Jul 28, 2017
Wakati Bora Wa Kufikia Mafanikio Yako Ni Huu…
Leo nimejikuta namkumbuka sana mwalimu wangu wa somo la
Kiswahili, moja kati ya vitu ambavyo vimenifanya niweze kumkumbuka ni vile
ambavyo alikuwa anajitoa kwa hali na mali katika kuhakikisha tunaelewa somo la
Kiswahili. Ni siku nyingi kidogo zimepita lakini kile ambacho alinifundisha
bado hakijafutika akili mwangu, na sina uhakika kama kitakuja kufutika.
Mwalimu wangu huyu sitachoka kumuombea kwa mwenyezi
Mungu kwa kila jambo ambalo analifanya aweze kufanikiwa Zaidi. Namkumbuka
kwa sababu kuna somo ambalo alitufundisha kwa kutumia nguvu zote, somo hili ni
somo la nyakati.
Na katika somo hili alisema zipo nyakati mbalimbali ambazo ni
wakati uliopita, wakati uliopo na wakati ujao. Pia alieleza ya kwamba nyakati
hizi zote humuhusu mwanadamu, katika kufanya na kusimulia mambo mbalimbali
ambayo yalikwisha fanyika au ambayo yatafanyika.
Na miongoni mwa vitu ambavyo nakumbuka aliweza kutushauri kuhusu
nyakati hizi alisema ya kwamba, mwanadamu yeyote yule ili aweze
kufanikiwa katika maisha yake ni lazima aweze kutambua ya kwamba katika nyakati
hizo ni nyakati moja tu ndiyo muhimu kwake.
Na nyakati hiyo ni wakati uliopo na si vinginevyo, kwani wakati
uliopita na wakati ujao si rafiki kwa mwadamu hata kidogo katika kutenda mambo
ya msingi, kwani watu wengi wamekufa na ndoto zao kwa sababu waliamini Zaidi
nyakati zijazo, wao pamoja na kuwa na mambo mazuri walijifariji na kusema
nitafanya kesho, kesho hiyo ikawa kesho mpaka siku wakazikwa na neno lao
nitafanya kesho.
Kwa maneno mengine kusema nitafanya kesho, kwa neno moja lenye
kujifariji tunasema“nimeahirisha”. Neno hili ni baya sana kwani
wale wote waliofanya kitendo hiki hawakuweza kufikia lengo lao kwa asilimia
zote. Kuahirisha kufanya jambo la msingi ni kutafuta visingizio.
Hivyo kama wewe ni mtu wa kuahirisha sana mambo, hasa kwa kile
kitu unachokifanya, elewa kabisa unapanda mbegu au unajitengenezea mazingira ya
kushindwa kwako. Kama kuna jambo ambalo unataka kulifanya leo, hebu lifanye
bila kusita sita au bila kuwa na shaka ya kitu chochote.
Hivyo kama kweli unataka mafanikio ya kweli jifunze kufanya
mambo kwa wakati, huku ukikimbia visingizio visivyokuwa vya msingi. Daima
ikumbukwe ya kwamba ni heri upate ugonjwa wa malaria, kwani ugonjwa
huu utatibika,Ila ukipata ugonjwa wa kuahirisha mambo ya msingi basi
jiandae kufa maskini.
Mwisho nikuache na nukuu isemayo; Kumbuka ukianza leo si sawa
na kuanza kesho.
Imeandikwa na uongozi wa mtandao huu wa dira ya mafanikio,
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.