google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Mar 16, 2018

Ili Kufanikiwa, Maisha Yanahitaji Sana Wewe Ufanye Kitu Hiki Kila Siku.

No comments :
Maisha kwa asili yalivyo, yana changomoto na matatizo sana, lakini je, hiyo ni sababu inayokufanya usiishi kwa furaha maisha yako?
Maisha hayawezi kukamilika kama unavyotaka wewe hata ufanyaje, sasa je, hiyo pia ni sababu inayokufanya ushindwe kuchukua hatua na ukabaki kama ulivyo?
Maisha yanakualika leo, yanakualika uishi katika ukamili wake pasipo kujali ni changamoto, hali au kitu gani kinatokea. Sasa kama iko hivyo unasubiri nini?

Muda ulionao, ndio muda pekee ambao unaweza ukafanya mabadiliko ya maisha yako. Maisha yanakualika ufanye kitu cha kubadili maisha yako na si kubaki hapo tu.
Maisha yana kualika ufanye mabadiliko makubwa ya maisha yako kutokana na yale uliyopitia na uzoefu ambao tayari umeshaupata.
Maisha yako hayataki wewe uendelee kulalama na kupiga kelele kwa sababu kwamba maisha ni magumu au hayawezekani, maisha yanataka ufanye mabadiliko.
Je, uko tayari kwa hilo? Kama uko tayari ukumbuke hutakiwi kuendelea kulalama au kuwalaumu watu wengine sana, unachotakiwa wewe ni kuchukua hatua.
Angalia fursa zinazokuzunguka na kisha fursa hizo zifanyie kazi mara moja. Angalia matatizo yaliyopo na kisha yafanyie kazi na yakupe mafanikio.
Hata inapotokea changamoto nyingi zimekuzunguka na unaona kama unapoteza weka kwenye akili yako kwamba kitu gani ambacho kinaendelea kwako.
Kitu pekee ambacho kinaendelea kwako ni kwamba maisha yanakualika na maisha yanakutaka wewe uweze kufanya kitu cha tofauti ambacho ni kuleta mabadiliko.
Wale wote wanaoitikia mwaliko wa maisha kwa kile yanachotaka ndio huweza kufaidi matunda kwa kufanikiwa maishani mwao.
Pasipo kujali unapitia katika hali gani au maisha duni sana, lakini unatakiwa kila wakati kukumbuka kwamba maisha yanakutaka sana wewe kuweza kufanya mabadiliko.
Mabadiliko ndio kila kitu, ila ukibaki hivyo tu hapo ulipo na ukawa hutaki kufanya kitu cha kubadili maisha yako basi hapo utakuwa upo kwenye hali ngumu sana.
Kile unachokijua vizuri, anza kukifanyia kazi leo kwa ukamilifu mkubwa, kwani maisha yanataka ufanye kitu hicho kila siku ili kiweze kukupa mafanikio yale uyatakayo.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,









No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.