Jul 19, 2017
Jinsi Ya Kujitoa Kikamilifu Na Kufanya Maisha Yako Kuwa Bora Na Ya Mafanikio.
Hitaji
lako la kwanza ambalo unatakiwa ulijue katika safari yako ya mafanikio ni
kwamba, unahitaji sana kujifunza, kukua na kuendelea kufanikiwa yaani learn,
grow and develop. Hilo ndilo hitaji lako la kwanza.
Kila
wakati utahitaji ujue ni nini ufanye ili kuboresha maisha yako au ufanye nini cha zaidi ili hicho
unachokifanya kikuletee matokeo makubwa na unayoyataka kwenye maisha yako leo
na hata kesho.
Unaweza
ukaanza kuboresha chochote kile hata kwa kidogo sana. Unaweza ukaanza kuboresha
tabia zako, unaweza ukaanza kuboresha biashara
yako au hata maarifa yako kwa kujisomea zaidi na zaidi kila siku.
Kuendelea
kujitoa kikamilifu na kuboresha maisha yako linatakiwa liwe zoezi endelevu, kila siku jiulize, ni kwa namna
gani unaweza ukafanya siku yako ikawa bora, ni namna gani unaweza kuboresha
maisha yako kuliko jana?
Kufanya
mabadiliko na kubadilisha maisha yako, ni jambo ambalo linachukua muda( Becoming
a master takes time). Unatakiwa kujifunza na kuchukua mazoezi tena na tena ili
kuwa mbobezi. Hakuna kikubwa ambacho utakachofanikisha kama usipofanya hivyo.
Hakuna
mpaka wa kuboresha maisha yako, hakuna mpaka unaokuzuia wewe kukua kimafanikio.
Kila iitwapo leo, endelea kuboresha maisha
yako kwa jinsi unavyoweza. Ukiendelea kufanya hivyo, uwe na uhakika
utafanikiwa.
Jiulize
kipi kinachokuzuia ili usifanye maisha yako yawe bora? Angalia usikwamishwe na
hofu wala usikwamishwe na tabia za kuahirisha mambo kila wakati. amua kufanya
kitu kitakachoyafanya maisha yako yaonekane ya maana.
Kama
nilivyosema mwanzoni mwa makala haya, unahitaji sana kujifunza, kukua na
kuendelea kufanikiwa. Kila siku jiulize, je, umejifunza nini? Je, kutokana na
kujifunza huko kuna hatua yoyote unayopiga?
Kama hujifunzi
elewa hautaweza kukua, wala hautaweza kufanikiwa. Maisha ya mafanikio ndivyo
yapo hivyo, yanahitajji kuweka juhudi nyingi katika .katika kila eneo ili uweze
kupiga hatua za kimafanikio.
Kila la
kheri katika safari ya mafanikio yako na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.comkila siku kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.