Jul 26, 2017
Kama Unashindwa Kufanya Mabadiliko Kwenye Maisha Yako, Basi Tatizo Ni Hili…
Kuna wakati
unaweza ukajikuta unataka kufanya mabadiliko kwenye maisha yako, lakini
unashindwa. Je, umeshawahi kujiuliza kushindwa huko kunatokana hasa na nini au
kitu gani. Najua hili linaweza likawa limekotekea.
Ikiwa kila
wakati unajaribu kufanya mabadiliko ya kitu fulani na unashindwa kuleta
mabadiliko hayo, basi tambua maumivu ya kushindwa hayajawa makubwa sana ndani yako
hadi uweze kuleta mabadiliko hayo.
Kwa mfano,
unataka kuwa na mtaji na unashindwa kila mara, basi elewa kabisa maumivu ya
kushindwa kupata mtaji hayajawa makubwa vya kutosha. Tuchukulie leo hii,
ukaambiwa usipokuwa na mtaji hadi mwaka huu unaisha, utapigwa risasi.
Jiulize
utakubali kufa kwa sababu ya kukosa mtaji huo unaoutaka? Bila shaka
haitawezekana, utafanya kila linalowezekana kufanikisha hilo. Hivyo, wakati
mwingine mabadiliko yanakuja kwenye maisha yako kwa sababu ya kule kuumia sana.
Wakati ulipokuwa
shule ulisoma sana na kuhakikisha unafaulu ili kukwepa maumivu ya kufeli. Pia
kuna wakati umeweka juhudi nyingi sana ili kukwepa maumivu ya aina fulani na
kutafuta mahala sahihi kwako.
Tunaambiwa kitu
chenye nguvu ya kubadili tabia yako na mafanikio ni maumivu. Waulize wote ambao
wamefanikiwa na ambao wanafikiri chanya kuhusu mafanikio, watakwambia maumivu
yamewasaidia sana kubadilika na kuweza kufika hapo walipo mpaka leo.
Hivyo basi, kila
wakati tambua hasira ya kushindwa kupata kile unachokita, maumivu ya kushindwa
kupata kile unachotaka kukibadili, yatumie maumivu hayo ili yaweze kukusaidia
kuweza kufanikiwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.