Jul 24, 2017
Utajiri Au Umaskini Wako, Unatokana Sana Na Maamuzi Haya.
Maisha
unayoishi sasa, kwa sehemu kubwa, yanatokana na maamuzi uliyoyafanya kipindi cha
nyuma na maisha utakayoishi kesho pia yanategemea sana maamuzi unayoyafanya leo
kwenye maisha yako.
Unauwezo
wa kuboresha maisha yako kwa kufanya uchaguzi sahihi wa hatua unazozichukua
kila siku. Moja ya kitu unachotakiwa uanze nacho ili uweze kuchukua hatua
sahihi ni kujifunza juu ya kutawala pesa zako.
Hivi
pengine nikuulize, umeshawahi kujiuliza katika maisha yako pesa ngapi zimepita
mikononi mwako? Ukiangalia, ni pesa nyingi sana, lakini cha ajabu kwa wengi
zimewaacha jinsi walivyo wakiwa hawana kitu.
Sasa
basi, ili kuendelea kukosa pesa kusitokee kwako, unahitajika sana kujifunza juu
ya kuwa na maamuzi sahihi ya kutawala pesa zako. Ukiipata elimu hii na
ukaielewa vizuri, utakuwa umefanya maamuzi sahihi ya kukupeleka kwenye utajiri
wako moja kwa moja.
Kwa
mujibu wa uchunguzi mdogo uliofanyika unaonyesha hivi, asilimia kubwa ya
watu waliomaskini wanaweka akiba chini
ya asilimi 2 na wengine hawaweki kabisa. Hiyo ikiwa na maana kipato chote
kinachobakia kinaingizwa kwenye matumizi.
Mpaka
hapo kwenye maamuzi hayo, ni moja ya maamuzi mabaya yanayowapeleka wengi kwenye
umaskini. Akiba au kujilipa mwenyewe
kiasi kidogo cha kila pesa unayopata ni kitu cha msingi sana kama unataka kesho
yako iwe ya mafanikio.
Ni
kweli swala la matumizi ya pesa zako liko mikononi mwako, lakini ili uwe tajiri
ni lazima ujue namna ya kutawala pesa zako. Sio kwa sababu una pesa unanunua
vitu hovyo na kujikuta hakuna hata kiasi kidogo cha pesa ulichobaki nacho.
Angalia
usije ukajikuta ukajuta kesho kutokana na maamuzi mabovu unayoyafanya leo juu
ya pesa zako. Fanya maamuzi leo bora
yatakayokufanya kesho ukajiona shujaa mkubwa kwa kujiona ulifanya kitu cha maana kwa
sababu ya pesa zako.
Ikiwa
unataka kuendelea kimaisha na hata kuwa tajiri elewa vizuri juu ya kutawala
pesa, yote haya unatakiwa ujifunze ukiwa bado kijana, kama hautafanya maamuzi
hayo sahihi, ni wazi hautafanikiwa.
Utajiri
au umaskini wako, siku zote upo mikononi mwako kutokana na maamuzi unayoyafanya
juu ya pesa. Leo jiwekee kiapo kwamba, kwa pesa yoyote unayoipata ni lazima
uweke kidogo kwa ajili yako.
Kwa
kuanzia, anza hata na asilimia kumi ya kile unachokipata, umeshindwa kabisa,
anza na kiasi chochote. Pesa hiyo kumbuka ni yako, unakuwa haujapoteza popote,
hivyo usiwe na wasiwasi, chukua maamuzi sahihi leo yatakaokupa utajiri.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kwa ajili ya kujifunza na
kuhamasika kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.