Jul 31, 2017
Nguvu Ya Kimafanikio Ipatikanayo Kwenye Uchaguzi Wako Sahihi.
Safari
ya kufikia mafanikio makubwa inaanza na kufanya uchaguzi uliobora. Hakuna
mafanikio makubwa yoyote ambayo yanakuja kwa bahati mbaya, mafanikio yote
makubwa yanaanza na uchaguzi uliobora na tena ambao unaufanya kila siku.
Uchaguzi
huu ambao nina uzungumzia hapa na ukabadilisha maisha yako si uchaguzi mkubwa
sana kama unavyofikiri. Huu ni uchaguzi mdogo mdogo ambao kuna wakati
unayafanya hata pengine bila kufikiri.
Uchaguzi
kama leo uamke saa ngapi, uchaguzi kama leo ujifunze nini au usijifunze,
uchaguzi kama leo utumie pesa zako vipi, hizi ni moja ya chaguzi ndogo ndogo
sana lakini ambazo ukizitumia vizuri zinabadilisha maisha yako kabisa na kuwa
wa tofauti.
Ukumbuke
kabisa kile unachokipata, ni matokeo ya kile unachokifanya, na kile
unachokifanya ni matokeo ya uchaguzi unaoufanya kila wakati kwenye maisha yako.
Kama unafanya uchaguzi mbovu, tegemea kupata maisha mabovu pia.
Matokeo
bora kwenye maisha yako yanakuja kwa kufanya uchaguzi uliobora. Hiki ndicho
kitu unachotakiwa ukielewe sana na kukifatilia. Ukijifunza kuwa na uchaguzi
sahihi, itakusaidia sana kuweza kutimiza ndoto zako.
Acha
kuendekeza uchaguzi mbovu utakaokangusha baadae. Acha kuendekeza kufanya uchaguzi
wa kufanya starehe na kusahau kufanya kazi. Acha kuendekeza uchaguzi wa kuishi
maisha uyatakayo badala ya kujenga nidhamu ya mafanikio.
Uchaguzi
wowote unaoufanya ni lazima ulete matokeo. Kwa chochote kile unachotaka
kukifanya wewe kifanye, ila hata hivyo uelewe majibu yake lazima utayapata,
yawe mazuri au mabovu lakini uyapata bila shida.
Uchaguzi
ule mdogo unaoufanya leo hata kama hautilii maanani, huo ndio unajenga msingi
wa mafanikio yako ya kesho. Kuwa makini usije ukaishia kuishi maisha ya hovyo
kama uchaguzi wako ni mbaya na haukusaidii.
Kumbuka,
maisha yako yanaweza kubadilika ikiwa kama utafanya uchaguzi na maamuzi sahihi
kila siku. Elewa hiyo ndiyo nguvu kubwa ya uchaguzi sahihi inavyofanya kazi na
hata kukupa mafanikio utakayo.
Kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jul 30, 2017
Tabia Tano Muhimu Ambazo Ukizifuata Zitaboresha Maisha Yako Sana.
Tabia ni msingi mkubwa sana
wa mafanikio yako. Ukijenga tabia njema uwe na uhakika utafanikiwa na kufika
mbali sana kimafanikio.
Leo nataka tuangalie kupitia
makala haya, tabia ambazo ukizifuata na kuzitekeleza zitafanya maisha yako kuwa
bora na ya thamani kila iitwapo leo.
Tumia tabia bora za mafanikio zikufanikishe. |
1.
Usifanye kazi mbili kwa wakati mmoja.
Mawazo yako yote weka kwenye
kitu kimoja unachokifanya. Ukiweka mawazo kwenye vitu viwili, utashindwa
kuvifanikisha vyote kwa ufasaha na utashindwa.
2.
Usigombane na mtu mpumbavu.
Kama kimetokea kitu cha kutoelewana
na mtu ambaye unamwona hajielewi, achana naye ili asije akakupotezea muda wako
bure.
3.
Usiingie kwenye mabishano yasiyo ya lazima.
Fanya kile unachokiamini,
kubishana kwingi na kujaribu kuonyeshana eti nani ni mshindi ni mambo ambayo
yanapoteza muda wako pia. Epuka kubishana.
4.
Usifanye maamuzi bila ya kufikiri sana.
Kama unataka kufanya maamuzi
bora na ya maana kwako, yafanye kile kipindi ambacho akili yako imetulia,
ukifanya maamuzi kwa haraka utajipoteza.
5.
Usiende kulala ukiwa na hasira.
Unapolala huku una hasira,
elewa kabisa hasira hizo utaamka nazo siku inayofuata, hivyo nenda kitandani
ukiwa na amani itakusaidi sana.
Hizo ndizo tabia tano za
msingi zenye uwezo wa kuboresha maisha yako ikiwa utaamua kuzifanyia kazi kwene
maisha yako.
Kila la kheri katika
kuboresha maisha yako na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com
kujifunza kila siku.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika
mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Mshauri
wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog,
dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano;
+255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Jul 29, 2017
Tafuta Sheria Zinazokuongoza Kwenye Maisha Yako.
Kwa
kawaida kila sehemu unayokwenda zipo sheria za kufuata. Zipo sheria za
kuendesha gari, zipo sheria za kufanya biashara, zipo sheria za kuingia ‘club’,
zipo sheria za mchezo wa mpira miguu. Inawezekana unajiuliza kwa nini
sheria hizi zipo? Jibu ni rahisi tu, zimewekwa ili kuleta ufanisi na mafanikio
katika maeneo hayo.
Kunapokuwa
na sheria zinazoongoza jambo lolote, zinafanya kwanza kunakuwa na nidhamu kubwa
ya ufanyaji wa jambo hilo na mwisho wa siku huleta mafanikio. Kwa mfano, kama
kungekuwa hakuna sheria ya mpira wa miguu, mchezo huo usingefanikiwa na badala
yake kungekuwa na fujo tu uwanjani.
Kama
kila kitu chenye mafanikio kinaongozwa na sheria, hata maisha yako yanatakiwa
kuwa na sheria ambazo utazifuata kila iitwapo leo ili uweze kufanikiwa. Kama
hautakuwa na sheria zinazoongoza maisha yako itakuwa ni ndoto kufanikiwa. Utakutana
na changamoto nyingi bila sababu kwa sababu huna sheria zako.
Labda
nikuulize kitu, je, una sheria zinazoongoza maisha yako? Kama huna tafuta
sheria za kuongoza maisha yako. Unapokuwa na sheria zako, zinakufanya kutawala
maisha yako na si kuishi ishi tu bila mwelekeo. Ishi kwa sheria zako, hiyo itakufanya kila wakati utakuwa
mshindi, tofauti na ambavyo kama huna.
Jul 28, 2017
Wakati Bora Wa Kufikia Mafanikio Yako Ni Huu…
Leo nimejikuta namkumbuka sana mwalimu wangu wa somo la
Kiswahili, moja kati ya vitu ambavyo vimenifanya niweze kumkumbuka ni vile
ambavyo alikuwa anajitoa kwa hali na mali katika kuhakikisha tunaelewa somo la
Kiswahili. Ni siku nyingi kidogo zimepita lakini kile ambacho alinifundisha
bado hakijafutika akili mwangu, na sina uhakika kama kitakuja kufutika.
Mwalimu wangu huyu sitachoka kumuombea kwa mwenyezi
Mungu kwa kila jambo ambalo analifanya aweze kufanikiwa Zaidi. Namkumbuka
kwa sababu kuna somo ambalo alitufundisha kwa kutumia nguvu zote, somo hili ni
somo la nyakati.
Na katika somo hili alisema zipo nyakati mbalimbali ambazo ni
wakati uliopita, wakati uliopo na wakati ujao. Pia alieleza ya kwamba nyakati
hizi zote humuhusu mwanadamu, katika kufanya na kusimulia mambo mbalimbali
ambayo yalikwisha fanyika au ambayo yatafanyika.
Na miongoni mwa vitu ambavyo nakumbuka aliweza kutushauri kuhusu
nyakati hizi alisema ya kwamba, mwanadamu yeyote yule ili aweze
kufanikiwa katika maisha yake ni lazima aweze kutambua ya kwamba katika nyakati
hizo ni nyakati moja tu ndiyo muhimu kwake.
Na nyakati hiyo ni wakati uliopo na si vinginevyo, kwani wakati
uliopita na wakati ujao si rafiki kwa mwadamu hata kidogo katika kutenda mambo
ya msingi, kwani watu wengi wamekufa na ndoto zao kwa sababu waliamini Zaidi
nyakati zijazo, wao pamoja na kuwa na mambo mazuri walijifariji na kusema
nitafanya kesho, kesho hiyo ikawa kesho mpaka siku wakazikwa na neno lao
nitafanya kesho.
Kwa maneno mengine kusema nitafanya kesho, kwa neno moja lenye
kujifariji tunasema“nimeahirisha”. Neno hili ni baya sana kwani
wale wote waliofanya kitendo hiki hawakuweza kufikia lengo lao kwa asilimia
zote. Kuahirisha kufanya jambo la msingi ni kutafuta visingizio.
Hivyo kama wewe ni mtu wa kuahirisha sana mambo, hasa kwa kile
kitu unachokifanya, elewa kabisa unapanda mbegu au unajitengenezea mazingira ya
kushindwa kwako. Kama kuna jambo ambalo unataka kulifanya leo, hebu lifanye
bila kusita sita au bila kuwa na shaka ya kitu chochote.
Hivyo kama kweli unataka mafanikio ya kweli jifunze kufanya
mambo kwa wakati, huku ukikimbia visingizio visivyokuwa vya msingi. Daima
ikumbukwe ya kwamba ni heri upate ugonjwa wa malaria, kwani ugonjwa
huu utatibika,Ila ukipata ugonjwa wa kuahirisha mambo ya msingi basi
jiandae kufa maskini.
Mwisho nikuache na nukuu isemayo; Kumbuka ukianza leo si sawa
na kuanza kesho.
Imeandikwa na uongozi wa mtandao huu wa dira ya mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
Jul 27, 2017
Hatua Hizi Ni Msingi Wa Mafanikio Yako.
Kuna
yale mambo ambayo kwenye maisha huwa yanaonekana ni rahisi kabisa kufanyika na
pengine kukupa mafanikio. Hata hivyo kitu cha kushangaza mambo hayo pamoja na
urahisi wake wengi huwa hawayafanyi.
Hali
hiyo huwa inatokea kwako kwa sababu ya kujikuta upo katika hali ya ‘easy
to do…also easy not do,’ yaani urahisi kwa hali ya kawaida unauona,
Lakini ndani yake kuna ugumu fulani hivi ambao unakuzuia kufanikiwa.
Ukweli
wa mambo ulivyo kwenye maisha yako, iwe afya, furaha au utajiri unaweza
kuvipata ikiwa utachukua hatua ndogo ndogo kila siku zile zinazowezekana ambazo
zitakusogeza kwenye lengo lako bila kudharau hatua yoyote ile.
Kama
ni rahisi hivyo, kwa nini watu wengi wanashindwa kufikia malengo yao? Hiyo yote
ni kwa sababu ‘easy to do…also easy not do,’ kama tulivyosema. Hatua ndogo ndogo
zinakuwa ni ngumu sana kuweza kutekelezwa na wengi wetu.
Jiulize
ni mambo mangapi katika maisha yako ulipoambiwa fanya kitu hiki, ulisema
kwamba, ‘aaah kitu hiki ni rahisi,
nitakifanya tu’. Lakini mwisho wa siku unajikuta unashindwa kuchukua hatua
kabisa.
Kuanzia
sasa, acha kuwa mtumwa wa ‘easy to do…also not easy to do.’
Chukua hatua ndogo ndogo bila kudharau udogo wa hatua hiyo. Ukifanya hivyo
utaweza kufanikiwa na kutimiza ndoto zako.
Jul 26, 2017
Kama Unashindwa Kufanya Mabadiliko Kwenye Maisha Yako, Basi Tatizo Ni Hili…
Kuna wakati
unaweza ukajikuta unataka kufanya mabadiliko kwenye maisha yako, lakini
unashindwa. Je, umeshawahi kujiuliza kushindwa huko kunatokana hasa na nini au
kitu gani. Najua hili linaweza likawa limekotekea.
Ikiwa kila
wakati unajaribu kufanya mabadiliko ya kitu fulani na unashindwa kuleta
mabadiliko hayo, basi tambua maumivu ya kushindwa hayajawa makubwa sana ndani yako
hadi uweze kuleta mabadiliko hayo.
Kwa mfano,
unataka kuwa na mtaji na unashindwa kila mara, basi elewa kabisa maumivu ya
kushindwa kupata mtaji hayajawa makubwa vya kutosha. Tuchukulie leo hii,
ukaambiwa usipokuwa na mtaji hadi mwaka huu unaisha, utapigwa risasi.
Jiulize
utakubali kufa kwa sababu ya kukosa mtaji huo unaoutaka? Bila shaka
haitawezekana, utafanya kila linalowezekana kufanikisha hilo. Hivyo, wakati
mwingine mabadiliko yanakuja kwenye maisha yako kwa sababu ya kule kuumia sana.
Wakati ulipokuwa
shule ulisoma sana na kuhakikisha unafaulu ili kukwepa maumivu ya kufeli. Pia
kuna wakati umeweka juhudi nyingi sana ili kukwepa maumivu ya aina fulani na
kutafuta mahala sahihi kwako.
Tunaambiwa kitu
chenye nguvu ya kubadili tabia yako na mafanikio ni maumivu. Waulize wote ambao
wamefanikiwa na ambao wanafikiri chanya kuhusu mafanikio, watakwambia maumivu
yamewasaidia sana kubadilika na kuweza kufika hapo walipo mpaka leo.
Hivyo basi, kila
wakati tambua hasira ya kushindwa kupata kile unachokita, maumivu ya kushindwa
kupata kile unachotaka kukibadili, yatumie maumivu hayo ili yaweze kukusaidia
kuweza kufanikiwa.
Jul 25, 2017
Kitu Pekee Cha Kukiogopa Pale Unapohitaji Mafanikio Ya Kweli.
Kuna wakati mwingine inabidi ujutie katika hali ambayo upo hivi sasa, nasema hivyo kwa sababu moja kati ya mambo ambayo inakubidi ujutie katika maisha yako ni kwa sababu umekuwa ni mtu wa kushangaa kuliko kutenda mambo ya msingi.
Tabia
hii ya kushangaa kila kitu pasipo wewe kuchukua hatua ndiyo ambayo kiukweli
inakufanya uje kujuta hapo baadae, na pia ikumbukwe wakati wewe unazidi
kushangaa wapo wengine ambao wanazidi kusonga mbele katika utendaji.
Tabia
hii ya kushanga ni mbaya sana katika safari ya mafanikio, kwa mfano, Utakuta
wao ni watu wa kushangaa na kuhamasika sana na miradi wanayofanya watu wengine,
ukija upande wao hakuna hata kitu kimoja wanachofanya.
Vilevile
utakuta watu hawa kazi yao ni kuingia
kundi moja, wanashangaa kinachoendelea humo na kutoka na kuingia tena kundi
lingine wanashangaa wee na kutoka tena, pia bila kuchukua hatua, endapo
utachukua jukumu la kuwauliza watu hawa watakwambia wanashangaa mataa.
Tabia
hii kama unayo ni vyema ukaamua kuiacha mara moja kwani dunia ya sasa hivi ni
ya mwendo kasi Zaidi ya kasi ya 4G hivyo kila wakati ni lazima uweze kufanya
kazi. Kama kuna fursa hata kama ni ndogo kiasi gani, itumie ikusaidie
kufanikiwa na acha kubaki tu kuwa mtu wa kushangaa. Kama ni kujifunza, jifunze kweli.
Uzuri
au ubaya wa maisha hakuna ubabaishaji, ukileta ubabaishaji wa aina yoyote ile,
utaumbuka tu na ni lazima utajibiwa na maisha kama vile wewe unavyobabaisha.
Badilika rafiki na achana na biashara ya kushangaa, kuwa mtendaji na aamua
kufanya kazi.
Hivyo
amua sasa kuwa ni mtu wa kuchua hatua kuliko kubaki kushangaa, kwani kufanya
hivyo ni kujichelewesha mwenyewe kumbuka ya kwamba kuendelea kushangaa ni
kupoteza muda na kupoteza muda ni sawa na kuacha pesa zipite machoni mwako.
Mpaka
kufikia hapo hatuna la ziada tukutakie siku njema na mafaniko mema, Mwenyezi
Mungu akubariki sana kwa kusoma Makala haya.
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
Jul 24, 2017
Utajiri Au Umaskini Wako, Unatokana Sana Na Maamuzi Haya.
Maisha
unayoishi sasa, kwa sehemu kubwa, yanatokana na maamuzi uliyoyafanya kipindi cha
nyuma na maisha utakayoishi kesho pia yanategemea sana maamuzi unayoyafanya leo
kwenye maisha yako.
Unauwezo
wa kuboresha maisha yako kwa kufanya uchaguzi sahihi wa hatua unazozichukua
kila siku. Moja ya kitu unachotakiwa uanze nacho ili uweze kuchukua hatua
sahihi ni kujifunza juu ya kutawala pesa zako.
Hivi
pengine nikuulize, umeshawahi kujiuliza katika maisha yako pesa ngapi zimepita
mikononi mwako? Ukiangalia, ni pesa nyingi sana, lakini cha ajabu kwa wengi
zimewaacha jinsi walivyo wakiwa hawana kitu.
Sasa
basi, ili kuendelea kukosa pesa kusitokee kwako, unahitajika sana kujifunza juu
ya kuwa na maamuzi sahihi ya kutawala pesa zako. Ukiipata elimu hii na
ukaielewa vizuri, utakuwa umefanya maamuzi sahihi ya kukupeleka kwenye utajiri
wako moja kwa moja.
Kwa
mujibu wa uchunguzi mdogo uliofanyika unaonyesha hivi, asilimia kubwa ya
watu waliomaskini wanaweka akiba chini
ya asilimi 2 na wengine hawaweki kabisa. Hiyo ikiwa na maana kipato chote
kinachobakia kinaingizwa kwenye matumizi.
Mpaka
hapo kwenye maamuzi hayo, ni moja ya maamuzi mabaya yanayowapeleka wengi kwenye
umaskini. Akiba au kujilipa mwenyewe
kiasi kidogo cha kila pesa unayopata ni kitu cha msingi sana kama unataka kesho
yako iwe ya mafanikio.
Ni
kweli swala la matumizi ya pesa zako liko mikononi mwako, lakini ili uwe tajiri
ni lazima ujue namna ya kutawala pesa zako. Sio kwa sababu una pesa unanunua
vitu hovyo na kujikuta hakuna hata kiasi kidogo cha pesa ulichobaki nacho.
Angalia
usije ukajikuta ukajuta kesho kutokana na maamuzi mabovu unayoyafanya leo juu
ya pesa zako. Fanya maamuzi leo bora
yatakayokufanya kesho ukajiona shujaa mkubwa kwa kujiona ulifanya kitu cha maana kwa
sababu ya pesa zako.
Ikiwa
unataka kuendelea kimaisha na hata kuwa tajiri elewa vizuri juu ya kutawala
pesa, yote haya unatakiwa ujifunze ukiwa bado kijana, kama hautafanya maamuzi
hayo sahihi, ni wazi hautafanikiwa.
Utajiri
au umaskini wako, siku zote upo mikononi mwako kutokana na maamuzi unayoyafanya
juu ya pesa. Leo jiwekee kiapo kwamba, kwa pesa yoyote unayoipata ni lazima
uweke kidogo kwa ajili yako.
Kwa
kuanzia, anza hata na asilimia kumi ya kile unachokipata, umeshindwa kabisa,
anza na kiasi chochote. Pesa hiyo kumbuka ni yako, unakuwa haujapoteza popote,
hivyo usiwe na wasiwasi, chukua maamuzi sahihi leo yatakaokupa utajiri.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kwa ajili ya kujifunza na
kuhamasika kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com.
Jul 23, 2017
KITABU; The Success System That Never Fails (Mfumo Wa Mafanikio Ambao Haushindwi)
Kwenye kitabu hiki mwandishi W. Clement Stone anaeleza upo mfumo katika maisha , ambapo
ukiutumia mfumo huo vizuri, utayafanya maisha yako yasiwe ya kushindwa kamwe,
bali yawe ya mafanikio siku zote.
Katika
mfumo huo mwandishi ameongelea mfumo usioshindwa katika maisha jinsi ulivyokuwa
wa muhimu katika maisha yako. Na mfumo huo umebebwa sana na mambo makubwa
matatu ambayo ni;-
Hatua/vitendo
(Action)
Hapa
inakubidi kuchukua vitendo kwa kitu unachotakiwa kufanya. Unatakiwa kuchukua
vitendo bila kujali kitu. Kitu unachokifanya kama umeamua kukifanya, kifanye.
Acha kupoteza muda chochote unachokiamini, hebu kifanye bila woga.
Kujua
namna ya kufanya (Know-how)
Kuchukua
hatua kwenye jambo lolote yenyewe haitoshi peke yake, unatakiwa sasa kujua
namna ya kufanya kitu hicho tena. Unatakiwa kujua namna ya kufanya katika hali
ambayo itakupa matokeo sahihi.
Maarifa
(Knowledge)
Maarifa
ni kitu cha msingi katika kufanikisha jambo lolote lile. Lazima uwe umeiva kwa
maarifa ya kutosha ili yakusaidie kufanya mambo yako kwa usanifu wa hali juu na
kukupa mafanikio. Ukikosa maarifa ya msingi kwa jambo lolote utashindwa.
Hayo
ndiyo mambo matatu ya msingi sana ambayo mwandishi ameyasititiza na kuyatilia
mkazo karibu katika kitabu chake chote. Mambo mengine ya kujifunza kwenye
kitabu hiki ni kama haya yafuatayo;-
1.
Maamuzi mazuri katika maisha yanaendana na kuchukua hatua. Kama huchukui hatua,
halafu ukasema eti una maamuzi mazuri, basi elewa unajidanganya na maamuzi hayo hayana maana yoyote kwako kwa
sababu hayawezi kukusaidia.
2.
Kama umeamua kufanya kitu fulani, iwe ni biashara , masomo au kitu chochote ambacho
kipo kwenye malengo yako, usirudi nyuma hadi umefanikisha kitu hicho.
Haijalishi njiani umekutana na changamoto nyingi kiasi gani, pambana mpaka
upate kile kitu ambacho ulikuwa umelenga kukifanikisha.
3. Unaweza
ukaongeza uwezo mkubwa wa kufanikiwa ikiwa utatumia kanuni za mafanikio na
kuzifanyia kazi kila siku. Unaweza pia ukapunguza hali ya kushindwa sana kwenye
maisha yako, ikiwa kama utaendelea kutumia kanuni hizo hizo za mafanikio. Kama
utafanya kinyume na hapo jiandae na anguko kubwa la maisha yako.
4.
Mafanikio yanakuja kwa wale wote wanaojaribu hiki au kile mara kwa mara bila
kujali wanashindwa kwa kiasi gani. Huwezi kuwa mshindi kama umekaa tu. Jaribu
kwa jinsi unavyoweza ili kujenga mafanikio yako.
5.
Kila wakati hakikisha unayatawala mazingira yako na sio mazingira yakutawale.
Epuka kila hali iwe mazingira au watu wakutawale. Hakikisha unatawala mazingira
yako vizuri ili yakupe nguvu ya kushinda.
7.
Kufikiri peke yake hakuwezi kukafanya wewe ukashinda uoga ulionao. Kitu
kitakachoweza kukufanya ukashinda uoga ulionao ni zile hatua unazochukua. Hatua
au vitendo ni dawa pekee ya kuondoa hofu au woga wowote ule kwako.
8. Kama
hujiwekei akiba yoyote, elewa kabisa ndani yako umekosa mbegu ya mafanikio.
Wanaojiwekea akiba hata kama ni pesa kidogo sana, hiyo inawasaidia kuweza
kukuza mbengu ya mafanikio iliyo ndani mwao. Angalia watu wengi ambao hawaweki
akiba, maisha yao sio mazuri na kufanikiwa inakuwa ni ngumu.
9.
Moja ya sifa kubwa ya mafanikio unayotakiwa kuwa nayo na kuiendeleza ni TABIA zako ulizonazo. Ukiwa na tabia
sahihi, uwe na uhakika zitakuongoza hadi kuweza kufikia mafanikio yako.
10.
Ukishakijua vizuri kile unachokitaka kwenye maisha yako, tafuta maarifa na
mbinu za kukichimba kitu hicho ndani, nje mpaka ukielewe vizuri. Kukijua vizuri
kitu hicho ndani, nje itakupa wewe uwezo wa kukifanya kwa ufasaha sana na
kupata matokeo chanya.
11.
Nguvu ya kuendelea kufanya jambo lolote itazidi kuchochewa ndani yako kama
moto, ikiwa ndani yako pia una hasira, imani ya kufanikiwa na pengine maumivu
ya kuumizwa na wengine. Kama ndani yako unavitu hivyo, itachochea nguvu kubwa
iliyoko ndani yako ya kufanikiwa na utafanya kila linawezekana kuhakikisha
unafanikiwa.
12.
Unapokuwa una hamu na hamasa ya kufikia malengo yako, ni lazima kutafuta njia
na kila aina ya maarifa yatakayokusaidia kufikia malengo yako. Maarifa hayo
utayapata kutoka kwa watu ambao tayari wameshafanikisha hicho unachokitaka au
hata kwenye vitabu mbalimbali vya kimafanikio.
13.
Ili ukijue vizuri hicho unachotaka kukifanya ni lazima uchuke hatua. Huwezi
kukijua kitu hicho kwa kusoma peke yake ni muhimu kuchukua hatua zitakazo kupa
uzoefu ambao uzoefu huo utapelekea wewe kujua namna ya kufanya kwa ubora wa
hali ya juu.
14.
Kama kuna jambo ambalo umelianzisha hata kama linakuletea utata endelea
kulifanya. Ikiwa kama utasimama inachukua muda mrefu tena kulianza jambo hilo
na kuwa kwenye mwendo sahihi kuliko ungeendelea na safari. Siri ya kuendelea
ipo kwenye kufanya sasa hicho unachotaka kukifanya. Acha kujisemea kuwa
utafanya kesho au lini, fanya sasa.
15. Siku
zote mafanikio ya mtu yanaanzia kwenye akili yake. Unachotakiwa kufanya ni
kuangalia fursa zinazokuzunguka au changamoto zinazoizunguka jamii yako na
kisha baada ya hapo tafutia majibu yake na utafanikiwa.
.16.
Maadili bora ni msingi mkubwa wa mafanikio yoyote. Kushindwa kwingi kunaanza
pale mtu anapokosa maadili na kujiingiza kwenye tabia za hovyo kama ulevi,
zinaa na hata wizi. Mafanikio hayajengwi kwenye misingi kama hiyo hata siku
moja.
Chukua
hatua kila siku kujifunza haya muhimu uliyojifunza kwenye kitabu hiki.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jul 22, 2017
Watu Wenye Sifa Hii…Ndiyo Wanaofanikiwa.
Linapokuja swala la
mafanikio zipo sifa na mambo mengi ambayo yanakuwa yanatajwa katika kumfikisha
mtu ili aweze kufanikiwa. Mambo au sifa hizo
huwa ni za msingi sana kwa kila mtu ili kufikia mafanikio.
Hata hivyo pamoja na sifa hizo,
ipo sifa moja muhimu sana ambayo kwa
mtafuta mafanikio kama unayo ni lazima utafanikiwa. Sifa hii muhimu ya kimafanikio ambayo nataka
kuiongelea hapa ni uvumilivu wako katika kuelekea mafanikio.
Unaweza ukawa unajituma
kweli, una nidhamu binafsi na unafanya juhudi za kuwekeza kila wakati, lakini
ukikosa uvumilivu hasa pale unapokutana na changamoto au pale unaposubiri
mafanikio yako makubwa huwezi kufanikiwa.
Uvumilivu
ni kitu cha muhimu sana kama umeamua kuishi maisha ya ndoto zako. Inabidi uvumilie
hali ngumu unazokutana nazo, inabidi
uvumilie kuishi wakati mwingine chini ya kipato ili kutimiza malengo ya ndoto
zako.
Kuna
kitu najua unataka kujiuliza nitavumilia mpaka lini, mbona maisha yangu naona
kama magumu, hayaeleweki na hii biashara italeta mafanikio lini? Ndio, najua
yote hayo unapitia, hakuna namna zaidi ya wewe kukomaa na kukubali kuvumilia.
Sikiliza,
kiuhalisia mara nyingi inachukua miaka 3 hadi 5, ili kuweza kupata mafanikio ya
uhakika kwa kile ambacho umekianzisha leo. Huo sio muda mrefu sana kama
unavyofikiri. Unachotakiwa kufanya ni kuwa na subira na kuweka juhudi sana kila
siku.
Hebu
jiulize kuna yale mambo ambayo uliyaanza miaka mitatu iliyopita, yanaonekana
kama yalianza jana tu. Kama hiyo iko hivyo hata maisha yako unaweza kuyabadili.
Kwa nini usikubali kuvumulia ili
kutengeneza ndoto zako za kimafanikio.
Hata
kila unayemwona amefanikiwa, au kila unayemwona yupo ngazi fulani ya
kimafanikio kuna mengi ambayo amepitia na kuvumulia hadi akavuna hicho
alichokivuna. Kama hutaki kuwa na uvumilivu, utajiweka pembeni kwenye njia ya
mafanikio wewe mwenyewe.
Huna
haja ya kujiona unachelewa, hebu jipe muda wa kubadili ndoto zako. Uwe na
uhakika hilo litafanikiwa na utajenga maisha ya mafanikio unayoyataka wewe. Watu
wenye sifa ya kuvumilia magumu mengi na kuweka juhudi hao ndio wanaofanikiwa.
Hakuna
hata siku moja mtu ambaye akipata hasara kidogo anaacha biashara eti
akafanikiwa, mtu hayupo. Uvumilvu wako ni muhimu sana katika safari ya mafanikio
uliyoichagua. Ukiona huna uvumilivu wa kutosha, SAHAU MAFANIKIO.
Tunakutakia
kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jul 21, 2017
Watu Wenye Hasira Na Kiu Kubwa Ya Mafanikio Wanafanya Mambo Haya Kwa Utofauti Sana.
Wapo
watu ambao ndani mwao wameamua kwa dhati kufanya mabadiliko katika maisha yao. Watu
hawa wana kiu, hasira na hamasa kubwa ya kufanya kila kinachowezekana ili kuweza
kufanikisha ndoto zao za kimaisha.
Watu
hawa juhudi zao nyingi huzielekeza kwa kufanya mambo kwa utofauti hali ambayo
huwaletea mafanikio. Inawezekana leo nitakuwa mbaya kwako, kama sitakwambia watu hawa wanafanya mambo
yapi kwa utofauti na yanayowapa mafanikio.
Ni
wakati sasa wa mimi na wewe kwenda pamoja katika makala yetu ya leo kujifunza
kwa pamoja mambo ambayo watu wenye hasira na kiu ya mafanikio huyafanya tofauti;-
1. Wanaongozwa sana na neno HAPANA.
Watu
wenye hasira na kiu ya mafanikio, kila wakati wanapoambiwa kitu ni watu wakusema
sana HAPANA. Wanafanya hivi ili kufatilia ndoto zao kwa ukaribu na kuachana na
kukubali kila kitu ambacho kinaweza kuwapoteza.
Watu
hawa wanajua pia kwa kusema hapana kwanza hata kama kitu hicho walichoambiwa wakagundua
kina faida kwao, ni rahisi kugeuza na kukubali pia. Kusema HAPANA ni jambo
ambalo haliogopwi na watu wenye hasira ya
mafanikio.
2. Kuamka asubuhi na mapema.
Naomba
nikupe tu ukweli mmoja, ukiachana na watu maskini, sijawahi kukutana na mtu
mwenye mafanikio makubwa ambaye kuamka kwake asubuhi ni kwa kuchelewa. Watu
wengi wenye mafanikio wanaamka mapema kabla jua halijatoka.
Asubuhi
ni muda mzuri unaowawezesha kupanga mipango ya siku husika kwa uhakika na
kufatilia mambo kwa ukaribu wakati wengine bado wamelala. Kuamka mapema mi kitu
ambacho wengi hawapendi, kwa watu wenye hasira na mafanikio hupenda sana muda huo.
3. Kujituma sana.
Kati
ya kitu ambacho watu wenye hasira na kiu ya mafanikio wanakifanya sana pia ni kujituma kwa nguvu
zote. Wanajua bila kujituma itakuwa ni kazi bure tu, hakuna mafanikio
yatakayojengwa.
Hujitahidi
kufanya kazi kwa muda mrefu sana kuliko watu wengine ili kuleta matokeo
chanya. Si ajabu kukuta usiku wa manane wakifanya kazi zao ili kufanikisha ndoto
zao. Kujituma na kwenda hatua ya ziada ni kitu ambacho kinafanywa na watu hawa.
4. Wanaongozwa na roho ya ung’ang’anizi.
Watu
wenye kiu ya mafanikio pia wanajaribu sana mambo mengi na kuhakikisha kila wanalolifanya
linafanikiwa. Wakianzisha jambo si rahisi sana kuliachilia njiani. Hung’ang'ana na
kuhakikisha mpaka kuona kutaka kuleta matokeo.
Kwa
kifupi, watu wenye hasira na mafanikio ni wabishi wa mafanikio yao. Hawakubali
kirahisi kushindwa. Wapo tayari kufanya mara elfu moja, ilimradi tu kuona
wanafanikiwa. Hiki ni kitu kimojawapo wanachokifanya kwa utofauti pia.
5. Si walevu wa mitandao ya kijamii.
Mitandao
ya kijamii ni mizuri kutusaidia kupashana habari , nafikiri hilo unalijua
vizuri sana. lakini kwa watu wenye kiu na hasira ya mafanikio wanaamini sana
kwamba mitandao ya kijamii imewekwa kwa ajili ya kuwapotezea au kuwaibia muda
wao.
Hivyo
kwa kulijua hilo wanaitumia mitandao ya kijamii kwa hesabu sana na kwa muda
maalumu. Tofauti na watu wengine wanavyofanya, wao wana muda maalumu kuingia
kwenye mitandao hiyo ya kijamii, lakini sio kuingia hovyo hovyo tu.
6. Kutokujali sana mambo ya wengine.
Kitu
kikubwa kilicho ndani ya watu wenye kiu ya mafanikio na kinachowapelekea wafanye
mambo yao kwa utofauti na kuleta mafanikio, ni kule pia kutokujali mambo ya
watu wengine. Hawajali sana fulani anafanya
kitu gani.
Kila
wakati ni watu ambao wanajihusisha sana na ndoto zao na kuangalia ni wapi
pa kuboresha hadi kuleta matokeo. Hawajali wanakoselewa vipi na nani. Huamua
kusonga mbele bila kujali vitu kama hivyo na hatimaye hufanikiwa.
7. Wasikilizaji wazuri wa mambo na
kuchukua hatua.
Kila
wakati watu wenye nia ya kufikia mafanikio,
ni wasikilizaji wazuri sana kwa wengine wanasema nini. Ni watu ambao wanajua
kusema sana kunapoteza mafanikio, hivyo huamua kusikiliza na kuweka kumbukumbu za
kimaandihi vile vitu ambavyo vinawasaidia.
Ndio
maana ukiwafatilia wengi ni watu ambao wapo makini na si waongeaji sana. Huamua
kujifunza kupitia maisha ya wengine, huchukua vitu vya msingi vinavyoweza
kuwasaidia kufanikiwa.
Kila
la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jul 19, 2017
Jinsi Ya Kujitoa Kikamilifu Na Kufanya Maisha Yako Kuwa Bora Na Ya Mafanikio.
Hitaji
lako la kwanza ambalo unatakiwa ulijue katika safari yako ya mafanikio ni
kwamba, unahitaji sana kujifunza, kukua na kuendelea kufanikiwa yaani learn,
grow and develop. Hilo ndilo hitaji lako la kwanza.
Kila
wakati utahitaji ujue ni nini ufanye ili kuboresha maisha yako au ufanye nini cha zaidi ili hicho
unachokifanya kikuletee matokeo makubwa na unayoyataka kwenye maisha yako leo
na hata kesho.
Unaweza
ukaanza kuboresha chochote kile hata kwa kidogo sana. Unaweza ukaanza kuboresha
tabia zako, unaweza ukaanza kuboresha biashara
yako au hata maarifa yako kwa kujisomea zaidi na zaidi kila siku.
Kuendelea
kujitoa kikamilifu na kuboresha maisha yako linatakiwa liwe zoezi endelevu, kila siku jiulize, ni kwa namna
gani unaweza ukafanya siku yako ikawa bora, ni namna gani unaweza kuboresha
maisha yako kuliko jana?
Kufanya
mabadiliko na kubadilisha maisha yako, ni jambo ambalo linachukua muda( Becoming
a master takes time). Unatakiwa kujifunza na kuchukua mazoezi tena na tena ili
kuwa mbobezi. Hakuna kikubwa ambacho utakachofanikisha kama usipofanya hivyo.
Hakuna
mpaka wa kuboresha maisha yako, hakuna mpaka unaokuzuia wewe kukua kimafanikio.
Kila iitwapo leo, endelea kuboresha maisha
yako kwa jinsi unavyoweza. Ukiendelea kufanya hivyo, uwe na uhakika
utafanikiwa.
Jiulize
kipi kinachokuzuia ili usifanye maisha yako yawe bora? Angalia usikwamishwe na
hofu wala usikwamishwe na tabia za kuahirisha mambo kila wakati. amua kufanya
kitu kitakachoyafanya maisha yako yaonekane ya maana.
Kama
nilivyosema mwanzoni mwa makala haya, unahitaji sana kujifunza, kukua na
kuendelea kufanikiwa. Kila siku jiulize, je, umejifunza nini? Je, kutokana na
kujifunza huko kuna hatua yoyote unayopiga?
Kama hujifunzi
elewa hautaweza kukua, wala hautaweza kufanikiwa. Maisha ya mafanikio ndivyo
yapo hivyo, yanahitajji kuweka juhudi nyingi katika .katika kila eneo ili uweze
kupiga hatua za kimafanikio.
Kila la
kheri katika safari ya mafanikio yako na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.comkila siku kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jul 18, 2017
MAFANIKIO TALK: Faida za Kushiriki Maonyesho Yoyote Yale Ya Kibiashara.
Nikualike
kwa mara nyingine tena katika kipindi hiki cha mafanikio talk ambacho kinakujia
kila siku ya jumanne. Na siku ya leo tupo Patrick
Kyando (star intergrated) kutoka Makambako.
Licha ya kuzungumza naye mambo mbalimbali ya kimafanikio , yeye yeye
aliweza kutushirikisha faida za mfanyabiashara kushiriki
katika maonesho.
Kwani
wafanyabiashara wengi na wasio wafanyabiahara wamekuwa hawafahamu umuhimu wa
kushiriki katika maonesho ya kibiashara ambayo yamekuwa yakifanyika ndani na nje
ya Tanzania. Kama wewe ni miongoni mwa watu hao makala haya yanakuhusu, hivyo
ni vyema twende sawa aya kwa aya.
Kuna
faida zaidi ya tatu kutangaza biashara ktk maonyesho yoyote :
1. Ukishiriki katika maonesho yeyote yale ya
kibiashara na ukiwa na
bidhaa ni rahisi kuuza kwa kuwa huwa kunakuwepo na watu tofauti toka sehemu
tofauti ambao si rahisi sana kukutana nao ukiwa kwenye kituo chako cha
biashara. Hivyo ni muhimu kwako kuchangamkia fursa ya maonyesho kila
yanapojitokeza ili kuweza kufaidika na faida hii.
2. Ukishiriki katika maonesho, ni fursa kwako
kwa sababu unafungua ukurasa mpya kupata wateja wapya hata kupelekea kupata ‘network’ ya kibiashara, na ‘network’ hii huwa ni endelevu kwa sababu utaweza kupata mawasiliano
endelevu ya watu tofauti tofauti.
3. Utajifunza kutoka kwa wengine
wanaozalisha au kuuza bidhaa kama zako kwasababu wao wanakuwa na nafasi ya kuzielezea kwa
uwazi zaidi.
4. Utajifunza vitu tofauti vya kibiashara na
hasa mambo ya kiteknolojia ambayo wewe mwanzoni mwa biashara hiyo ulikuwa
huijui.
5. Pia taasisi mbali mbali za serikari
zinakuwepo kutoa elimu na huduma pia huwa
ni rahisi zaidi kuzipata eneo hilo la maonyesho kuliko wakiwa kwenye
vituo vyao vya kazi.
6. Makampuni mengi hutangaza ofa za
maonyesho husika hivyo ni nafasi ya kupata bidhaa kwa bei za ndogo zaidi.
Hivyo ni vyema na wasaa mzuri kwa wewe
mfanyabiashara na usiye mfanyabiashara kuweza kushiriki kwa namna moja ama nyingine katika maonyesho
ya kibiashara kwani kuna faida lukuki.
Kwa niaba ya uongozi wa mtandao huu wa dira ya
mafanikio, nipende kumshukuru sana ndugu Patrick
Kyando wa star intergrated kwa
somo hilo zuri.
Mpaka
kufikia hapo sina la ziada nikutakie siku njema na mafanikio mema. Tukutane
jumanne ijayo katika kipindi hiki cha mafanikio talk. Kama unatamani siku ya jumanne ijayo tuweze kutupa
somo kutoka kwako tuma neno mafaniko
talk kwenda 0757 909 942 au
tuma neno hilohilo kwenda e-mail yetu dirayamafaniko@gmail.com
nasi tutakutafuta kwa ajili ya mahojiano mubashara.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kwa ajili ya kujifunza na
kuhamasika.
Habari
njema, kama wewe ni mfugaji wa kuku, kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana na DM POULTRY FARM PROJECT, hawa ni
wauzaji wa vifaranga vya kuku wa KIENYEJI
ASILIA, SASSO NA KUROILER. Bei ya kifaranga kimoja ni Tsh 2000 pia kuna punguzo la bei kwa wateja watakaonunua vifaranga
500 na kuendelea. Pia tunatoa elimu ya ufugaji wa kisasa kwa wateja wa
vifaranga. Hii elimu ni bure. Kwa mawasiliano zaidi tupigie simu namba 0767 04 80 35/ 0686 14 10 97. Tupo
TANGA na vifaranga unatumiwa popote pale ulipo kama upo nje ya TANGA.
Ndimi
afisa mipango Benson Chonya,
bensonchonya23@gmail.com.
Jul 17, 2017
Muda Ulionao Ndio Kila Kitu Kwenye Maisha Yako.
Moja
ya kitu cha thamani sana maishani mwetu
ni muda. Hata hivyo ingawa huwezi kuona muda, huwezi kuugusa muda, lakini muda
unaongoza maisha yetu na kuamua maisha yetu yaweje yaani ya mafanikio au ya
kushindwa?
Muda
unaweza kufanya chochote kwenye maisha yako. Kama leo hii ukitumia dakika 20 tu
kufanya mazoezi baada ya miezi sita mwili wako unakuwa umebadilika. Leo pia
ukiamua kujifunza vitu kwa nusu saa tu, baada ya muda unakuwa mtaalamu.
Kipi
ambacho hakiwezi kuleta matokeo mbele ya muda, ikiwa muda huo utatumiwa kwa
busara? Muda ndio mwisho wa kila kitu, muda unasawazisha kila kitu, ‘time
is a greater equalizer’. Kama unaona maisha yako magumu, jipe muda na
fanya kazi kweli, kila kitu kitabadilika.
Leo
hii pengine unaitwa mtu wa kushindwa, au pengine unaitwa ni mtu usiyeweza kitu,
usiumie juu ya hilo, amua sasa kutumia muda wako kwa busara kuwekeza kwa
uhakika katika eneo unalotaka. Miaka mitatu au mitano mbele utakuwa mtu wa
tofauti sana.
Jifunze
kuufanya muda wako ukupe matokeo chanya. Jifunze kuufanya muda wako ukufanyie
kazi kwa faida, ‘PUT TIME TO WORK.’ Ukizingatia hilo maisha yako yatabadilika
hata kama hayataki, ila usiwe na haraka sana na mabadiliko hayo, JIPE MUDA.
Jul 16, 2017
Yafanye Maisha Yako Yawe Ya Mafanikio Kwa Kuanza Kuchukua Hatua Hii…
Kama unakumbuka kupitia historia ujenzi wa piramidi
kubwa za Misri, haukuanza kwa kujengwa na mawe mengi kwa pamoja, bali zilianza
kujengwa kwa jiwe moja tu, tena jiwe hilo ambalo liliwekwa na mhudumu mmoja
katika siku hiyo ya kwanza ya ujenzi.
Hilo jiwe moja liloanza kujenga piramidi hizo
kubwa kihistoria na kupelekea mamilioni ya watu leo hii kutembelea Misri, lilionekana
jiwe hilo ni la kawaida tu na wala halina chochote na wala mchango wake haukuweza
kuonekana mara moja.
Hata yule mfanyakazi mtumwa ambaye aliweza
kuweka lile jiwe la kwanza katika kujenga piramidi hizo hakuweza kutambuliwa
wala kuonekana ana mchango wowote zaidi alizidi kuonekana ni mtumwa tu na asiye
na maana yoyote.
Pamoja na kwamba umuhimu wa kujenga piramidi
haukuonekana na mtu yeyote, na pia wala hakuna aliyejali ni nini kinaendelea,
lakini kutokana na nguvu ya kuanza mwisho wa siku piramidi zilisimama na
kushangaza watu wengi.
Kama nilivyotangulia kusema, leo mamilioni ya watu
duniani wanasafiri tena kwa gharama kubwa kwenda kuangalia piramidi hizo za
kihistoria ambazo ni matokeo ya kazi iliyoanzishwa na uwekaji wa jiwe moja
moja.
Hata kwenye maisha yetu inabidi tuelewe kwamba,
siku zote kuanza jambo lolote ni kitu kigumu sana. Mara nyingi inahitjika
juhudi sana ili kuanza jambo, vinginevyo huwezi kuanza kabisa na pia najua unaelewa vizuri hili kuwa kuanza ni kugumu.
Kama wewe usipokuwa makini, utakuwa unatumia muda mwingi
sana kufikiria kuhusu kuanza hasa ukifikiria ukubwa wa jambo unalotaka kulifanya
na kujikuta unakata tamaaa au kuahirisha kwamba nitafanya siku nyingine.
Ni rahisi sana kupata msisimko na hamasa mara tu
pale unapojiwekea malengo yako, lakini kwa wengi linapokuja suala la kuchukua
hatua hapo ndipo ugumu unapoanza na wengi husau kabisa kwamba siri ya mafanikio
yao ipo kwenye kuanza.
Ili ufanikiwe unatakiwa uelewe hivi, chochote
kitu kikubwa unachotaka kukitimiza, kinaanza na wewe kuchukua hatua ya kufanya
au kinaanza na wewe kuchukua hatua ya
kuweka jiwe la kwanza ili kukamilisha
piramidi ya mafanikio yako.
Mwanzoni unapoanza kujenga mafanikio yako,
unaweza ukaonekana si kitu wala huna chochote na hakuna unachofanya, lakini
elewa huo ni mwanzo. Maajabu ya maisha yako ndipo yanapoanzia hapo kwa wewe
kuamua kufanya.
Hutasogea na hautafanya mabadiliko yoyote ya maisha
yako, ukiamua kutulia bila kufanya kitu. Fanikisha maisha yako na kuwa ya mafanikio
kwa kuanza kitu kitakachokusogeza kwenye maisha yako.
Kila la kheri katika kufikia
mafanikio makubwa na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA
MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)