Jul 6, 2017
Usikatishwe Tamaa Kwa Kukataliwa Na Dunia.
Kama
upo kwenye mbio sahihi za mafanikio, kati ya kitu ambacho unatakiwa kujifunza
sana ni kutokukatishwa tamaa na kukataliwa. Upo wakati utakataliwa kwenye
biashara yako na kukosa wateja.
Hiyo
haitoshi kuna wakati utakataliwa sana kwa kazi unayoomba na pia kuna wakati
unaweza kukataliwa na mazingira na kushindwa kuvuna hata kile ulichopanda. Hiyo
ni mifano michache kati ya mingi.
Kitu
cha kujiuliza kukataliwa kwa namna yoyote kunapotokea kwako, huwa
unachukuliaje? Huwa unajiona ni mpumbavu au mjinga au unakuwa unatumia kukataliwa
huko kama sababu ya kusonga mbele?
Kwa
wengi sina shaka sana kukataliwa kokote kunapotokea, ndani mwao hujisikia
vibaya sana kiasi cha kwamba kutokutamani kuendelea tena. Je, hi ndiyo hali
ambayo hutokea hata ndani mwako?
Usichokijua
wapo watu wengi sana ambao walikataliwa mwanzoni na kazi zao lakini leo ni
mabilionea. Sylvester Stalone alimaarufu Rambo alishindwa kupata uzamini wa
kutoa filamu yake ya kwanza hadi aliuza mbwa wake.
Naye
pia Alexander Graham Bell alipopeleka kwa mara ya kwanza kuiza teknolojia yake
ya Simu kwa Carl Orton ambaye ni mmliki
wa Western union aliambiwa kampuni kubwa kama yake haiwezi kununua doli kama
hilo.
Hebu
jiulize ni kitu gani ambacho alikuwa akiwaza Rambo pale alipoambiwa hawezi
kuigiza, au ni kitu gani alichokuwa akifikiri Bell pale alipoambiwa kazi yake
ni hovyo na kufananishwa na doli?
Kwa ujasiri
na ushujaa, hakuna aliyekata tamaa, waliamua kusonga mbele, leo hii dunia nzima
inatumia simu na leo hii wengi wanamfahamu Rambo. Katika mazingira yoyote
ulionayo hapo ulipo, usikubali kukatishwa tamaa na kukataliwa, simamia ndoto
yako kikamilifu.
Ni kweli
kuna wakati utapita katika mazingira magumu na kuonekama kila kitu kimekataa kabisa
kwenye maisha, lakini hiyo usichukulie kwamba ndio uhalisia ulivyo. Chukua jukumu
la kuendelea kusonga mbele.
Asikuzuie
mtu kwa maneno yake, yasikuzuie mazingira yoyote yale, kitu cha msingi
usikubali kushindwa kwenye akili yako kwanza, ukishindwa huko na huku nje
utakuwa umeshindwa. Kabisa.
Hapo
ulipo unajijua vizuri hali uliyonayo, hali hiyo kama huipendi sana amua
kuibadili mara moja, kama unaona huoni matokeo ya haraka usikate tamaa, vumulia
mambo yatakaa sawa kadri siku zinavyokwenda.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni wako rafiki
katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.