Jul 29, 2017
Tafuta Sheria Zinazokuongoza Kwenye Maisha Yako.
Kwa
kawaida kila sehemu unayokwenda zipo sheria za kufuata. Zipo sheria za
kuendesha gari, zipo sheria za kufanya biashara, zipo sheria za kuingia ‘club’,
zipo sheria za mchezo wa mpira miguu. Inawezekana unajiuliza kwa nini
sheria hizi zipo? Jibu ni rahisi tu, zimewekwa ili kuleta ufanisi na mafanikio
katika maeneo hayo.
Kunapokuwa
na sheria zinazoongoza jambo lolote, zinafanya kwanza kunakuwa na nidhamu kubwa
ya ufanyaji wa jambo hilo na mwisho wa siku huleta mafanikio. Kwa mfano, kama
kungekuwa hakuna sheria ya mpira wa miguu, mchezo huo usingefanikiwa na badala
yake kungekuwa na fujo tu uwanjani.
Kama
kila kitu chenye mafanikio kinaongozwa na sheria, hata maisha yako yanatakiwa
kuwa na sheria ambazo utazifuata kila iitwapo leo ili uweze kufanikiwa. Kama
hautakuwa na sheria zinazoongoza maisha yako itakuwa ni ndoto kufanikiwa. Utakutana
na changamoto nyingi bila sababu kwa sababu huna sheria zako.
Labda
nikuulize kitu, je, una sheria zinazoongoza maisha yako? Kama huna tafuta
sheria za kuongoza maisha yako. Unapokuwa na sheria zako, zinakufanya kutawala
maisha yako na si kuishi ishi tu bila mwelekeo. Ishi kwa sheria zako, hiyo itakufanya kila wakati utakuwa
mshindi, tofauti na ambavyo kama huna.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.