Jul 7, 2017
Fanya Mambo Haya Tu, Utakuwa Na Furaha Wakati Wote.
Kati
ya hitaji kubwa la binadamu ambalo
analihitaji kila siku ni kutafuta furaha ya kweli. Ukiangalia shughuli nyingi
na vitu vingi ambavyo anakuwa anafanya binadamu, karibu vyote, vinakuwa
vinalenga katika kupata furaha halisi na ya kweli.
Pamoja
na kwamba furaha inatakiwa sana, lakini bado wapo watu ambao hawana furaha hiyo
kabisa maishani mwao. Watu hawa wamekuwa ni watu wa kuishi maisha yanayowanyima
furaha na wakati mwingine unaweza ukashangaa.
Sina
shaka katika maisha yako umeshawahi kuwaona watu ambao ukiwaangalia, unaweza ukawaona kama ni
watu ambao wanafuraha karibu siku zote na pia wapo watu ambao ukiwaangalia
unaona kama ni watu ambao hawana furaha.
Umeshawahi
kujiuliza tena ni nini siri iliyopo kwa wale watu wenye furaha na kwa nini pia
wale watu wengine hawana furaha? usihangaike sana kutafuta jibu, leo nataka
nikupe siri yakutengeneza furaha kubwa ikiwa lakini utafanya mambo haya;
1. Samahe.
Dunia
ina kero na maudhi mengi sana.ikiwa utakuwa
ni mtu wa kukasirika, unaweza ukakasirika mpaka upasuke. Siri ya kubaki wewe
kama wewe na kujilinda na furaha yako ni kusamehe pale unapokosewa.
Ukishikilia
mambo na kuweweka sana kifuani, hautaweza kuwa na furaha kamwe. Kuna mtu amekuuzi,
msamehe na kisha endelea na maisha yako. Hautapungukiwa na kitu ukiamua kutoa
msamaha wa bure, zaidi utajipa baraka.
Ishi sasa kwa furaha kubwa. |
2. Ishi sasa.
Utajipoteza
kwenye maisha ikiwa wewe ni wa kuishi jana au kesho sana. Siri ya kutengeneza
furaha ya kudumu wakati wote pia ipo kwenye kuishi sasa. Acha kuchukua mambo
ya jana au kesho ukaishi nayo leo, kwa kufanya hivyo utajibebesha mzigo mzito
ambao utakufanya moja kwa moja ukupotezee furaha.
3. Acha kuchukulia mambo kwa ujumla.
Inapofika
wakati mtu mwingine akakufanyia kitu ambacho hakieleweki na kumwona ndivyo kama
alivyo, utakosea, acha kuchukulia mambo kwa ujumla. Acha kuwaza kwa sababu fulani kasema hivi ndivyo
ilivyo, au kwa sababu fulana kanifanyia hivi ndivyo ilivyo, fanya uchunguzi
pata majibu ya jumla, kisha amua.
4. Elewa siku mbaya ipo.
Sisi
binadamu tunakutana na mengi. Kuna wakati unaamka unajikuta yaani hujisikii
kufanya kitu cochote na uko hovyohovyo. Hili linamtokea karibu kila mtu na sina
shaka na hilo, kama siku hizo zipo, jiandae, ili usije ukapoteza furaha yako. ikitokea
namna hiyo ujue jinsi ya kukabiliana na hilo.
5. Thubutu kufanya jambo jipya.
Watu
waliofanikiwa kila wakati wanajaribu kufanya mambo mapya ya kuwapa mafanikio.
Ni watu ambao hawachoki kujaribu mpaka kuhakikisha wanapata wakitakacho. Kwa
kujaribu huko hujikuta wanapata uzoefu na kuondoa hofu na matokeo yake wanajenga furaha ambayo inawasaidia kwenye
maisha yao.
6. Chukua jukumu lote la maisha yako.
Ukiuelewa
ukweli kwamba, maisha yao yanakuhusu wewe, hutakiwi kumlaumu mtu yoyote iwe
serikali, mzazi au mwajiri wako basi utakuwa na furaha.kwa sababu kila
kinachotokea utaona ni chako na kinakuhusu kwa asilimia zote utakuwa huna haja ya
kulaumu mtu yoyote zaidi yako wewe.
7. Acha mambo mengine yaende.
Huna
haja ya kung’ang’ania hofu, huna haja ya
kung’ang’ania kushindwa kwa jana wala huna haja ya kung’ang’ania mambo yale
uliyoumizwa nayo na kuyaweka kwenye akili yako. Yaruhusu mambo hayo yaende, jukumu lako ni
kujifunza, kuishi na kutabasamu ili kupata furaha ya kweli. Hayo mengine
yote yameisha.
8. Kuwa mtu wa shukrani.
Kati
ya kitu cha msingi sana katika maisha ni kujijengea utaratibu wa kuwa na
shukrani. Kua mtu wa shukrani, kushukuru kile ulichonacho, kushukuru afya
uliyonayo na kushukuru kila unachokipata. Ukifanya hivyo utataweza kuwa na
furaha na hutapata shida hata ikitokea umekosa mambo mengine.
9. Jenga tabia ya kujiamini.
Amini
kila wakati unaweza ukafanikiwa. Amini kla wakati una uwezo mkubwa ndani yako
na pia waamini wengine kwa yale majukumu unayowapa. Ukiweza kujiamini wewe na
hata kuwaamini na wengine, basi hautakuwa na wasiwasi katika maisha yako, kwa
hali hiyo itukapa furaha.
10. Wasaidie wengine.
Unapokuwa
msaada kwa wengine kwa kuwapa kile kitu ambacho unaona kuitawasaidia basi hio
ni njia mojawapo ya kutengeneza furaha halisi na ya kudumu. Kuanzia leo anza
kuwasaidia wengine kwa chochote ulichonacho. Fanya kile unachoweza na sio lazima
iwe pesa., toa msaada wowote kwako na utajisikia vizuri.
Kwa
kujua mambo hayo naamini yatakusaidia sana kuweza kukujengea furaha ya kweli ambayo
itadumu maishani mwako. Kitu cha msingi kwako chukua hatua na utaona maisha
yako yakibadilika.
Kila la kheri
katika kufikia mafanikio makubwa na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.
Ni wako rafiki
katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.