google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 19, 2017

Kama Usiposhinda Kwenye Vitu Hivi, Sahau Mafanikio.

No comments :
Kitu ambacho natamani kila mtu angalau aelewe, ni kwamba huwezi kupata ushindi mkubwa kama haujawahi kupata hata ushindi kidogo. Hiyo ikiwa na maana, ili uweze kushinda makubwa lazima ushinde kwanza madogo.
Unapokuwa unapata ushindi mdogo, ni rahisi kukupa hamasa, mzuka, nguvu na hata jeuri ya kuendelea kufanya mambo mengine kwa uhakika ambapo utashangaa mambo hayo yanakupa mafanikio hata bila kutarajia.
Hali hii ndio tunayoiita nguvu au majabu ya mafanikio madogo madogo. Kuna nguvu sana ya kufanikiwa kwa vitu vidogo vidogo na kuweza kukusaidia kufanikiwa. Kile unachokiona ni kidogo kwako, lakini kina nguvu ya kuweza kukuvusha na kukupa mafanikio.

Ushindi mdogo, ni nguzo ya mafanikio makubwa.
Unatakiwa utulie na uelewe ili kuweza kutawala makubwa, kwanza unatakiwa kutawala mambo madogo. Ili kutawala biashara kubwa unayoitaka, ni lazima na muhimu sana kwanza kutawala biashara ndogo tena kwa mafanikio.
Mafanikio  makubwa yanakuja kutokana na nguvu ya kufanikisha mambo madogo madogo. Sasa nguvu hii haiji kwa bahati mbaya bali ni kutokana na ushindi mdogo unaoupata. Hivyo unaona ili uweze kuwa mshindi kwa chochote kikubwa, ushindi mdogo ni muhimu sana.
Huhitaji kujiuliza sana ushindi mdogo utaupata vipi wakati huna hata kitu cha kufanya. Sikiliza, kuamka asubuhi na mapema yenyewe na kufanya majukumu uliyojiwekea na ukafanikisha huo ni ushindi. Kusoma kitabu angalau kurasa 20 kwa siku pia huo ni ushindi.
Au labda nikueleze hivi haijalishi  hapo ulipo una kazi maalumu au huna, lakini kama unafanya vitu fulani hata kama ni vidogo sana na ukavifanikisha huo ni ushindi pia ambao unatakiwa kuuzingatia.
Inawezekana ukawa huoni maendeleo ya ushindi wako kwa sababu hufatilii, lakini hebu leo anza kufatilia ushindi wako mdogo. Utashangaa unavyofatilia unazidi kupata nguvu ya kufanya tena na tena.
Mafanikio wakati mwingine yana kawaida ya kuja kwa ‘rekodi’ zake. Kwamba kutokana na umekuwa ukishinda hili na lile basi upo uwezekano na hili hata kama linaonekana gumu sana, uwezo wa kulishinda unalo kwa sababu tu ya ‘rekodi zako’ zinaonyesha hivyo.
Kuelewa vizuri hapa angalia timu mbili za mpira kabla hazijaanza kucheza, kwanza zinawekwa kumbukumbu za michezo waliyowahi kucheza na nani ameshinda mara ngapi na kuna matarajio gani.
Kama si hivyo hata mchezo wa ngumi uko hivyo hivyo zile ‘rekodi’ za nyuma zinaanza kuwekwa kwanza kabla mchezo haujachezeka. ‘Rekodi’ hizo zinawekwa kuangalia nani alikuwa mshindi kwenye mapambano mangapi na upo uwezekano wa nani leo kushinda.
Mpaka hapo, sina shaka sasa kwa sehemu unanielewa juu ya umuhimu wa kuweka kumbukumbu juu ya ushindi wako mdogo anaoupata. Kumbuka, ushindi mdogo unaoupata unaweza kutumika kama ngazi ya kukupeleka kwenye mafanikio ya juu.
Elewa unaposhinda kwenye vitu vidogo, unapata nguvu ya kujiamini na kuamini alaa kumbe inawezekana. Pia unapokosa ushindi mdogo ni ngumu sana kufanikiwa kwani ndani mwako zinajengeka fikra za kuona kwamba huwezi kufanikiwa kwa kila kitu.
Nikutakie siku njema, endelea kusheherekea ushindi mdogo unaoupata kwenye maisha yako kila wakati, lakini elewa ushindi mkubwa unakusubiri na unakuja pia.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.