Jul 10, 2017
Jifunze Namna Ya Kupiga Hatua Za Kimafanikio Kila Wakati.
Moja
kati ya siri kubwa iliyopo katika mafaikio yako ni vile utakavyoamua wewe
kuchukua hatua kwa kile kidogo au kikubwa ambacho unakifahamu. Huwezi kusema
unataka kufanikiwa wakati maarifa uliyonayo, ambayo ndiyo nguzo ya mafanikio
hayo unayaweka pembeni.
Hata
hivyo watu wengi wanaamini ya kwamba siri kubwa ya kufanikiwa kwao ipo katika
kuendelea kujifunza vitu vipya pekee, jambo hili kwa macho mawili huenda likawa
ni sawa, ila kwa jicho la tatu kufanya hivyo pekee yake haitoshi.
Nimesema
haitoshi kwa sababu watu wengi wana maarifa mengi sana na ya kutosha katika halmashauri zao za vichwa, ila
wao tatizo linakuja kuweza kubadilisha maarifa hayo kuwa bidhaa au huduma
ambazo zitawaingizia wao kipato.
Zijue hatua za mafanikio yako. |
Na
ukweli ambao hauna kificho ni kwamba kitu
pekee kitakacho kufanikisha kuweza kufika mbali zaidi kimafanikio si wingi wa
maarifa ya mafanikio unayoyapata kila siku. Mafanikio yako utayapata kwa wewe
kuamua kuyatumia maarifa hayo tena kwa uhakika.
Lakini
pia jambo la msingi ambalo huna budi kujiuliza kila wakati ni hili, Jiulize, tokea
uanze kujifunza juu ya mafanikio, umechukua hatua kiasi gani? Au umebakia kuwa
ni mtu wa kushangilia na kuwaacha wengine wachukue hatua za kimafanikio? Mara
baada ya kujiuliza naomba usinipe majibu, kwani ukweli wa majibu hayo unao
wewe.
Lakini
kama umepata majibu ya kwamba hakuna jambo lolote lenye heri ambalo umelifanya
tangu uanze kujifunza mambo ya mafanikio ni vyema kuanzia sasa kuamua kuwa mtu
wa vitendo zaidi kuliko maneno.
Kwani
yale maneno ambayo umekuwa ukijfariji kila wakati ya kwamba nitafanya kesho, ni
maneno yenye faraja na yenye kuleta msisimko mzuri maishani. Ila ukweli ni
kwamba maneno hayo hayo pasipo kuweka
katika matendo ni maneno yajengayo majuto maishani, hivyo ni vyema kuwa ni mtu wa kusema kwa matendo kuliko maneno.
Kwani upo usemi usamao ya kwamba matendo ni maneno halisi.
Hivyo
kabla sijaweka nukta siku ya leo naomba
niseme ya kwamba kwa kila kitu ambacho unajifunza kila siku ni heri kuchukua
hatua zaidi, kwani ni heri kuwa na hamsini nzima kuliko kuwa na mia mbovu. Na
ukitaka kufanikiwa zaidi maishani ni vyema kuacha maneno na uweke vitendo.
Imeandaliwa na
mtandao huu wa dira ya mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.