Jul 9, 2017
Jenga Nguvu Kubwa Ya Mafanikio Yako Kwa Kufanyia Kazi Mambo Haya Matatu.
1. Kila
wakati tafuta mafanikio yako kwa kufanya kile unachokipenda. Unapofanya kile
unachokipenda utake usitake ni lazima utajituma tu bila hata kusukumwa. Kupenda
kile unachokifanya, kazi kwako itakuwa ni kama mchezo na kwa kifupi ni rahisi
tu kuwa mlevi wa kazi yaani ‘workaholic’
hasa kama unafanya kile unachokipenda.
Mara
nyingi unapoona watu wanasukumwa sana katika kazi zao, na ni watu ambao kama
hawajitumi ni rahisi kujua watu hao wanafanya kazi ambazo hawazipendi na wala
hazipo kwenye mioyo yao. Wanafanya ili mradi siku ziende. Timiza mipango
uliyojiwekea, kwa kuchagua kile unachokipenda kwenye maisha yako na kifanye.
2. Je,
inafika wakati wakati katika maisha yako, wakati unang’ang’ana na kutimiza
ndoto zako unajiona kama vile ndoto zako zinakuchanganya na kukukosesha raha?
Kama
iko hivyo kwako, ni ishara tosha kabisa kwamba hutaki maisha yako yabaki hivyo,
yaani kuna kitu ambacho unakitafuta na unataka kukibadili mara moja.
Mafanikio
katika maisha hayaendi kwa watu walioridhika bali yanawafikia watu ambao kila
wakijiangalia wanajiona hawana mafanikio kabisa.
3. Kipo
kitu ambacho lazima unatakiwa kukifanya haijalishi una huzuni au unachangamoto
nyingi sana, lakini unayo nafasi ya kufanya kitu ambacho kitaboresha maisha
yako hata kama upo kwenye wakati mgumu sana.
Tuchulie
huna pesa na limetokea tatizo kubwa, angalia kitu cha kufanya kitakachoweza
kubadilisha hali yako hata kama ni kwa kidogo. Unapochukua hatua hiyo hata kama
huwezi kubadili changamoto yako kabisa, lakini wewe utabadilika kwa sehemu.
Hivi
ndivyo changamoto kubwa au matatizo makubwa yanatakiwa kukabiliwa. Haina maana
kuiona nyumba yako ikiungua moto na kuiacha hivyo hivyo, kisa umeshindwa kuzima
moto huo. Fanya kitu cha kukutoa katika hali ya yoyote uliyopo.
Kila la kheri
katika kufikia mafanikio makubwa uliyojiwekea.
Ni wako rafiki
katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.