Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, May 4, 2016

Namna Ya Kupata Wazo Bora Lenye Kukuletea Mafanikio.

No comments :
Mara kadhaa watu wengi wamekuwa wakiniuliza wafanye nini ili waweze kufanikiwa zaidi. Nimekuwa nikiwaambia kuwa wazo bora ndio siri ya kufanikiwa. Wazo ni bora ndilo linalomfanya mtu aweze kufanikiwa. Watu wengi wana maisha yaleyale, hii ni kutokana na kutokuwa na mawazo bora ya nini wafanye ili kiwaletee faida. Tumekuwa tunatamani kuwa maisha mazuri na yenye mafanikio makubwa kwa muda mfupi huku tukisahau ya kuwa siku zote safari ya tamu huanza na chachu. Inawezekana hujanielewa hakuna mafanikio makubwa bila kuanza na mambo madogo. Usidharau hicho unachokifanya inawezakana ndilo wazo bora la kuweza kufanikiwa kwako zaidi.

Kuna wakati tunafanya vitu kawaida sana kwa maneno mengine wanasema bora iende. Kuna mwandishi mmoja amawahi kusema ili uweze kufanikiwa ni lazima uheshimu kile unachokifanya. Jaribu kuelewa ya kwamba Mafanikio yeyote hubebwa na wazo bora baada ya hapo ndio uanza kufikiri mbinu za kupata mtaji kwa ajili ya utekelezaji huo. Usifikirie na kuona eti kisa mtu fulani amefeli katika jambo lake na wewe utafeli la hasha ila amini ya kwamba unaweza kufanikiwa ndani ya dakika chache endapo utaishi namawazo bora katika utendaji.

Zifutazo ndizo mbinu za kupata mawazo bora.


1. Andika kila wazo bora la kimafanikio.

Kwa siku binadamu huwaza zaidi ya mawazo sitini hiyo ni kutokana na tafiti zilizowahi kufanywa miaka ya nyuma. Lakini kutokana na tafiti hizo kuna mawazo mabaya na mazuri. Na ukichunguza mawazo mabaya ndiyo ambayo hufanyiwa kazi kuliko mawazo mazuri. Usishangae huo ndio ukweli. Tupo baadhi yetu tumekuwa hatupo katika kuamini mawazo yetu kama yatakwenda kuleta mapinduzi katika dunia.

Waza wazo bora la kukufanikisha.

Tupo baadhi yetu tupo na tunafurahia mawazo ya watu wengine katika kufanya mambo yetu. Kwa mfano aliyegundua mtandao wa whats app yeye alikuwa anatuwaza sisi na leo tunafurahia wazo lake la kutukutanisha pamoja na kuifanya dunia kuwa kijiji. Swali dogo la kujiuliza ni lini wazo lako watu wengine watakwenda kunufaika nalo kama wewe unavyofurahia mawazo ya watu wengine? Ukweli ni kwamba hata wewe unaweza kufanya hivyo endapo utakwenda kulitekeleza wazo lako. Tuna mawazo mazuri ila hutuamini kama tunaweza kuyatekeleza. Jambo la msingi ni kwamba kila mawazo mazuri yakija upande wako yaandike na uyaweke sehemu inayoonekana ili kila wakati unakuwa unayaoona hiyo itakupa hamasa na kuona na kuanza kuwaza ni jinsi gani utaanza kuyatekeleza.

2. Tafuta sehemu iliyotulia na anza kuwaza mawazo mazuri.

Kumbuka ya kwamba ni lazima ujue ya kwamba mafanikio yanatokana kwa kufikiri mawazo mazuri. Hivyo jambo la msingi ni kutafuta sehemu nzuri kwa ajili ya kuwaza mambo yako. Wanasema sehemu nzuri ya kuwaza mawazo mazuri ni  pale akili yako inapokuwa imetulia kabisa. Inaweza ikawa nyakati za asubuhi au wakati mwingine ulio bora kwako kama usiku wa manane. Jambo la kuzingatia ni kwamba kila wazo bora linalokujia liandike ili uweze kulitekeleza. Pia Mafanikio unayoyahitaji yanatokana na wewe kuendelea kujifunza kwa kuendelea kusoma.

Mwandishi: Benson chonya
Simu: 0757-909942
E-mail: 
bensonchonya23@gmail.com

No comments :

Post a Comment