Jul 14, 2017
Misingi Bora Ya Kufuata Ili Kujenga Afya Ya Mwili Wako.
Katika maisha moja ya kitu
cha msingi sana ambacho hutakiwi kukikosa ni afya bora. Kosa yote, lakini
usikose afya bora, afya bora ina muunganiko na mambo mengi sana kwenye maisha
yako ikiwa pamoja na mafanikio.
Naomba uelewe hivi, unapokuwa
hauna afya nzuri, hakuna ambacho unaweza ukakifanikisha, utashindwa kwenye
mambo mengi kwa sababu ya kushindwa kuweza kuyafanya kwa ufanisi kutokana na
tatizo la afya yako.
Kwa mantiki hiyo, mpaka hapo unaona ni kwa namna gani afya ilivyokuwa
ya muhimu sana kwenye maisha yako. Sio suala la kuhoji tena ni lazima uwe na
afya bora. Ni kwa namna gani utaweza kutengeneza afya bora?
Ifuatayo Ni Misingi Bora Ya
Kufuata Ili Kujenga Afya Ya Mwili Wako.
Msingi
wa kwanza, kunywa maji kwa wingi.
Maji mengi mwili yanasaidia
mwili wako kuwa katika hali nzuri wakati wote na kusababisha baadhi ya viungo
kufanya kazi kwa ufasaha. Hivyo, unalazimika kunywa maji kwa wingi kila wakati
ili kuweza kulinda afya ya mwili wako ili iwe bora wakati wote, kinyume cha
hapo itakuwa ni shida kwako.
Kunywa maji kwa wingi kila siku. |
Msingi wa pili, soma kabla hujalala.
Unaposoma kitu kipya kabala
hujalala unaifanya akili yake iende kupumzika huku ikiwa na wazo jipya au kitu cha
kufanyia kazi usiku wote. Ukumbuke hapa mawazo yako ya kina yanafanya kazi muda
wote kwa saa 24 . Soma kitu kipya chanya angalau nusu saa kabla hujalala kila
siku itakusaidia sana.
Msingi wa tatu, fanya tahajudi (Meditation).
Tafuta eneo lilotulia na
kila siku jitahidi kufanya tahajudi ama ‘meditation.’ Hiki ni kipindi ambacho
unatakiwa ukae kwa utulivu ukitafakari maisha yako na kutafakari kile
unachokitaka katika maisha. Unaweza ukafanya tahajudi/meditation angalau hata
kwa dakika 15 kila siku.
Msingi wanne, fanya mazoezi.
Unatakiwa pia ujenge tabia
ya kufanya mazoezi kila siku ili kuupa mwili wako afya. Fanya mazoezi ya
kukimbia, fanya mazoezi ya kuruka au fanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito. Ukifanya
mazoezi kila siku na ikawa ndio kitu endelevu mwili wako utakaa katika afya
nzuri sana kila wakati.
Msingi wa tano, kula chakula bora.
Mwili wako haujengwi kwa matofali,
mwili wako unajengwa kwa chakula safi. Kwa kulijua hili kila wakati jitahidi sana
kuulisha mwili wako chakula ambacho kitakusaidia wewe kuweza kuujenga mwili
wako kwa afya bora. Tafuta vyakula safi
vitakavyo ulinda mwili wako na magonjwa.
Kimsingi, afya yako
haijengwi kwa kubahatisha. Afya inajengwa kwa kuzingatia msingi ya afya bora
kama ilivyoainishwa katika makala haya ya leo. Usisubiri hadi uende kwa
daktari, zingatia mambo haya nawe utakuwa na afya bora.
Endelea kujifunza kupitia
dira ya mafanikio.blogspot.com kila siku kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.