo.
Sheria hii kiini chake kipo hivi. POPOTE UNAPOELEKEZA UMAKINI WAKO AU FOCUS YAKO PANAKUA. Unapoelekeza
ufahamu wako katika hali fulani, mawazo fulani, ufahamu fulani, utaona ufahamu huo
unakua.
Buddha aliwahi kusema hivi,”Chochote unachokiwekea umakini ni lazima kikue”
Mfano ukiwa unanyanyua vyuma misuli itatumika sana,
halafu baada ya kutumika kunyanyua vyuma hukua na kujaa. Chochote unachokitumia
sana kinakua au kinaboreka ili ukitumia vizuri.
Hii sio sheria ya ufahamu tu bali hii ni sheria ya
ulimwengu, ni sheria ambayo Uasili au ‘Nature’
imekua ikitumia kufanya kazi yake. Mnyama akitumia kiungo fulani sana kiungo
kile kinakua na kuboreka kumsaidia akitumie vyema na kwa zaidi. Kisichowekewa
mtazamo au matumizi kunapotea. Hii nisheria ya asili, na hata akili ni asili hivyo
ipo mpaka kwenye fikra, mawazo au misimamo.
Mfano unaweza kukuta mtu anaamini kitu fulani, ameweka
ufahamu wake wote hapo na anaamini hivyo na huwezi kumbadili hivyo. Naye anaona
anachoamini ni uhalisia kabisa. Kumbe ‘reality’
yake imetokana na kujizoesha kuamini hivyo na kuelekeza ufahamu wake huko
mwishowe anajikuta anaamini hivyo na yeye mwenyewe hajui hilo kwani hafahamu
kuwa kuna sheria kama hii duniani.
Kufahamu ufahamu huu itakusaidia kuuliza unachokiamini.
Je ni kweli ‘reality’ yako imetokana
na umejizoesha kuamini hivyo au kufahamu hivyo na kupelekea wewe leo hii kuona
hivyo au ni reality?
Wewe ni ufahamu wako, wewe unajitambua kupitia ufahamu
wako, Hakuna kitu kingekwepo bila ufahamu. Ufahamu ni kinachouona ulimwengu.
Kwa sasa ufahamu wako unategemea milango yako ya ufahamu (macho, pua, ulimi,
ngozi, masikio) kuutazama ulimwengu.
Ulimwengu huu ni ulimwengu wa milango ya ufahamu. Shida
unazoziona, raha unazoziona zote unazihukumu kwa kusema hiki ni shida na hiki
ni raha kwa kutumia milango yako ya ufahamu na sio ufahamu wenyewe.
Ungezaliwa katika ulimwengu unaoamini maumivu ni raha
ungeona ni raha kwani ufahamu wako hauna uhusiano na kitu au hali yenyewe.
Ufahamu unaweza kubadilika na kupelekea hali kuonekana tofauti kwani ni ufahamu
unaohukumu hali na sio hali yenyewe.
Kuelewa sheria hii utajifunza kuwa kuna umuhimu wa kuwa
makini na unachokiamini, kuwa makini na kinachoendelea katika akili yako, kuwa
makini na matumizi ya hisia zako, kuwa makini na kutazama mawazo yako, kuwa
makini kwa kutazama imani na maamuzi yako halafu linganisha na maisha yako ya
nje. Kuelewa sheria hii ni kuelewa kuwa ulimwengu wa ndani yetu unaumba
ulimwengu wa nje.
Watu walioweza kujitambua na kufahamu sheria hii waliweza
kujitahidi kuongoza fikra zao kwa kuumba uhalisia wao. Mtu makini ni mwenye
ufahamu kuwa yeye na mchango mkubwa katika kubadili maisha yake na sio kingine.
Haijalishi unaishi katika hali gani, ni kubadili mtazamo wako na KUUTAZAMA MTAZAMO WAKO.
Una maumivu kwenye bega. Unaweza ukaamua kuweka fikra
yako katika kuwaza jinsi ulivyo na maumivu katika bega na kukosa raha au
unaweza kuweka umakini wako kwa sehemu nyingine za mwili ambazo ni nzima na
kushukuru kwa kila jambo. Lakini kuna ambao wataelekeza akili yao kwenye
maumivu na wengine wanakata taamaa kabisa na kuona hatapona.
Unaweza ukahisi unaumwa ugonjwa fulani na kuona unaanza
kuumwa ugonjwa huo. Upo ushahidi wa kisayansi kuwa kuna magonjwa yanachangiwa
na akili. Kuna dalili nyingine zimetokana na mtu kuwaza ugonjwa sana na anaanza
kuona dalili.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA APOLINARY
MACHA WA JITAMBUE SASA.
Oct 24, 2016
Unachotakiwa Kufanya Pale Unapoiona Fursa.
Siku kadhaa zilizopita nieleza namna ambavyo utaweza kuzitambua
fursa mahali ambapo unapoishi, na siku ya leo nitaeleza kitu cha kuzingatia
pale uonapo fursa.
Jifunze kupitia hadithi hii;
Ilikuwa ni majira ya asubuhi, ambapo hali ya hewa haikuwa
shwari, mawingu mazito yaliyoambatana na radi pamoja na ngurumo ndizo ambazo
zilikuwa zimetawala siku hiyo.
Wanyama wengi walishukuru sana kwani walidhani mvua kubwa
ingenyesha siku hiyo kwani ni siku nyingi zilipita bila mvua kunyesha na
kupelekea baadhi ya mazao yaliyokuwako shambani kuendelea kunyauka.
Hata hivyo cha ajabu pamoja na kuwako kwa hali hiyo yenye ishara
ya kunyesha mvua kubwa itanyesha, lakini mvua haikuweza kunyesha. Kila Mnyama
alisikitika sana kutokea kwa hali hiyo. Kadri siku zinavyozidi kwenda njaa kali
ilitawala mahala pale hata kupelekea kwa idadi kubwa ya wanyama wengi kufa.
Chunguza kwa makini fursa mpya. |
Kati ya wanyama walioathiriwa na hali hiyo ni fisi, kwani ndiye alikuwa mnyama mwenye watoto ambao walikuwa
ni bado wadogo hivyo hawakuwa na uwezo wa kujitafutia chakula hivyo ilimpasa
fisi huyo kila wakati kwenda kutafuta chakula kwa ajili ya wanae.
Fisi huyo pamoja na kuwako kwa hali ngumu ambayo iliwatala
mahali pale, kila alipojaribu kuwinda alikuwa anapata kitoweo kidogo sana
ambacho kutokana na idadi kubwa ya watoto ambao alikuwa akiwamiliki kitoweo
hicho kilikuwa hakiwatoshi watoto wake.
Kuna wakati zilipita siku tatu mvululizo bila ya kupata kitu
chochote, hata kupelekea watoto wake kudhoofu sana. Kutokea kwa hali ile
kulimchanganya sana mama fisi.
Siku moja mnamo usiku wa maneno watoto wa fisi kutokana na njaa
ambayo walikuwa nayo waliweza kulalamika kwa mama yao ya kwamba njaa kali
inawasumbua sana hivyo ingefaa kwa mama yao aende mawindoni angepata chochote
ambacho kiwafaa kwa siku ile.
Pasipo kupoteza muda mama fisi alifanya kama ambavyo wanawe
walimtaka afanye japo ilikuwa ni majira ya usiku. Mama fisi aliaamka na kuanza
harakati za kutafuta chakula usiku ule, japo usiku ule haukuwa na giza kubwa
kwa sababu kulikuwa na mbalamwezi ambayo ilimsaidia kumpa mwanga wakati wa
mawindo yake.
Mama fisi alizunguka sana usiku ule pasipo kupata chochote.
Lakini kadri alivyozidi kutembea kwa mbali aliona kama maji. Baada ya dakika
chache kufika mahali pale cha ajabu alikutana na kisima ambacho kilikuwa
kimejaa maji.
Mama fisi alimshukuru sana Mungu kwa kuyaona maji yale kwani
alikuwa amebanwa sana na kiu pamoja na njaa isiyoelezeka. Hata hivyo wakati
mama fisi akitaka kunywa maji yale aliona kitu ambacho kinaelea juu ya maji.
Mama fisi alijaribu kufanya uchunguzi juu ya kile kitu ambacho
kilikuwa kinaelea, kadri alivyozidi kufanya uchunguzi aligundua kwamba ulikuwa
ni mfupa. Mmmh si unajua tena fisi na mfupa.
Mama fisi pasipo kupoteza muda alijitupa ndani ya maji kwa ajili
ya kuuchukua mfupa ule. Lakini pamoja na kufanya uchunguzi wake wa kina ukweli
ni kwamba kilichokuwa kikielea juu ya maji haukuwa mfupa bali ilikuwa ni
mbalamwezi.
Baada ya kuingia kwenye kisima kile mama fisi alishangaa kuona
hakuna mfupa ambao aliuona wakati yupo nje ya maji. Na kwa kuwa kisima kilikuwa
ni kirefu sana mama fisi hakuweza kutoka hivyo alikufa ndani ya kisima kile.
Watoto wa mama fisi walisubiri kwa siku kadhaa bila mafanikio ya
mama yao kurudi, hivyo na wao waliliwa na wanyama wengine. Na historia ya mama
fisi pamoja na wanawe ikaishia pale.
Tafsiri ya hadithi hii ni nini?
Ukweli ni kwamba watu wengi hulalamika katika mambo ambayo huwa
wanayaanzisha, na mwishowe wanajikuta wanashindwa katika mambo hayo. Lakini
moja ya tatizo kubwa ambalo hufanya kutokea kwa hali hiyo ni;
Kutofanya uchunguzi wa fursa ambazo unazoziona, hili ndilo
tatizo kubwa sana ambalo huwakumba watu wengi sana.
Unakuta mtu anaiona fursa fulani na fursa hiyo ana uhakika kwa
kiwango kikubwa kuweza kibadili maisha yake kwa kiwango cha hali ya juu lakini
cha ajabu unakuta mtu anashindwa sana katika fursa hiyo kwa sababu hakufanya
uchunguzi wa kutosha juu ya fursa hiyo.
Huenda ukawa unataka kufanya jambo fulani la msingi sana katika
maisha yako, lakini nikwambie jambo moja ya kwamba usikurupuke bali tafakari
kwa kina kuhusu faida na changamoto ya jambo hilo.
Hivyo jambo la msingi ambalo ni vyema kulizingatia ili uweze
kufanikiwa unahitaji kufanya uchunguzi wa kutosha kwa kila fursa ambayo
unaiona. Kwani endapo hautafanya hivyo ipo siku utalalamika tu , pia utayaathiri
maisha yako na watu wengine kama tulivyoona kwa fisi.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada, tukutane siku nyingine.
Pia napenda kukukaribisha
rafiki yangu kwenye kundi la Whats App
ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na
namba yako kwenda 0713 04 80 35 ili uanganishwe.
Ndimi;afisa mipango Benson Chonya.
Oct 21, 2016
Usiruhusu Makosa Haya Yawe Sehemu Ya Maisha Yako.
Yapo
makosa ambayo hutakiwi kuyaruhusu mara kwa mara kutokea katika maisha yako. Ni
muhimu kuzingatia hilo kwa sababu maisha tuliyonayo ni mafupi na kila hatua
inatakiwa tuifanye kwa uhakika ili tusipoteze muda sana.
Kumbuka hata
hivyo wengi wetu kuna wakati tunashindwa kufanikiwa sana kutokana na kuruhusu
makosa ya aina fulani yatokee sana katika maisha yetu. Makosa haya ndio yamekuwa
yakipelekea mipango mingine kuweza kukwama.
Je, ni
makosa gani ambayo hutakiwi kuyaruhusu katika maisha yako mara kwa mara ili
uweze kufanikiwa?
1.
Usiruhusu kutawaliwa na watu hasi.
Hata kidogo
usiruhusu kuweza kutawaliwa na watu hasi. Usiwape nafasi kubwa ya kuweza
kuwasikiliza. Ikiwa utafanya hivyo kuwaruhusu watu hasi, watakuharibia maisha
yako sana kwa kukupa ushauri wa kukatisha tamaa na mwisho utaona maisha
hayawezekani tena.
Acha kuruhusu woga utawale maisha yako. |
2.
Usiruhusu woga ukutawale.
Woga ni
sumu kubwa sana ya mafanikio yako. Acha kuruhusu woga ukatawale sana. Kwa wale
ambao huruhusu woga uwatawale kwa kiasi kikubwa hawafanikiwi. Hiyo hutokea hivyo
kwa sababu hata hushindwa kuchukua hatua za kujaribu kufanya jambo jipya kwa
sababu ya woga.
3. Usiruhusu
kuiga sana.
Inapotokea
ukawa unaiga sana kwa kawaida unaua ule ubunifu wako wa ndani. Hivyo kama
unaiga kitu uwe na mipaka, lakini lilokubwa kwako unatakiwa kuwa mbunifu sana
ili iweze kukusaidia kutengeneza mafanikio makubwa.
4.
Usiruhusu kufanya jambo usiloweza.
Kama kuna
kitu hukiwezi ni vyema usikifanye. Kukifanya kitu hicho huku ukiwa huwezi au
huna hakuna na matokeo chanya hiyo itakuharibia sana sifa na maisha yako. Kila
unapotaka kulifanya jambo fulani, hakikisha unalijua vizuri kwa undani ili
likupe mafanikio.
Hivyo ni
vyema ukatambua kwamba hayo ndiyo makosa ambayo hutakiwi kutokuyaruhusu sana yatokee ili uweze
kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kama itatokea unaruhusu makosa hayo sana
maishani mwako, basi utakuwa unajitengenezea mazingira ya kushindwa mwenyewe.
Nikutakie
siku njema na ansante sana kwa kutembelea
DIRA YA MAFANIKIO kwa ajili ya kujifunza. Kitu cha kufanya kwako, washirikishe
na wengine waweze kupata maarifa haya bora.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Oct 20, 2016
Mfumo Unaotengeneza Maisha Yako.
Upo
mfumo unaotengeneza maisha yako na kuyafanya yawe hivyo kama yalivyo. Hapo ulipo upo
hivyo kimaisha si kwa bahati mbaya, mkosi au laana kama ambavyo unajifikiria
kila wakati, bali upo hivyo ni kwa sababu ya mfumo.
Kwa
bahati mbaya au nzuri mfumo huu mara
nyingi unautengeneza wewe iwe kwa kujua au kutokujua. Habari njema kubwa kwako ni kwamba, kwa vyovyote vile iwavyo, mfumo huo unao uwezo wa kuutawala hata kama
umejitengenezea mfumo mbovu.
Mfumo
huu ambao ninauzungumzia hapa na ambao unatengeneza maisha yako upo kwenye
mawazo yako. Mawazo yako ni kila kitu ikiwa utajua namna ya kuyatawala na kuyatumia
vizuri ili yakupe mafanikio.
Tatizo
kubwa la sasa ni kwamba, ulimwengu umejazwa na watu wengi ambao hawajui jinsi
ya kutawala mawazo yao. Kwa sababu hiyo
hujikuta ni watu wa kuishi tu kwa kupoteza muda bila ya kuwa na mafanikio
makubwa.
Kila wakati fikiria kile unachokitaka kwenye maisha yako. |
Na
kitendo cha kutokutawala mawazo yao kinasababishwa na watu wengi kushindwa
kuelewa kile kinachoweza kutawala maisha yao. Nikiwa na maana ule mfumo ambao
unaweza ukatawala maisha ya mtu.
Mfumo
huu unaotengeneza maisha yako umefundishwa tokea miaka mingi sana na
umefundishwa pia karibu na dini zote. Kwa
mfano tukisoma bibilia mithali 23;07 inatuambia “maana aonavyo mtu nafsini mwake, ndivyo alivyo…”
Andiko
hilo linatuthibitishia na kutuonyesha kwamba mfumo unaoendesha maisha ya
binadamu upo kwanza kwenye mawazo yake. Kipi unachokifikiri? Kipi unachoendelea
kukiwaza kila wakati hicho ndicho kinaunda maisha yako.
Wanasaikolojia
pia wanatufundisha kwamba kila mtu ana kitu anachokiwaza au kile anachokiweka akilini
kwa muda mrefu. Kitu hicho ambacho
kinakuwa kipo akilini au picha ambazo unaziweka ndizo zinazo tengeneza maisha
yako.
Ukichunguza
utaelewa hicho kinachozungumzwa kipo na tunakiishi. Hiyo ikiwa na maana mfumo
unaoendesha maisha ya mwanadamu upo kwenye kile anachokifikira kia wakati.
Hakuna ubishi juu ya hili, ushahidi upo karibu kila kona.
Kwa
mfano tunaona, watu maskini wanaendelea kuwa maskini zaidi kwa sababu ya mawazo
au picha zile wanazoziweka kwenye akili zao. Kila wanachokiwaza au kikiona ni
umaskini na mwisho wa siku huushia kuupata huo umaskini.
Pia
watu matajiri wanaendelea kuwa matajii zaidi, lakini hiyo yote inatokana na
kile wanachokiwaza kwa muda mrefu. Watu hawa kila wakati huwaza mafanikio,
hivyo kwa sababu hiyo huvuta mafanikio na utajiri maishani mwao.
Kama
kila wakati unaona umaskini, ni wazi utakuwa maskini. Kama kila wakati unawaza
utajiri na kuweka picha za utajirii nalo hilo utalifanikisha bila shida yoyote.
Mfumo unaotengeneza maisha yako yawe ya kushindwa au mafanikio haudanganyi,
unakupa kile unachokizingatia akilini mwako.
Kwa
kuwa mfumo huu upo, kila mmoja wetu anatakiwa kujua namna ya kujifunza kutumia
na katawala mawazo yake kwa ufasaha ili yaweze kumpa mafanikio makubwa.
Lakini
ikiwa endapo utaacha mawazo yako yakutawale, hutaweza kufanikiwa zaidi utabaki na
utaendelea kuishi maisha ya kuwasindikiza wengine kwenye maisha na utashangaa huoni
mafanikio yoyote yale.
Ili
sasa uanze kuufaidi mfumo unaoutengeneza maisha yako na ukafikia mafanikio
makubwa kama wengine, kila wakati unatakiwa kuwaza kile unachokitaka. Acha
kuwaza na kinyume unachokitaka.
Jaza
picha za kule unakokwenda. Jaza picha za kile unachotaka kukifanikisha. Jaza picha
za kiwango cha pesa unachokitaka mwaka huu. Ukifanya hivyo kila wakati huku
ukichukua hatua za utendaji UTAFANIKIWA.
Kwa
kifupi hivyo, ndivyo ambavyo mfumo unaotengeneza maisha yako jinsi unavyofanya
kazi. Kumbuka kila wakati hakuna bahati, muujiza wala mkosi katika maisha bali
upo mfumo unaotengeneza maisha yako.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Napenda
pia kuchukua fursa hii kukukaribisha wewe rafiki yangu kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi. Kujiunga
tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha
ikifuatia na jina lako kwenda 0713 04 80 35
ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)