Jul 23, 2017
KITABU; The Success System That Never Fails (Mfumo Wa Mafanikio Ambao Haushindwi)
Kwenye kitabu hiki mwandishi W. Clement Stone anaeleza upo mfumo katika maisha , ambapo
ukiutumia mfumo huo vizuri, utayafanya maisha yako yasiwe ya kushindwa kamwe,
bali yawe ya mafanikio siku zote.
Katika
mfumo huo mwandishi ameongelea mfumo usioshindwa katika maisha jinsi ulivyokuwa
wa muhimu katika maisha yako. Na mfumo huo umebebwa sana na mambo makubwa
matatu ambayo ni;-
Hatua/vitendo
(Action)
Hapa
inakubidi kuchukua vitendo kwa kitu unachotakiwa kufanya. Unatakiwa kuchukua
vitendo bila kujali kitu. Kitu unachokifanya kama umeamua kukifanya, kifanye.
Acha kupoteza muda chochote unachokiamini, hebu kifanye bila woga.
Kujua
namna ya kufanya (Know-how)
Kuchukua
hatua kwenye jambo lolote yenyewe haitoshi peke yake, unatakiwa sasa kujua
namna ya kufanya kitu hicho tena. Unatakiwa kujua namna ya kufanya katika hali
ambayo itakupa matokeo sahihi.
Maarifa
(Knowledge)
Maarifa
ni kitu cha msingi katika kufanikisha jambo lolote lile. Lazima uwe umeiva kwa
maarifa ya kutosha ili yakusaidie kufanya mambo yako kwa usanifu wa hali juu na
kukupa mafanikio. Ukikosa maarifa ya msingi kwa jambo lolote utashindwa.
Hayo
ndiyo mambo matatu ya msingi sana ambayo mwandishi ameyasititiza na kuyatilia
mkazo karibu katika kitabu chake chote. Mambo mengine ya kujifunza kwenye
kitabu hiki ni kama haya yafuatayo;-
1.
Maamuzi mazuri katika maisha yanaendana na kuchukua hatua. Kama huchukui hatua,
halafu ukasema eti una maamuzi mazuri, basi elewa unajidanganya na maamuzi hayo hayana maana yoyote kwako kwa
sababu hayawezi kukusaidia.
2.
Kama umeamua kufanya kitu fulani, iwe ni biashara , masomo au kitu chochote ambacho
kipo kwenye malengo yako, usirudi nyuma hadi umefanikisha kitu hicho.
Haijalishi njiani umekutana na changamoto nyingi kiasi gani, pambana mpaka
upate kile kitu ambacho ulikuwa umelenga kukifanikisha.
3. Unaweza
ukaongeza uwezo mkubwa wa kufanikiwa ikiwa utatumia kanuni za mafanikio na
kuzifanyia kazi kila siku. Unaweza pia ukapunguza hali ya kushindwa sana kwenye
maisha yako, ikiwa kama utaendelea kutumia kanuni hizo hizo za mafanikio. Kama
utafanya kinyume na hapo jiandae na anguko kubwa la maisha yako.
4.
Mafanikio yanakuja kwa wale wote wanaojaribu hiki au kile mara kwa mara bila
kujali wanashindwa kwa kiasi gani. Huwezi kuwa mshindi kama umekaa tu. Jaribu
kwa jinsi unavyoweza ili kujenga mafanikio yako.
5.
Kila wakati hakikisha unayatawala mazingira yako na sio mazingira yakutawale.
Epuka kila hali iwe mazingira au watu wakutawale. Hakikisha unatawala mazingira
yako vizuri ili yakupe nguvu ya kushinda.
7.
Kufikiri peke yake hakuwezi kukafanya wewe ukashinda uoga ulionao. Kitu
kitakachoweza kukufanya ukashinda uoga ulionao ni zile hatua unazochukua. Hatua
au vitendo ni dawa pekee ya kuondoa hofu au woga wowote ule kwako.
8. Kama
hujiwekei akiba yoyote, elewa kabisa ndani yako umekosa mbegu ya mafanikio.
Wanaojiwekea akiba hata kama ni pesa kidogo sana, hiyo inawasaidia kuweza
kukuza mbengu ya mafanikio iliyo ndani mwao. Angalia watu wengi ambao hawaweki
akiba, maisha yao sio mazuri na kufanikiwa inakuwa ni ngumu.
9.
Moja ya sifa kubwa ya mafanikio unayotakiwa kuwa nayo na kuiendeleza ni TABIA zako ulizonazo. Ukiwa na tabia
sahihi, uwe na uhakika zitakuongoza hadi kuweza kufikia mafanikio yako.
10.
Ukishakijua vizuri kile unachokitaka kwenye maisha yako, tafuta maarifa na
mbinu za kukichimba kitu hicho ndani, nje mpaka ukielewe vizuri. Kukijua vizuri
kitu hicho ndani, nje itakupa wewe uwezo wa kukifanya kwa ufasaha sana na
kupata matokeo chanya.
11.
Nguvu ya kuendelea kufanya jambo lolote itazidi kuchochewa ndani yako kama
moto, ikiwa ndani yako pia una hasira, imani ya kufanikiwa na pengine maumivu
ya kuumizwa na wengine. Kama ndani yako unavitu hivyo, itachochea nguvu kubwa
iliyoko ndani yako ya kufanikiwa na utafanya kila linawezekana kuhakikisha
unafanikiwa.
12.
Unapokuwa una hamu na hamasa ya kufikia malengo yako, ni lazima kutafuta njia
na kila aina ya maarifa yatakayokusaidia kufikia malengo yako. Maarifa hayo
utayapata kutoka kwa watu ambao tayari wameshafanikisha hicho unachokitaka au
hata kwenye vitabu mbalimbali vya kimafanikio.
13.
Ili ukijue vizuri hicho unachotaka kukifanya ni lazima uchuke hatua. Huwezi
kukijua kitu hicho kwa kusoma peke yake ni muhimu kuchukua hatua zitakazo kupa
uzoefu ambao uzoefu huo utapelekea wewe kujua namna ya kufanya kwa ubora wa
hali ya juu.
14.
Kama kuna jambo ambalo umelianzisha hata kama linakuletea utata endelea
kulifanya. Ikiwa kama utasimama inachukua muda mrefu tena kulianza jambo hilo
na kuwa kwenye mwendo sahihi kuliko ungeendelea na safari. Siri ya kuendelea
ipo kwenye kufanya sasa hicho unachotaka kukifanya. Acha kujisemea kuwa
utafanya kesho au lini, fanya sasa.
15. Siku
zote mafanikio ya mtu yanaanzia kwenye akili yake. Unachotakiwa kufanya ni
kuangalia fursa zinazokuzunguka au changamoto zinazoizunguka jamii yako na
kisha baada ya hapo tafutia majibu yake na utafanikiwa.
.16.
Maadili bora ni msingi mkubwa wa mafanikio yoyote. Kushindwa kwingi kunaanza
pale mtu anapokosa maadili na kujiingiza kwenye tabia za hovyo kama ulevi,
zinaa na hata wizi. Mafanikio hayajengwi kwenye misingi kama hiyo hata siku
moja.
Chukua
hatua kila siku kujifunza haya muhimu uliyojifunza kwenye kitabu hiki.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.