Jan 31, 2018
Mawazo Yanayofanya Maisha Yako Yabadilike Ni Haya Hapa.
Maisha
uliyonayo mara nyingi sana ni matokeo ya yale mawazo ambayo unayo wewe. Uumbaji
wa maisha yako yawe ya mafanikio au kushindwa, unaanza na mawazo.
Mawazo
ndiyo chanzo cha uhalisia ambao unaona kwa nje. Kitu chochote unachokiona,
kabla hakijawa hivyo, kilianza kama mawazo.
Mawazo
yako yanapoanzia, hayaanzii sehemu nyingine zaidi kwenye akili. Hapa nikiwa na
maana akili yako ndiyo inayotengenezea uhalisia wa matokeo ya nje.
Hiyo
ikiwa na maana, chochote kile unachokiweka kwenye akili yako kwa mda mrefu, ujue kitu hicho itafika muda
utaona matokeo yake yakitokea kwa nje.
Hakuna
namna ambavyo unaweza ukaficha, wewe ni matokeo ya vile unavyoviweka ndani yako
na sio matokeo ya kitu kingine.
Ubora
wa maisha yetu unategemea sana ni kwa namna gani, ambavyo tunajilisha mambo ya
aina gani kwenye akili zetu.
Mawazo
yanayofanya maisha yetu yabadilike iwe yawe mazuri au mabaya si mawazo mageni sana
kwetu, ni mawazo yaleyale ambayo tunakuwa nayo kwa muda mrefu.
Inapotokea
ukawa na mawazo ya aina fulani na kwa muda mrefu kwenye akili yako na yakijirudia
tena na tena, mwisho wa siku hutokea kwa uhalisia.
Haupo
muujiza katika hili hata kidogo, maisha yako yapo hivyo hapo kutokana na mawazo
ambayo unayo wewe na umeyashikiria pengine kwa muda mrefu sana.
Kwa hiyo
mpaka hapo unaona ni kwa jinsi gani ambavyo unatakiwa kuwa na mawazo tulivu,
mawazo ambayo yatakusaidia na si kuweza kukubomoa.
Haijalishi
kiwango cha elimu ulichonacho, pesa ulizonazo au umri ulionao, lakini unao
uwezo wa kufikiria mawazo yako kwa kwa ubora zaidi siku hadi siku.
Jiulize
ni kitu gani ambacho unachagua kufikiri kwa kadri siku zinavyozidi kwenda? Je,
unachagua kufikiri mawazo ya faida au ya mawazo yale ya kushindwa kwako?
Ruhusu
ndani yako uwe na mawazo mazuri ya kukusaidia. Yale mawazo uliyo ndani, yana
uwezo wa kutoka nje na kuleta matokeo uyatakayo.
Kitu
ambacho unapaswa kuchukua hatua ili uweze kuleta mabadiliko ya maisha yako ni kwa
wewe kuanza kuwa na mawazo ya thamani ndani mwako.
Kila
siku hakikisha unaingiza mawazo ya thamani na ya kukusaidia kufanikiwa na si
mawazo yale mabovu ya kukurudisha nyuma.
Mawazo
haya unaweza kuyapata kwa kujisomea vitabu vizuri au hata kwa kujifunza kupitia
watu chanya wenye mafanikio makubwa kukuzidi.
Hauwezi
kushindwa katika hili, ni swala la kuamua tu wewe mwenyewe. Ikiwa lakini
utashindwa kutengeneza thamani ndani mwako, nakuhakikishia utashindwa.
Hakuna
bahati mbaya inayotokea au hakuna maisha ambayo unayapata ni ya bahati mbaya,
yote yanatokana na wewe mwenyewe.
Kama
nilivyosema uchaguzi ni wako, kuendelea kuingiza mawazo mabovu ambayo
yatakupoteza au kuwa na mawazo chanya ya kukujenga.
Kumbuka,
mawazo yanayoumba maisha yetu, mawazo yanayotengeneza kufanikiwa au kushindwa ni
yale mawazo ambayo tunakuwa nayo kwa muda mrefu ndani mwetu.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jan 30, 2018
Vitu Vya Kufanyia Kazi Sana Katika Maisha Yako Ya Mafanikio.
Yapo mambo mengi sana ya kufanyia kazi katika safari ya
mafanikio ili uweze kupiga hatua. Kwa bahati nzuri sana mambo hayo tumekuwa tukijifunza
hapa DIRA YA MAFANIKIO karibu kila
siku, naamini hilo unalijua vyema.
Leo hii kupitia makala haya, tumekuandalia vitu
vingine vya msingi vya kufanyia kazi sana katika safari yako ya maisha ya
mafanikio. Soma kwa makini na kutendea kazi, na maisha yako utayabadili ikiwa utachukua hatua.
1. Njia ya mafanikio ni njia ambayo ina changamoto nyingi sana
katikati yake. Pale tu unapoanza safari yako ya mafanikio kwa chochote kile
unachotaka kukifanya elewa mbele yako kuna changamoto tayari zinakusubiri. Huwezi
kukwepa changamoto.
2. Ikiwa utakosa nidhamu
kwenye maisha yako, basi dunia itakuonyesha jinsi nidhamu inavyotakiwa iwe.
Utapewa adhabu kulingana na kukosa kwako huko nidhamu. Matokeo yoyote
utakayoyapata maishani kwa sababu ya kukosa nidhamu usilaumu.
3. Jiruhusu mwenyewe katika
siku hii ya leo uishi kwa kutoa thamani yote uliyonayo. Usiishi nusu nusu kwa
kuwaza mambo ya jana au juzi. Usiishi nusu nusu kwa kufikiria kwamba kesho
itakuwaje, ishi leo kwa siku nzima kama ilivyo ili kupata matokeo bora.
4. Kila mafanikio ambayo
umeyapata, ni matokeo ya kwamba kuna vitu ambavyo ulivifanya na vikakupa
mafanikio hayo. Kwa kujua hilo, endelea kufanya vitu hivyo, endelea kuchukua hatua
ili upate mafanikio mengine zaidi na zaidi tena.
5. Maisha yako yanaishia
wapi au yatafika wapi, inategemea sana na vitu viwili ambavyo ni mtazamo na
jinsi unavyochukulia mambo. Mtazamo wako na jinsi unavyochukulia mambo ndivyo
vinavyoamua maisha yako yaweje.
6. Chochote unachokizingatia
kwenye maisha, kitu hicho kinakua. Kama unasahau kuzingatia kile kinachokupa
matokeo ya kubadili maisha yako, hiyo itakuwa ni kazi bure hata kama ungekua
unatunza muda vizuri sana. Anza leo kuzingatia sana kile kinachobadili matokeo
ya maisha yako na utafika mbali kimafanikio.
8. Miaka kumi ijayo kuanzia
leo ikifika, haitajali ulivaa kwa sasa kiatu cha aina gani au ulivaa nguo za
mtindo upi zilizotoka au ulitembelea sana maeneo yapi au uliangalia ‘movie’ ipi
nzuri kwako. Miaka hiyo kumi ijayo itajali na itakuja na matokeo ya
ulichowekeza leo, bila kujali uliwekeza kitu cha aina gani.
9. Usijaribu kuangalia nyuma
kwenye maisha yako na kuchunguza yale maeneo kila wakati uliyokwama na kujiona
huwezi kitu. Ni vyema kuangalia maeneo uliyofanya vizuri na kuedelea
kujiboresha na hadi kuweza kufanikiwa zaidi ya hapo.
10. Moja ya tabia ambayo
unatakiwa kuiendeleza ndani mwako na katika maisha yako kwa ujumla, ni kwa wewe
kutokuruhusu, kuwahukumu watu wengine. Usiumize kichwa chako sana kuwahukumu
watu wengine, utapotea. Waache waishi maisha yao. Kuwahukumu watu mara kwa mara
inaweza hata ikakuletea msongo wa mawazo.
11. Kila mtu unayekutana
naye kuna vitu vitatu ambavyo anavyo ndani yake;-
Kuna kitu anachokipenda.
Kuna kitu anachokiogopa.
Kuna kitu ambacho
amekipoteza.
12. Watu wengi katika maisha
hawasikilizi ili kuelewa, bali wanasikiliza ili kukimbilia kujibu. Kuwa msikivu
mzuri unapoongea na watu wengine, hiyo itakusaidia sana kudumisha mawasiliano
yako na kwa bora kabisa.
13. Katika hii dunia, hakuna
kitu ambacho kinaitwa ulinzi bali kuna fursa. Kama unafanya kazi na kutegemea
sana ulinzi au ‘security’ kama wengi
wanavyodai unajipoteza. Tafuta fursa za kukusaidia kufanikiwa na si kutafuta
ulinzi.
14. Siri ya kuweza kusonga mbele kwa chochote
kile unachokifanya ni kuanza. Usijidanganye sana kama unapiga hatua mbele kama
hujaanza. Ni muhimu sana kuanza, kwani unapoanza unajenga ‘momentum’ ya kukusaidia kuweza kusonga mbele zaidi kila siku
kuliko usingeanza kabisa.
15. Kupata utajiri ni zaidi
ya mawazo na mipango uliyonayo. Ili uwe tajiri ni lazima uwe na akili ya
kitajiri/rich mindset na sio mawazo na mipango peke yake. Mawazo mazuri na
mipingo mizuri haiwezi kukusaidia kama una ‘poor
mind set.’
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jan 29, 2018
Sahau Kabisa Hali Hii, Ili Utimize Ndoto Zako.
Kila
mtu anahitaji mafanikio ya aina fulani kwenye maisha yake, ikiwemo hata wewe
unahitaji ufikie mafanikio ya aina fulani.
Pamoja
na kwamba wengi wetu wana kiu kubwa ya
kuhitaji kufikia mafanikio ya aina fulani, lakini linapokuja swala la kufanya
kazi hapo tena kuna shida.
Kuna
wakati unapotakiwa kuweka kazi hasa ili uweze kufanikiwa, utajikuta mwili umechoka
na hujisikii kufanya kazi kabisa na kuamua pengine kutulia.
Hali
kama hizo zinakuwa zinatokea sana, kwa hiyo utakuta mtu anajivuta sana katika
utendaji wake kitu ambacho husababisha uzalishajji wake unakuwa mdogo.
Ili uweze
kufanikiwa na kupata matokeo chanya ya kimafanikio ambayo utaridhika nayo, unahitaji
kufanya kazi bila kujali hali yoyote inayotokea ndani mwako.
Unapokuwa
na hali ya hisia ambayo unaona kabisa kwa jinsi ulivyo huwezi kufanya kazi,
basi tambua hali hiyo inaweza ikakuzuia sana kufanikiwa kwako.
Maisha
ya mafanikio hayaendeshwi kwa hisia za mwili wako hata siku moja, yanaendeshwa
kwa zile hatua ambazo unazichukua kila siku.
Uwe unajisikia
au hujisikii kufanya hicho unachokifanya, unatakiwa kukumbuka kwanza, kuchukua
hatua hata kama ni kwa kidogo sana.
Watu
wengi wanajiangusha kwenye maisha yao kwa sababu ya kuongozwa na hisia kama hizi ambazo kila
wakati zinasema nao kwamba usifanye saa hivi umechoka.
Unatakiwa
uwe jasiri ili kuweza kuzishinda hisia zako ambazo zinaweza kukukwamishwa kwa namna
yoyote ile na hapo utakuwa mshindi.
Usipofanya
hivyo mwili wako utakuendesha sana na mwisho wa siku unajikuta unaanza
kudondokea kwenye kundi la watu wavivu.
Kitu
ambacho unachotakiwa kufanya kwa sasa, usikubali hata kidogo kuacha kuchukua
hatua kwa sababu eti hujisikii kufanya kile unachokifanya.
Wewe
unachotakiwa kufanya ni kuchukua hatua, bila kujali unajisikia au hujisikii. Ukishachukua
hatua basi, kama ni hamasa itakuja mbele kwa mbele.
Ukumbuke
maisha ya mafanikio yanahitaji uvumilivu mwingi na hilo nalo unatakiwa
kulivumulia, lakini usipofanya hivyo utashindwa.
Kumbuka,
ndoto zako zitatimia tu, kama utachuka hatua na kutokujali hali hii ya hisia
ambayo inatokea ndani mwako.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia
kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya
uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga
wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686
141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jan 28, 2018
Unahitaji Sana Kuwa Na Jambo Hili, Ili Kupiga Hatua Endelevu Za Mafanikio.
Kama
kuna kitu fulani hukijui, kuwa na shukrani. Unatakiwa kuwa na shukrani kwa sababu,
kwa kutokujua huko inakupa wewe sababu ya kujifunza.
Kama
mambo yanakuwa magumu kwako sana, kuwa na shukrani pia. Ugumu huo utakusaidia
kuwa jasiri na shujaa mkubwa kwenye maisha yako.
Kama
umefika wakati umekimbia changamoto zako, kuwa na shukrani tena. Hapo ni wakati
wa kutafuta wakati wa kuweza kujiboresha sana ili wakati mwingine usikimbie changamoto kama hizo.
Kama
kuna wakati umechoka kwa kushindwa kendelea kwa sababu huoni mafanikio tena,
pia kuwa na shukrani kwani huo ni wakati wa kuwa wa tofauti.
Kama
kuna wakati umekosea sana si wakati wa kujuta kupitiliza, kuwa na shukrani
kwani makosa hayo hutaweza kuyafanya tena.
Kama
kuna wakati umekula hasara kwenye biashara yako, kuwa na shukrani. Kupata kwako
hasara kutakusaidia sana kuongeza umakini mkubwa.
Ni
rahisi sana kushukuru katika mambo mazuri, lakini si rahisi kuweza kushukutru
katika yale mambo ambayo tunaona mabaya kwetu hata kama yana mafundisho
tusiyoyaona.
Unatakiwa
kuzingatia mabadiliko chanya kwenye kila unachokutana nacho, hata kama kitu hicho
kinaonekana hakifai, elewa kuna fundisho la kujifunza.
Shukrani
zako ni muhimu sana katika kuweza kubadili mtazamo ule wa kushindwa ulionao na
kuleta mafanikio kwa yale utarajiayo.
Ni jukumu
lako kuweza kujifunza na kukua kutokana na shukrani ulizonazo. Wewe utakuwa ni
watofauti sana ikiwa maisha yako yakiwa amejaa shukrani.
Zipo
fursa nyingi ambazo utaziona kupitia shukrani na hata ushirika na ikiwezekana
misaada ya watu utapata kulingana na shukrani zako.
Waangalie
watu ambao wana shukrani kwenye maisha na wale watu ambao hawana, utakuja kuona
watu hawa maisha yao ni tofauti kabisa.
Maisha
ya watu wenye shukrani utakuja kugundua yamejawa na utele wakati maisha ya watu
ambao hayana shukrani yamajawa na utupu.
Kila
siku ianzapo, kumbuka kuanza kumshukuru Mungu, shukuru upo kwenye siku ya
kipekee ambayo unaenda kufanya mabadiliko makubwa.
Hiyo
haitoshi shukuru pia juu ya kila unachokipata hata kama ni kidogo. Usipokuwa na
shukrani hata hicho kidogo unaweza kukikosa.
Msingi wa maisha yako pia unatakiwa kujenga kwenye shukrani hapo pia utakuwa umefanya jambo la maana sana la kuweza kukusaidia.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
KIPAJI CHAKO; Wosia Wa Mafanikio Kutoka Kwa Mama, Sehemu Ya 02
Ilipoishia wiki iliyopita
“Mama
Ester mke wangu kwa kweli mimi hali yangu siku ya leo naona haipo sawa kabisa
hivyo sidhani kama nitapona mke wangu ” sauti ile ya baba yenye kila aina
zote upole na ukarimu zilinifanya
niamini ya kwamba baba alikuwa amezidiwa sana usiku ule.
Sasa
endelea nayo………
“Kwa
kweli mke wangu hali yangu ni mbaya sana, najisikia joto sana harafu na kifua
changu kinawaka moto hivyo nakuomba uchukue japo nguo unipepee mke wangu”
Pamoja
hali ya baridi iliyokuwepo usiku ule, nilishangaa kwanini baba alikuwa anahisi
joto?
Huku
nikiwa nimesimamisha masikio yangu yalikuwa yamesimama dede kama mnala wa
baberi kusikiliza kile kilichojili chumbani kwa wazazi wangu,
Kwa wakati huo waoga ndio
uliokuwa umetawala akili mwangu……..
Nikiwa nikiendelea
kusikiliza kile kilichokuwa kikijili chumbani kwa wazazi wangu, nilimsikia mama
akinyanyuka na kwenda kufanya kile baba alichomuagiza, japo
na yeye mama yangu alikuwa ni mjamzito si ujauzito tu, bali ulikuwa ni ujauzito
wa miezi saba na nusu.
Wakati
maongezi ya baba na mama yakiendelea chumbani, nami huku nilikuwa nasali kwa
kasi zaidi ya 4G ili mwenyezi Mungu aweze kumponya baba yangu, kwani yeye ndiye
aliyekuwa msaada mkubwa sana katika familia yetu na masomo yangu kwa ujumla.
Wakati
nikiendelea kumuomba Mwenyezi Mungu aweze kumsaidia baba yangu aweze kupona
haraka, nilimsikia baba akisema;
“mke
wangu naomba unisamehe sana!” mama alihoji kwa sauti ya chini
“nikusamehe
kwa lipi tena mume wangu?
Naomba
unisamehe kwa sababu enzi za uzima wangu sikutaka kabisa kukufundisha kufanya
biashara yeyote, zaidi ya kukufundisha kulima, japo ilikuwa ni kwa asilimia
chache sana na kama unavyojua ya kwamba
kwa hapa kijini kwetu kitu pekee ambacho hutufanya sisi kupeleka mkono kinywani
ni kilimo pamoja na biashara ambayo nilikuwa naifanya mimi pekee yangu pasipo
kukufundisha wewe.
Na
siku ya leo kifo kinanikabiri na nikikutazama nagundua nakuacha katika mateso
makali sana, kwani nakucha pasipo kukuachia ujuzi wowote ambao utakusaidia
katika kufanya biashara, lakini pia nasononeka kwani najua familia yangu
itaishi maisha magumu sana.
Lakini
jambo la mwisho nawaza juu ya ujauzito ulionao kwani nafahamu fika mwanagu
atakua bila kujua sura ya mimi baba yake......
Wakati
baba anaendelea kusema maneno yale nilijawa na simanzi mayoni....... Niliwaza
ndani ya nafsi yangu, ni kwanini baba alisema maneno yale? Wakati baba
akiendelea kuzungumza na mama, nilimsikia baba sauti ikizidi kufifia huku
akizidi kuongea kwa tabu.
Mmmmmke
wangu, nananaku.......pe........nda sana, nakuomba nawe umpende mwaaaaanangu
Ester pamoja na huyo Mmm____mmtoto wetu mwingine ambaye atazaliwa.
Mara
baada ya baba kusema maneno hayo sikuisikia tena sauti ya baba zaidi ya
kuisikia sauti ya mama, ikisema;
Baba
Ester........ Bababa ester........
Mume
wangu baba ester.......amka mume wangu...........
Baba
Ester tafadhari nakuomba uamke mume wangu
Niliendelea
kumsikia mama akimuita baba pasipo mafanikio. Wakati kule chumbani kwangu
nikiwa katika hali ya ulutivu, nilimsikia mama akiniita kwa sauti ya juu,Ester
mwanangu njooooo.
Sauti
ile ya mama ilinifanya niogope, kwani ilikuwa si sauti ya kawaida ambayo mimi
binafsi nilikuwa nimeizoea, nilikaa kimya kidogo pasipo kuitika, mama alirudia
kunita tena kwa sauti nyingine.
Ester
mwanagu njooo, baba ako anaku……..
Nilitoka
mbio chumbani kwangu hadi chumbani kwa kina mama ambapo sauti ya mama ilinita
huko. Nilifika mlangoni wa chumba cha wazazi wangu na kubisha hodi,,,,,,, hooo
kabla sijamalizia kusema hodi, mama aliniamulu nipite.
Je
ni nini ester alikikuta huko chumbani, usikose muendelezo wa hadithi hii nzuri
ya kusimumua sehemu ya tatu siku ya jumamosi ijayo.
Mtunzi: Benson chonya
0757909942
Jan 27, 2018
Utengenezaji Wa Chakula Cha Kuku Kwa Kutumia Mchwa.
Rafiki, mchwa na funza
ni chakula bora sana kwa kuku. Chakula hiki kina protini kwa wingi sana
kwa mifugo yetu, ili kuku aweze kukua vizuri na kuwa na uzito mzuri anahitaji
vyakula vyenye protein kwa wingi.
Wadudu jamii ya funza
na mchwa ni jamii ya wadudu ambao wana protin nyingi, iwapo kuku wako utawapa
chakula hiki basi kuku wako watakuwa kwa haraka na watakuwa na uzito mkubwa
ambao itakua ni faida kwako.
Pia chakula hiki cha
mchwa na funza kinapunguza changamoto ya magonjwa kwa kiasi fulani hasa yale
magonjwa yanayotokana na lishe. Mpaka hapo unaona faidaya wazi itokanayo na
chakula hiki cha mchwa na funza.
1. UTENGENEZAJI WA FUNZA.
Ili uweze kutengeneza
funza unahitaji kuwa na vitu vifuatavyo; Nailon, samadi, maji na jembe na eneo
la kutengenezea.
Jinsi ya kutengeneza funza;
Tengeneza tuta.
Weka nailoni katika
tuta lako.
Weka samadi yako
(samadi mbichi ya Ng'ombe)
Weka udongo kwa mbali
kwa juu katika samadi yako.
Mwagia mwagia maji,
ninaposema mwagia mwagia maji namaanisha nyunyuzia maji katika tuta lako kwa
kiasi kidogo.
Funika juu kwa nailoni
katika eneo ambalo umetengeneza tuta lako hakikisha kusiwe na jua kali.
Katika tuta lako
hakikisha kunakuwa na unyevu unyevu.
Baada ya siku kumi
funua nailoni lako utakuta kunafunza wengi waache kuku wako wale hadi
watakapomaliza.
Baada ya kumaliza kula
funika tena na nailoni baada ya siku mbili utakuta tena kuna funza wakutosha
hivyo unatakiwa utengeneze matuta mawili au zaidi kwa ajili ya chakula kwa
mifugo yako,
2. UTENGENEZAJI WA MCHWA.
Ili kutengeneza mchwa
unahitaji kuwa na vitu vifuatavyo;
Samadi ya ng'ombe, maranda
ya mbao au majani makavu au mabua mahindi,
Mabox au chungu.
Jinsi ya kutengeneza mchwa.
Chukua samadi ya ng'ombe
changanya na maranda ya mbao vizuri mwagia maji michanganyiko wako
ulowane vizuri.
Weka kwenye
chungu au box michanganyiko wako.
Chukua chungu/box lako
weka katika njia ya mchwa kwa maana sehemu yenye asili ya mchuguu ambapo mchwa
wanapatikana.
Baada ya siku tatu
utaona box lako linamejaa mchwa chukua ka wape kuku wako wale.
Hapa ndipo mwisho wa
somo letu la leo natumaini umejifunza mengi katika somo la leo nenda kayafanyie
kazi haya uliyojifujifunza ili kuboresha mifugo yako.
MUHIMU;- Chakula hiki kitumike
kama chakula cha ziada.
Nikutakie utekelezaji
mwema na tutaonana wakati ujao, usipange kukosa mfululizo wa makala hizi.
NI MIMI RAFIKI YAKO,
FRANK MAPUNDA,
0758918243/0656918243.
Jan 26, 2018
Hata Kama Unaona Unashindwa Sana, Ipo Sehemu Hii Yenye Ushindi Wako.
Pamoja
na kwamba maisha yana changamoto nyingi sana, lakini kipo kitu cha kijifunza
kupitia changamoto hizo hata kama zinakukatisha tamaa sana.
Pamoja
na kwamba unaweza kudondoka au ukashindwa kwa namna fulani kwenye maisha yako,
lakini upo uwezekano wa kuamka na ukawa mshindi tena.
Pamoja
na kwamba unaweza ukapata hasara sana kwenye biashara au chochote kile
ukifanyacho, lakini upo uwezekano wa kupata faida iliyo kubwa tena.
Pamoja
na kwamba kuna kukakatishwa sana tamaa kwenye maisha yako, lakini tambua
tumaini la kukuwezesha kusonga mbele kwenye mafanikio uyatakayo lipo.
Ushindi wa mafanikio yako upo, ukiamua. |
Pamoja
na kwamba umekuwa ukikosea na kufanya mambo mengi kwa njia ambayo si sahihi,
lakini upo wakati ambao utaweza kufanya mambo yako kwa usahihi pia.
Unachopaswa
kuelewa hapa ni kwamba, kwa sura yoyote ile ambayo maisha yanakujia, hata kama
ni kwa sura mbaya, tambua ushindi upo.
Huhitaji
kulia, huhitaji kulalamika sana kwamba maisha yako ni hovyo sana, upo upande wa
pili ambako kuna ushindi wako pia.
Hata
inapotokea hali unaona kama umekandamizwa na maisha, huwezi kunyanyuka, nikwambie
tu uwezekano wa kunyanyuka tena upo, unatakiwa kulijua hilo akilini mwako.
Kitu
kikubwa unachotakiwa kuelewa, kama upo kwenye upande wa kushindwa, unatakiwa kufanya
jitihada za kuwa kwenye upande wa ushindi kimafanikio.
Maisha
hayapo kwenye upande wa ubaya tu, maisha yana pande mbili, upande wa hasi na
upande wa chanya ambao ni ushindi.
Kwa hiyo
kila unapoona kama dunia inakuonea au unajiona kuna vitu umekosa kabisa, unatakiwa
kukumbuka upo wakati utakuwa huru na hautaweza kuonewa.
Unatakiwa
uondokane na fikra za kufikiri sana ubaya katika maisha yako, mambo yakija
kinyume na ulivyotarajia, ujue ushindi pia upo.
Upo upande
wa ushindi, upo upande ambao unatakiwa uufanyie kazi na uweze kushinda kwenye
safari ya mafanikio.
Upande
wa mafanikio upo, hilo unatakiwa kulijua kila wakati, nakukumbusha tena hutakiwi
kukata tamaa au kujiona huwezi tena, mafanikio yako yapo.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Jan 25, 2018
Mbinu Itakayokufanya Ukue Kibiashara Ili Upate Faida Ni Hii...
U hali gani mpenzi
msomaji wa mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO bila shaka u mzima
na unaendela vyema na majukumu yako ya kila siku, naomba nichukue wasaa huu
nikukaribishe siku ya leo ili tuweze kujifunza kwa pamoja mbinu moja ya
muhimu ambayo itakufanya ujiongee thamani na wateja kwa ujumla katika biashara
unayofanya.
Nimekuletea mbinu hii
moja muhimu kwa sababu nimegundua ya kwamba ni mbinu ambayo imekuwa
ikiwasaidia wafanyabiashara wengi wakubwa kwa wadogo, ambao wamekuwa
wakiiitumia mbinu hiyo.
Naomba pia niwe muwazi
kwako kama endapo mbinu hiyo haitukusaidia endapo utaamua katika biashara
yako naomba tuwasiliane nipo tayari kurudisha kiwango cha Mega bites(Mb)
zako ambazo utatumia kusoma makala hii.
Pasipo kupoteza muda
mbinu hiyo ni kutoa ofa kwa wateja wako au ‘promotion’ kama wengi
wanavyopenda kuita.
Kanuni hii kwa
mfanyabishara mdogo anaweza akasema labda kanuni hii hamhusu ila ukweli ni
kwamba kanuni hii ni nzuri sana kwa mfanyabishara mdogo na mfanyabishara mkubwa
pia, hii ni kwa sababu mbinu hii ina mashiko sana katika kuikuza biashara yako.
Hata ukifanya
uchunguzi wako usio rasmi utagundua makampuni yaliyo mengi yana ushindani
mkubwa katika jambo hili la utoaji wa ofa, yaani wengi wao wamekuwa
wakiishinda kuleta ofa mbalimbali mpya zitakazowavutia wateja wa zamani
na wateja wapya.
Na katika ofa hizo
huendana na maneno mazuri yenye kuleta hamasa za kumvutia mteja, wapo
ambao utawasikia wanasema ya kwamba jaza ujazwe, wapo wengine ambao husema onja
msimumuko, wapo wengine husema jipimie, wapo wengine husema usipoelewa
utarudishiwa ada yako na maneno mengine kama hayo.
Yupo mfanyabishara
mwingine nimewahi kukumbana na bango dukani kwake lenye maneno yanasomeka
hivi “ ofa ofa piga picha mbili kwa bei ya moja” mwisho
wa kunukuu. Kwa maneno kama haya unadhani mteja hawezi kwenda kweli? Naomba
majibu ya swali hilo uyaweke ‘password.’
Hivyo haijalishi ni
biashara ndogo au kubwa ni vyema kuna wakati uweze kutoa ofa kwa wateja
wako na katika kutoa ofa hii ni lazima uzingatie ya kwamba ni lazima iwe ofa
ambayo haitakuletea maumivu makubwa katika biashara yako, bali iwe ni ofa
ambayo itakuongezea faida kwani siku zote ikumbukwe utoaji wa ofa katika
biashara huleta faida.
Mwisho nisikuchoshe
kwa maneno mengi, kwani maneno mengi hayavunji mfupa bali nikwambie ya kwamba
biashara ili iweze kwenda vizuri inahitaji pia ni ofa na ofa huleta faida na wateja kemkem. Hivyo walau kwa mwaka ukiweka ofa moja katika biashara
yako basi itapendeza zaidi.
Ndimi: Benson chonya
0757909942
Jan 24, 2018
Hukuna Kinachoshindikana Kwenye Maisha Yako Ukiamua Hivi…
Upo uwezekano
mkubwa sana kwa kile unachokifanya pengine unakiona kama hakiwezekani na hauna
nafasi tena ya kufanikiwa kwa hicho na hata kwa maisha yako kwa ujumla. Hali hiyo
inaweza ikawa inakutokea sana na kujiona wewe si kitu.
Lakini
kabla hujakata tamaa naomba nikwambie hivi, kwa vyovyote vile iwavyo mtu pekee
ambaye ana uwezo wa kubadilisha maisha yako ni wewe mwenyewe. Kukata tamaa
hakuwezi kukusaidia kwa namna yoyote ile zaidi ya wewe kuamua kuchukua hatua.
Maisha ya mafanikio ni matokeo ya kuthubutu sana kuchukua hatua hadi kuweza
kufanikiwa kwako. Ikiwa lakini utakuwa unachukua hatua za kukata tamaa hutaweza
kufika popote zaidi utaweza kukwama.
Ukiweza
kuthubu kila siku na kila wakati hakuna maisha ambayo hutaweza kuyapata. Ngazi ya
mafanikio fulani utaifikia tu kama wewe ni mchukuaji wa hatua na hakuna
kinachoshindikana juu ya hilo hata siku moja.
Tatizo
walilonalo watu wengi ni kule kukaa na kufikiri kwamba maisha yao ya leo jinsi
yalivyo na ndivyo jinsi yatakavyokuwepo vivyo hivyo hata kwa miaka ijayo. Hicho
unachokifikiri sio sahihi na kinakupoteza kabisa.
Leo unaweza
ukawa na maisha mabaya sana, lakini kesho ukumbuke hayawezi kuwa hivyo kama
unachukua hatua. Kila siku mpya inakuja na fursa zake, kwa nini ugande na fikra
potofu kwa kukariri kwamba maisha yako ya leo ni sawa na ya kesho?
Hutakiwi
kuwaza hivyo hata siku moja, chukua hatua za kubadilisha maisha yako, hata kama
maisha yako unaona hayabadiliki mara moja, lakini elewa kuna wakati itafika
maisha yako hayo yatabadilka hata kama yana hali ngumu sana.
Ndio
maana nakwambia hakuna kinachoweza kushindikana kwenye maisha yako kama ukiamua
kuchukua hatua za kuthubutu. Watu wote wenye mafanikio wanathubutu, kama itatokea
huwezi kuthubu ni ngumu sana kuweza kufanikiwa.
Anza
leo kufanya jambo ambalo umekuwa ukilitamani sana kulifanya. Huwezi kulifanya
lote zima zima anza kulifanya kwa kidogo kidogo hata kwa mithili ya nukta
lakini anza. Kwa kuanza kwako unakuwa ndio unathubutu na kubadilisha maisha
yako.
Kile
utakachokifanya leo hata kama ni kidogo sana lakini ina nafasi kubwa ya kuweza
kubadilisha maisha yako na kuwa bora hata kama huoni matokeo ya ghafla
yakitokea. Kikubwa thubutu na chukua hatua.
Unapaswa
kuelewa kwamba hakuna kitakachoweza kushindikana kwenye maisha yako kama wewe
hautaweza kuchukua hatua za kuthubutu na kuhakikisha ndoto zako zinaweza
kutimia. KILA KITU KINAWEZEKANA.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia rafiki,
kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)