Feb 9, 2016
Maswali 10 Ya Kujiuliza Kila Wakati, Kama Una Nia Ya Kuwa TAJIRI.
Wengi
wetu mara nyingi huwa tuna nia ya kufikia mafanikio makubwa na hatimaye kuwa
matajiri. Lakini, kwa bahati mbaya sana huwa pia hatujui tuanzie wapi hasa ili
kufikia hilo lengo. Matokeo yake hujikuta tukifanya hiki mara kile bila kupata
matokeo ya kutufikisha kwenye lengo husika.
Kwa
kawaida, ili kuwa tajiri huwa zipo kanuni zake za msingi kabisa ambazo
ukizifuata ni lazima uwe tajiri. Kwa
kutumia kanuni hizi huwa haijalishi wewe ni nani, unaishi kijijini au mjini,
umesoma au hujasoma lakini ukizifuta ni lazima ufanikiwe na kuwa TAJIRI.
Kutokana
na umuhimu wa hilo, leo hii ningependa nikushirikishe kanuni mojawapo
itakayokusaidia kukufikisha kwenye UTAJIRI. Kanuni zingine tutaendelea
kujifunza polepole katika makala zinazofuata
hapa kwenye mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO.
Kanuni
hii ambayo tunajifunza leo ni kanuni ya kujiuliza maswali ambayo yatakusaidia
kufikia lengo lako. Hii ni kanuni ya msingi sana ambayo unatakiwa uitambue ipo
na inafanya kazi. Je, unataka kujua kivipi? Twende pamoja nami, kujua maswali
muhimu ya kujiuliza ili uwe TAJIRI.
1. Jiulize, ni kwanini unataka kuwa
tajiri?
Hili
linaweza likaonekana ni swali la kawaida sana kwako, lakini ni lazima uwe na
sababu kwa nini unataka kuwa tajiri. Bila kuwa na sababu ya msingi inayokusukuma
wewe kuwa tajiri huwezi kupata msukumo
utakaokufanya utafute pesa kwa nguvu zote hadi ufikie lengo hilo unalolitaka.
Hapa
sio suala tu la kusema ‘Oooh nataka kuwa
tajiri’ ni lazima ujue sababu ipi inayokufanya utake kuwa tajiri. Je, unataka kuwa tajiri ili uwe huru kifedha?
Au je, unataka kuwa tajiri ili kusaidia jamii inayokuzunguka? Ni muhimu sana
kuwa na sababu yenye mashiko ili kufikia malengo yako.
TOA THAMANI, UPATE PESA. |
2. Jiulize, una imani ya kutosha kukusaidia
kufikia lengo lako?
Unaweza
ukawa una sababu nzuri inayokufanya utake kuwa tajiri. Lakini hiyo peke yake
haitoshi ni lazima uende hatua ya ziada kwa kujiuliza wewe mwenyewe je, una imani ya kufikia malengo
yako? Unaamini kabisa kwamba hayo malengo ya kuwa tajiri utayafikia?
Ili
uweze kufanikiwa ni lazima kupima imani hii. Kumbuka hakuna mafanikio
yanayoweza kuja pasipo kuhusisha imani hata iweje. Hapo ulipo kimaisha ni
matokeo ya imani fulani hivi ambazo unazo au ulizibeba na kuziamini sana. Kwa
imani hizo ndizo zimekufikisha hapo ulipo. Kupima imani, ni lazima sana kwako
ili kufikia mafanikio.
3. Jiulize, ni tabia zipi za
kimafanikio zitakazokusaidia kufanikiwa?
Najua
tayari una sababu na imani ya kukutosha
kukupeleka kwenye utajiri. Kitu kingine kwako cha kujiuliza je, una tabia zipi
za kimafanikio zenye uwezo wa kukufikisha kwenye mafanikio makubwa unayoyataka.
Kama tabia hizi unazo upo kwenye njia sahihi.
Huwezi
kuwa unasema unataka kuwa tajiri wakati huo huo una tabia mbaya zinazokurudisha
nyuma kimafanikio. Tabia hizi zinaweza zikawa ukosefu wa nidhamu, matumizi
mabaya ya pesa, muda na nyinginezo. Kwa kuendekeza tabia hizi na zinazofanana
nazo hata ulie machozi ya damu huwezi kuwa tajiri.
4. Jiulize, je, unatoa thamani
inayoendana na unachokitaka?
Kwa
kawaida ili ufanikiwe ni lazima utoe thamani kwa jamii ili ikulipe pesa. Kama
ni huduma fulani ipe jamii husika itakulipa tu hizo pesa hata kama umelala.
Kinyume cha hapo, yaani nikiwa na maana kushindwa kutoa thamani huwezi
kufanikiwa wala kupata pesa yoyote.
Sasa
hapa ndipo unatakiwa jiulize je, wewe binafsi unatoa thamani kwa jamii. Nini
ulichonacho ambacho ni msaada kwa watu
wengine. Kama huna kitu hiki unalazimika kukitafuta haraka sana vinginevyo
huwezi kufanikiwa. Na ndiyo maana unalazimka kujiuliza kila wakati ‘je,
ninatoa thamani’. Hii itakuwa njia
bora sana kwako ya kuufikia utajiri.
5. Jiulize, una mipango imara ya
kukufikisha kwenye utajiri?
Sawa,
inawezekana una toa thamani inayotakiwa, lakini je una mipango imara ya
kukufikisha kwenye lengo la mafanikio hayo makubwa. Hapa ili ufanikiwe ni
lazima kwako uwe na mipango iliyo sawa ambayo unatakiwa uifate kila siku.
Na
katika kuhakikisha hili linatimia ni vyema ukawa umejitengenezzea mpango wa siku,
juma, mwezi na hata mwaka na utekelezaji unatakiwa uanze mara moja. Lakini bila
ya kufanya hivi kufanikiwa na kuwa tajiri inaweza ikawa ndoto kama ndoto
zingine. Kuwa na mipango imara ni nguzo imara ya kukufikisha kwenye utajiri.
6. Jiulize, je, una hofu zinakuzuia
kufanikiwa?
Mara
nyingi na kwa asilimia kubwa kinachomzuia binadam kufanikiawa si yale mambo ya
nje tunayoyaona, hapana. Kitu kikubwa kinachomzuia binadamu kufanikiwa ni mambo
yanayoendelea ndani yake ikiwamo pamoja na hofu.
Unapokuwa
na hofu ni adui mkubwa sana wa mafanikio yako kwa ujumla. Acha kuruhusu hofu
ikachukua nafasi kwenye moyo wako kwa nama yoyote ile. Kwa vyovyote vile kama
utairuhusu hofu ni lazima itakurudisha nyuma. Hivyo inabidi ujifunze
kukabiliana nayo mpaka kuweza kuishinda.
ZUNGUKWA NA WATU WENYE MAFANIKIO. |
7. Jiulize, unazungukwa na watu wenye
mafanikio?
Ukichunguza
kidogo maisha ya watu wenye mafanikio, utagundua wanazungukwa na watu wenye
mafanikio pia. Hapa ndipo ilipo pia siri ya kuufikia utajiri. Huwezi kufanikiwa
kama wanaokuzunguka ni watu maskini na ambao maisha yao ya kushindwa siku zote.
Unataka
kuwa tajiri, jiulize tu swali hili rahisi ‘ni
watu gani wanao nizunguka? Ukiona umezungukwa na watu wengi maskini
nakushauri kubadili mwelekeo haraka sana kutafuta watu wenzako wasaka
mafanikio. Kwa kuwa na watu hawa watakutia moyo na kukupa hamasa ya kuendelea
mbele.
8. Jiulize, uko tayari kujifunza?
Kama
una nia ya kuwa TAJIRI lakini wakati huo huo hujajitoa kwenye kujifunza, sahau
mafanikio hayo. Kujifunza kila siku iwe kwenye vitabu au pale tunapokosea ni
jambo la msingi sana kwa msaka maendeleo yoyote yule. Bila kufanya hivi hakuna
mafanikio.
Unashangaa,
ndiyo huwezi kufanikiwa. Kitakachokufanya usifanikiwe kwa sababu utarudia
makosa yake yale kila wakati na hutaweza kupiga hatua. Maisha ya watu wenye
mafanikio ni ya kujifunza siku zote. Kwa hiyo kama unataka kuwa tajiri jiulize
unajifunza. Kama hufanyi hivyo huwezi kupingana na ukweli mbio za kuelekea
kwenye utajiri sio zako.
9. Jiulize, uko tayari kukubaliana na
vizuizi?
Kwenye
safari yoyote ya mafanikio changamoto huwa hazikosekani. Changamoto hizi
usipokuwa makini nazo ni rahisi sana kuweza kukurudisha nyuma. Sasa kitu cha kujiuliza hapa je, unapokutana
na changamoto uko tayari kukabiliana nazo?
Jiulize
ni mara ngapi ulishindwa au uliona wengine wakishindwa kwa sababu ya
changamoto? Hapa ndipo wewe unatakiwa uoneshe utofauti wa kuweza kukabiliana na
changamoto. Amua tu kwamba utafanikiwa, hata kitokee kitu gani mbele yake
lazima ukishinde.
10. Jiulize, una tabia ya kutathmini
safari ya mafanikio yako?
Hakuna
mafanikio ambayo unaweza ukayapata bila ya kujiwekea tathmini. Ni lazima kujiuliza
na kutathmini safari nzima ya mafanikio yako? Kama hufanyi hivo unatakiwa
kuanza mara moja. Utayafikia mafanikio yako kwa kujiwekea tathmini kila wakati?
Anza
kujiwekea tathmini ya siku, kisha jiwekee tathmini ya juma hata mwezi. Kwa
kufanya hivyo utaboresha sana maisha yako. Hiyo itakusaidia kurekebisha yale
maeneo ambayo hujafanyi vizuri na kujiweka sasa kwenye nafasi nzuri ya
kuendelea mbele kimafanikio.
Je, una nia, hamasa na shauku kubwa ya kuufikia UTAJIRI? Kama jibu ni ndiyo jifunze kutumia mbinu hii kwa kujiuliza maswali yatakayokusaidia kuufikia UTAJIRI.
Je, una nia, hamasa na shauku kubwa ya kuufikia UTAJIRI? Kama jibu ni ndiyo jifunze kutumia mbinu hii kwa kujiuliza maswali yatakayokusaidia kuufikia UTAJIRI.
Ansante kwa kutembelea na kufatilia DIRA YA MAFANIKIO kila wakati. Waalike na wengine ili wafaidike na makala tunazozitoa hapa.
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email; dirayamfanikio@gmail.com
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.