Jul 16, 2017
Yafanye Maisha Yako Yawe Ya Mafanikio Kwa Kuanza Kuchukua Hatua Hii…
Kama unakumbuka kupitia historia ujenzi wa piramidi
kubwa za Misri, haukuanza kwa kujengwa na mawe mengi kwa pamoja, bali zilianza
kujengwa kwa jiwe moja tu, tena jiwe hilo ambalo liliwekwa na mhudumu mmoja
katika siku hiyo ya kwanza ya ujenzi.
Hilo jiwe moja liloanza kujenga piramidi hizo
kubwa kihistoria na kupelekea mamilioni ya watu leo hii kutembelea Misri, lilionekana
jiwe hilo ni la kawaida tu na wala halina chochote na wala mchango wake haukuweza
kuonekana mara moja.
Hata yule mfanyakazi mtumwa ambaye aliweza
kuweka lile jiwe la kwanza katika kujenga piramidi hizo hakuweza kutambuliwa
wala kuonekana ana mchango wowote zaidi alizidi kuonekana ni mtumwa tu na asiye
na maana yoyote.
Pamoja na kwamba umuhimu wa kujenga piramidi
haukuonekana na mtu yeyote, na pia wala hakuna aliyejali ni nini kinaendelea,
lakini kutokana na nguvu ya kuanza mwisho wa siku piramidi zilisimama na
kushangaza watu wengi.
Kama nilivyotangulia kusema, leo mamilioni ya watu
duniani wanasafiri tena kwa gharama kubwa kwenda kuangalia piramidi hizo za
kihistoria ambazo ni matokeo ya kazi iliyoanzishwa na uwekaji wa jiwe moja
moja.
Hata kwenye maisha yetu inabidi tuelewe kwamba,
siku zote kuanza jambo lolote ni kitu kigumu sana. Mara nyingi inahitjika
juhudi sana ili kuanza jambo, vinginevyo huwezi kuanza kabisa na pia najua unaelewa vizuri hili kuwa kuanza ni kugumu.
Kama wewe usipokuwa makini, utakuwa unatumia muda mwingi
sana kufikiria kuhusu kuanza hasa ukifikiria ukubwa wa jambo unalotaka kulifanya
na kujikuta unakata tamaaa au kuahirisha kwamba nitafanya siku nyingine.
Ni rahisi sana kupata msisimko na hamasa mara tu
pale unapojiwekea malengo yako, lakini kwa wengi linapokuja suala la kuchukua
hatua hapo ndipo ugumu unapoanza na wengi husau kabisa kwamba siri ya mafanikio
yao ipo kwenye kuanza.
Ili ufanikiwe unatakiwa uelewe hivi, chochote
kitu kikubwa unachotaka kukitimiza, kinaanza na wewe kuchukua hatua ya kufanya
au kinaanza na wewe kuchukua hatua ya
kuweka jiwe la kwanza ili kukamilisha
piramidi ya mafanikio yako.
Mwanzoni unapoanza kujenga mafanikio yako,
unaweza ukaonekana si kitu wala huna chochote na hakuna unachofanya, lakini
elewa huo ni mwanzo. Maajabu ya maisha yako ndipo yanapoanzia hapo kwa wewe
kuamua kufanya.
Hutasogea na hautafanya mabadiliko yoyote ya maisha
yako, ukiamua kutulia bila kufanya kitu. Fanikisha maisha yako na kuwa ya mafanikio
kwa kuanza kitu kitakachokusogeza kwenye maisha yako.
Kila la kheri katika kufikia
mafanikio makubwa na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kwa ajili ya kujifunza na kuhamasika kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA
MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.