Jul 15, 2017
Njia 10 Za Kupunguza Magonjwa Ya Mlipuko Wa Kuku.
Mlipuko
wa magonjwa ni moja ya sababu za hasara kubwa kwa wafugaji na vifo vinavyotokea
kwa wakati mmoja. Pindi mfugaji anapokumbwa na janga la vifo vya ndege, kabla
ya kufikia mwisho wa mzunguko wa uzalishaji hivyo basi asitarajie kupata faida
nzuri mara baada ya mauzo.
Hasara
itokanayo na vifo inaweza kuepukika au kupunguzwa na kutokea kwa kiasi kidogo.
Hili linawezekana, ifuatayo ni namna ya kufanikisha hilo;-
1. Osha vyombo vya maji kila wakati na
mwaga maji yaliyobaki.
Hakikisha
unamwaga maji yaliyosalia mbali na kuosha chombo na sabuni kila siku, weka maji
safi yasiyo na dawa na wala usitumie maji ya mto au yale usiyoyajua chanzo
chake. Kama utaweka maji dawa basi tumia ‘vitamini’
muhimu kama ‘vitalyte’ ambazo
zinasaidia kuua vijidudu.
2. Wape maji kabla ya chakula.
Ndege
wapo tofauti na binadamu au wanyama wengine. Hakikisha unawapa maji kabla ya
chakula hasa kama unatumia maranda, hii ni kuhakikisha hawakanyagani
wanapogombania chakula sehemu moja.
3. Usiwape chakula chenye uvundo.
Ni hatari
sana kuwapa ndege/kuku wako chakula chenye ukungu, ni kama kuwalisha sumu.
Ukungu au uvundo huwafanya kuku waugue kirahisi sana au kuwasababishia madhara
mengine kiafya.
4. Fuatilia kwa makini ratiba za chanjo
na tiba.
Mfugaji
unatakiwa kupata tiba na chanjo sahihi kwa ndege unaowafuga. Kuchanja ndege
kutasaidia sana kuimarisha kinga yao dhidi ya magonjwa hatari kama kideri,
ndui, gumboro na mareksi. Dawa kama vile za minyoo na antibayotiki ni muhimu
sana kwenye afya ya kuku na ndege wengine.
5. Nunua na fuga vifaranga wenye afya
njema.
Matatizo
mengi ya afya ya ndege au kuku ni matokeo ya maisha duni ya awali ya kuku hao au huwa
wanarithi. Itambulike hivi, baadhi ya ndege/kuku hurithi afya mbovu kutoka kwa
wazazi wao. Hata hivyo baadhi ya watotoleshaji pia wanafuga kuku ambao wana afya
mbovu na hivyo huuza vifaranga au mayai dhaifu na waathirika na hivyo mnunuzi anajikuta
ananunua matatizo.
6. Zuia mkusanyiko wa hewa ya ammonia.
Maranda
yakikaa muda mrefu bandani, hufanya hewa ya ammonia kuzalishwa kwa wingi, hewa
hii hufanya ndege wapaliwe hadi kufa. Kila mara ondoa maranda mabichi au yaliyovunda
na weka mengine haraka iwezekanavyo ili kuepuka vifo vitokanavyo na kupaliwa au
magonjwa ya mfumo wa hewa.
7. Zuia panya na vicheche.
Banda
la ndege linatakiwa lisiruhusu panya au wanyama wadogo jamii ya kicheche
kuingia ndani, na ndege wa mwituni kwa kuweka nyavu au kupulizia dawa, ikiwa
watapata upenyo wataua na kula ndege/kuku wako na kuacha vimelea vya magonjwa
wanapokula vyakula au kunywa maji ya ndege wako.
8. Zingatia usafi na usalama.
Kipengele
hiki cha usafi na usalama ni kipana ila
unachotakiwa kufanya ni kuzingatia usafi nje na ndani ya banda. Unatakiwa ukamilishe
usalama wa afya ya ndege/kuku wako kila wakati, jambo ambalo wafugaji wengi
hutekeleza pindi wanapo shitukizwa na mlipuko wa magonjwa.
9. Wape chakula cha kutosha.
Ndege
kama walivyo wanyama wengine, hawawezi kukua na kuzalisha vizuri endapo
wanapewa chakula duni na kidogo. Chakula bora ni msingi imara na ni kinga kwani chakula duni hupelekea uzito
kupungua na kinga kuwa chini na hivyo hufa mapema. Jitahidi wape kuku chakula
cha kutosha ila usiwazidishie.
10. Wakinge dhidi ya baridi kali.
Baridi
kali ni adui kwa afya ya wanyama, ndege na binadamu. Jaribu kila uwezavyo
kuwakinga kuwakinga ndege wako na baridi kali kwani inaua haraka sana kama
sumu. Wawekee chanzo cha joto wakati wa baridi au jenga banda ambalo
halipitishi baridi kali.
Hizo
ndizo njia muhimu ambazo ukiwa mfagaji unazoweza kuzitumia ili kukinga magonjwa
yanatokanayo na kuku.
Kama
wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji huduma ya kuuziwa vifaranga wa kuku kienyeji, kuroiler na sasso,
unakaribishwa pia. Tunao vifaranga ambao wanauwezo wa kuhimili magonjwa na
wanawahi kutaga mapema. Bei zetu kwa sasa ni shilling 2000/= kwa kila kifaranga kimoja cha umri wa wiki moja. Kwa mahitaji
ya vifaranga wasiliana na 0767 048 035/0686
141 097.
Pia tunauza
incubators za kisasa kutoka kiwandani kuanzia mayai 48 mpaka mayai 5200. Kwa
mahitaji pia ya incubators, wasiliana na
0628 929 816 utapatiwa incubators bora zitakazokupa faida mfugaji.
Kila
la kheri katika harakati za ufugaji bora,
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni wako rafiki
katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.