google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Aug 20, 2017

Acha Kuharibu Hatma Ya Maisha Yako Yote, Kwa Sababu Ya Kitu Hiki Tu.

No comments :
Kwa kawaida vipo vitu vingi vinavyopelekea maisha ya mtu kuharibika na kuwa ya kushindwa kabisa. Vitu hivi kuna wanaovijua kwa uwazi na pia kuna ambao hawavijui au hawana habari kwamba ndio chanzo cha kushindwa kwao.
Kama nilivyokwambia  vipo vitu vinavyopelekea kushindwa kwa wengine katika maisha. Lakini leo kupitia makala haya, nataka nikwambie kitu kimoja tu, ambaco kama utakibeba sana,utake usitake utashindwa na  kuharibu maisha yako yote.
Kitu hicho sio kingine bali ni kukata tamaa mapema. Kama unakata tamaa mapema tambua kabisa unakua umeamua kuharibu hatma ya maisha yako mwenyewe. Hakuna mtu aliyefanikiwa mwenye sifa ya kukata tamaa mapema.
Watu waliofanikiwa ni wabishi, wanakomaa na ndoto zao hadi kuweza kufanikiwa. Lakini kama una ndoto yako, halafu kutokana na changamoto ukaamua kuachana na ndoto hiyo, elewa kinachotokea sio tu unajiumiza sasa, bali pia unapoteza kesho yako sana.

Usikate tamaa mapema.
Kila maamuzi unayoyachukua kwenye maisha yako, yanamuathiri mtu mmoja muhimu sana kwenye maisha, ambaye ndiye wewe. Hata uamuzi wa kukata tamaa na kuacha ndoto zako zisifike mwisho, pia ni uamuzi ambao ni hatari na unaharibu kesho yako.
Hatma ya maisha yako ya kesho, inategemea sana maamuzi unayofanya leo. Inapotokea ukafanya maamuzi ya kukata tamaa kwa kitu unachokifanya, elewa unajitengenezea mazingira ya kuharibu sana maisha yako kesho.
Hivyo kutokana na kukata tamaa mapema unajikuta unakuwa ni mtu wa kuanza jambo hili leo, tena kesho unaanza lingine. Kwa maisha hayo unashangaa unapoteza muda na pia unapoteza mafanikio yako ya kesho kwa sababu ya kukaa tamaa.
Kama una wewe ni mtu wa kukata tamaa sana, ukumbuke katika maisha yako hakuna kitufe cha kubonyeza kurudisha maisha yako yakarudi nyuma, maisha yanavyosonga mbele, hayarudi nyuma hata kidogo.
Kikubwa unachotakiwa kujua ni kwamba ili kufanikiwa unatakiwa kukomaa na kuvumilia kila hali. Hakuna anayepitia mteremko wa maisha, kila mtu anachangamoto zake. Ukifanya mchezo na ukaendeleza  kukata tamaa hutafanikiwa.
Kama unaona maisha ni magumu, elewa huo ugumu ndio unatakiwa kukomaa nao na kuushinda. Hata hivyo ukiangalia nani aliyekupa ahadi kwamba maisha ni mepesi? Changamoto kwenye maisha zipo toka enzi za mababu, kuwa mvumilivu ili kufanikiwa.
Jaribu kukaa chini na kujiuliza, kesho yako itakuwaje ikiwa kila kitu unakata tamaa mapema? Nikwambie kitu rafiki yangu, usikubali hata kidogo kuharibu hatma yote ya maisha yako kwa sababu ya kukata tamaa, nimesema kuwa mvumilivu utashinda.
Nakutakia mafanikio mema na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku kwa ajili ya kujifunza maisha na mafanikio.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.