Jul 11, 2017
MAFANIKIO TALK : Jinsi Ya Kujenga Mafanikio Ukiwa Na Mtaji Wako.
Nikualike
kwa mara nyingine tena katika kipindi hiki cha MAFANIKIO TALK ambacho kinakujia kila siku ya jumanne. Na siku ya
leo tutakwenda kujibu moja ya swali
ambalo tumekuwa tukiulizwa sana na wasomaji wetu kwamba ni
jinsi gani mtu anavyoweza kujijengea mafanikio ukiwa na mtaji wako.
Nasi
kwa kuwa hatufungamani na upande wowote tutakwenda kujibu swali hili pasipo kuona aibu, hii kwa sababu moja ya kati ya
kauli mbiu yetu inayotuongoza katika
kufanya kazi, ni kuwafanya watu wote pasipo kuangalia dini wala kabila wawe na
fikra sahihi kila wakati ili waweze
kufanikiwa.
Na
ukweli ni kwamba moja kati ya maswali ambayo watu wengi wanayo ni pamoja na
hili, hii ni kwa sababu watu wengi huwa wanasema hawajafanikiwa kwa sababu
hawana mtaji, lakini mara baada ya kupata mtaji utakuta watu haohao wanakosa katika
mtaji huo wafanye kitu gani, swali linakuja hivi hujawahi kukutana na mtu
akakwambia ya kwamba nina mtaji wa shilingi laki mbili lakini sijui nifanye
kitu gani?
Bila
shaka umewahi kukutana aina hii ya watu na kama hujawahi kukutana nao basi
yawezekana ukawa ni wewe. Najaribu kujiohoji kwa sauti kubwa hivi hapa tatizo
huwa linakuwa ni nini, mtu asipo fanikiwa atakwambia tatizo ni mtaji ila mara
baada ya kupata mtaji atakwambia hajui afanye nini katika mtaji alionao.
Kwa
muktadha huo hapa utagundua ya kwamba tatizo ni mawazo, narudia tena tatizo la
watu wengi kutofanikiwa aidha kwa kuwa na mtaji au kwa kutokuwa na mtaji tatizo
huwa ni mawazo chanya ni nini mtu afanye
ili aweze kufanikiwa.
Hivyo
kitu cha msingi cha kuzingatia ili uweze kufanikiwa ukiwa na mataji wako ni kujua
unataka nini katika maisha yako, hiki ndiyo kiwe kitu kikubwa cha
kuzingatia kitakachokufanya wewe uweze kufanikiwa Zaidi.
Haijalishi
ni kiasi gani ambacho kipo mkono mwako, kama lengo ni kuwa mfanyabiashara wa
aina fulani ni vyema ukakaa chini na kutafakari kwa kina, tafakari kwa kina
pasipo kuchoka. Na kutafakari huku kwa kina hakikisha anafanya uchanganuzi wa
kutosha juu ya jambo unalitaka kulifanya.
Kwa
mfano mkononi unayo laki tano kwa ajili ya mtaji fanya tathimini ya biashara
ambayo unataka kuifanya, na tathimini hiyo hakikisha haimalizi mtaji wote kwa
mara moja. Kama nilivyosema hapo awali
kama una mtaji wa shilingi laki tano basi tathimini ya biashara yako iwe ni la
shilingi laki nne. Kufanya hivi kutakusadia laki moja iliyobaki kuweza kutatua
changamoto ndogondogo ambazo zitajitokeza katika biashara yako.
Hata
hivyo katika biashara hiyo ambayo utakuwa umeanza kuifanya ni lazima uwe na
daftari la mahesabu ya biashara yako, daftari hili utaandika mapato na matumizi
katika biashara yako, kufanya hivi itakusaiadia kujua kama unapata faida au
laah. Pia mali bila daftari hupoteaa bila habari.
Lakini
jambo jingine katika mtaji ulionao hakikisha unaulinda kwa nguvu zote kama
mboni ya jicho lako, kufanya hivi kutakutoa wewe katika orodha ya watu ambao
huanzisha miradi au biashara kisha biashara hizo kufa.
“Je una mtaji na hujui ni nini cha kufanya,
kama jibu ni ndiyo basi uongozi wa dira ya mafanikio unatoa mawazo ya biashara
kwa mtaji ulionao, hivyo wasiliana nasi ili tukuhudumie kwa 0713-048 035 au barua pepe
dirayamafanikio@gmail.com”
Mpaka
kufikia hapo sina la ziada nikutakie siku njema na mafanikio mema. Tukutane
jumanne ijayo katika kipindi hiki cha Mafanikio talk. Kama unatamani siku ya
jumanne ijayo tuweze kutupa somo kutoka kwako tuma neno MAFANIKIO TALK kwenda 0757909942
au tuma neno hilohilo kwenda e-mail yetu dirayamafaniko@gmail.com nasi
tutakutafuta kwa ajili ya mahojiano mubashara.
Ndimi afisa mipango Benson
chonya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.