Jul 4, 2017
MAFANIKIO TALK: Mbinu Za Kupata Masoko Katika Biashara.
Uhali
gani mpenzi msomaji wa mtandao huu wa dira ya mafanikio, husasani kipindi hiki
cha mafanikio talk
kinachokujia kila siku ya jumanne, ambapo madhumuni ya kipindi hiki ni wewe
kutushirikisha kile ulichonacho kinachohusu mafanikio.
Kinachofanyika
hapa ni kwamba, mtandao huu wa DIRA YA
MAFANIKIO unakupa fursa wewe mtanzania na usiye mtanzania kuweza
kutushirikisha jambo moja lenye kuleta tija katika safari yetu ya mafanikio kwa
namna moja ama nyingine.
Je,
ungependa kushiriki katika kipindi hiki cha mafanikio talk siku ya jumanne ijayo? Kama jibu ni ndiyo
nakusihi usome mpaka mwisho wa makala haya, tutakueleza namna ya kushiriki na
ukawa msaada kwa wengine.
Kwa
hayo machache kati ya mengi kuhusu namna ya kushiriki kipindi hiki cha mfanikio
talk nadhani inatosha, hivyo nikukaribishe kwa moyo mkunjufu katika kipindi
chetu cha leo na siku ya leo tupo na mwanaharakati kutoka mkoa Tabora, anaitwa Justin Kasubi.
Tengeneza soko lako kwa uhakika. |
Hata
hivyo pia ameshukuru kwa kwa elimu nyingine ambayo hutolewa katika makundi yetu ya Whatsapp, anasema binafsi yamemsaidia
sana kuweza kuimarika kifikra na kuweza kukua kibiashara kila kukicha.
Lakini
licha ya kuzungumza mambo mengi na mwanaharakati huyu kubwa zaidi anasema
anatamani sana kufahamu mambo mbalimbali yatakayomsaidia kuweza kutafuta masoko
katika biashara yoyote ile.
Nasi
kwa kuwa hatufungamani na upande wowote siku ya leo tutaeleza namna ya kutafuta
masoko katika biashara kama ifuatayo;
Utafutaji
wa masoko katika biashara yeyote ile ni muhimu sana, na tendo hili ni kila
mmoja wetu ambaye anatamani kuingia katika ulimwengu wa biashara aweze kujua
somo hili.
Kwanza
kabisa utafutaji wa masoko ni hatua za awali ambapo mfanyabiashara ni lazima
aweze kuelewa, kwani wengi wetu huingia katika biashara kisha wanaanza kutafuta
wateja, kufanya hivi ni sawa na kuvaa
viatu kwanza, kisha soksi zinafuata.
Kwa
muktadha huo ni kujichelewesha mwenyewe katika safari yako ya mafanikio, hivyo
mbinu bora ya kutafuta masoko ni heri kufikiri kwa umakini mwanzoni kabisa kabla ya kuanza kufanya biashara fulani.
Unatakiwa
ujenge tabia ya kujiuliza kwamba katika kitu hiki ninachotaka kufanya hivi
wateja wangu watakuwa ni wakina nani? Na wanapatikana wapi? Unatakiwa upate
majibu halisi ya haya maswali ili ujue ni kipi cha kufanya.
Mara
baada ya kupata majibu ya maswali hayo?
Nenda mahali husika na kutazama wafanyabiashara wengine wenye biashara
kama ya kwako, na kuangalia wao
wanatumia mbinu zipi kupata wateja wengi?
Mara
baada ya kupata majibu hayo, zama katika halmashauri ya ubongo wako na ufikiri
kwa kina namna ambavyo utaweza kuwa mbunifu kuwashinda washindani hao. Tafuata
majibu pia ni ubunifu upi utakaouweka.
Lakini
mwisho kabisa mbinu bora ya kutafuta masoko ni kutangaza biashara yako,
asikwambie mtu biashara ni matangazo. Unaweza kutangaza biashara kupitia vyombo
vya habari, mitandao ya kijamii na sehemu zinginezo.
Hivyo
kwa mbinu yeyote ambayo utaamua kuitumia ni vyema ukahakikisha inaleta wateja
wapya, na wateja hao hakikisha pia huwapotezi. Ikiwa unawapoteza wateja wako,
basi utakuwa hufanyi kitu, unakuwa kama unacheza.
Mpaka
hapo hatuna la ziada siku ya leo tukutane jumanne ijayo katika kipindi hiki cha
mafanikio talk. Kama
unatamani siku ya jumanne ijayo tuweze kutupa somo kutoka kwako tuma neno mafaniko talk kwenda 0757909942 au tuma neno hilohilo kwenda
e-mail yetu dirayamafaniko@gmail.com
nasi tutakutafuta kwa ajili ya mahojiano mubashara.
Asante
sana kwa kuwa nasi nikutakie siku njema
na mafanikio mema. Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza na kupata mwangaza halisi wa maisha yako.
Ni
wako afisa mipango Benson Chonya,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.