Jul 5, 2017
Misingi Minne (4) Ya Kufikia Mafanikio Makubwa Katika Kila Eneo La Maisha Yako.
Kila
mtu ana ndoto na maono ya kufikia mafanikio makubwa maishani mwake. Binafsi,
nimekutana na watu wengi sana ambao ukiwasikiliza hisia zao wanataka kufikia
mafanikio makubwa kwenye shughuli wanazozifanya..
Lakini
pamoja na ndoto hizo, cha kushangaza, bado watu wengi ambao wanataka kufikia
mafanikio makubwa, wamekuwa wakiishi kwa matumaini sana pasipo kuchukua hatua au
kufanya mambo yatakayowafikisha huko.
Watu
hao wamekuwa wakisahau kwamba kufikia mafanikio makubwa ni safari ambayo sio
rahisi na hiyo haitoshi, ni safari ambayo inahitaji kujitoa sana na kujua
misingi yake vyema, bila ya hivyo hakuna mafanikio tena.
Kupitia
makala haya ya leo, nataka twende pamoja kujua misingi minne ya lazima
itakayokusaidia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Katika misingi
hiyo, mimi na wewe tunatakiwa kuijua vizuri ili kufikia mafanikio makubwa.
1. Amua kuwa mwenyewe.
Kila
mtu anataka mafanikio makubwa, lakini si kila mtu anataka kupita kwenye njia
inayoleta mafanikio makubwa. Njia ambayo inaweza ikakufanya ukawa na mafanikio
makubwa ni wewe kuamua kuwa mwenyewe.
Unajiuliza
kivipi? Sikiliza, wakati wengine wanafanya kazi saa 8 kwa siku, wewe fanya kazi
saa kumi na mbili. Wakati wengine wanaamka saa kumi na mbili asubuhi, wewe amka
saa kumi na moja alfajiri na kuanza kutekeleza majukumu yako.
Ijue vyema misingi ya kufikia mafanikio makubwa. |
Unafanya
yote hayo si kwa kutaka sifa, bali unatengeneza mafanikio yako na njia hiyo ya
kupata mafanikio makubwa wengi hawataki kupita huko. Ikiwa hutaki kufanya hivyo
utaambulia patupu, mafanikio makubwa hutaweza kuyapata.
Kama
ingekuwa rahisi kupata mafanikio makubwa kama wengi wanavyotaka na kusema, basi
kila mtu angekuwa nayo hayo mafanikio, lakini inataka kazi, kuwekeza juhudi na
kulipa gharama ambazo wengine hawataki kulipa, ukifanya hivyo, hapo mafanikio
makubwa utayanasa.
2. Tengeneza imani zinazokuongoza kwenye
mafanikio yako.
Linapokuja
suala mafanikio makubwa, wewe binafsi unaamini kitu gani? unaamini ili upate mafanikio
makubwa ni lazima utumie uchawi au ni kitu gani ambacho unachoamini? Imani yako
hapa ni muhimu sana katika kukuongoza kufanikiwa.
Wakati
mwingine unatakiwa ujenge imani tofauti, utumie kanuni kinyume na wengi
wanavyofikiri mafanikio yanataka yawe. Amua kufanikiwa katika eneo ambalo hata
wengine hawaoni kama kweli utaweza kufanikiwa.
3. Tengeneza maono makubwa.
Kinachotofautisha
kati ya watu ambao wamefanikiwa na wale ambao hawajafanikiwa si kitu kingine bali
ni maono. Watu waliofanikiwa wanaongozwa na ndoto au maono makubwa ya kimafanikio
tofauti na ambao hawajafanikiwa.
Unapotengeneza
maono yako makubwa na ukaamua kuyafatilia kila siku, ni wazi ipo siku utafikia
ndoto zako. Hakuna kinachoweza kushindikana katika kufikia mafanikio makubwa
kama kweli una maono makubwa na yaliyowazi.
4. Fanya mambo yako kwa ubora.
Mafanikio
makubwa yanajengwa kwa kufanya vitu kwa ubora na umakini wa hali ya juu. Kama
unafikiri mafanikio yanakuja hivihivi tu yaani kwa kulipua mambo uwe na uhakika
huwezi kufanikiwa.
Kila
wakati kaa chini na anza kufikiri jinsi ya kufanya mambo yako kwa ubora, yaani
‘how to commit to excellence’. Siri
ya mafanikio makubwa unayoyataka ndivyo inavyotakiwa kufanyiwa kazi na kuleta
matokeo.
Kwa
kufanya mambo hayo kikamilifu basi utakuwa ni moja ya watu ambao utaweza
kufikia mafanikiio makubwa.
Kila
la kheri katika kufikia mafanikio makubwa na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com
kila siku kujifunza.
Kama
unataka kufanya biashara au upo kwenye biashara na unataka wazo bora kabisa la
kuboresha biashara yako, usisite kuwasiliana nasi mara moja kwa 0713 04 80 35
au tutumie email dirayamafanikio@gmail.com kwa
msaada zaidi.
Ni wako rafiki
katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog, dirayamafanikio.blogspot.com
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.