Jun 30, 2016
Siri Nzito Za Kufanikiwa.
Safari ya kuelekea
kwenye mafanikio inahitaji ujasiri, sio ujasiri tu bali ujasiri wa hali ya juu
sana, kama ilivyo ujasiri alionao simba awapo mwituni, katika kusaka riziki
yake ili kuhakikisha ya kwamba halali au hafi kwa sababu ya njaa.
Ujasiri huo huo
alikuwa nao simba ndio ambao unauhitaji wewe ndugu yangu, katika safari ya
kujifunza, chukua muda wa kujivika taswira ya kiujasiri ili ufanikiwe zaidi.
Nafahamu ya kwamba
ipo haja ya wewe kuendelea kujua mbinu ambazo zitakufanya upate ujasiri huo.
Hata hivyo niweze kushukuru Mungu kwa kunipa kalama hiyo ya kuweza kutumia
fikra chanya ambazo zinanifanya nikupe baadhi ya mambo yatakayokusaidia kwa
namna moja ama nyingine katika kusaka mafanikio hayo.
Kama alivyo simba kuishi
katika misingi ya kujiamini ,basi ndivyo ambavyo nilivyo na hasira juu ya neno
mafanikio.
Laiti ungelifanya uchunguzi siku moja kumchunguza simba ungaligundua ya kwamba simba anaishi kwa kujiamini ili aendelee kuishi miaka mingi zaidi, pia simba huyo huyo anaishi kwa hofu ambayo itafanya asilale au afe njaa.
Laiti ungelifanya uchunguzi siku moja kumchunguza simba ungaligundua ya kwamba simba anaishi kwa kujiamini ili aendelee kuishi miaka mingi zaidi, pia simba huyo huyo anaishi kwa hofu ambayo itafanya asilale au afe njaa.
Kupitia hilo ifike
mahali na wewe pia uishi kwa kujiamini ya kwamba unajua ambacho unakihitaji,
pia uishi kwa hofu ya kushindwa katika mafanikio pia uishi kwa kuwa na hofu ya
Mungu kwa kila hambo ambalo unalifanya siku zote.
Watu wengi ambao wamefanikiwa na ambao hawajafanikiwa wanafanana katika masuala ya kuishi bila hofu ya Mungu. Wapo wale ambao licha ya kwamba maisha yao ni kitajiri, lakini bado wanaishi katika misingi ya kutenda mambo yao bila kumshirikisha Mungu, maisha ambayo kiukweli yanafanya waishi kwa wasiwasi licha ya maisha yao kuwa mazuri.
Watu wengi ambao wamefanikiwa na ambao hawajafanikiwa wanafanana katika masuala ya kuishi bila hofu ya Mungu. Wapo wale ambao licha ya kwamba maisha yao ni kitajiri, lakini bado wanaishi katika misingi ya kutenda mambo yao bila kumshirikisha Mungu, maisha ambayo kiukweli yanafanya waishi kwa wasiwasi licha ya maisha yao kuwa mazuri.
Nikija upande wa
pili wa shilingi ambapo watu wengi wanaishi maisha ya duni, ambapo wengi
wetu tupo pia tumekuwa ni watu wa kukata tamaa siku zote na imefiki mahali
tumejikuta tunamsahau Mungu, sio kumsahau Mungu tu bali imefika kipindi mpaka
tunakufuru, unaweza kusema leo nahubiri la hasha ila ukweli ubaki palepale kwa
jambo lolote ambalo unalifanya ili uweze kufanikiwa unatakiwa uishi kwa kuwa na
HOFU YA MUNGU.
Zifuatazo ndizo
kanuni ambazo unatakiwa kuzitumia kufanikiwa;
1. Kuwa tayari
kujifunza.
Moja ya njia ya kukusaidia kufanikiwa zaidi ni lazima uweze kujifunza, huenda ukawa hajanipata vizuri ila ukweli wenyewe ndio huu hapa, watu wengi wanataka kupanda ngazi ya kimafanikio, bila kujua namna ya kuitumia ngazi hiyo ya kupata mafanikio.
Moja ya njia ya kukusaidia kufanikiwa zaidi ni lazima uweze kujifunza, huenda ukawa hajanipata vizuri ila ukweli wenyewe ndio huu hapa, watu wengi wanataka kupanda ngazi ya kimafanikio, bila kujua namna ya kuitumia ngazi hiyo ya kupata mafanikio.
Kwa mfano leo hii
utamkuta mtu anataka kuwa mfanyabiashara mkubwa lakini ukimwambia kuwa jambo
hilo linahitaji ulazima wa kujifunza, utakuta mtu huyo hayupo tayari kujifunza
juu ya biashara hiyo.
Lakini mimi huwa
naamini jambo lolote ukitaka kulifanya kwa weledi ni lazima uwe tayari
kujifunza, fikiria kwa umakini kisha uone ni kitu gani ambacho hauitaji
kujifunza ambacho kinahusiana na mafanikio?
Ukitafakari kwa
umakini utagundua ya kwamba hakuna jambo hata moja. Mambo ambayo hutakiwi
kujifunza labda matendo ya hiari na yasiyo ya hiari yanayotokana na msukumo wa
mwili tu yatokanayo na mawazo ya binadamu hasa hisia.
Kujifunza huku
hakuhitaji wewe kukaa darasani miaka mingi, mpaka ufanikiwe ila inahitaji kujua
unataka nini? Baada ya hapo ndio utagundua unatakiwa kujifunza nini.
Nikuibie siri ambayo
hajawahi mtu yeyote kukuambia kwamba siri ya utajiri ipo kwenye
"maandishi" siri hii usimwambie mtu bali chukua hatua pindi
utakapopata ukweli juu ya jambo hilo, wengine wakikuuliza juu ya
mafanikio yako ndipo uwambia siri ya mafanikio ilipo.
2. Kuwa tayari
kulipa gharama.
Mara kadhaa niwehi kuandika ya kwamba "chochote bila chochote huwezi kupata chochote" wengi walikuwa hawajanielewa ila leo ndio uwanja wako wa kuweza kunielewa juu ya jambo hilo.
Mara kadhaa niwehi kuandika ya kwamba "chochote bila chochote huwezi kupata chochote" wengi walikuwa hawajanielewa ila leo ndio uwanja wako wa kuweza kunielewa juu ya jambo hilo.
Iko hivi kwa
chochote kile ambacho unakitaka leo kina gharama zake, kama maelezo ya hapa juu
yanavyojieleza kwamba unahitaji kuwa tayari kujifunza, basi jambo hili huenda
sambamba na kulipa gharama, gharama hizi ni kama vile za kujifunza kwenye makongamono,
kununua vitabu, majarida, magazeti ,vipeperushi kulipa ada za mafunzo
mbalimbali ikiwemo semina au shule.
Ukiyafanya hayo utakuwa
kwa ubora na weledi wa hali ya juu, utakuwa ni miongoni mwa watu ambao
wanafanya mambo ya kimaendeleo kila siku, pia jamii ambayo inakuzunguka
watatamani kwa kiwango kikubwa kitu ambacho unafanya wewe.
Kwa kuwa siri ya
utajiri ipo kwenye mandishi endelea kufuatana nami kupitia mtandao huu wa Dira
ya Mafanikio mpaka maisha yako yaimarike, nikutakie siku njema na Mafanikio
mema.
Jun 28, 2016
Tumia Njia Hizi Kujua Kipaji Chako.
Moja ya
changamoto kubwa inayowakabili watu wengi ni kutojua kwa undani kipi
kipaji chako ambacho Mungu amekupa na ambacho unaweza ukakitumia kwa namna moja
ama nyingine ili uweze kuleta mabadiliko chanya katika jamii na wewe binafsi.
Na kwa kuwa kuna
watu wengi ndio wapo kundi hilo, kuna usemi unasema ya kwamba wengi wape basi
ngoja nifanye hivyo kuweza kuwapa somo hilo la namna ya kujua kipaji
chako kwani hii itamsadia kila mmoja ambaye atakwenda kufuatana nami
mwanzo hadi mwisho katika mukutadha wa makala haya.
Tunapozungumzia
neno kipaji huenda kila mmoja akawa na maana yake ambayo anaifahamu, lakini kwa
namna moja ama nyingine ni lazima mtu aweze kuzaliwa nacho hivyo Mwenyezi Mungu
huhusika pia katika kumpa mtu kipaji.
Hivyo endapo mtu
atakifahamu kipaji chake inampasa sasa ajue namna ya kukiendeleza kipaji hicho
ili kisife. Pia ikumbukwe ya kwamba tunapozungumzia kipaji tunamzungumzia
binadamu na maisha yake kwa ujumla.
Katika
tafiti ambazo zimewahi fanywa na Dr.
Fred Luskin kutoka Stanford
university yeye aliweza kugundua ya kwamba asilimia 65 ya watu wengi
hawajui vipaji vyao na katika kundi kubwa la idadi hii ya watu ndio ambao wanafanya
vitu ambavyo sio vyao.
Na pia asilimia 35 iliyobaki hawa ndio ambao wameweza
kuvijua hivyo vipaji vyao ingawa haviwasadii katika maisha yao na wengine kwa
asilimia 100, hii ni kutoka mafanikio yatokanayo vipaji hivyo huwa ni ya muda
mrefu.
Hivyo kwa kuwa watu
wengi tunataka mafanikio ya muda mfupi uvumilivu hufika ukomo na kujikuta
tunaviacha vitu hivyo na kuingia kufanya vitu vingine.
Mfano mtu anakuwa na
kipaji cha kucheza mpira katika timu kubwa hapa nchini na nje ya nchi,na kwa
kuwa huenda amecheza kwa muda mrefu bila matarajio yake kutimia mtu huyo huacha
kile ambacho hukifanya na kuamua kufanya kitu kingine ambacho sio kipaji chake
mwishowe mtu huyo anajikuta anafanya hiki anakiacha mara kile nacho anakiacha.
Ukiona hicho
unachokiita kipaji chako hakitoi burudani, hakifundishi, hakishangazi basi
hicho sio kipaji.
Namna ya kugundua kipaji chako.
1. Kumuomba Mungu.
Hapa huwa
pananifanya nimkumbuke sana rafiki yangu Samweli Salali kwani aliwahi kuniambia
ya kwamba kipaji ni kusudio la Mungu kwa kila mja wake. Kwani katika mafundisho
yake katika vitabu vya dini vinasema kabla sijaumba nilikujua.
Hii inamaana kila
mwanadamu aliyeumbwa na Mungu ana kipaji chake, hivyo kinauwezo mkubwa wa
kubadili maisha yake na jamii kwa ujumla, ila kipaji hicho watu wengi hawahujui
mpaka dakika hii kuwa kipi kipaji chake ambacho Mungu kampa.
Hivyo kama wewe ni
miongoni mwa watu hao ni muda wako muafaka wa kutumia Muda huu kumuomba Mungu
akuonyeshe kipaji chako hasa na kipi kwa sasa?
Tumia kipaji chako kikusaidie kufanikiwa. |
2. Marafiki, ndugu na wazazi.
Hili ni kundi muhimu sana ambalo litakusaidia wewe kujua kipaji chako. Labda unaweza ukajiuliza ni kivipi? Tulia leo nipo kwa ajili yako. Watu ambao wanakuzunguka ndio wana picha kamaili juu ya maisha yako.
Hili ni kundi muhimu sana ambalo litakusaidia wewe kujua kipaji chako. Labda unaweza ukajiuliza ni kivipi? Tulia leo nipo kwa ajili yako. Watu ambao wanakuzunguka ndio wana picha kamaili juu ya maisha yako.
Kwa mfano mtu akiwa
mlevi hawezi kusema mimi ni mlevi ila watu ambao wanakuzunguka ndio ambao
watasema yule jamaa ni mlevi sana. Picha hiyohiyo ya kumuona mtu mwingine tabia
yake ndiyo ambayo inatumika kujua kipaji chako.
Hebu waulize nyie
mnanionaje, mna picha gani? Mnahisi nina kipaji Gani? Baada ya kuwauliza hayo
wao ndio watakupa picha kamili juu ya kipaji chako na maisha yako kwa ujumla.
3. Matatizo.
Matatizo
ni njia nzuri ya bora sana ya kugundua kipaji chako. Ulimwegu wa leo ni ulimwengu
wenye changamoto nyingi sana, hata hivyo kutokana na suala hilo, pale matatizo
yanapotokea na kuyapatia ufumbuzi sahihi hapo ndipo utakapojua kipaji chako.
Kwa mfano watu wengi
leo hii wanapenda maisha ya kufanyiwa kila kitu. Tuchukulie leo hii unamtegemea
mtu fulani ili aweze kukutimizia lengo lako. Halafu siku ya siku mtu huyo
anakufukuza nyumbani kwake na kukuambia nenda kajitegemee.
Baada ya kuambiwa
hivyo ndipo unakuja kugundua ni kipi kipaji chako baadala ya kuendelea
kuwa tegemezi. Hebu tuone mfano mwingine unakuta mtu alikuwa ni mfanyakazi wa
ofisini ila baada ya kustafu unajikita katika ufugaji mwisho wa siku unagundua
wewe ulikuwa una kipaji cha ufugaji badala ya kufanya kazi za maofisini.
Hivyo wito wangu
kwako ni vyema ukagundua kipaji chako mapema usisubiri changamoto fulani
zitokee ndipo ugundue kipaji chako.
4. Mashindano.
Kuna
baadhi ya nchi huandaa mashindano mbalimbali kwa ajili ya kusaka vipaji, hili
jambo jema sana hata hapa kwetu nchini kuna baadhi ya mashindano hufanyika ambayo
husaidia kujua vipaji vya watu kama vile bongo star search, fiesta, DJ
compition, umiseta na mangineyo mengi.
Hivyo kama kweli
unataka kujua kipaji chako endapo yatatokea mashindano yoyote yale jitahidi
sana kwenda kushiriki kwani hii itakusaidia kwa kiwango kikubwa kuweza kujua ni
kipi kipaji chako.
Mpaka
kufikia hapo niweke nukta kwa kusema kama ukwisha kugundua hicho kipaji chako
ni vyema ukajua ni namna gani ya kugeuza hicho kipaji chako kuwa pesa, kwani
hapo ndipo palipo kuwa na changamoto kubwa.
Ndimi
Afisa mipango Benson Chonya.
Simu( 0757909943)
bensonchonya23@gmail.com
Simu( 0757909943)
bensonchonya23@gmail.com
Jun 27, 2016
Mambo Muhimu Ya Kukumbuka Kama Unataka Kuwa Mjasiriamali Mwenye Mafanikio.
Kila
kitu katika maisha ya binadamu kinaanza kama wazo. Haijalishi kitu hicho kimeleta
mafanikio au la, lakini mwanzo wake huwa unaanzia kwenye wazo analokuwa nalo
mtu.
Kumbuka
siku zote, mawazo yako ndiyo
yanayokufanya uwe na maamuzi ya aina fulani. Maamuzi hayo pia ndiyo yanakufanya
uwe na matendo ya aina fulani. Na matendo hayo ndiyo yanayotoa matokeo ya kile
ukifanyacho.
Kwa
hiyo, ikiwa unataka kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio, kitu cha kwanza unachotakiwa
kuwa nacho ni mawazo sahihi. Unapokuwa na mawazo sahihi yatakusaidia kufanya
maamuzi na matendo sahihi.
Hivyo,
mafanikio utayaona kwa sababu maamuzi na matendo yako yatakuwa sawa kukusaidia
kufanikiwa. Kwa sababu hiyo, ni lazima kukumbuka mambo ya msingi kama unataka
kuwa mjasiramali mwenye mafanikio. Kwa vipi?
Yafuatayo
Ndiyo Mambo Muhimu Ya Kukumbuka Kama
Unataka Kuwa Mjasiriamali Mwenye Mafanikio.
1.
Jifunze kuwajibika.
Mjasiriamali
mwenye mafanikio ni yule ambaye anawajibika na kuweka mambo sawa kila wakati na
sio kusubiri hali fulani ndizo zimletee mafanikio. Mjasiriamali huyu anakuwa
tayari kukabiliana na kila changamoto na kutatua.
Hili
ni jambo muhimu sana la kukumbuka na kuweka kwenye akili ikiwa unataka kuwa
mjasirimali mwenye mafanikio. Wakati wote usisubiri matokeo ya aina fulani bali
pambana mpaka kieleweke.
Jifunze kuwajibika. |
2.
Jifunze kuwa mbunifu.
Ubunifu
ni njia pekee itakayokufanya uwe mjasiriamali wa mafanikio. Hakuna mafanikio
kwenye ujasiriamli kama wewe si mbunifu. Karibia kila kitu kinaweza kufa kwako
usipochukua hatua za kuwa mbunifu.
Jifunze
kufikiri tofauti na wajasiriamali wengine. Kwa mfano kila wakati unaweza ukawa
unajiuliza ufanye nini cha ziada ili uongeze idadi ya wateja kwenye biashara
yako? hapo ndipo unatakiwa kubuni mambo ya ziada ambayo wengine hawana.
3.
Jiamini.
Vipo
vikwazo vingi katika safari ya mafanikio. Lakini yote hayo yanapotokea ni
wakati wa kujifunza kujiamini wewe mwenyewe na kuamini ndoto zako kuwa unaweza
kuzifikia. Hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya hivyo zaidi yako. Ni lazima
ujue kujiamini kwako ndio msingi mkubwa wa mafanikio.
Wajasiriamali
wenye mafanikio wana hulka au tabia ya kujiamini sana. Hicho ndicho
kinachowasaidia waweze kufikia viwango vya juu vya mafanikio. Hata wewe kama
usipochukua jukumu la kuweza kujiamini hakuna utakachoweza kufanikisha sanasana
utazidi kushindwa.
4.
Usikate tamaa mapema.
Hakuna
kitu kibaya kama kukata tamaa mapema. Unapokuwa unakata tamaa unakuwa
unaitangazia dunia kwamba wewe huwezi tena. Na kimsingi hakuna faida hata moja
ambayo mtu anaweza kuipata eti kwa sababu ya kukata tamaa.
Wajasiriamali
wakubwa wenye mafanikio ni ving’ang’anizi wakubwa wa malengo na ndoto zao. Wanajua
bila kufanya hivyo hakuna kitakachofanikiwa. Siku zote mafanikio yanakutaka
usikate tamaa mapema la sivyo, utayasikia mafanikio kwa wengine.
5.
Jitoe mhanga.
Je,
wewe ni miongoni mwa watu wanaojitoa mhanga kuhakikisha ndoto zao zinatimia? Kama
jibu ni ndiyo basi wewe ni miongoni mwa wajasiriamali wenye mafanikio makubwa.
Sifa
kubwa ya wajasiriamali wenye mafanikio ni kujitoa. Mara nyingi huwa hawaangalii
hasara watakazozipata zaidi sana huangalia kile watakachokipata. Hili ni jambo
muhimu sana la kulielewa na kuliweka kwenye akili yako ikiwa wewe unataka kuwa
mjasiriamali wa mafanikio.
6.
Nenda hatua ya ziada.
Jifunze
kujiongeza na kuongeza vitu vya ziada ambavyo ni tofauti na wajasiriamali
wengine. Ikiwa huwezi kujitofautisha wewe na wajasiriamali wegine, basi moja
kwa moja upo kwenye hatari pengine ya kushindwa kwa baadae.
Hapa
unatakiwa kujitoa na kufanya kazi zako kwa uhakika na muda mrefu. Hiyo haitoshi
unatakiwa kujifunza kila wakati yale ambayo wenzio wanayafanya. Kwa kwenda
hatua za ziada ni silaha muhimu ya kukufanya ukawa mjasiriamali wa mafanikio.
Naamini
umejifunza kitu cha kukusidia kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio. Lakini usiishie
hapa endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kupata maarifa yatakayoboresha
maisha yako.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048 035,
Jun 24, 2016
Aina Tatu Za Mawazo Zinazokufanya Ushindwe Au Ufanikiwe.
Kiasili
binadamu tumepewa uwezo mkubwa wa kufikiri ukitofautisha na wanyama wengine.
Uwezo huu tulionao huwa unakuja hasa kutokana na matumizi ya mawazo au kufikiri
kwetu. Kufikiri huko ambapo tunafanya kila siku na kila wakati ndipo
kunapotufanya tuwe na maisha ya aina fulani, haijalishi yawe ya mafanikio au
kushindwa.
Lakini
hata hivyo wengi wetu huwa tunafikiri au tuna mawazo ya kimazoea na kushindwa
kutambua kwamba hayo mawazo yetu pia yamegawanyika. Kwa mawazo yoyote uliyonayo
mara huwa yamegawanyika katika sehemu. Kwa mfano unapowaza wazo fulani, wazo
hilo linakuwa lipo moja kwa moja kwenye sehemu ya kwanza, au ya pili au ya tatu
ya mawazo yako.
Kivipi
hili linatokea? Fuatana nami katika makala haya kujua aina tatu za mawazo
zinazokufanya ushindwe au ufafanikiwe katika maisha yako.
1.
Mawazo elekezi.
Haya
ni mawazo yanayoleta mafanikio. Kwa lugha nyingine haya ni mawazo chanya. Mawazo
yenye uwezo wa kutubalisha na kutufanya tuwe na mawazo bora. Haya ni mawazo
yanakufanya uamini unaweza kufanya biashara, unaweza kuwa tajiri au unaweza
kuacha chochote.
Kwa
kifupi, haya ni mawazo yanayokupa mwongozo wa kufanikiwa. Unapokuwa na mawazo
haya kila wakati, elewa kabisa upo kwenye njia sahihi ya kuelekea kwenye
mafanikio. Ni mawazo yanayotoa hatma ya kesho yetu itakuwaje.
2.
Mawazo ya kuharibu.
Kama
huna mawazo chanya au mawazo elekezi ya kukusaidia basi elewa utakuwa na mawazo
ya kuharibu. Mawazo haya wakati mwingine yanafahamika kama mawazo hasi. Haya ni
mawazo ambayo kila wakati yanakwambia
huwezi kufanikiwa au huwezi kufanya hili.
Haya
ni mawazo yanayoua na kuharibu maisha ya wengi. Jaribu kujiuliza utakuwa ni mtu
wa aina gani ikiwa kila unalolifanya unaona kama haliwezi kufanikiwa? Ukiwa na
mawazo haya, tambua una mawazo ya kuharibu ambayo hayawezi kukusaidia kwa
chochote.
3.
Mawazo ya hovyo.
Unapokuwa
na mawazo haya mara nyingi yanakuungoza katika vitu kama kupoteza muda au
kufanya mambo yasiyo na faida. Utakuta badala ya kukaa chini na kufanya mambo
ambayo yanaweza yakakusaidia kufanikiwa, badala yake unajikuta unafanya mambo
ambayo hayana msaada kama kupiga soga na marafiki.
Kumbuka,
aina hizi za mawazo ndizo zinazokufanya ufanikiwe au ushindwe katika jambo
unalolifanya. Jambo kubwa kwako la kujiuliza je, ni aina gani ya mawazo
uliyonayo ambayo inakutawala sana? Kwa aina hiyo ya mawazo uliyonayo ndiyo
itakayoamua maisha yako yaweje.
Nikutakie
siku njema na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku. Hakikisha
pia usikose kuwashirikisha wengine waendelee kujifunza kupitia mtandao wako
huu.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Jun 23, 2016
Je, Unahitaji Mafanikio Ndani Ya Muda Mfupi?
Kuna wakati inakupasa uweze kuondokana kwenye jopo la watu ambao wanalalamika
na kuingia kwenye kundi la watu ambao ni watu wasaka mafanikio daima na sio
walalamikaji. Kuna baadhi ya watu huelekeza mawazo yao hasi katika kulaumu watu
wengine kuliko kuwaza ni kwa jinsi gani wataweza kuyasaka mafanikio kiurahisi
kabisa.
Mara nyingi sana tunatumia muda
mwingi katika kufanya mambo ambayo hayana manufaa katika maisha yetu. Kwa
mfano, tumekuwa tukipoteza muda kwenye mitandao au kupenda mazungumzo yasiyo na
msaada kwetu. Kwa kuwa tunapoteza muda huo mwingi katika mambo yasikuwa na tija
inafika mahali tunakuwa ni watu maisha ya kawaida kila siku.
Na ili kutoka hapo kwenye kuishi
maisha ya kawaida, hakuna dawa nyingine zaidi ya kuacha kufanya mambo yasiyo na
manufaa kwetu. Ukiweza kufanya hivyo, mafanikio utayapata tena kwa muda mfupi. Siri
kubwa ya kupata mafanikio kwa muda mfupi ipo kwenye kufanya mambo yenye manufaa
kwako kila siku na si kinyume cha hapo.
Najua unakuna kichwa unawaza “daaaah!
sasa Afisa mipango kama nikitaka mafanikio kwa muda mfupi nafanyaje tena?” Kama
ni hivyo na unataka kusikia jibu kutoka kwa afisa Benson nisikilize. Ili kupata
mafanikio kwa muda mfupi, mbali na kutokufanya mambo ambayo hayana manufaa
kwako pia zingatia sana yafuatayo:-
1. Amini nguvu iliyopo ndani yako
kwamba unaweza.
Watu wengi hawaamini nguvu ambazo zipo ndani yao. Wengi huamini ya kwamba mafanikio
huja kwa watu mafisadi peke yao. La hasha mafanikio yapo kwa kila mtu ambaye anamini
ya kwamba yeye ni mshindi katika maisha yake, bila kuangalia ni changamoto
ngapi ambazo amezipitia.
Unapokuwa unaamini uwezo na nguvu
kubwa uliyonayo ndani mwako, inakusaidia sana kufikia mafanikio yako kwa muda
mfupi. Kwa kadri utakavyozidi kuamini na kutumia vipawa na nguvu zilizopo ndani
yako, utajikuta mambo mengi yanaenda vizuri tofauti na ulivyokuwa ukiwaza.
Tumia muda sahihi, kufikia mafanikio yako. |
2. Kuwa na kusudi maalamu kwa
chochote anachotaka kufanya.
Moja ya changamoto ya watu wengi ambao walifeli kimaisha ni kwamba watu hao walifanya vitu bila kujua ni nini kusudio lao maalumu, hata hivyo ikawapelekea watu hao kuweza kuwa na malengo ambayo hayana tija. Unakuta mtu anafanya biashara ukimuuliza kusudio la kufanya biashara hiyo utakushanga ya kwamba hata mfanyabiashara huyo huenda ukawa hajui pia.
Unahitaji kuwa na picha kamili ya jambo ambalo unalifanya kwa miaka ya mbeleni. Picha hii ndiyo ambayo itakuonesha utaweza kufanikiwa kwa kiasi gani? Au utashindwa kwa kiasi gani. Kama ni biashara ni lazima uwe na mlolongo mzima wa biashara yako jinsi itakavyokuwa kwa siku za mbeleni.
3. Usichukue ushauri wa kila mtu.
Kimsingi maneno ya watu yapo ambayo yanajenga kwa namna moja ama nyingine. Ila maneno ambayo hajajengi ndiyo yapo mengi zaidi, kwa mfano leo hii utaka kufanya biashara utakwenda kumshirikisha mtu ambaye yupo karibu yako unakwenda kuomba ushauri, mtu huyo atakwambia biashara hiyo hafai.
Kimsingi maneno ya watu yapo ambayo yanajenga kwa namna moja ama nyingine. Ila maneno ambayo hajajengi ndiyo yapo mengi zaidi, kwa mfano leo hii utaka kufanya biashara utakwenda kumshirikisha mtu ambaye yupo karibu yako unakwenda kuomba ushauri, mtu huyo atakwambia biashara hiyo hafai.
Utakapoambiwa biashara hiyo haifai mwishowe
unajikuta unawabadilisha mawazo na kufanya jambo jingine na kwa kuwe wewe haujia
amini unajikuta huna hata jambo hata moja ambalo unalifanya kwa uhakika.
Mwishowe unakosa hata jambo moja ambalo lina manufaa kwako.
4. Fanya jambo la kwako.
Ili kufanikiwa kwa muda mfupi ni lazima kujua u wewe wako ndio siri ya mafanikio kwani moja ya watu wengi walioshindwa katika maisha ni kwamba waling'ang'ana kufanya vitu visivyokuwa vya kwao. Nikuache na swali la kujiuliza je jambo ambalo unalifanya ni lako?
Pia kumbuka maisha ya mwanadamu yanafanana na miiba ya michongoma kwa maana ya kwamba kila wakati uwe tayari katika kupambana na changamoto ambazo zinajitokeza kama ilivyo kwa miiba ya michongoma, maana miiba hii kila wakati upo tayari kwa ajiri ya upambanaji tu.
Mwisho Afisa nimalizie kwa kusema akili ikiamua kufanya jambo inawezekana hivyo inahitajika nguvu ya mwili katika kuisaidia akili katika utekelezaji. Naamini ukifanya mambo hayo yatakusaidaia kufikia mafanikio yako kwa muda sahihi unaohitajika.
ANGALIZO; Lengo la makala hii ni kukuhamasisha kufikia mafanikio yako kwa muda sahihi kama inavyotakiwa iwe. Lakini usije ukafikiri makala hii inakutaka utumie njia za mkato ili ufikie mafanikio yako kwa muda mfupi. Makala hii inahitaji uachanae na mambo yote yatakayokupelekea uchelewe sana kufanikiwa.
Imeandikwa na afisa mipango: Benson Chonya.
Jun 22, 2016
Kijana Wa Umri Wa Chini Miaka 30 Anayemiliki Kampuni Yake Binafsi.
"Endapo utafika miaka 25 hujui unapoelekea
ujue fika umekwisha potea"
Hayo ni maneno ambayo aliwahi kuniambia mama yangu mpendwa, hivyo kila nikikaa huwa yanajirudia sana kichwani mwangu. Maneno hayo ndiyo ambayo yananipa hamasa kwa kila jambo ambalo nalitenda siku zote, pia hunifanya niongeze juhudi na maarifa zaidi kwa kila jambo ambalo nalifanya.
Hayo ni maneno ambayo aliwahi kuniambia mama yangu mpendwa, hivyo kila nikikaa huwa yanajirudia sana kichwani mwangu. Maneno hayo ndiyo ambayo yananipa hamasa kwa kila jambo ambalo nalitenda siku zote, pia hunifanya niongeze juhudi na maarifa zaidi kwa kila jambo ambalo nalifanya.
Kwani juhudi
nilizonazo hunifanya niwe mbunifu kila jua lichomazapo. Ubunifu huu huwa
unanijenga hasa pale ninapoyakumbuka maneno ya mwalimu wangu wa somo la brand
Tanzania Mr. Nduku Jr kwani mara kadhaa alikiwa ananiambia ya kwamba kwa kuwa
zama zimebadilika hauhitaji kupeleka hirizi kwenye biashara bali unahitaji
ubunifu utakao kutofautisha na watu wengine.
Hivyo katika kuthibisha juu ya kauli hizo ambazo nimezieleza, mara namuona kijana kwa mbali ambaye amevalaa tisheti nyeupe ambaye yupo ofisini kwake ila kadri nivyozidi kusogea nagundua ya kwamba wapo na vijana wenzake, huku kijana huyo aliyevalia tisheti ya nyeupe akiwa anazungumza.
Hivyo katika kuthibisha juu ya kauli hizo ambazo nimezieleza, mara namuona kijana kwa mbali ambaye amevalaa tisheti nyeupe ambaye yupo ofisini kwake ila kadri nivyozidi kusogea nagundua ya kwamba wapo na vijana wenzake, huku kijana huyo aliyevalia tisheti ya nyeupe akiwa anazungumza.
Loooh! Kadri
ninavyozidi kusogea na gundua ya kwamba tisheti hilo limeandikwa Tim success ltd. Mmh kama ilivyokuwa
kawaida yangu nikiona neno success (Mafanikio) huwa mishipa ya aldenalini huwa inashutuka kama nimepita
sehemu yenye giza huku nikiwa na hofu fulani.
Hivyo kwa kuwa nimeona fulana imeandikwa success (Mafanikio) nikataka kujua mawili matatu kutoka kwao na kuwaomba nifanye mazungumzo japo ya dakika chache na kijana huyo.
Hivyo kwa kuwa nimeona fulana imeandikwa success (Mafanikio) nikataka kujua mawili matatu kutoka kwao na kuwaomba nifanye mazungumzo japo ya dakika chache na kijana huyo.
Baada ya
kujitambulisha mimi, kisha kijana huyo akaanza kujitambulisha kwa kusema; "Kwa
jina naitwa Tamimu ni kijana ambaye mnamo mwaka 2008 niliweza kuhitimu chuo
kilichopo mkoani morogoro, pia pale morogoro niliweza kusomea masomo masuala ya
tekinolojia ya habari ya mawasiliano(IT).
Baada ya kumaliza
niliungana na wanafunzi wengine mbalimbali katika kuandika barua kwa ajili ya
kuomba ajira kama wafanyavyo vijana wengi baada ya kumaliza vyuo.
Muda mwingi ulipita bila kuona mafanikio ya kupata ajira, kila tangazo ambalo lililotoka kuhusiana na ajira ambalo lilikuwa linahusu ilikuwa ni lazima niweze kutuma barua ya maombi. Mara kadhaa nilikuwa nachaguliwa mpaka kufanya usaili lakini matokea yake nilikuwa ninaishia kufanya usali tu, licha yakuwa nilihitimu na kuwa nawastani mkubwa wa alama. Ilifika mahali mpaka nikaanza kulaumu ni kwanini nilikwenda kusoma?
Miaka mitatu ilikatika bila mafanikio yeyote ya kupata ajira, mnamo mwaka 2012 nilikutana na kaka mmoja huko maeneo ya kwetu songea, ambaye alikuwa ni rafiki wa kaka yangu ambaye alikuwa anaishi huko jijini Dar-es-salaam.
Muda mwingi ulipita bila kuona mafanikio ya kupata ajira, kila tangazo ambalo lililotoka kuhusiana na ajira ambalo lilikuwa linahusu ilikuwa ni lazima niweze kutuma barua ya maombi. Mara kadhaa nilikuwa nachaguliwa mpaka kufanya usaili lakini matokea yake nilikuwa ninaishia kufanya usali tu, licha yakuwa nilihitimu na kuwa nawastani mkubwa wa alama. Ilifika mahali mpaka nikaanza kulaumu ni kwanini nilikwenda kusoma?
Miaka mitatu ilikatika bila mafanikio yeyote ya kupata ajira, mnamo mwaka 2012 nilikutana na kaka mmoja huko maeneo ya kwetu songea, ambaye alikuwa ni rafiki wa kaka yangu ambaye alikuwa anaishi huko jijini Dar-es-salaam.
Hivyo kwa kuwa
nilikuwa naamini ya kwamba Dar-es-salaam ni njia panda ya kuelelekea
ulaya hivyo niliamini ya kuwa huko kila kitu kipo, hii ni kutokana jinsi ambavyo
huwa nasikia na kuona habari mbalimbali juu ya jiji hilo hivyo niliamini
kupitia huyo rafiki yake kaka, nitakwenda kupata jawabu tosha juu ya tatizo
langu la ajira.
Hivyo nilimueleza changamoto kubwa ambayo ilikuwa inanisibu, baadae kaka huyo(jina limehifadhiwa) alinimbia ya kwamba kutoka na kitu ambacho nimesomea nina uwezo kufanya kitu kikubwa na kutengeneza kipato changu ambacho kitasaidia kutatua changamoto zangu binafsi pasipo kutegemea suala la ajira ambalo ni changamoto sana kwa wengi.
Baada ya siku chache tangu siku ambayo tulizungumza maneno yale, tuliweza kusafiri kwenda Dar, huko niliweza kujifunza masuala ya kutengeneza mabango ya kutangaza biashara mbalimbali, bussiness card yaani kwa ufupi naweza sema nilijifunza masuala yote yanayohusiana na designing kwa ujumla.
Hivyo nilimueleza changamoto kubwa ambayo ilikuwa inanisibu, baadae kaka huyo(jina limehifadhiwa) alinimbia ya kwamba kutoka na kitu ambacho nimesomea nina uwezo kufanya kitu kikubwa na kutengeneza kipato changu ambacho kitasaidia kutatua changamoto zangu binafsi pasipo kutegemea suala la ajira ambalo ni changamoto sana kwa wengi.
Baada ya siku chache tangu siku ambayo tulizungumza maneno yale, tuliweza kusafiri kwenda Dar, huko niliweza kujifunza masuala ya kutengeneza mabango ya kutangaza biashara mbalimbali, bussiness card yaani kwa ufupi naweza sema nilijifunza masuala yote yanayohusiana na designing kwa ujumla.
Pia nilijikita zaidi
zaidi katika kuweka alarm za magari, muziki kwenye magari pamoja na stika za
magari na ufundi mwingine. Kufanya hivi kukanifanya niweze
kupata kipato ambacho nilijitahidi kuweka akiba, akiba ambayo ilinifanya nije
nimiliki kampuni yangu ambayo inaitwaTim success Ltd kama unavyoona
kwenye tishiti hii.
Kijana Tamimu katikati, akiwa na mwandishi wa makala haya Benson Chonya, Kushoto kabisa. |
Pamoja na misukosuko
mingi ambayo nilikuwa naipata wakati wa kusajili kampuni hii nilijipa moyo
pasipo kuwa na hata chembe ya kukata tamaa. Ilifika kipindi hata pesa ya
kuendesha maisha yangu ilikuwa ngumu kwa kuwa pesa nyingi zilitumika katika
nauli pamoja na usajili wa kampuni.
KUHUSU KAMPUNI
Kwa kifupi ni kwamba
mimi kama ndiye mwazilishi wa kampuni niliwaza ya kwamba katika nchi yetu lina
jopo kubwa ni vijana. Na kwa kuwa asilimia kubwa ya vijana hao ni wale wasomi
na wasio wasomi, lakini changamoto kubwa ambayo inatukabili ni suala la ajira,
nikaona ni vyema kwangu niifanye kama fursa ili niweze kuwasaidia vijana
wenzangu, hivyo nikawakusanya vijana wenye ujuzi na wasio na ujuzi tukajifunza
pamoja kuweza kufanya mambo mbalimbali.
Mambo hayo ni kama
vile umeme , mapambo ya nyumba, kufunga kamera za ulinzi majumbani, kufanya
designing, kupima viwanja(land survey),kuandika miradi mbalimbali na kuwashauri
vijana wengine ambao wamekata tamaa na Maisha haya.
Kama timu ya mafanikio mnaleta suluhisho na changamoto gani ambayo inaihusu jamii kwa ujumla? Kama timu tumeamua kuja na suluhisho la changamoto ya maji. Kwa kuwa tunasema kwa kuwa maji ni uhai, hivyo tukaona ni vyema tuweze kuja na majibu kwani changamoto ya maji ni kubwa.
Kama timu ya mafanikio mnaleta suluhisho na changamoto gani ambayo inaihusu jamii kwa ujumla? Kama timu tumeamua kuja na suluhisho la changamoto ya maji. Kwa kuwa tunasema kwa kuwa maji ni uhai, hivyo tukaona ni vyema tuweze kuja na majibu kwani changamoto ya maji ni kubwa.
Unajua ndugu
mwandishi licha ya kuendelea kusema ile sera ya kilimo kilimo kwanza lakini
tunashidwa kufikia sera hiyo kwa kiwango cha juu, hii ni kutokana hatuna kilimo
cha umwagiliaji, hivyo tunajikuta tunafanya kilimo kilekile miaka nenda miaka
rudi. Pia ukijaribu kufanya uchunguzi mdogo utagundua ya kwamba majimbo mengi
yana changamoto ya maji.
Hivyo sisi kama
vijana wachapa kazi tumeamua kuja na suluhisho ambapo tunatengeneza visima
ambavyo maji mengi yatavunwa kwa kutumia nguvu ya upepo, hapa ndugu mwandishi
haitaji uwepo wa Umeme, au kupungua kwa maji kwenye chanzo bali mashine hii
itatoa maji muda wote, nafikiri hii itasaidia sana hasa maeneo ya mjini na
vijini ambayo kiuhalisia yana changamoto ya maji, wito wetu kwa viongozi Wa
serikali na watu wengine hii ni fursa ambayo itabadili Tanzania kwa asilimia
kubwa sana, kwani tutakwenda kuwa wakulima bora ambao hatutegemei misimu
kufanya kilimo chetu tu.
Neno langu la mwisho ni kwamba kupata maendeleo kwa kiwango kikubwa inawezekana lakini jambo la msingi la kuzingatia ni kwamba inahitajika ushilikishwaji wa wananchi katika kutoa maamuzi yao kwani ni muhimu sana, mwisho kabisa nawashauri sana vijana ambao hawana ajira ni kwamba wazipe nafasi bongo zao kuweza kufikiri kwa umakini ni jinsi gani wataweza kuondokana na adhaa hii ya ajira kama tulivyofanya sisi
Neno langu la mwisho ni kwamba kupata maendeleo kwa kiwango kikubwa inawezekana lakini jambo la msingi la kuzingatia ni kwamba inahitajika ushilikishwaji wa wananchi katika kutoa maamuzi yao kwani ni muhimu sana, mwisho kabisa nawashauri sana vijana ambao hawana ajira ni kwamba wazipe nafasi bongo zao kuweza kufikiri kwa umakini ni jinsi gani wataweza kuondokana na adhaa hii ya ajira kama tulivyofanya sisi
Kama una swali lolote kwa Mr tamimu piga au sms kwenda
0714-800922.
Kama una hadithi kama hizi zenye ukweli na ubunifu wasiliana na afisa mipango Benson chonya (0757-909942).
0714-800922.
Kama una hadithi kama hizi zenye ukweli na ubunifu wasiliana na afisa mipango Benson chonya (0757-909942).
Jun 21, 2016
Malezi Mabaya Ya Familia Ni Adui Wa Mafanikio.
Miongoni mwa sababu
kubwa iliyonifanya leo kuchukua kalamu kuweza kumwaga wino wangu juu ya
karatasi ni kwamba uvumilivu umenishinda ndani ya moyo wangu. Mambo yamenifika
shingoni ni lazima niyaseme leo kabla umri wangu hajaelekea jioni (uzeeni).
Hata nikiangalia saa nayo bado mishale inazunguka pia hata siku nazo hazijawahi
kumsaliti lady jay dee kwamba siku
zinaganda.
Siku chache
zilizopita tuliadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kama ambavyo huadhimishwa
kila mwaka kitu hiki ni kizuri ambacho kinafaa kiendelezwe katika jamii
tunazoishi kwenu kufanya hivi ni kudumisha amani na upendo kwa watoto wetu.
Tuachane na hayo kwani hayo yamekwishapita na
wala haina haja tena kuzungumzia masuala ya maadhimisho hayo. Ila leo
nimeona ni vyema tuzungumzie kwa uchache juu ya MADILI BORA YA FAMILIA.
Jamii ya leo imekosa elimu tosha juu ya malezi bora kwa familia.
Hebu jaribu
kuzunguka mtaa wa kwanza utagundua kati ya watoto 9 kati ya 10 wanazungumza
lugha za matusi zaidi kama wanaimba nyimbo za injili au bongo fleva.
Ukitoka mtaa wa kwanza pita mtaa wa pili huko nako utastajabu ya Musa maana
huko watu wazima na akili zao wanacheza nyimbo za vigodoro, baikoko pamoja na
watoto wao.
Watu wazima hao
ukichungunza kwa umakini utagundua nguo ambazo wamezivaa ni fupi mithili ya
mabawa ya nzi, watu hao nguo ndefu na za heshima kwao huwa ni zenye upupu. Mmmh
tunakwenda wapi?
Tena toka mtaa pili
ingia mtaa wa tatu huko nako utashangaa kuokota dhahabu mchangani, watoto
wadogo wamekuwa ndio wanaigizwa kununua bia, madawa ya kulevya na mengineyo
mengi. Ukitoka mtaa huo jaribu kuingia mtaa mwisho huko nako kweli utaamini
dunia inaelekea ukiongoni maana kuna mambo ya ajabu sio kawaida ya nchi, kama
Tanzania huko utakutana na watoto ambao ni omba omba wengi ambao waliletwa
duniani na wazazi wenye akili timamu kabisa, wazazi hawa huwa napenda kuwaita
"sura ya mzee akili ya mtoto" maana hawafai hata kidogo.
Tunasema mara kadhaa kuwa kijana ni taifa la
kesho. Maneno hayo yatadhibitisha ukweli huo kwa malezi mtindo huo? Ya kuwalea
watoto malezi yasikuwa na heshima wala utukufu Mbele za Mungu. Kiukweli
najaribu kujiuliza kwa umakini bila hata kupata majibu sahihi tunaelekea wapi
kwa maisha ya aina hiyo?
Kimsingi ni kwamba
ugumu wa maisha haya tunayasababisha sisi wenyewe walezi wa familia zetu kwa
namna moja ama nyingine. Mara kadhaa tumekuwa tukiwatamkia maneno mabaya sana
watoto zetu hata hivyo kupelekea madili mabovu kwa jamaii hii. Mfano wa maneno
hayo wapo wale wanaowambia kuwa watoto wao ni wezi au vibaka.
Kila kukicha watoto wa mitaani wanaongezeka kwa idadi kubwa, ukichunguza kwa umakini juu ya hilo utagundua ya kwamba chanzo la ongezeko hilo ni mateso na mihangano mingi ya kifamilia ambayo kila baada ya sekunde inafanya ongozeko la watoto hao.
Kila kukicha watoto wa mitaani wanaongezeka kwa idadi kubwa, ukichunguza kwa umakini juu ya hilo utagundua ya kwamba chanzo la ongezeko hilo ni mateso na mihangano mingi ya kifamilia ambayo kila baada ya sekunde inafanya ongozeko la watoto hao.
Wapo pia baadhi ya
wazazi huwakatisha tamaa watoto wao kwa namna moja ama nyingi pindi wakiwa
wadogo na kusababisha maisha magumu kwa watoto na kuwapotezea dira ya maisha.
Watoto yatima wanaachwa katika mazingira magumu sana ambayo kila mwanajamii
hufumba macho pindi anapo watoto wa aina hiyo na kuona mtu huyo hausiki.
Tunaelekea wapi?
Ikiwa tunasema ya kuwa dalili ya mvua ni mawingu kwa methali hiyo tunaweza tukafananisha na kusema ya kwamba dalili ya umaskini wa nchi ni mateso, chuki na migogoro ya kifamilia inaandaa kizazi chenye maisha duni ambacho kinaamini katika misingi ya kuombaomba, wizi, utumiaji wa madawa ya kulevya na tabia nyingine ambazo hazipendezi machoni pa Mungu na kwa watu wenye heshima zao. Nauliza tena tunaandaa kizazi cha aina gani?
Ikiwa tunasema ya kuwa dalili ya mvua ni mawingu kwa methali hiyo tunaweza tukafananisha na kusema ya kwamba dalili ya umaskini wa nchi ni mateso, chuki na migogoro ya kifamilia inaandaa kizazi chenye maisha duni ambacho kinaamini katika misingi ya kuombaomba, wizi, utumiaji wa madawa ya kulevya na tabia nyingine ambazo hazipendezi machoni pa Mungu na kwa watu wenye heshima zao. Nauliza tena tunaandaa kizazi cha aina gani?
Hebu kabla sijaenda kuweka nukta tuangalie
malezi ya watoto katika baadhi ya familia nyingi. Katika kufanya utafiti
nimegundua ya kwamba malezi ndiye ambaye yanaandaa kwa kiasi kikubwa mafanikio
ya mtu kwa namna moja ama nyingine. Wazazi wengi hawana muda wa kukaa na
kuzungumza na watoto wao, ili kujua watoto wao wanahitaji nini katika maisha
yao, wazazi wengi wamekuwa wanafahamu ya kuwa mtoto ni lazima aende shule,
apete mahitaji mengine kama kula, malazi pamoja na chakula huku wamesahau watoto
wanahitaji zaidi ya hayo.
Hebu tujiulize ya
kwamba ni mara ngapi umekaa na watoto wako kuongea nao kuhusu mambo mbalimbali
yatakayomjenga kwa hapo baadae? Tujiulize tena hili tatizo na ongezeko la
watoto yatima chanzo chake ni nini? Halafu kwa nini kila huwa hatujali
juu ya jambo hili.
Wito wangu ni kwamba tuache kuchukulia vitu
katika taswira ya kawaida, najua suluhu juu ya jambo hili lipo payana kabisa,
tuache kupita na gari kwa mwendo wa kasi ili tuone mambo haya yanavyowadhuru
watoto wengi katika nchi yetu. Kuna usemi unasema mtoto wa mwenzio ni wako.
Ukweli juu ya kauli
hii upo wapi? Kauli hiyo ipo kwa baadhi ya vituo vya kulelea watoto yatima na
mazingira magumi ila katika taasisi na watu wengi kauli hiyo imekuwa haikuhusu.
Tafadhari najua ujumbe umefika mahali pake hivyo ni wakati muafaka wa kuchukua
hatua mahususi kuondokana na suala hili.
Ndimi, Afisa
mipango Benson chonya.
Jun 20, 2016
Mambo 8 Ambayo Watu Wenye Mafanikio Hawapotezi Muda Kuyafanya.
Katika
harakati za kutafuta maisha si ajabu sana kukutana na watu walio kata tamaa au
watu wenye msongo wa mawazo inayotokana hasa na kuona ndoto na malengo yao
hayatimii. Ni jambo ambalo huwa linatokea sana miongonii mwetu na kufikia
mahali kuona maisha kama hayafai.
Lakini
kitu nilichokuja kugundua, kipo chanzo kikubwa kimoja tu ambacho hupelekea
kuona ndoto au malengo ya wengi kutokutumia na kusababisha msongo wa mawazo au
kukata tamaa. Chanzo hiki si kingine bali ni kupoteza muda kwa mambo madogo
madogo.
Ukiwa
kama mjasiriamali ni muhimu sana kujua thamani ya kila sekunde unayoitumia.
Sasa wengi hawalijui hili, wanapoteza muda hovyo na kujifanya wanatafuta
mafanikio. Wajasiriamali waliofanikiwa hawapotezi muda wao kwa mambo yasiyowasadia.
Ni
wakati umefika wa kujua kila thamani ya muda wako unaoutumia kuanzia dakika,
saa mpaka siku nzima. Usipoteze muda kufanya mambo yanayokurudisha nyuma. Anza
sasa kuishi kwa mafanikio, kwa kujifunza mambo ambayo wajasiriamali wenye
mafanikio hawapotezi muda kabisa kuyafanya:-
1.
Hawapotezi muda kwenye mitandao ya kijamii.
Kuingia
kwenye mitandao ya kijamii kama face book, twitter au instagram kuangalia
taarifa za hapa na pale ni moja ya sehemu ya maisha yetu ya sasa. Lakini ikiwa
utashindwa kutawala muda wako na kujikuta wewe ni mtu wa kuperuzi utapoteza
muda mwingi sana ambao ungekusaidia kwa mambo mengine.
Watu
wenye mafanikio wana nidhamu kubwa sana juu ya hili, na wakati wote huwa makini
na mitandao hii ili isiwapotezee muda. Kama wewe ni mlevi wa mitandao ya
kijamii, jiwekee muda wa kuingia huko na kuangalia mambo yako. Usiingie tu kwa
kuwa unao muda. Yapo mambo mengi ya kufanya na muda ikiwa pamoja na kujisomea.
2.
Hawapotezi muda kufikiria makosa yaliyopita.
Kila
mtu anafanya makosa kwenye maisha yake, halikadhalika hata watu wenye mafanikio
wanafanya makosa pia. Siri kubwa ya mafanikio ni pale unapokosea jifunze juu ya
makosa hayo na ya kusaidie kuweza songa mbele zaidi ya pale ulipokuwa.
Inapotokea
unafanya kosa, huhitaji kulia sana zaidi ya kujifunza na kuchukua hatua za
kukusaidia kufanikiwa. Hata watu wenye mafanikio katika maisha yao wanapokosea,
huwa hawapotezi muda kufikiria makosa yao na kikubwa wanachokifanya ni
kuhakikisha wanajifunza na kuendelea mbele.
3.
Hawapotezi muda kuanza siku yako bila kuipangilia.
Watu
wenye mfanikio wana mipango ya kuwaongoza kufanikiwa kila siku. Ni watu wa
kuandika mipango yao ya kesho siku moja kabla. Hivyo, wanapoianza siku wanakuwa
wanajua ni wapi wanapotakiwa kuanzia na wapi wanapotakiwa kuishia kwa siku
inayofuata.
Kimsingi,
hakuna kitu kizuri kama kuianza siku yako kwa kuipangilia kwanza kabla
hujaifikia. Ni utaratibu mzuri sana ambao haukupotezei muda na unakufanya uishi
kwa ushindi. Watu wenye mafanikio hawapotezi muda kuainza siku yao bila
kuipangilia, nawe pia unatakiwa kujifunza juu ya hilo.
4.
Hawapotezi muda kufikiria mambo yanayofanywa na wengine.
Watu
wenye mafanikio ni mara nyingi hawapotezi muda wao wa thamani kujilinganisha na
watu wengine. Kwa kifupi, ni watu ambao hawaangalii sana wengine wanafanya nini
ili nao wafanye. Ni watu ambao wana misimamo yao wenyewe na kuamini kile
wanachokifanya kwamba kitawasaidia kufanikiwa hata kama ni kidogo.
Hata
hivyo kumbuka si vibaya kuangalia au kushindana na yale ambayo wengine
wanayafanya. Mtu pekee ambaye unaweza kushindana naye kwa yale unayoyafanya ni
wewe mwenyewe. Kila siku unatakiwa kuwa bora zaidi ya jana ili kuyaweka maisha
yako katika nafasi nzuri ya kufanikiwa.
5.
Hawapotezi muda kuwa na watu hasi.
Kwa
mujibu wa wataalamu wa mambo ya mafanikio wanatuambia kwamba, tabia na mienendo
yako kwa ujumla inaathiriwa sana na watu wanaokuzunguka. Watu wanaokuzunguka
wana athari kubwa sana juu ya maisha yako, haijalishi athari hizo ni chanya au
hasi.
Kwa
kulijua hilo watu wenye mafanikio, huwa ni watu ambao hawapotezi muda wao
kabisa kuwa na watu hasi. Kwa sababu wanajua watu hao watawakatisha tamaa na
kuwafanya washindwe kufikia malengo yao waliyojiwekea. Hivyo hicho ni kitu
amabacho huwasaidia sana kufanikiwa.
6.
Hawapotezi muda kwa mambo wasiyoyaweza kuyatawala.
Katika
maisha ya binadamu huwa yapo mambo na matukio ambayo katika hali ya kawaida
huwa si rahisi kuyatawala. Matukio haya yanaweza yakawa kama ajali, ugonjwa,
kufikiwa au hali mabaya ya uchumi. Haya ni baadhi ya matukio ambayo binadamu
huweza kukutana nayo na sio rahisi kwake kuyatawala.
Kwa
watu wenye mafanikio, wanapokutana na matukio ya aina hii, kwao huwa si rahisi
sana kupoteza muda na kuendelea kuyafikiria. Kitu wanachokifanya yanapowakuta
matukio kama hayo ni kuyapokea kama yalivyo, kisha baada ya kuyatatua basi
huachana nayo na si kuendelea tena kuyafikiria kila wakati.
Kwa
kuhitimisha makala haya, naamini umejifunza kitu kuhusiana na mambo amabayo
watu wenye mafanikio ambayo hawapotezi muda wao kuyafikiria sana. Kitu cha
kufanya chukua hatua za kuelekea kubadilisha maisha yako.
Tunakutakia
kila la kheri katika safari ya maisha yako. Kitu kikubwa ambacho kama DIRA YAMAFANIKIO tunakuomba ni kwamba endelea kuwashirikisha wengine ili waweze
kujifunza kama wewe unavyofanya sasa.
DAIMA
TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email;
dirayamafanikio@gmail.com
Jun 17, 2016
Jinsi Ya Kutengeneza Tomato Souce.
Mara kadhaa nimekuwa nikileta Makala mbalimbali
ambazo zinakupa hamasa tu ila Makala ya leo ni pesa mkononi. Pesa mkononi ndiyo
ambayo kila mtu anahitaji. Pia nimeamua kukuletea makala haya ili tuendane sawa
na Tanzania ya viwanda.
Najua inawezekana kabisa kila mtu kuwa na
kiwanda, unashangaa wala usishangae maana huo ndio ukweli maana kila kitu
kinapatikana kiurahisi katika mazingira yetu.
Unajua kuwa mikono yako ndiyo itakayokupa pesa?
Kama hufahamu basi nimekuja kukujuza ni kivipi utatumia mikono yako ili uweze
kuwa tajiri.
Yafuatayo ndiyo mahitaji ya kutengeneza tomato
source.
1. Nyanya kilo 1.
2. Vitunguu maji viwili.
3. Vinegar vijiko 3 vya chai.
4. Sukari vijiko 2 vya chai.
5. Chumvi kijiko kimoja cha chai
6. Maji ya moto kikombe kimoja cha chai.
7. Mafuta ya kula vijiko 7 ya vyakula.
Haya ndiyo mahitaji ya kutaka kutengeneza tomato souce, hata hivyo kama unataka kutengeneza zaidi ya hapo unatakiwa kuongeza uwiano wa mahitaji hayo.
JINSI YA KUTENGENEZA TOMATO SOURCE.
HATUA YA KWANZA.
a) Menya nyanya na vitunguu kisha vikate vipande vidogo vidogo.
b) Tumia Brenda kusaga mchanganyiko wako.
c) Anza kuweka malighafi namba 1 hadi namba 4 katika brenda yako kutokana na ratio (uwiano ) uliopewa hapo juu. Saga kwa dakika kadhaa hadi uone imetokea rojo laini.
HATUA YA PILI.
a) Tumia sufuria yenye nafasi kupika mseto huu.
b) Weka sufuria yako jikoni tia mafuta ya kula acha yachemke kisha mwagia mseto wako na kisha uanze kukoroga kwa dakika 30 kuelekea upande mmoja huku ukichemka.
c) Baada ya hapo epua mseto huo utakuwa tayari imeshakuwa tomato funga vizuri na kisha peleka sokoni.
Mpaka kufikia hapo wewe Tajiri, na mafanikio makubwa ambayo yatakuwa upande wako endapo utakuwa umeamua kuondokana na umaskini kwa njia ya kutengeneza vitu mbalimbali kwa ajili ya kuuza.
Nikusihi uendelee kufuatana nami katika Makala zijazo ili tuweze kufika mahali ambapo tunatamani kufika.? Endelea kufuatana nasi hapa dira ya mafanikio kwa masomo mengine yanayokuja.
1. Nyanya kilo 1.
2. Vitunguu maji viwili.
3. Vinegar vijiko 3 vya chai.
4. Sukari vijiko 2 vya chai.
5. Chumvi kijiko kimoja cha chai
6. Maji ya moto kikombe kimoja cha chai.
7. Mafuta ya kula vijiko 7 ya vyakula.
Haya ndiyo mahitaji ya kutaka kutengeneza tomato souce, hata hivyo kama unataka kutengeneza zaidi ya hapo unatakiwa kuongeza uwiano wa mahitaji hayo.
JINSI YA KUTENGENEZA TOMATO SOURCE.
HATUA YA KWANZA.
a) Menya nyanya na vitunguu kisha vikate vipande vidogo vidogo.
b) Tumia Brenda kusaga mchanganyiko wako.
c) Anza kuweka malighafi namba 1 hadi namba 4 katika brenda yako kutokana na ratio (uwiano ) uliopewa hapo juu. Saga kwa dakika kadhaa hadi uone imetokea rojo laini.
HATUA YA PILI.
a) Tumia sufuria yenye nafasi kupika mseto huu.
b) Weka sufuria yako jikoni tia mafuta ya kula acha yachemke kisha mwagia mseto wako na kisha uanze kukoroga kwa dakika 30 kuelekea upande mmoja huku ukichemka.
c) Baada ya hapo epua mseto huo utakuwa tayari imeshakuwa tomato funga vizuri na kisha peleka sokoni.
Mpaka kufikia hapo wewe Tajiri, na mafanikio makubwa ambayo yatakuwa upande wako endapo utakuwa umeamua kuondokana na umaskini kwa njia ya kutengeneza vitu mbalimbali kwa ajili ya kuuza.
Nikusihi uendelee kufuatana nami katika Makala zijazo ili tuweze kufika mahali ambapo tunatamani kufika.? Endelea kufuatana nasi hapa dira ya mafanikio kwa masomo mengine yanayokuja.
Imeandikwa na Afisa mipango; Benson Chonya.
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)