Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Wednesday, November 25, 2015

Mambo 5 Yatakayokusaidia Kutokuwa Na Mawazo Mengi Yaliyopitiliza.

No comments :
Kati ya tatizo ambalo huwa ni kubwa na linawakabili baadhi yetu bila kujua ni tatizo la kuwa na mawazo mengi. Wapo watu ambao huwa wanafikiria sana matatizo yao, shida zao au changamoto zao kiasi kwamba kwa wengine hupelekea kama kuchanganyikiwa. Natambua umeshawahi kukutana na watu wa namna hii mara kwa mara tu.
Kuna ambao ulipokutana nao walikuwa ni watu wa kuongea peke yao njiani. Pia kuna wengine ambao uliwahi kukutana nao wakiwa ni watu wa kujiinamia tu muda wote. Lakini watu hawa chanzo chao kikubwa ni nini kila ulipowafatilia, hakuna tatizo lingine, zaidi ya hili la kuwa na mawazo mengi ambayo yapo akili mwao muda mrefu.
Kitu kibaya kuliko vyote kwa binadamu ni kwamba, tatizo hili kwa bahati mbaya linapoanza kwa mtu kuisha kwake huwa sio rahisi sana. Tuchukulie kwa mfano umekuwa una mawazo mengi ya mara kwa mara yaliyokupelekea ukaanza kuongea mwenyewe. Tatizo kama hili likisha kuanza, kukuisha litachukua muda mwingi au linaweza lisiishe kabisa na ukawa ndiyo umechanganyikiwa. kwa hiyo ni lazima kuepuka kutokujiweka katika hali ya kuwa na mawazo mengi  hasa kutokana na ukubwa wa athari zake.
Sasa unawezaje kutoka kwenye tatizo hili la kuwa na mawazo mengi?
1. Ishi sasa.
Wengi wanapata tabu na kujikuta wakiwa na mawazo sana kutokana na wao kuamua kuishi jana au kesho. Hapa ili uweze kuondokana na mawazo yanayokutesa unatakiwa kusahau kila kitu kinachokusumbua kiwe kimetokea jana au kiwe kinakuja kesho. Kama kuna deni unalotakiwa ulilipe kesho lisahau mara na ishi sasa kesho hiyo ikifika itaeleweka hapo hapo.
Ruhusu mawazo yako yafikirie pale ulipo. Acha kujibebesha mizigo mingi ambayo huwezi kuibeba kwa pamoja. Acha kujibebesha matatizo ya jana na ya kesho halafu yote ukawa nayo leo. Kwa hilo hutaweza zaidi utazidi kuwa na mawazo kama uliyonayo sasa. Weka maisha yako yawe huru kwa kuamua kuishi sasa na sio kesho.

2. Jijengee mitazamo chanya.
Siri nyingine itayokufanya uishi kwa kutokuwa na mawazo mengi sana ambapo wakati mwingine unahisi hata kuchanganyikiwa ni kwa wewe kujijengea mtazamo chanya. Fikiria yale mambo yanayokufurahisha na kukupa matumaini. Acha kuweka fikira zako sana kwenye jambo linalokusumbua, hiyo itakuongezea mawazo zaidi.
Kwa jinsi utakavyoendelea kufikiria yale mambo yanayokupa furaha, ndivyo ambavyo utajikuta mawazo mengi ambayo ulikuwa nayo yanazidi kupungua kidogo kidogo. Kumbuka, unapata kile unachikzingatia. Kama unazingatia furaha basi basi utapata furaha. Kama unazingatia matatizo halikadhalika utapata hayo hayo matatizo kwenye maisha yako.
3. Kuwa makini na mawazo yako.
Katika kipindi ambacho unakuwa na mawazo mengi zaidi, jambo ambalo unatakiwa kuchunga sana ni mawazo uliyonayo. Ni kipindi ambacho unatakiwa kuwa makini na jinsi unavyoruhusu mawazo yako yaingie akilini mwako. Wengi ukumbuke huwa tunapata mawazo hasi pengine kutokana na maneno ya watu ambayo huwa tumeambiw.  Sasa hayo ni moja ya mambo ambayo tunayotakiwa kuwa makini nayo sana.
Hata hivyo, kumbuka mara nyingi jamii tunayoishi ni hasi sana hivyo kuweza kuwa chanya wakati wote inaweza ikawa ni jambo gumu zaidi. Hivyo kitu cha kufanya ni kuhakikisha kila mara na kila wakati kama mtu akikuuzi achana naye na usipeleke hayo mawazo kichwani mwako moja kwa moja. Hiyo itakuwa njia rahisi sana ya kukufanya usiwe na mawazo mengi akili mwako.
4. Badilisha mazingira.
Inawezekana ukawa unazidi kuwa na mawazo zaidi kutokana na mazingira uliyopo. Kitu pekee cha kufanya kwako ni kuhakikisha unabadili mazingira hayo yanayokuplekea uwe na mawazo hayo. Unaweza ukaenda katika eneo tulivu kama baharini au ziwani kupata upepo mwanana. Kwa mazingira kama hayo ni lazima mawazo yako yabadilike.
Kwa hiyo ni lazima uendelee kutokung’ng’ania mazingira ambayo kwako siyo rafiki yanayokufya uendelee kuwaza mawazo yaleyale kila wakati. Kaa mbali na mazingira hayo hiyo itakusaidia sana katika hali ya kuweza kuondokana na mawazo hasi yanakusumbua. Ukitumia mbinu hii itakupa matokeao chanya na ya muda mfupi kuliko unavyofikiri.
5. Fanya tahajudi(Sala).
Ni jambo zuri sana pale unapokuwa na mawazo ikiwa utafanya tahajudi au sala. Hiyo itakusaidia kuyaweka mawazo yako katika hali tulivu zaidi. Unaweza ukafanya hili kwa kutafuta eneo ambalo ni tulivu na ukawa unafanya sala au tajudi angalau kwa muda mchache sana kwa siku. Hiyo itakusaidia kujenga kupunguza mawazo mengi uliyonayo.
Nakutakia siku njema na endelea kujifunza kila siku ila usikose  kumshirikisha na mwingine aweze kujifunza kupitia matandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Kama una maoni, ushauri au changamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio yako wasiliana nasi kwa:-
Simu; 0713 048 035,

No comments :

Post a Comment