Jul 25, 2017
Kitu Pekee Cha Kukiogopa Pale Unapohitaji Mafanikio Ya Kweli.
Kuna wakati mwingine inabidi ujutie katika hali ambayo upo hivi sasa, nasema hivyo kwa sababu moja kati ya mambo ambayo inakubidi ujutie katika maisha yako ni kwa sababu umekuwa ni mtu wa kushangaa kuliko kutenda mambo ya msingi.
Tabia
hii ya kushangaa kila kitu pasipo wewe kuchukua hatua ndiyo ambayo kiukweli
inakufanya uje kujuta hapo baadae, na pia ikumbukwe wakati wewe unazidi
kushangaa wapo wengine ambao wanazidi kusonga mbele katika utendaji.
Tabia
hii ya kushanga ni mbaya sana katika safari ya mafanikio, kwa mfano, Utakuta
wao ni watu wa kushangaa na kuhamasika sana na miradi wanayofanya watu wengine,
ukija upande wao hakuna hata kitu kimoja wanachofanya.
Vilevile
utakuta watu hawa kazi yao ni kuingia
kundi moja, wanashangaa kinachoendelea humo na kutoka na kuingia tena kundi
lingine wanashangaa wee na kutoka tena, pia bila kuchukua hatua, endapo
utachukua jukumu la kuwauliza watu hawa watakwambia wanashangaa mataa.
Tabia
hii kama unayo ni vyema ukaamua kuiacha mara moja kwani dunia ya sasa hivi ni
ya mwendo kasi Zaidi ya kasi ya 4G hivyo kila wakati ni lazima uweze kufanya
kazi. Kama kuna fursa hata kama ni ndogo kiasi gani, itumie ikusaidie
kufanikiwa na acha kubaki tu kuwa mtu wa kushangaa. Kama ni kujifunza, jifunze kweli.
Uzuri
au ubaya wa maisha hakuna ubabaishaji, ukileta ubabaishaji wa aina yoyote ile,
utaumbuka tu na ni lazima utajibiwa na maisha kama vile wewe unavyobabaisha.
Badilika rafiki na achana na biashara ya kushangaa, kuwa mtendaji na aamua
kufanya kazi.
Hivyo
amua sasa kuwa ni mtu wa kuchua hatua kuliko kubaki kushangaa, kwani kufanya
hivyo ni kujichelewesha mwenyewe kumbuka ya kwamba kuendelea kushangaa ni
kupoteza muda na kupoteza muda ni sawa na kuacha pesa zipite machoni mwako.
Mpaka
kufikia hapo hatuna la ziada tukutakie siku njema na mafaniko mema, Mwenyezi
Mungu akubariki sana kwa kusoma Makala haya.
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya,
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.