google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Jan 10, 2018

Sahau Jambo Hili Na Fanya Mambo Makubwa Maishani Mwako.

No comments :
Kila siku inapoanza ni siku kubwa sana kwako ya kuweza kufanya mambo makubwa kuliko unavyoweza kufikiria. Kila siku ina fursa fulani hivi kubwa ambayo unatakiwa uitumie kwa ufasaha ili uweze kupiga hatua za kwenda mbele.
Kama vile mwaka mpya unavyoanza na wengi wanakuwa na hamasa ya kufanya mambo makubwa, hamasa hiyo unatakiwa uiendeleze kila siku, kwani wewe unaishi kwa siku moja tu, siku ambayo unatakiwa kuiboresha sana na kufika mbali.
Kama kila siku ni mpya na unatakiwa ufanye mambo makubwa, ila unatakiwa ukumbuke mambo hayo makubwa hutaweza kuyafanya kama utasau jambo moja tu. Jambo hili ni vizuizi na changamoto ulivyokutana navyo tayari maishani mwako.
Najua kuna changamoto za aina fulani ambazo wewe bila hata kupenda uliweza kukutana nazo na ambazo uliona kama zinakukwamisha. Sasa ili uweze kufanikiwa unatakiwa na kupiga hatua kubwa maishani unatakiwa kuzisahaua changamoto hizo.

Unachotakiwa kukijua vizuri ni kwamba changamoto ulizopitia tayari zimeshapita. Hutakiwi changamoto hizo kuzibeba sana na kuzishikilia na kuziwekea kumbukumbu kwa muda mrefu kama vile maisha yako yameishia hapo.
Kila kitu kinaweza kubadilika, unatakiwa kuishi kwa kwenda mbele na si kuishi kwa kurudi nyuma ambako unafikiria mambo yaliyopita sana, kuna msemo usemao yaliyopita si ndwele tugange yajao ni kweli ni wakati wa kuganga yajao.
Zile changamoo za nyuma unatakiwa kuzitumia kama fundisho kwamba vitu gani ubadilishe na vipi usibadilishe lakini usizitumie kama sehemu ya kujilaumu sana ni wapi ulipokosea na kujiona hufai kabisa.
Sasa unatakiwa kufikiri ni namna gani utakavyoweza kufanya mambo makubwa na kusahau kabisa jinsi ambavyo ulipokwama wakati uliopita. Kila kitu kinawezekana ukiamua fikra zako uziweke kwa namna hiyo.
Jipe ahadi ya kusahaua yote yaliyo nyuma na shughulika  na yale mambo yote yaliyo mbele yako kwa uhakika zaidi wa kuweza kufanikiwa. Uamuzi wa kufikia kufanya mambo makubwa unao ikiwa usipojifunga sana na vizuizi vilivyopita.
Kumbuka kuchukua hatua, sahau vizuizi na changamoto za nyuma, leo ni siku mpya ya kuweza kufanya mambo makubwa maishani mwako. Kuanzia sasa songa mbele na acha kurudi nyuma hata kidogo.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.