Jul 3, 2017
Kwanini Watu Wengine Wanapenda Kukuona Ukiwa Unashindwa?
Ni
jambo lilowazi kila mtu katika maisha ana harakati za kutafuta mafanikio yake.
Pilika pilika za kila siku, zote hizo huonyesha jinsi binadamu anavyosaka
mafanikio wakati mwingine hata usiku na mchana.
Pia
katika haraka za kutafuta mafanikio, kipo kipindi mbacho kuna wakati tunaweza
kusaidiana kwa hili au lile, ili kuweza kutimiza ndoto zetu. Na kuna wakati
hata tunapongezana kwa hatua tulizofikia.
Lakini
pamoja na kuona wengi wakipongezana kwa hatua walizofikia kimafanikio, bado
wapo watu ambao hawataki kabisa kuona wengine wakifanikiwa. Kila wakati elewa
kabisa watu hawa wapo, ingawa huwezi kuwajua kirahisi.
Swali
la kujiuliza ni kwa nini watu wengine hawapendi kukuona wewe ukiwa umefanikiwa?
Je, watu hawa wana roho mbaya? Au shida iliyo ndani mwao ni nini hadi kutotaka
wewe usifanikiwe wakati hara wakati mwingine mafanikio yako hayawahusu.
Acha wivu na mafanikio ya wengine. |
Jibu
ni rahisi tu, watu hawa hawataki ufanikiwe kwasababu , watu huwa wanapoona
umefanikiwa kwa kiwango chochote kile, wao wanajisikia vibaya kwa sababu katika
maisha yao hakuna walichofanikiwa kikubwa au hawajapiga hatua kabisa pale walipo.
Sasa
wanapogundua kwamba unayaendea mafanikio, wakati wao hata hayo mafanikio
hawana, wanakuwa wanajisikia vibaya na kutamani tu wewe ushindwe kwa hicho
unachokifanya ili muwe sawa.
Jambo
hili hutokea sana kwa watu wanaofanya kazi au biashara ya aina moja, watu kila
wanapoona mwenzake amefanikiwa kwenye biashara ile ile, hataki kuona akifanikiwa
kwa sababu ataona kama atanapitwa vile.
Watu
ambao wanachukia mafanikio yako ni wale watu ambao wanaona hawawezi kufanikiwa
kama wewe hata iweje. Ujasiri wa kufika sehemu na kuona kama watafanikiwa
hawana, ndio maana wanaamua kuchukia kile unachofanikiwa nacho.
Jaribu
kujiangalia hata wewe mwenyewe, je kuna wakati inafika unachukia mafanikio ya watu wengine? Kama ndiyo, unajitengenezea
shimo kubwa na kuendelea kushindwa kwenye maisha yako.
Kama unatabia ya kuchukia mafanikio ya watu
wengine, achana na hiyo tabia, badala yake anza kujenga tabia itakayokusaidia
wewe kuweza kujifunza mafanikio ya hao watu wengine na wewe ukawa kama wao.
Mpaka
hapo utakuwa umeelewa vyema kwa nini watu wengine wanachukia kila wakiowaona
watu wengine wakifanikiwa.
Endelea
kuweka juhudi katika kufikia mafanikio yako makubwa.
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.