Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Monday, October 10, 2016

Mambo Ya Kufanya Kila Siku Ili Kujenga Mafanikio Makubwa.

No comments :
Siri ya kubwa ya kufikia mafanikio makubwa, siku zote haipo kwenye kipaji, bahati au matumizi makubwa sana ya akili kama wengi wanavyofikiri, bali siri hiyo ipo kwenye namna unavyoitumia siku yako tokea kunapambazuka mpaka jua linazama.
Watu wengi linapokuja suala la mafanikio huwa wanafikiri mambo mengi sana, lakini kitu wanacho sahau ambacho na pia kinapoteza mafanikio yao ni matumizi ya siku yao moja tu. Watu wenye mafanikio, wanajua hili na ndio maana siku zao huzitumia kwa ufasaha sana.
Kimsingi, ili uweze kufanikiwa yapo mambo mengi ambayo unatakiwa kuyafanya  kila siku ili yaweze kukusogeza kwenye ndoto zako. Ikiwa hutafanya mambo hayo, basi utakaa pembeni kwenye mbio za mafanikio na kuwacha wengine wakifanikiwa.
Hebu twende pamoja tupitie nukta kadhaa za kutusaidia kuyajua mambo ya msingi kuyafanya kila siku ili kujenga mafanikio makubwa na ya kudumu.
1. Pangilia siku yako mapema.
Ili kuifanya siku yako ikawa na maana na usipoteze muda kufanya hili au lile, ni muhimu sana kuipangilia siku yako mapema. Ni lazima ujue kesho utakwenda kufanya nini wapi na muda gani.
Haya yote yatawezekana ikiwa utaipangilia siku yako mapema siku moja kabla kwa kuandika vitu vyote utakavyokwenda kufanya siku inayofuata. Hili ni zoezi litakalo kuokolea muda wako sana, lakini hata hivyo litakusaidia kuifanya siku yako iwe ya ushindi.

Usijadanganye hata kidogo kuanza siku yako mpya bila kuipangilia. Kama utaanza siku yako bila kuipangilia, hiyo itakuwa ni sawa na kupoteza muda wako mwenyewe ni bora urudi ukalale. Watu wenye mafanikio makubwa wanapangilia sana siku zao mapema na ndiyo moja ya siri kubwa ya mafanikio yao.
2. Anza siku yako mapema.
Kuipangilia siku yako mapema hiyo peke yake haitoshi. Kitu kingine unachotakiwa kukiongeza ni kuianza siku yako asubuhi na mapema sana. Acha kujivuta kitandani na kuchelewa kuamka, hiyo itakupotezea mafanikio mengi sana.
Kwa jinsi utakavyojifunza kuamka asubuhi na mapema , itakusaidia kufanya yale majukumu ya mahimu asubuhi na mapema kabla kelele zingine za dunia hazijaanza. Mara nyingi asubuhi na mapema ni kipindi ambacho hata akili yako inakuwa ipo kwenye utulivu mkubwa hivyo ni rahisi hata kugundua kitu.
3. Fanya jambo moja kwa uhakika.
Najua unakuwa una mambo mengi ambayo unakuwa umejipangia kuyafanya katika siku yako. Sasa ili uweze kupata nguvu zaidi ya kufanya mambo yote kwa ufasaha chagua jambo moja tu ambalo kila siku utakuwa unaanza nalo kwa kulifanya kwa ufasaha.
Kila utakapoanza jambo hilo litakusaidia kujiona mshindi kwa sehemu, hivyo hata majukumu mengine yatakayoendelea utakuwa unafanya kwa kujiamini. Jambo hilo linaweza likawa kuandika, kusoma au kitu chochote lakini ni muhimu jambo hilo kulifanya asubuhi na mapema sana.
4. Fanya jambo la kukusogeza kwenye ndoto yako.
Kati ya jambo unalotakiwa pia kulifanya kila siku ili kujihakikishia ndoto yako inatimia ni kuchua hatua za kukusogeza kwenye ndoto zako. Haijalishi hatua hizo ni kubwa au ndogo vipi lakini ni lazima uchukue hatua kila siku hata kama upo kwenye mazingira ya kukatisha tamaa.
Siku zote kuna msemo unaosema hatua ni hatua, hiyo ikiwa na maana ni bora ukachukua hatua kidogo kuliko ukabaki hujachukua hatua yoyote. Hivyo, kama umejitoa kweli na kuhakikisha malengo yako yanatimia, fanya jambo hata dogo la kukufikisha kwenye malengo yako.
5. Tunza muda wako vizuri.
Kila sekunde, dakika vina umuhimu sana mkubwa katika kubadili maisha yako. Hivyo kwa kila siku iliyo mkononi mwako jua kabisa upo umuhimu wa kutumia muda wako vizuri ili uweze kukusaidia kufanikiwa. Mambo mengine yote unaweza kupoteza lakini sio muda.
Ikiwa utashindwa kutumia muda wako vizuri, sitashangaa sana kukuona ukiwa na maisha ya hovyo kwa baadae. Kwa mujibu wa tafiti nyingi zinaonyesha moja ya sababu inayopelekea watu kuwa na maisha mabovu pia matumizi mabovu ya muda yanachangia kwa kiasi kikubwa sana.
6. Jifunze kila siku.
Ukiangalia watu wengi wakati mwingine wanashindwa kufikia mafanikio kwa sababu tu ya kushindwa kujifunza. Je, jiulize hata wewe mwenyewe binafsi unajifunza kila siku vya kutosha ili kuhakikisha kile unachokifanya unakijua vizuri na kikuletee manufaa?
Mara nyingi ukiangalia wengi hatupo tayari kujifunza zaidi ya kutaka kufanikiwa kwa maarifa yetu. Kutokana na kosa hilo hapa ndipo anguko kubwa la kushindwa huanzia. Wengi hujikuta wameshindwa kutokana na kukosa maarifa au ujuzi fulani na sio mtaji.
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Napenda pia kuchukua fursa hii kukukaribisha kwenye kundi la Whats App ili tuweze kujifunza pamoja na kwa ukaribu zaidi. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifutia na namba yako kwenda 0713 04 80 35 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni wako rafiki,
IMANI NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com  

No comments :

Post a Comment