Sep 30, 2016
Mbinu Za Kukuza Biashara Ndogo.
Ni
ukweli usiofichika zipo changamoto nyingi sana hasa pale unapukuwa unaanzisha
biashara na kuitaka ifike mahali ikue na kujitegemea. Pamoja na changamoto
nyingi kama za masoko au ushindani pia huwa ipo changamoto nyingine ya namna ya
kukuza biashara yako.
Wafanyabiashara
wengi wadogo inakuwa inafika mahali hujikuta wako palepale miaka nenda rudi bila
kupiga hatua kubwa mbele. Hiyo yote hutokea hivyo kwa sababu wanakuwa wamekosa
maarifa ya kukuza biashara zao kwa namna moja au nyingine.
Kwa
kusoma makala haya inakusaidia kujua mbinu zitakazo kusaidia kama wewe ni
mfanyabiashara mdogo kuweza kukuza mtaji wako taratibu na kufika mahali na wewe
ukawa na biashara yako kubwa kama wengine unavyowaona.
Je,
mbinu hizo ni zipi? Fuatana nami mwanzo hadi mwisho kuweza kuzijua mbinu hizo
na kuzifanyia kazi.
1.
Jitume sana.
Inawezekana
biashara yako ikawa ni kuuza matunda. Pia inawezekana biashara yako ikawa ni ya
uchuuzi yaani kutoa badhaa eneo moja na kuzipeleka eneo lingine kuziuza.
Sasa
unapokuwa na biashara ndogo kama za namna hii, ili uweze kufanikiwa ni lazima
ufanye kazi kwa bidii sana na kujituma kwa nguvu zote bila kuchoka.
Kuwa mbunifu. |
Ikiwa
hautafanya hivyo ni lazima hautapiga hatua na biashara yako itakufa. Unajua ni
kwa nini itakufa? Ni kwa sababu katika kipindi hiki biashara yako inapokuwa
ndogo inataka uangalizi wa hali ya juu sana ili iweze kukua.
Hivyo,
utalazimika kujituma sana na kufanya kila aina ya jitahada ambazo zitapelekea
kuifanya biashara yako ikaweza kukua na kufika mahali ikajitegemea yenyewe.
2.
Kuwa mbunifu.
Mbali
na kujituma kapindi ambacho unakuwa una biashara ndogo, jitahidi uwe mbunifu.
Unapokuwa mbunifu inakusidia sana kugundua ni kitu gani ambacho wateja wako
wanataka au ni kipi ambacho hawataki. Hiyo ni njia bora sana itakayokusaidia
kuboresha pale kwenye mapungufu na itakusaidia sana pia kuweza kuikuza biashara
yako.
3.
Sikiliza malalamiko ya wateja.
Ni
vyema pia ukawa ni mtu wa busara kuweza kusikiliza kile ambacho wateja wako
wanakisema katika kipindi hiki cha kukuza biashara yako. Hiyo itakusaidia
kutimiza matakwa yao na itakupelekea kuwa na wateja wengi ambao watasaidia kuifanya biashara yako ikue.
4.
Tafuta msaada.
Katika
kipindi cha kukuza bishara yako na kuifanya iwe kubwa, acha kujaribu kuishi
kama kisiwa. Tafuta msaada wa ushauri kwa wale waliofanikiwa wakusaidie
kimawazo wao walifanya nini hadi wakafikia huko waliko sasa.
5.
Punguza utegemezi kwenye biashara yako.
Pia
unapokuwa unaikuza biashara yako acha kutegemea sana pesa unayoipata kwenye
biashara yako ndiyo iendeshee maisha yako. Jaribu kuwa na pesa nyingine,
vinginevyo bila kufanya hivyo unaweza ukaua kila kitu bila kujijua.
6.
Jifunze kukuza mtaji.
Kwa
namna yoyote ili biashara yako ikue na ikafika mahali inajitegemea unalazimika
sana kujifunza mbinu za kukuza mataji
wako. Hilo ni somo ambalo unatakiwa ulizingatie sanaa na kujiuliza kila wakati
ni nini kifanyike ili mtaji uweze kukua.
kwa
kifupi, hayo ndiyo baadhi ya mambo machache yanayoweza kukusaidia kuweza kukuza bishara yako kama
unaanzia chini.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza na kuhamasika.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO,
IMANI
NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com
0713048035.
Sep 29, 2016
Msingi Imara Wa Mafanikio Yako.
Ipo faida kubwa maishani mwako endapo
utaamua leo kuchukua hatua mathubuti ya kutaka kufanikiwa. Tupo hivi tulivyo
kwa sababu hututaki kuchua hatua sitahiki za kiutendaji kwa yale yalipo akilini
mwetu na kuyaweka katika matendo. Watu wana maarifa lakini suala la kuyaweka
maarifa hayo katika matendo.
Kuwepo kwa hali hii ndiyo ambayo inasababisha
kuweza kuyatamani mafanikio na si kuyaishi. Hata hivyo moja ya siri nzito ya
mafanikio yako husukumwa na kiu kubwa sana aliyonayo mtu kutaka
kufanikiwa, lakini kiu hiyohiyo huendana na msukumo na nia thabiti ya kuyaweka
yale unayoyajua katika matendo.
Nasisitiza hili kwa sababu moja kubwa
watu wengi wanaishi maisha ya kawaida kwa sababu wameamua hali hiyo kutokea,
lakini ili kuondokana na hali hii huna budi leo hii kuacha kuishi kikawaida kwa
sababu wewe sio mtu wa kawaida.
Huenda ukawa unajiona wewe ni mnyonge
katika maisha kwa sababu labda uliwahi kufeli kwenye jambo fulani ambalo
ulitegemea ya kwamba litakupa matokeo chanya lakini matokeo yake yakawa kinyume
chake. Lakini Amini usiamini ila ukweli ni kwamba watu wengi ambao wamefanikiwa
wao walikuwa ni watu ambao hawakutaka kuishi kikawaida.
Hivyo hajalishi umefeli kwa kiwango
gani ila lakini iambie nafsi yako ya kwamba wewe si mtu wa kukata tamaa bali ni
mtu wa kusonga mbele kivitendo zaidi.
Tengeneza msingi bora wa mafanikio yako kwa kuamua kutokuwa wa kawaida. |
Kuishi kikawaida ni sumu sana katika
maisha yako. Wapo baadhi ya watu wamefeli kimaisha kwa sababu walikatishwa
tamaa na watu wengine, huenda ukawa ni wewe ambaye unasoma makala haya ila
ukweli ni kwamba maisha halisi ya kwako unayo wewe na si mtu mwingine
haijalishi watasema nini ? Ila we songa mbele kivitendo ila pale unapofanikiwa
wabaki midomo wazi. Maana dunia hii imejaa wakatishaji tamaa.
Na kila mara tuzidi kuukumbuka ule
usemi mtamu ambao unasema usiwambie watu ndoto yako, bali waosheshe ndoto hiyo
kwa vitendo zaidi. Kwani kuwashirikisha watu juu ya ndoto yako, wapo baadhi ya
watu endapo utawaambia jambo lako asilimia kubwa watakwambia haiwezekani.
Pia kwa kuwa maneno yana nguvu sana
utajikuta kweli umeshindwa kuifanya hiyo ndoto yako . Simama imara kila mara
kwa sababu wewe ni mshindi katika ulimwengu huu.
Kabla sijaweka nukta siku ya leo,
nikandamizie maneno haya ya kwamba ili uweze kushinda vita vya umaskini,
hautitaji uongozi imara kama ambavyo tumekalilishwa mashuleni, ila unahitaji
kuwa bora kwa jambo lolote unalolifanya.
Kama ni biashara hakikisha unazalisha
bidhaa yenye ubora kila mara, ukifanya hivi ni chachu kubwa sana ambayo
itafanya wateja waongezeke wenyewe na si kuwa na kiongozi bora katika eneo lako
unaloishi.
Nasema masuala haya ya uongozi
kwa sababu idadi kubwa wanahusisha masuala ya maisha yao kuwa magumu na
masuala mazima ya uongozi, lakini ukweli ni kwamba ukifanya uchunguzi wa
kutosha juu ya maisha yako utagundua ni nini ambacho nasema.
Maisha yako kuwa magumu usiyahusishe
na masuala ya uongozi, bali tafakari katika kila kona ambayo unafanya kazi kwa
kufikiri ni namna gani unaweza kuwa bora? Ukipata majawabu sahihi ya jinsi ya
wewe kuwa bora hiyo siri kubwa ambayo ipo kwako ya wewe kufanikiwa.
Kama ni mwanafunzi fikiri jinsi
ambavyo utakuwa bora katika taaluma yako, kama wewe ni msanii katika eneo
lolote lile fikiri ambavyo utaweza kufanikiwa na sio kushirikisha imani potofu
kutofanikiwa kwako na imani ambazo sio za msingi.
Dunia ni pana ila kwa maneno machache
sana, kwa leo niishie hapo tukutane mara nyingine ambapo tutazidi kuelimishana
masuala mazima ya mafanikio. Hivyo nikunong'oneze badili mfumo wa maisha yako
kwa kuwa na fikra sahihi.
Endelea kujifunza kupitia
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama makala hii
imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la Whats App ili
uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO
YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI
KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Na; Afisa mipango Benson Chonya,
Sep 28, 2016
Hatua Muhimu Za Kutengeneza Uhuru Wa Kifedha.
Ili
uweze kuishi maisha ya mafanikio makubwa kwako na kuwasaidia wengine ni lazima
kwanza uwe huru kifedha. Unapokuwa upo huru kifedha ni hatua inayokufanya
kuweza kutekeleza mahitaji yako yote ya kifedha, ikiwa pamoja na hata kusaidia
wengine bila tatizo lolote lile.
Hivyo
mpaka hapo unaona kwamba, ni lazima sana kuufikia uhuru wa kifedha ili kuishi
maisha yenye manufaa kwetu na kwa wengine wanaotuzunguka. Sasa jambo la muhimu
kuelewa hapa, tunawezaje kuufikia huo uhuru wa kifedha? Ni hatua zipi ambazo
tunatakiwa tuzifuate?
Zifuatazo
Ni Hatua Muhimu Za Kutengeneza Uhuru Wa Kifedha.
1.
Jiwekee malengo ya kifedha.
Tambua kwamba Ili
kufikia uhuru wa kifedha, kabla ya kuanza kuwekeza, kuweka akiba, kutengeneza
bajeti au kuweka pesa ya dharura, kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya ni
kujiwekea malengo ya kifedha. Hiki ni moja ya kitu muhimu sana katika kuufikia
uhuru wa kifedha.
Jiwekee malengo ya kifedha. |
Jiwekee
malengo ya kifedha yaliyowazi na yanayoeleweka. Kwa mfano, unaweza ukajiwekea
malengo kwamba baada ya miaka mitano ijayo
nataka kumiliki milioni mia moja. Pengine unaweza ukajiwekea malengo ya kifedha
kwamba ili kutimiza lengo hilo, kila mwaka ni lazima niingize milioni ishirini.
Unapokuwa
na malengo ya wazi kama hivi ya kifedha, inakuwa ni rahisi kwako kuufikia uhuru
wa kifedha. Unajua ni kwa nini? Ni kwa sababu unakuwa unajua unakotaka kufika
kifedha na pia inakuwa sio rahisi kwako kupoteza pesa zako kwa mambo yasiyokusaidia
kuufikia uhuru huo unaotaka.
Kwa
hiyo, ili uweze kuufikia uhuru wa kifedha, jambo la kwanza la kuzingatia,
jiwekee malengo ya kifedha. Tafuta daftari lako la kumbukumbu na andika
unahitaji pesa ngapi kwa mwaka, unahitaji pesa kiasi gani baada ya miaka
mitano. Kwa kufanya hivyo utaufikia uhuru wa kifedha kwa sababu juhudi zako
zitakuwa kubwa sana kukusaidia kutimiza lengo lako.
2.
Tengeneza bajeti.
Mara
baada ya kujiwekea malengo ya kifedha, hatua inayofuata ni kutengeneza bajeti yako. katika hiyo bajeti
utakayoitengeneza ni lazima uifuate na kuitekeleza kila siku. Unapokuwa
unaifuata bajeti yako inakusaidia zaidi kuwa karibu na lengo lako la kuufikia
uhuru wa kifedha.
Ili
kufanikisha hili vizuri, kabla hujapata pesa andaa orodha ya vitu
utakavyokwenda kununua kabla. Kisha baada ya hapo fanya manunuzi kama orodha
yako inavyosema na sio kinyume chake. Kwa hiyo unaona, Kila unapokuwa na bajeti
yako na ukaitekeleza, inasaidia kuokoa pesa ambazo zingepotea bila sababu na
inakuwa ni chanzo cha kuufikia uhuru wa kifedha.
3.
Weka akiba.
Kwa
kiasi chochote cha pesa unachokipata hata kiwe kidogo vipi, jifunze kuweka
akiba angalau kwa sehemu. Watu wengi hili ni somo gumu sana kulielewa juu ya
uwekaji wa akiba na ni kiwazo kikubwa cha kuufikia uhuru wao wa kifedha.
Sasa
kwa lugha rahisi ili uweze kuufikia uhuru wa kifedha ni lazima uweke akiba. Unapokuwa
unaweka akiba inakuwa inakusaidia sana kutengeneza mtaji kidogo kidogo kama
huna mtaji huo au unaazia chini kabisa kimaisha.
4. Jiwekee pesa ya dharura.
Hata
uwe unaingiza pesa nyingi vipi lakini moja ya jambo ambalo unatakiwa kulifanya
ili uweze kuufikia uhuru wa kifedha ni kutenga fedha ya dharura. Kiuhalisia binadamu
tunachangamoto nyingi sana. Hivyo ni lazima pesa hii uwe nayo unapoelekea
kwenye uhuru wa kipesa.
Hakuna
sababu ya kusema sina mtaji au sijawekeza katika hili kwa sababu pengine
niliumwa na nikatumia pesa zote. Ili kuepuka ‘majanga’ kama hayo unatakiwa kujiwekea pesa ya dharura. Pesa hiyo
inakuwa mkombozi wako kwa lolote linatokea ambalo hukupanga.
5.
Wekeza.
Sasa
baada ya hatua hizo ambazo tumetoka kuzijadili, ili kuufikia uhuru wa kifedha
kiuhakika hatua inayofuata ni kuwekeza. Bila kuwekeza itakuwa ni kazi ngumu
sana kuweza kuufika uhuru wa kifedha.
Hapa
ni lazima ukae chini na kutafuta ni kitu gani ambacho unakiwa ufanye au uwekeze
na kikakuletea pesa nyingi. Kwa kitu hicho utakachokichagua, anza kukitekeleza mara
moja kwani kitakufanikisha na kukupa uhuru wa kifedha.
Kama
kweli nia yako ni kuufikia uhuru wa kifedha, unalazimika sana kujiwekea malengo
ya kifedha, kutengeneza bajeti yako, kutenga pesa za dharura, kuweka akiba na
kuwekeza katika eneo ambalo litakupa faida kubwa. Hizo ndizo hatua muhimu za
kutengeneza uhuru wa kifedha.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la
Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
Sep 27, 2016
Jinsi Ya Kupata Mafanikio Makubwa Kwa Kuboresha Mambo Haya Matatu.
Kimsingi,
mafanikio yoyote unayoyatafuta yanaongozwa na kanuni. Kanuni hizo ndizo huamua
ufanikiwe au usifanikiwe kwa kiasi gani kulingana na jinsi unavyozitumia.
Bila
kuzijua kanuni hizo na kuzifanyia kazi, ni kazi bure utahangaika sana kutafuta
mafanikio na utaambulia patupu. Wengi wanaoingia kichwa kichwa kutafuta
mafanikio bila kuzijua kanuni hizo, huwa si rahisi sana kufanikiwa.
Kama
ambavyo umekuwa uijifunza mara kwa mara kupitia mtandao huu, zipo kanuni nyingi
za mafanikio ambazo unatakiwa kuzitumia na kuziishi kila siku ili zikuletee
manufaa makubwa kwako.
Moja
ya kanuni hizo za mafanikio, ambayo leo kupitia makala haya nataka ujue ni kanuni ya kuboresha. Hii ni moja ya
kanuni ambayo ni rahisi, ila itakupa mafanikio makubwa sana endapo utaamua
kuifanya iwe sehemu ya maisha yako.
Kivipi?
Ipo hivi. Kanuni hii inatueleza, kwa chochote unachokifanya, kadri siku
zinavyokwenda lazima ukiboreshe na kuwa bora kuliko mwanzoni au ulivyokuwa ukianza.
Ulazima wa kufanya hivyo upo kwa sababu ya mabadiliko yanayotokea kila siku.
Boresha mbinu na bidhaa zako, pesa utapata tu. |
Na
mabadiliko yanapotokea yakakuta hujaboresha mambo yako vizuri, kwa vyovyote vile ni lazima utakwama. Hivyo ndio
maana unatakiwa kuwa bora kila wakati.
Lakini
hata hivyo ili kanuni hii iweze kufanya vizuri na kukupa matokeo ya haraka,
yapo maeneo ya msingi amabayo unatakiwa kuyaboresha. Kwa kuboresha maeneo haya
ni lazima ufanikiwe.
Hebu
bila kupoteza muda, twende pamoja kuangalia maeneo ambayo unatakiwa
kuyaboresgha ili kujitengenezea mafanikio makubwa maishani mwako.
Kwanza,
boresha
bidhaa zako. Kama wewe ni mzalishaji au muuzaji wa bidhaa za aina
fulani, kitu cha kwanza ambacho unatakiwa kujua ni kuboresha hizo bidhaa zako
kwa kiwango cha juu sana.
Hakuna
mteja ambaye anapenda kuuziwa kitu ambacho si kizuri au ni feki. Hivyo ili umshawishi
awe mteja wako wa kudumu katika kipindi hiki cha ushindani ni lazima ujifunze
kwa kiasi kikubwa kuboresha bidhaa zako kwa viwango vya juu.
Hebu
jaribu kuangalia kampuni nyingi kitu kikubwa ambacho zinafanya, utakuta karibu
kila siku wanaboresha bidhaa zao. Kama ni kampuni ya usafirishaji, utawaona
kila wakati wanajitahidi kama ni mabasi yao kuyafanya yawe bora zaidi.
Kila
kitu chenye mafanikio makubwa katika hii dunia ili kifanikiwe ni lazima kwanza
kiboreshwe. Bila kuboreshwa hakuna mafanikio ambayo yanaweza kupatikana ya
maana.
Pili,
boresha
mbinu zako. Kama ilivyokuwa kwenye kuboresha bidhaa zako, pia
unalazimika kutumia kanuni ya kuboresha
mbinu zako ili kupata kile unachokipata sasa kwa uhakika mkubwa.
Ili
uweze kuboresha mbinu zako, kila wakati jaribu kuwa mbunifu na kujiuliza ni njia
gani nyingine unaweza ukaitumia na ikakupa mafanikio makubwa. Ukishaipata njia
hiyo itumie mara moja.
Kwa
jinsi utakavyozidi kuwa mbunifu na kuwaza tena na kuwaza, namna ya kuboresha
njia nyingine za mafanikio, ni uhakika mafanikio utaanza kuyaona bila tabu
yoyote. Kikubwa boresha sana mbinu zako.
Tatu,
chukua
jukumu la kujiboresha wewe. Hakuna unachoweza kukibadili katika maisha
yako, ikiwa kama wewe mwenyewe umegoma kuchukua hatua zitakazopelekea uwe bora
katika maisha yako.
Oooh
unajiuliza linawezekana vipi? Ni rahisi tu kwa kujifunza kwa wengine na
kujisomea karibu kila siku, ndivyo unazidi kuwa bora na kupelekea mafanikio ya
wazi kutokea kwenye maisha yako.
Kama
kuna eneo unajiona ni mdhaifu au huwezi kwa namna moja au nyingine, lifanyie
kazi eneo hilo mara moja. Kwa mfano, unataka kuwa mwimbaji bora, fanya mazoezi
kila siku bila kuchoka.
Kumbuka,
hakuna mafanikio ya kubahatisha hata siku moja. Kama unataka mafanikio ni
rahisi tu, fuata kanuni za mafanikio kila siku na hakikisha unaboresha mbinu
zako, unaboresha bidhaa zako bila kusahau ni lazima wewe ujiboreshe pia wakati
wote.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la
Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
Sep 26, 2016
Mambo Muhimu Ya Kuzingatia, Ili Kujenga Hamasa Ya Kudumu.
Kuna
wakati katika maisha unaweza ukajikuta una wazo la kufanya biashara au una wazo
la kusoma kitabu au una wazo la kufanya kitu fulani kwa hamasa kubwa sana.
Lakini
kitu cha kushangaza pale tu unapoanza kufanya jambo hilo, hamasa hiyo huanza
kupungua kidogo kidogo na wakati mwingine hujikuta imeisha kabisa na wewe kujikuta
huwezi tena kuendelea.
Wakati
huo huo unakuwa unashangaa na kujiuliza sana, hamasa yote kubwa uliyokuwa nayo
imekwenda wapi? Hapa kuna wakati unakuwa huelewi kabisa ni nini kilichopoteza
hiyo hamasa?
Pia
hata hivyo, unakuwa tena unashangaa kuwaona watu wengine wakifanya kitu hicho
hicho, ambacho wewe umekishindwa. Tena unakuwa unajiuiza hamasa ya wao kufanya
inatoka kwao wapi? Wakati wewe umeshindwa?
Kumbe,
kitu usichokijua ni kwamba hamasa ni kitu ambacho huzaliwi nacho. Hakuna mtu
ambaye anazaliwa akiwa na hamasa ya kufanya kila siku zaidi ya wewe kuamua
kuitengeneza.
Inapofika
mahali unajihisi kabisa umekosa hamasa, tambua kabisa ipo namna ambayo unaweza
ukaiongeza hamasa hiyo. Lakini, kuongeza huko au kuchochea huko hamasa hakuji
hivi hivi tu, mpaka uzingatie mambo muhimu ya kujenga hamasa.
Yafuatayo
Ni Mambo Muhimu Ya Kuzingatia, Ili Kujenga Hamasa Ya Kudumu.
1. Anza kwa kidogo.
Kwa chochote kile unachotaka kukifanya hata
kama unahamasa nacho kubwa vipi, anza kidogo. Hiyo itakusaidia kutokuta tamaa
au kukupunguza hamasa, endapo itatokea umepata matokeo ya tofauti.
Kwa jinsi unavyoanza kwa kidogo inakuwa sio
rahisi kwako, kukosa hamasa kwa urahisi. Inatokea hivyo kwa sababu kila siku
unavyofanya kwa kidogo, unakuwa unajitengenezea nguvu ya mwendelezo wa kusonga
mbele.
Tafuta sababu ya kufanya. |
2. Fanya jambo hilo kwa sababu.
Chochote unachokifanya ili kikujengee hamasa
ya kudumu ni lazima uwe na sababu ya kufanya. Kosa wanalofanya watu wengi,
sababu zinakuwa sio nzito sana au hazijitoshelezi.
Je, unaweza ukajiuliza binafsi, hilo jambo
unalolifanya sasa, ni sababu ipi inayokuongoza hadi ukalifanya? Je, ni kwa sababu
ya pesa au kwa sababu unalipenda au kwa sababu unataka kusaidia jamii?
Ukishajua sababu inakuwa sio rahisi kwako kukata tamaa, hata pale yanapotokea mazingira ya kukatisha tamaa.
Ukishajua sababu inakuwa sio rahisi kwako kukata tamaa, hata pale yanapotokea mazingira ya kukatisha tamaa.
3. Kuwa na maono.
Wakati wengi wetu hamasa inapungua kwa sababu
ya kushindwa kuwa na maono maalumu ya kule tunakokwenda na kile tunachokifanya.
Lakini ikiwa maono yako wazi, ni rahisi kudumisha hamasa yako wakati wote.
Jaribu kujiuliza kama hicho unachokifanya
kitakupa faida kubwa sana na pesa nyingi huko unakokwenda, je unaweza ukakiacha
kwa urahisi? Ukiwa na picha ya namna hiyo itakusaidia sana wakati wote
kujijengea hamasa ya kudumu maishani mwako.
4. Tengeneza tabia ya mwendelezo.
Kuna siku tunajikuta kweli tumechoka na hatuwezi kufanya
lile jambo tunalolifanya na akili inakuwa inatuambia tulia, utafanya kesho. Ukikubali
kuisikiliza hiyo sauti, utapotea.
Kuwa na tabia ya kukifanya kile unachokifanya
kila siku hata kama ni kwa dakika kumi tu inatosha. Haijalishi umejisikia au
haujisikii wewe fanya. Tengeneza
mwendelezo wa kufanya kila siku(Consintence). Ikiwa utafanya hata pale ambapo
hujisikii kufanya ni lazima utajenga hamasa yako sana.
5. Tumia kushindwa kama chanzo cha hamasa kubwa.
Hata inapotokea pale unaona kama umeshindwa,
tumia kushindwa huko kama sababu kubwa ya kuelekea kwenye mafanikio yako.
hakuna mtu ambaye hashindwi kwenye safari ya mafanikio.
Achana na habari ya kulalamika pale
unashindwa zaidi ya kujifunza. Ukishalijua hilo, jifunze sana kutokana na
makosa yako na chukua hatua ya kuweza kuendelea mbele hatua kwa hatua.
Kwa kuzingatia mambo hayo machache, hivyo
ndivyo unavyoweza ukajikuta umejenga hamasa ya kudumu wakati wote katika maisha
yako.
Endelea
kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Kama
makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye kundi la
Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO.
Ni
wako rafiki,
IMANI
NGWANGWALU,
Sep 23, 2016
Fahamu Kwanini Kesho Si Rafiki Wa Mafanikio Yako.
Katika maisha yetu ya kila siku, neno "Kesho" linatumika
sana kama njia pekee ya kuahirisha mambo mengi, ambayo kimsingi yalitakiwa
yafanyike "leo" .
Kesho ni miongoni
mwa maneno yanayopendwa kutumiwa kama kinga ya kukataa kutimiza majukumu fulani
ya leo. Badala ya mtu Kusema "HAPANA" Kitu hiki, utakuta mtu
huyo anajibanza nyuma ya kesho, Huku akidhani Kuwa ataweza
kufanya au kutimiza majukumu ya leo siku ya Kesho.
Matokeo yake, kesho ikifika anasogeza
tena mbele kwa sababu kuna kesho nyingi mbele yake. Kwa maneno mengine ni
kwamba, tunahitaji kujiadhari sana na "kesho" kwani bila kufanya
hivyo, tutajikuta kwenye hali ya umaskini mkubwa sana bila kujua.
Ni Ukweli usiopingika kuwa neno baya
kuliko maneno mengine na linaloongoza kwa kuharibu maisha ya binadamu ni neno liitwalo "kesho".
Watu wengi hasa maskini, watu ambao
hawajafanikiwa, wasiokuwa na furaha, na wale wasiokuwa na afya njema ni kundi
la watu ambao upendelea sana kutumia neno " Kesho" .
Ndiyo maana watu wa namna hii, mara
nyingi hupendelea kusema maneno kama"nitaanza uwekezaji kesho au "
nitaanza kutumia lishe bora kesho " au nitaanza mazoezi
ya kupunguza uzito Kesho! Wengine husikika wakisema" nitaanza
kusoma labda kesho.
Anza siku yako leo, kama hakuna kesho. |
Ukichunguza kwa undani unagundua kuwa
neno "Kesho" linatumika sana kumaanisha kuwa jambo
fulani litaanza kufanyika siku ambayo siyo ya leo. Ndiyo maana utasikia
nitaanza hiki siku Ya kesho, wiki, mwezi, mwaka kesho au wakati ujao.
Kwanini
Watu hupendelea Kusema Kesho?
Sababu ni moja tu kwamba tunayo HULKA
ya kupenda kufanya Vitu vingi kwa mara moja na ambavyo haviko hata kwenye mpango
maalum.
Tunapenda sana kufanya kazi kwa
kufuata kasi ya matukio yanayoendelea kutokea. Kwahiyo, mambo au shughuli
za leo zinapozidi uwezo unaamua kuzipeleka siku ya kesho.
Kwa mfano unaweza kukuta kwamba kufika
saa sita mchana ya leo, Tayari umekwisha kuahirisha shughuli nyingi za leo na
kuzipeleka kesho. Lakini uzoefu unaonyesha kuwa unapoona kitu hujakifanya leo,
basi ujue siyo muhimu.
Kuhusu kitu gani muhimu ufanye leo,
hakiji hivi hivi, ni lazima shughuli zako nyingi za kila siku zifanyike kwa
kulenga ndoto yako ya maisha yaweza kuwa ni miaka mitano, kumi au na zaidi.
Bila kuwa na ndoto au maono juu ya maisha
unayotaka kuyaishi, Lazima utaendelea kufanya kazi zako nyingi kwa kufuata
matukio ya siku husika.
Mwisho wake kila utakapofanya
Tathmini ya miaka 5 au 10 iliyopita unajikuta umezidi kurudi nyuma, hapo ndipo
utaanza kutafuta wa kumlaumu. Kuchanganyikiwa kwa Watu Wengi ambako huambatana
na msongo mkubwa wa Mawazo, mara nyingi huja kwa njia hii.
Kwahiyo, ni muhimu sana kwetu
tunaotaka maisha huru ya mafanikio kutambua kuwa vitu vyote muhimu kwa maisha yetu
ni inatakiwa vinavyofanyika leo.
Maisha yako siyo kesho, wiki, mwezi,
mwaka au miaka kumi ijayo bali maisha halisi, ambayo una fursa ya kufanya kazi
itakayo kuletea mafanikio makubwa siku za mbeleni ni leo.
Ni muhimu tukafanya yale yote yaliyo
muhimu leo. Ukishatambua hilo, utakuwa wa kwanza kuona umuhimu wa kuianza
siku yako mapema Alfajiri.
Kushindwa katika maisha yako hakuji
siku moja bali ni matokeo ya kushindwa kidogo kidogo kila siku. Ukiona
umeshindwa au unakabiliwa na umaskini usifikiri ni jambo ambalo limetokea leo
bali ni kutokana Na wewe kuchezea yale masaa ya kuanzia unapoamka hadi
unapolala.
Kwa hiyo kwa maneno au lugha rahisi "LEO
Ndiyo Dili" kubwa ya kubadili maisha yako. Hii ikiwa na maana kwamba
tukifanya kazi sana leo tutapata ushindi au mafanikio kidogo na kesho tukifanya
kama au zaidi ya leo tutapata mafanikio Kidogo.
Yale mafanikio kidogo kidogo
tunayovuna kila siku ndiyo kwa ujumla wake yatatufanya kuwa na mafanikio makubwa
miaka 5 au 10 ijayo na hapo ndipo Wengi watakapoanza kukutambua kwamba na wewe
huwa upo!
Jitahidi kuipenda na kuikumbatia leo
na uachane kuwa na mpenzi wa kesho kwasababu, neno Hili linaharibu sana maisha
ya watu wengi kuliko maneno mengine.
Achana na neno "Kesho" kwasababu
haitatokea uione kesho. Kesho huwa haipo. Kesho huwa ipo tu kwenye
akili za watu waota ndoto bila vitendo na washindwaji.
Nimalizie kwa Kusema Kuwa sijawahi
kuiona "Kesho" Kitu tulichonacho Pekee ni "Leo". LEO
ni neno la washindi na Kesho ni neno la washindwa.
Endelea kujifunza kupitia
dirayamafanikio.blogspot.com kila siku.
Makala hii imeandikwa na Cypridion Mushongi wa MAARIFA SHOP.
Sep 22, 2016
Jinsi Ya Kukabiliana Na Changamoto Ili Kupata Mafanikio.
Kila mmoja anahitaji mafanikio makubwa kwa kile anachokifanya
siku zote, japo tatizo huwa ni namna ya kukabiliana na changamoto zinazomsonga
ili asifike malengo.
Kuna wakati mwingine tunajikuta tunakata tamaa baada ya kuona
baadhi ya changamoto zinatokea na kuzuia mafanikio ambayo tumejipangia.
Changamoto hizi zimekuwa zikijitokeza katika biashara, elimu, kazini hata mara
nyingine kufiwa na mtu ambaye ulikuwa una mtegemea kwa namna moja ama nyingine
pamoja na changamoto nyingine nyingi.
Wakati mwingine changamoto zikitokea, wengi hukata tamaa na muda
mwingine kujiona hufai kuendelea kuishi. Wapo wanaofikia hatua ya kukufuru kwa
kutoa kauli kama vile Mungu anapendelea, dunia haina usawa na maneno mengine
mengi yanayofanana na hayo.
Lakini wasichokielewa watu ni kwamba changamoto ni njia ya
kufikia mafanikio tunayoyahitaji. Pia changamoto huja ili kupima imani na uwezo
wako kama kweli unaweza kupambana vitani.
Kabiliana na changamoto mpaka uzishinde. |
Zifuatazo ni baadhi ya njia ya jinsi ya kukabiliana na
changamoto katika maisha ya kila Siku;
Kwanza, zikubali changamoto; Kama nilivyoeleza hapo awali,
changamoto ni lazima zitokee katika safari yako ya mafanikio, hivyo hakikisha
na kisha utafute mbinu zakuweza kupambana nazo.
Unaweza kuanzisha biashara, lakini katikati ya safari ukakimbiwa
na wateja, jambo la msingi ni kufanya uchunguzi ni nini kimesababisha hali
hiyo, ili uweze kuchukua hatua badala ya kulalamika na kuwanyoshea vidole
wengine kwa kuona wao ndio chanzo.
Epuka kukimbilia kwenye imani za kishirikina au mitazamo potofu
kama vile chuma ulete, nguvu za giza na mengineyo mengi kwani kufanya kinyume
chake kwa kuamini imani hizo si kutatua tatizo bali ni kuliongeza tatizo.
Pili, tafuta washauri. Nafahamu ya kwamba baadhi yetu tuna watu
wa karibu ambao huwa tunawaeleza shida zetu. Mfano wazazi, ndugu, marafiki na
wengineo.
Pia unaweza kuwatumia viongozi wa dini kwa jambo linao kutatiza,
kwani ni watu ambao wana nguvu sana katika jamii hususani suala zima la masuala
ya ushauri hasa katika mambo yanayotutiza katika kufikia malengo yetu. Pia
unaweza kujifunza kupitia mafunzo mbalimbali kama vile semina kwani kufanya
hivyo utaweza kupata majibu ya changamoto zinazokukabili.
Vile vile katika utatuzi wa changamoto, watu wengi huwa
tunakosea sana. Huwa tunaanza kuangalia matokeo ya jambo, badala ya kuangalia
vyanzo ya matokeo hayo.
Nitaomba kukupa ufafanunuzi wa nukta hii kwa kuangalia mfano
mdogo wa ugonjwa wa mlipuko maarafu kama kipindupindu ambao umekuwa ukizuka
sana maeneo kadha wa kadha ikiwepo na jiji la Dar-es-salaam, ambapo kila
kipindi cha muda fulani huzuka na kuwaathiri watu wengi.
Tatizo kubwa la ugonjwa huu ni kuwa siku zote tunatibu
matokeo, yaani unapotikea viongozi serikalini wanajihimu kuandaa
mazingira ya kuwapatia wagonjwa tiba.
Kufanya hivo ni kushughulika na matokeo ya tatizo na kuacha
chanzo cha tatizo ambacho kwa mujibu wa wataalamu wa afya ni wananchi kuendelea
kuishi kwenye mazingira machafu yanayotoa mwanya watu kula vinyesi kitendo
kinachosababisha with kuugua ugonjwa huo.
Tukifuata kanuni hii ya kuangalia chanzo kisha tuangalie
matokeo, kuna uwezekano mkubwa wa kushinda changamoto zinazotukabili katika
shughuli zetu za kila siku iwe kwenye biashara, kazini, masomoni na maeneo
mengine.
Pia naomba usemi huu kila mara "usizibe ufa uktani kabla ya
kujua chanzo cha ufa huo"
Endelea kujifunza kupitia dirayamafanikio.blogspot.com kila
siku. Kama makala hii imekusaidia na unapenda kujifunza zaidi, karibu kwenye
kundi la Whats App ili uweze kujifunza. Kujiunga tuma neno MAFANIKIO YANGU, kisha ikifuatia na jina lako kwenda 0713 048035 ili uanganishwe.
Ndimi: Benson chonya
Sep 21, 2016
Mambo Ya Kujifunza Pale Unapokosa Tumaini La Kufanikiwa.
Kipo
kipindi katika safari yako ya mafanikio kutokana pengine na changamoto za kimaisha,
unajikuta unakata tamaa na matumaini yote yanapotea.
Katika
kipindi hiki, kila unachokifanya kinakuwa hakileti matokeo na mbele yako
unakuwa unaona giza na hakuna hata njia wala mwanga wa matumaini. Je, kwa hali kama hii inapokutokea unafanyaje?
Kwa
mfano, tuchukulie umeanzisha mradi fulani, lakini umejitahidi sana ili ukuletee
angalau faida imeshindikana, hapo inapokuwa hivyo unawaza nini au unachukua
hatua gani?
Najua
kuna mambo mengi yanakuwa yanapita kichwani mwako, ikiwa nia pamoja na kuachana
kabisa na kitu hicho ambacho sasa unaona hakifai tena na hakina manufaa kwako.
Lakini
leo hapa kwa kupitia makala haya, naomba nikushirikishe mambo ya msingi ya
kujifunza hasa inapotokea pale umekata tamaa na kukosa matumaini kwa kile unachokifanya.
Unapokosa tumaini, panga mipango yako upya. |
Jambo
la kwanza unalotakiwa kujifunza na kulitambua ni kwamba hakuna mafanikio ya mara moja. Hapa hii
yote inatuonyesha ili tuweze kufanikiwa inatakiwa tujaribu tena na tena hadi
kufikia mafanikio.
Inapotokea
unaona kama umekosa tumaini unaonyeshwa kwamba sasa huu sio wakati wa kutulia
na kujiona mnyonge uliyopoteza karibu kila kitu, bali ni wakati wa kunyanyuka tena na
kujaribu njia zingine za kukupa mafanikio yako.
Jambo
la pili unalotakiwa kujifunza ni kwamba katika maisha hakuna kukata tamaa. Ni kweli,
unakuwa unajiona umekosa matumaini na huna chako tena, lakini ni wakati wako wa
kijiamini tena na kushikiria ndoto zako upya mpaka kufanikiwa.
Hata
kama unaona dunia na kila hali kama imekutenga, jifunze hapo ulipo sio ndio
mwisho wa mafanikio yako ipo nafasi ya kufanya tena na ukafanikiwa sana kuliko
unavyofikiri.
Jambo
la tatu la kujifunza hasa pale unapokosa matumaini tena ni panga mipango yako
upya. Hiki hasa ndicho kitu ambacho unachokuwa unaambiwa na maisha.
Badala
ya kukaa chini na kulia na kuanza kulalamika kwa kushindwa kwako kufanikiwa,
lakini unachoambiwa na maisha panga mipango yako upya, tafuta njia nyingine na
tumia akili yako vizuri hadi ufanikiwe.
Tambua, ili kufanikiwa inatakiwa ujue hakuna mafanikio ya mara moja, hakuna kukata
tamaa na inabidi kila wakati kupanga mipango upya. Hayo ndiyo mambo ya msingi unayotakiwa ujifunze hasa pale unapokata tamaa
na kukosa.
Endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza na kuhamasika.
TUNAKUTAKIA
KILA LA KHERI KATIKA SAFARI YAKO YA MAFANIKIO,
IMANI NGWANGWALU,
dirayamafanikio.blogspot.com
0713048035.
Sep 20, 2016
Faida Kubwa Za Kujijengea Mtazamo Chanya.
Kuna jambo kubwa sana ambalo linaweza
kubadili maisha yako ndani ya muda mfupi, ambalo siku ya leo ni vyema
kulifahamu, na si kulifahamu tu bali kuamua kulichukua jambo hili na kulifanya
libadili maisha na jambo lenyewe si jingine bali ni mtazamo ulionao.
Mtazamo ni vile ambavyo unaamini
huenda ikawa ni katika fikra chanya au fikra hasi. Lakini katika makala haya
nitazungumzia umuhimu wa kuwa na mtazamo chanya, kwani mitazamo ya watu ndio
ambayo humueleza kwa undani zaidi ni kwa njisi gani mtu alivyo kutokana na vitu
ambavyo anavyovifanya na asivyovifanya.
Na jambo hilo huleta tofauti uliyopo
kati ya walinacho na wasionacho, na tofauti hiyo ni kwamba waliofanikiwa wao
wanaamini ya kwamba katika dunia hii hakuna kisichowezekana ila watu ambao hawajafanikiwa
wao huamini ya kwamba mambo mengine hayawezekani hii ni kutokana wao
hukata tamaa mapema zaidi kabla ya kuanza kufanya, hali hii hutokea kwa sababu
watu wengi ambao maisha yao duni huishi kwa kuogopa sana wakati ujao.
Jenga mtazamo chanya, ukusaidie. |
Pia akili za mwanadamu zimetawaliwa
kwa kiwango kikubwa na vitu ambavyo havionekani, hapa ndipo lile somo la kujipa
majibu hasi linapofanya kazi, kwa vitu ambavyo anaviwaza ambavyo kimsingi bado
havijawekwa katika utekelezaji.
Kwa mfano unakuta mtu ana mawazo
mengi ambayo ukiyatazama kwa "jicho la tofauti" mawazo hayo yatawezwa
kubadilishwa na kuwa katika matendo yana uwezo mkubwa sana wa kubadilisha
maisha ya mhusika huyo kwa asilimia mia moja, ila changamoto kubwa pindi mtu
awazapo huanza kuja na vikwazo ambavyo kimsingi huwa na vitu ambavyo havimpi
nguvu ya kuthubutu kutenda jambo hilo.
Hii huwa ni ishara mawazo yetu huwa
ni chanya mara nyingi lakini suala zima la utekelezaji wa suala hilo huwa ni
kikwazo kikubwa, lakini nikwambie neno moja ya kwamba kuanza sasa unahitaji
ubongo wa ziada.
Unaweza ukajiuliza ubongo wa ziada
labda ni kuwa na ubongo mwingine, la hasha sina maana hiyo ila ukweli ni kwamba
uanze kufikiria katika akili nyingine ambayo itakufanya uwe mpya, katika fikra
mpya hususani suala zima la kuwa na mtazamo chanya.
Inawezekana ukajiuliza unawezaje kuwa
mtazamo chanya?
Suala zima kuwa mtazamo chanya huwa
linatokana na kujiuliza katika mambo ambayo unayofanya, je mambo hayo yana
matokeo gani katika maisha yako na watu wengine?
Watu ambao wanakuzungua huwa
wanatazamo gani juu yako? Na mara zote ikumbukwe ya kwamba maisha yako
yanatazamwa kwa asilimia kubwa na watu wengine, watu wanaokuzunguka
wakikutazama katika jicho chanya hata kile kitu ambacho unakifanya kinaweza
katika kuwa bora zaidi.
Ifike pahala jamii ambayo inakutazama
wakufikirie kwamba ni mtu chanya, kufanya hivi kutakufanya uweze kujitangaza
jina na kujiongezea thamani.
Amua sasa kutenga muda wa kujiuliza
mambo ya msingi ambayo yatakusaidia kuwa na mtazamo chanya kwa kila jambo
amabalo unakiwaza au ambalo unalitenda. Pia ikumbukwe ya kwamba ni vyema
ukaamua kubadili maisha yako kwa kuwa na mtazamo sahihi.
Afisa mipango Benson Chonya.
0757909942
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)