Jul 13, 2017
Mambo Manne (4) Ya Kufanya Kila Siku Ili Kutengeneza Utajiri Endelevu.
Kwa kawaida
yapo mambo ya msingi sana ambayo kwa mtu yoyote mwenye nia ya kuwa tajiri
lazima ayafanye mara kwa mara au kila siku ili kufikia utajiri huo. Pasipo kufanya
mambo hayo hakuna kitu ambacho kinaweza kusimama na kuleta mafanikio.
Kwa wengi
ambao hawayajui mambo hayo ndio hujikuta wakiishi maisha magumu karibu kila
siku yasiyo na unafuu. Kwa kuwa DIRA YA
MAFANIKIO haina choyo na wewe, leo tutajifunza pamoja mambo ya kufanya kila
siku ili kutengeneza utajiri endelevu.
1.
Toa visingizio vyote.
Kati
ya jambo ambalo nimekuwa nilikilisema sana kwa mtu yeyote anayetafuta mafanikio
ni kuachana na visingizio. Hilo liko wazi hivi, hauwezi kuwa tajiri kama wewe
ni mtu wa visingizio kila siku, hapo elewa kabisa mafanikio kwako hayapo.
Sababu
unazozitoa kwamba hujafanikisha jambo hili au lile, kweli ni nzuri, lakini
haziwezi kukusaidia, kwani dunia haielewi sababu hizo zaidi ya kukutaka wewe ulete matokeo ya mafanikio.
Hata
kama ukiendelea kutoa sababu haitasaidia kitu, kikubwa, amua kutoa visingizio
vyote na kama ni nguvu, tumia nguvu zako zote na kuhakikisha unaweza kufanikiwa
kwa hicho unachokifanya na kujenga utajiri mkubwa kwenye maisha.
Jenga tabia ya kuwekeza maeneo mengi utafanikiwa. |
2.
Wekeza.
Jambo
lingine mbali na kutoa visingizio
unalotakiwa kulifanya maishani mwako na kutengeza utajiri ni kuwekeza.
Inatakiwa kila wakati upime na kuangalia ni wapi uwekeze nini ambacho kitakua na
manufaa.
Uelewe
tu kwamba utajiri unajengwa kwa kuwekeza, utajiri haujengwi kwa mshahara mkubwa,
utajiri haujengwi kwa njia za mkato mkato kama unavyofikiri, siri kubwa ya
utajiri mwingi ni kuwekeza.
Ikiwa
hujaanza kuwekeza kwa uhakika, anza leo kuwekeza chochote unachoona kinaweza kikakupa
pesa kwa hapo baadae na kufanikiwa kujenga utajiri mkubwa. Ukifanya hivyo,
maisha yako yatabadilika sana.
3.
Piga hatua kila siku.
Usikubali
kusimama hapo ulipo hata siku moja, jitahidi sana kwenye maisha yako kupiga
hatua kila siku. Piga hatua za kuelekea kwenye ndoto zako, yaani fanya kitu angalau
kidogo ambacho kitakusogeza karibu kabisa na ndoto zako.
Unapofanya
hivi siku hadi siku, utashangaa unasogea pasipo hata kujua. Maisha kwa jinsi
alivyo yamekaa katika hali ya mwendo. Hivyo unatakiwa kuchukua hatua za
kuelekea mbele bila kujali hatua hizo ni kidogo au kubwa.
Hata
watu wenye mafanikio, karibu kila wakati ni watu wa kuchukua hatua, hufanya
hiki na kile, ilimradi kuhakikisha wanasogea pale walipo. Ukifanyia kazi hili
kila siku, uwe na uhakika hivyo ndivyo utakuwa unajenga utajiri wako.
4.
Jenga matandao wa kimafanikio.
Mafanikio
hayawezi kuja kwa kuyapata peke yako. Jitahidi sana kujenga mtandao wa
kimafanikio ambao utakusaidia kila siku. Unapokuwa na mtandao huu inakuwa ni rahisi
kupiga hatua kuliko ungekuwa huna.
Iko hivyo
kwa sababu, utapata ushirikiano mkubwa, isitoshe mtandao wako huo kuna wakati
utakupa habari za fursa kiasi cha kwamba hiyo pekee inakurahisishia wewe kujua
maeneo ya kuwekeza ambayo hukuyajua.
Kwa kuhitimisha,
huhitaji kujiuliza sana ufanye nini ili uwe tajiri, hebu kwa kuanzia fanya
mambo hayo. Kama ukifanya mambo hayo kwa uhakika na usipokuwa na pesa ndani ya
miaka mitano, basi naweza nikasema wewe ndio basi tena.
Nikutakie
kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com
kila siku kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni wako
rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.