google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Oct 11, 2017

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutabiri Mafanikio Yako Ya Kesho Yatakuwaje.

No comments :
Wapo watu ambao wana uwezo wa kutabiri maisha yao ya kesho yatakuwaje. Watu hawa wapo na wanafanya hivyo na kufanikiwa, lakini  si kwa sababu wana kipaji, au wana uwezo wa ziada, wanafanya hivyo kwa sababu wana mbinu au njia za kuwawezesha kujua hivyo.
Mbinu hizo ambazo wanazitumia na kuweza kuelewa kesho yao katika maisha itakuwa vipi, hata wewe unaweza ukawa na mbinu au njia hizo na kujua kwa wazi kumbe 'aah kesho au baada ya muda fulani maisha yangu yatakuwa hivi au vile.'
Kama nilivyokwambia mbinu hizi kumbuka hazitegemei sana uwezo wako, wala hazitegemei sana unawajua wakina nani au wewe una kipaji fulani ndani yako ndio uzitumie kuweza kufanikiwa, hapana.
Watu waliofanikiwa wamemudu sana katika hili kuweza kutumia mbinu hizo na kuwawezesha kufanikiwa kila siku iitwapo leo. Na kwa msingi huo huendelea kutumia mbinu hizi tena na tena kupata mafanikio zaidi.

Ni rahisi tu kuweza kuzijua mbinu hizi ambazo zinaweza zikakufanya na wewe ukajua kesho yako itakuwaje. Kivipi hili linawezekana? Ni kitendo cha wewe kuweka malengo yako na kuamua kuchukua hatua kila siku za kukufikisha kwenye ndoto zako. Ni rahisi tu kama hivyo, huamini?
Ipo hivi, unapoweka malengo halafu ukaamua kufa na ndoto zako, hakuna kitu ambacho kitaweza kukuzuia kuweza kufanikiwa. Hapo ni lazima utaweza kufanikiwa na kufika juu kwenye mafanikio yako.
Hii haijalishi unaishi wapi au wewe ni mtu wa kutoka koo au kabila gani, ukijua malengo yako vizuri ambayo unayoyahitaji na halafu ukaweka mikakati ya kuweza kuchukua hatua kila siku utatake usitake utaweza kufanikiwa.
Umeiona eeeh jinsi ilivyo rahisi kuweza kujua kesho yako itakuwaje? Huhitaji kwenda kwa mganga wa kienyeji wala huhitaji kupiga ‘ramli’, kama huna malengo na huchukui hatua yoyote, tegemea anguko kubwa la maisha yako.
Lakini ukijitoa kweli usiku na mchana na kujipa ahadi kwamba mimi nitafanya kila linalowezekana mpaka natimiza ndoto zangu uwe na uhakika utafanikiwa katika hilo na hivyo ndivyo utamudu kuwa mtabiri mkubwa wa maisha yako.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,




No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.