Jul 21, 2017
Watu Wenye Hasira Na Kiu Kubwa Ya Mafanikio Wanafanya Mambo Haya Kwa Utofauti Sana.
Wapo
watu ambao ndani mwao wameamua kwa dhati kufanya mabadiliko katika maisha yao. Watu
hawa wana kiu, hasira na hamasa kubwa ya kufanya kila kinachowezekana ili kuweza
kufanikisha ndoto zao za kimaisha.
Watu
hawa juhudi zao nyingi huzielekeza kwa kufanya mambo kwa utofauti hali ambayo
huwaletea mafanikio. Inawezekana leo nitakuwa mbaya kwako, kama sitakwambia watu hawa wanafanya mambo
yapi kwa utofauti na yanayowapa mafanikio.
Ni
wakati sasa wa mimi na wewe kwenda pamoja katika makala yetu ya leo kujifunza
kwa pamoja mambo ambayo watu wenye hasira na kiu ya mafanikio huyafanya tofauti;-
1. Wanaongozwa sana na neno HAPANA.
Watu
wenye hasira na kiu ya mafanikio, kila wakati wanapoambiwa kitu ni watu wakusema
sana HAPANA. Wanafanya hivi ili kufatilia ndoto zao kwa ukaribu na kuachana na
kukubali kila kitu ambacho kinaweza kuwapoteza.
Watu
hawa wanajua pia kwa kusema hapana kwanza hata kama kitu hicho walichoambiwa wakagundua
kina faida kwao, ni rahisi kugeuza na kukubali pia. Kusema HAPANA ni jambo
ambalo haliogopwi na watu wenye hasira ya
mafanikio.
2. Kuamka asubuhi na mapema.
Naomba
nikupe tu ukweli mmoja, ukiachana na watu maskini, sijawahi kukutana na mtu
mwenye mafanikio makubwa ambaye kuamka kwake asubuhi ni kwa kuchelewa. Watu
wengi wenye mafanikio wanaamka mapema kabla jua halijatoka.
Asubuhi
ni muda mzuri unaowawezesha kupanga mipango ya siku husika kwa uhakika na
kufatilia mambo kwa ukaribu wakati wengine bado wamelala. Kuamka mapema mi kitu
ambacho wengi hawapendi, kwa watu wenye hasira na mafanikio hupenda sana muda huo.
3. Kujituma sana.
Kati
ya kitu ambacho watu wenye hasira na kiu ya mafanikio wanakifanya sana pia ni kujituma kwa nguvu
zote. Wanajua bila kujituma itakuwa ni kazi bure tu, hakuna mafanikio
yatakayojengwa.
Hujitahidi
kufanya kazi kwa muda mrefu sana kuliko watu wengine ili kuleta matokeo
chanya. Si ajabu kukuta usiku wa manane wakifanya kazi zao ili kufanikisha ndoto
zao. Kujituma na kwenda hatua ya ziada ni kitu ambacho kinafanywa na watu hawa.
4. Wanaongozwa na roho ya ung’ang’anizi.
Watu
wenye kiu ya mafanikio pia wanajaribu sana mambo mengi na kuhakikisha kila wanalolifanya
linafanikiwa. Wakianzisha jambo si rahisi sana kuliachilia njiani. Hung’ang'ana na
kuhakikisha mpaka kuona kutaka kuleta matokeo.
Kwa
kifupi, watu wenye hasira na mafanikio ni wabishi wa mafanikio yao. Hawakubali
kirahisi kushindwa. Wapo tayari kufanya mara elfu moja, ilimradi tu kuona
wanafanikiwa. Hiki ni kitu kimojawapo wanachokifanya kwa utofauti pia.
5. Si walevu wa mitandao ya kijamii.
Mitandao
ya kijamii ni mizuri kutusaidia kupashana habari , nafikiri hilo unalijua
vizuri sana. lakini kwa watu wenye kiu na hasira ya mafanikio wanaamini sana
kwamba mitandao ya kijamii imewekwa kwa ajili ya kuwapotezea au kuwaibia muda
wao.
Hivyo
kwa kulijua hilo wanaitumia mitandao ya kijamii kwa hesabu sana na kwa muda
maalumu. Tofauti na watu wengine wanavyofanya, wao wana muda maalumu kuingia
kwenye mitandao hiyo ya kijamii, lakini sio kuingia hovyo hovyo tu.
6. Kutokujali sana mambo ya wengine.
Kitu
kikubwa kilicho ndani ya watu wenye kiu ya mafanikio na kinachowapelekea wafanye
mambo yao kwa utofauti na kuleta mafanikio, ni kule pia kutokujali mambo ya
watu wengine. Hawajali sana fulani anafanya
kitu gani.
Kila
wakati ni watu ambao wanajihusisha sana na ndoto zao na kuangalia ni wapi
pa kuboresha hadi kuleta matokeo. Hawajali wanakoselewa vipi na nani. Huamua
kusonga mbele bila kujali vitu kama hivyo na hatimaye hufanikiwa.
7. Wasikilizaji wazuri wa mambo na
kuchukua hatua.
Kila
wakati watu wenye nia ya kufikia mafanikio,
ni wasikilizaji wazuri sana kwa wengine wanasema nini. Ni watu ambao wanajua
kusema sana kunapoteza mafanikio, hivyo huamua kusikiliza na kuweka kumbukumbu za
kimaandihi vile vitu ambavyo vinawasaidia.
Ndio
maana ukiwafatilia wengi ni watu ambao wapo makini na si waongeaji sana. Huamua
kujifunza kupitia maisha ya wengine, huchukua vitu vya msingi vinavyoweza
kuwasaidia kufanikiwa.
Kila
la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.