Mar 31, 2018
Fursa Na Mipango Peke Yake Sio ‘Tiketi’ Ya Kukupa Mafanikio.
Kuna watu wanaofikiria, kwa kuwa wana mipango mizuri na kwa kuwa wana fursa nzuri basi hapo mafanikio ndio tayari. Kama una ndoto za namna hiyo hata wewe, nikwambie unajidanganya na bado haitoshi hiyo, ila unahitaji kitu cha ziada ili kufanikiwa.
Najua
unao uwezo wa kufanya kile unachokitaka, lakini uwezo huo bado hautoshi. Najua unayo
fursa ya kuweza kufanikiwa lakini fursa hiyo bado pia haitoshi. Pia najua unayo
mipango mizuri sana ya kukusaidia
kufanikiwa, lakini mipango hio pia haitoshi.
Ni nini
kinachotosha au nini sasa unachotakiwa kufanya ikiwa unayo mipango, uwezo na
fursa lakini tu haitoshi? Kinachotosha kwako ni wewe kuamua kuchukua hatua. Hata
kama una kila kitu kizuri cha kukufanikisha sana kama huchukui hatua ni sawa na bure.
Hatua
zinatakiwa ili uwezo ulionao ufanye kazi vizuri. Hatua zinatakiwa ili uweze
kutumia fursa zako vizuri na pia hatua zinatakiwa ili uweze kufanya mipango yako
vizuri. Kujidanganya kwako wewe una mipango halafu huchukui hatua ni kazi bure.
Hatua
ndogo ambazo utakazoamua kuchukua ni za maana kwako sana kuliko mipango mikubwa
uliyonayo ambayo huifanyii kazi. Kipi ambacho unasubiri, unatakiwa kuanza
kuchukua hatua sasa za kukupeleka kwenye ndoto zako hata kama ni kidogo sana.
Leo ni
siku ambayo unaweza ukaamua kutumia kila aina ya fursa iliyopo mbele yako kubadili
maisha yako. Leo ni siku ambayo unaweza ukaitumia mipango yako na uwezo wako wote
kukusaidia kufanikiwa.
Chochote
ulichonacho hakina maana, chochote ulichonacho hakiwezi kutosha kama hutaweza
kuchukua hatua. Kitu cha msingi kabisa ni kuchukua hatua za kubadilisha ndoto
zako. Hatua ndizo zitakazokupa kile ukitakacho.
Lakini
kitendo cha kuringa au kujidai eti kwa sababu wewe una mipango mizuri na
ukaishia kwenye mipango hiyo, nakwambia hiyo itakupelekea kwako itakuwa ni
ngumu sana kuweza kuchukua hatua za kimafanikio.
Washindi
katika mafanikio wanajua vizuri mafanikio makubwa yanakuja kwa wewe kuchukua hatua.
Hizo zote zingine zinaweza zikawa ni kelele, lakini kufanikiwa kwako kunatengenzwa
sana na wewe kuweza kuchukua hatua.
Huhitaji
kuendelea kuwa na matamanio ya ndoto zako wakati wote, unachotakiwa kukifanya
sasa ni kubadili matamanio hayo na kuwa ya kweli. Hiyo ukumbuke lakini haiwezi
kutokea mpaka uchukue hatua.
Yajaze
maisha yako hatua na itafika mahali utaona matunda ya kile unachokifanya, hata
kama kitu hicho ni kidogo sana. Hakuna kinachoshindikana kwenye kuchukua hatua.
Mafaniko na mabadiliko katika maisha ni lazima yaonekane.
Hatua
ndio kitu cha kitakachokufanya ufanikiwe. Kuwa na wazo, mipango na fursa hiyo
haitoshi kwamba ndio ‘tiketi’ ya
mafanikio. Unatakiwa kuchukua hatua, unatakiwa kufanya kazi ili uweze
kufanikiwa, lakini sio kusema umefanikiwa na kumbe bado.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mar 30, 2018
Jikumbushe Kila Mara Mambo Haya Ili Yakupe Hamasa Ya Kufanikiwa.
Najua hapo ulipo, kwa chochote kile unachokifanya, lengo lako kubwa ni kuhitaji maisha mazuri na bora. Kuna maisha ambayo najua unayatamani, maisha hayo unataka kuyafikia na pengine una kiu nayo sana.
Hata
hivyo kabla hujafikia mahali ukayatamani sana maisha hayo unayoyataka, hebu
jiulize, kwa jinsi maisha yako unavyoyaendesha na kwa jinsi unavyoendesha
maisha yako kwa kila siku je, jinsi hiyo inakurushu kuyapata maisha hayo?
Ni wajibu
wako kujikagau na kujiangalia wewe mwenyewe hatua kwa hatua kwa jinsi
unavyoishi maisha yako. Kama kuna kitu unaona hakijakaa sawa na unaendelea nacho
ujue kitu hicho kitakunyima kuweza kufanikiwa.
Mwenendo
wa wewe jinsi unavyoishi siku moja tu, unaweza ukatoa picha kamili ya kwamba
unafanikiwa au hufanikiwi bila kujali ni kitu gani ambacho unakifanya. Mara nyingi
nasema kwenye kufanikiwa hakuna uchawi ni kanuni na sheria tu.
Unaweza
ukajiuliza mwenyewe kama kweli unataka mafanikio hasa, je, ni kweli mafanikio
hayo utayapata kwa jinsi unavyopoteza muda hovyo. Jiulize wewe mwenyewe na
usimwambie mtu yeyote, lakini ujipe majibu sahihi pia.
Tena
jiulize, kama unataka mafanikio ni kweli mafanikio hayo utayapa kwa wewe
kuendelea kuwa mzembe na wala huweki juhudi zinazotakiwa? Je, ni rahisi kuyapata
mafanikio hayo ambayo unayataka?
Na tena
jiulize ama kweli unataka mafanikio, je mafanikio hayo utayapa kwa mwendo huo
ambao unao ambao unaishi kiholela na hutaki kujifunza mambo mapya na hata kujichanganya
na watu wengine?
Ongeza
tena swali lingine hapo, kama unataka kweli mafanikio, je, mafanikio hayo
utayapata kweli kwa jinsi unavyotapanya pesa zako huko na huko na kushindwa
hata kujiwekea akiba ambayo itakusaidia?
Hutakiwi
haya maswali ujiulize huku watu wengine wakisikia, unatakiwa kujiuliza wewe na
kuangalia kule unakokwenda na pale ulipo ni nini unachokifanya, hatua zipi
unazozichukua na zinakupeleka kwenya mafanikio au la.
Ili kufafanikiwa
na kufikia mafanikio siku zote unatakiwa sana wewe kuwa makini kwa kila hatua.
Unatakiwa kuwa makini kwa kuangalia mwenendo wako. Watu wengi wanapotea kwenye
safari ya mafanikio kwa sababu si watu makini na wanakuwa wapo wapo tu.
Amua
kuwa ‘siriazi’ kufatuta mafanikio
yako na kuamua kuachana na kila aina ya uzembe ambao umekuwa ukikukwamisha hata
wakati mwingine pasipo wewe kuweza kujua. Tupilia mbali uzembe huo na
jikumbushe misingi ya mafanikio jinsi ilivyo.
Kila
hatua unayoipiga,ujue kabisa ni kitu gani ambacho unakifanya, kuwa makini na
kila hatua, hiyo itakuwa ni njia bora na ya pekee sana kuweza kukusaidia kuweza
kufanikiwa na kufikia mafanikio makubwa uyatakao.
Ukipoteza
umakini kwenye maisha yako na ukasahau kujikumbusha mambo ya kukusaidia
kufanikiwa, basi hicho ni chanzo kikubwa sana cha wewe kuweza kuanza kupotea na
kushindwa kuweza kufanikiwa. Unataka kufanikiwa usipoteze umakini.
Usikubali
kushindwa, usikubali kupoteza maisha yako ya mafanikio eti kwa sababu ya
kuendesha maisha yako kiholela. Kuwa makini na kila kinachokuzunguka katika
kuhakikisha unafikia mafanikio pasipo kizuizi kikubwa sana.
Kila
wakati jenga utaratibu wa kujikumbusha na kuangalia jinsi unavyoishi, je, kwa
mwendo huo unaoishi, utakupa mafanikio au hautakupa mafanikio zaidi ya kuweza
kukuangusha wewe mwenyewe?
Fanyia kazi hiki
ulichojifunza leo kwa kuhakikisha kwamba, unajikumbusha yale maisha unayoishi
au matendo unayoyafanya kama matendo hayo yanakusaidia kukupeleka kwenye
mafanikio uyatakayo au yanakupeleka kwenye kushindwa.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
MUHIMU ZAIDI; kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Mar 29, 2018
KUMBUKUMBU; Kama Kupenda Kwako Ni Hivi, Tayari Umeshapotea.
Msichana mdogo wa miaka 18 aliwahi kuja kwangu na kuniomba msaada. Hakuhitaji msaada mkubwa sana kama mwenyewe alivyosema, kwani alitaka kusaidiwa kupata jibu la swali ambalo lilikuwa likimtatiza kwa muda mrefu.“Nataka kujua maana ya kupenda.” ilikuwa ndiyo kauli yake, fupi na inayoeleweka. Sikujibu swali lake moja kwa moja bali nilimwambia, ”umesema unahitaji msaada mdogo, lakini unayemwomba hana uwezo wa kukusaidia.” Nilizidi kumwambia kwamba, hata mimi nimekuwa kwa muda mrefu nikitafuta jibu la swali hilohilo.
Hivyo, sikuweza kumsaidia na niliona jambo lile lilinipa
changamoto nami kuanza kusaka jibu la swali lile. Lakini, bahati nzuri ni
kwamba, kabla yule msichana hajaondoka kwangu nilimuuliza nami swali moja. “Ni
kwa nini unataka kujua maana ya kupenda”?
Alinijibu bila kufikiri mara mbili kwamba, ni
kwa sababu gani anataka kujua kama mpenzi wake anampenda. Pengine jibu lake
lilinizindua na nilihisi kama vile ndani ya jibu hilo kungeweza kupatikana pia
jibu la lile swali lake. ”Ukishajua kama anakupenda ndiyo itakuwa nini baada ya
hapo?” Nilimuuliza, pengine nikiwa sitegemei jibu.
Alikuwa ni msichana ambaye
majibu yake yameandaliwa tayari kutolewa. ”si ndiyo nijue hanidanganyi, sasa
nitampenda vipi kama yeye hanipendi!” alipomaliza kunijibu, nami nikawa
nimepata jibu la swali lake.
Wengi husubiri kupendwa kwanza, siyo msichana yule tu, bali wengi miongoni mwetu tunasubiri kupendwa au huwa tunataka kwanza kuwa na uhakika kuwa tunapendwa, ndipo nasi tupende.
Wengi husubiri kupendwa kwanza, siyo msichana yule tu, bali wengi miongoni mwetu tunasubiri kupendwa au huwa tunataka kwanza kuwa na uhakika kuwa tunapendwa, ndipo nasi tupende.
Penda kwanza, kabla hujapendwa. |
Ukimfuata mtu na kumwambia
kuwa unampenda, ungependa awe mpenzi wako au mwezi wa baadaye maishani na mtu
huyu akawa mkweli na kukuambia kwamba, yeye hakupendi, utaumia sana. Utaanza
hapohapo kumchukia au hata kumfanyia visa.
Unakuwa katika hali hiyo kwa sababu kuu mbili. Kwanza, ni kwa
sababu hujui kwamba, kinyume cha kupenda siyo kuchukia. Unapomtaka mtu uhusiano
na akasema hapana, unamchukulia kuwa anakuchukia kwa sababu, kwako kama hakuna
kupenda, basi ni lazima kuwe na kuchukia.
Tumelelewa na kukulia katika
mazingira ambayo yametufundisha kukitazama kila kitu katika uwili. Kwa hiyo,
`sikupendi`masikioni mwetu inasikika kama, `nakuchukia`. Pili, ambavyo
ni kubwa, ni kwa sababu kila binadamu anahitaji kupendwa. Wataalamu wengi wa
saikolojia wanabainisha kupendwa kama moja ya mahitaji muhimu kwenye ngazi ya
mahitaji ya binadamu.
Tangu tukiwa na umri wa siku moja, tunataka kukubaliwa
kupokelewa na kulindwa. Haya ya kupendwa ni kama jambo la kimaumbile kwa
binadamu. Unapogundua kuwa watu wote hawakupendi ni lazima utababaika,
utachanganyikiwa na kwako maisha yanaweza kupoteza maana.
Wengi tunafanya tuyofanya au
kuacha kufanya katika kutafuta kupendwa. Kwa hiyo, kila mmoja wetu ana kiu
kubwa ya kupendwa. Hapa ndipo linapochipuka tatizo kubwa linalofanya wengi
kushindwa kujibu swali la , `kupenda ni nini?`
Hushindwa kwa sababu, hakuna
anayejali kupenda, karibu wote tunajali kupendwa, tuna kiu ya kupendwa, siyo
kupenda. Kama nguvu zetu zote tumeziweka kwenye kupendwa, kupenda kunakuwa na
nafasi gani kwetu? Ndiyo maana wengi hatuju kupenda ni nini?
Ni kitu gani kinatokea? Ni
kwamba, badala ya kuwekeza kwenye kupenda, tunawekeza kwenye kupendwa ambako
hakutuhusu. Ni sawa na mtu kuchukua fedha zake na kuziingiza kwenye akaunti ya
mwingine akiamini kwamba anaziingiza kwanye akaunti yake. Siku anapokuja kutaka
kutoa fedha na kukuta hazipo atazusha zogo kubwa na balaa lisilowezekana.
Atadai kwamba benki hazifai na hazina ukweli.
Unaposubiri au kutarajia na mbaya zaidi kudai kupendwa, unapoteza muda wako bure, kwa sababu hilo ni jambo lisilokuhusu. Ni jambo ambalo huwezi kulipanga wala kulidhibiti kwa sababu linamhusu mtu wa upande wa pili. Inawezeakana vipi wewe umalazimishe mtu akupende? Haiwezekani, lakini tunafanya. Tunafanya lisilowezekana.
Unaposubiri au kutarajia na mbaya zaidi kudai kupendwa, unapoteza muda wako bure, kwa sababu hilo ni jambo lisilokuhusu. Ni jambo ambalo huwezi kulipanga wala kulidhibiti kwa sababu linamhusu mtu wa upande wa pili. Inawezeakana vipi wewe umalazimishe mtu akupende? Haiwezekani, lakini tunafanya. Tunafanya lisilowezekana.
Lakini unaweza kupenda,
kwani ni jambo linalotoka kwako , lililo ndani ya uwezo wako. Kwa hiyo,
unapokutana na mtu, kama amekuvutia, wewe ndiye unayetakiwa kumpa upendo, bila
kujali kama naye anakufanyia hivyo. Huna haja ya kujali kama naye anakufanyia
hivyo kwa sababu, wewe umeamua kumpenda, lakini huna haki na huwezi kumfanya
akupende kama yeye hataki.
Bila shaka huwa unakutana na vituko vya karne kila siku kuhusu jambo hili. Mtu anaambiwa na mwingine kwamba hampendi. Inawezekana kuwa ni wapenzi wa muda mrefu-mke na mume au hata wa muda mfupi.
Bila shaka huwa unakutana na vituko vya karne kila siku kuhusu jambo hili. Mtu anaambiwa na mwingine kwamba hampendi. Inawezekana kuwa ni wapenzi wa muda mrefu-mke na mume au hata wa muda mfupi.
Badala ya huyu anayeambiwa
hapendwi kukubali jambo hilo kwa sababu hawezi kulibadili, huanza kupinga.
Wengine huenda hata mahakamani au kuwauwa wapenzi waliowakataa, ni kweli hii?
Vituko hivi viko hata katika
mazingira ambapo hakuna ugomvi au kutoelewana. Inawezekana ni katika mazingira
ya kawaida kabisa, ambapo mpenzi anamuuliza mwenzake , ”hivi, unanipenda kweli,
hebu nithibitishie”.
Shabashi! Ni kitu gani hiki!
Tangu lini kupendwa limekuwa ni jukumu lako? Jukumu lako ni kupenda, basi. Hili
jukumu la kupendwa muachie mwingine. Kupenda ni hisia na ndiyo maana imekuwa
vigumu sana kwa watu kumudu kusema mapenzi ni nini.
Jambo loloto la kuhisi ni
gumu kuelezewa kwa maneno. Kupenda kunapoelezeka kwamba ni kitu fulani, ni
lazima kuna mushkeli. Watu wengi ambao huwa ninazungumza nao katika
kushauriana au kufundishana kuhusu kupenda, huwa ninawauliza swali hili
”Umempendae kitu gani mwenzako?” Wengi huwa wanatoa maelezo kama vile,
”nimempendea upole wake” au ”nimempenddea ukarimu wake” ama ”nimempendea tabia zake”.
Lakini hakuna kabisa ambao wamewahi kusema wamempenda mwingine kwa sababu ya sura au maumbile yao au kwa sababu ya utajiri ama umaarufu wao . Kwa nini?
Ni kwa sababu, ndani ya nafsi zetu tunajua kwamba kupenda sifa za nje ni jambo linalopingwa na kila mtu na ni aibu kulitamka, labda tu miongoni mwa watu waliozoeana sana na kuaminiana.
Lakini hakuna kabisa ambao wamewahi kusema wamempenda mwingine kwa sababu ya sura au maumbile yao au kwa sababu ya utajiri ama umaarufu wao . Kwa nini?
Ni kwa sababu, ndani ya nafsi zetu tunajua kwamba kupenda sifa za nje ni jambo linalopingwa na kila mtu na ni aibu kulitamka, labda tu miongoni mwa watu waliozoeana sana na kuaminiana.
Hata hivyo, miongoni mwa
wapenzi, jambo hilo huwa linasemwa sana bila wenyewe kungámua. ”Unaniacha hoi
kwa macho yako,” ni kauli za kawaida kwa wapenzi. Kusikia mpenzi akimwambia
mwingine ”nimekupenda kwa kweli, guu unalo,” ni jambo la kawaida.
Mwanamke na kuita hali hiyo
kuwa ni kupenda. Hutamani sana sura, miguu, matiti, makalio, macho na hata
midomo na pua. Hili ni jambo la kimaumbile zaidi. Ndiyo maana wanawake wanajipamba
na kujikwatua. Hufanya hivyo ili kuwavuta wanaume, kwani wanaume hujali
muonekano wa nje zaidi.
Kuna wakati hapa nchini suala la wanawake kubabua ngozi au kupaka dawa nywele zao lilikuwa ni suala la mjadala mkubwa. Baadhi ya wanawake ambao walitakiwa kutoa maoni yao kuhusu jambo hili walisema, wao hawapendi sana kufanya hivyo, bali wanaume ndiyo wanaowalazimisha kufanya hivyo.
Kuna wakati hapa nchini suala la wanawake kubabua ngozi au kupaka dawa nywele zao lilikuwa ni suala la mjadala mkubwa. Baadhi ya wanawake ambao walitakiwa kutoa maoni yao kuhusu jambo hili walisema, wao hawapendi sana kufanya hivyo, bali wanaume ndiyo wanaowalazimisha kufanya hivyo.
”Mwanaume anaweza kukuacha
kwa sababu tu kaona mwingine mwenye ngozi nyeupe na nyororo au nywele laini
zilizoangukia mabegani. Inabidi ujitahidi kumlinda.” walisema baadhi ya
wanawake. Pamoja na kuwa ni kauli zenye kuonyesha unyonge, lakini zina ukweli.
Wanaume hukimbilia sifa za nje zaidi.
Wanawake kwa upande wao, huvutwa zaidi na wanaume ambao wanaweza kuwalinda au kuwapa uhakika fulani wa kimaisha. Hata hivyo, unapowauliza kwa nini wamempenda fulani, nao hawawezi kusema ni kwa sababu ana fedha au kwa sababu ana jina, hapana. Ni aibu kukiri hivyo au pia kwa sehemu kubwa huwa hawajui kwamba wamevutwa na sifa hizo.
Wanawake kwa upande wao, huvutwa zaidi na wanaume ambao wanaweza kuwalinda au kuwapa uhakika fulani wa kimaisha. Hata hivyo, unapowauliza kwa nini wamempenda fulani, nao hawawezi kusema ni kwa sababu ana fedha au kwa sababu ana jina, hapana. Ni aibu kukiri hivyo au pia kwa sehemu kubwa huwa hawajui kwamba wamevutwa na sifa hizo.
Ni wachache sana ambao
hutokea wakajibu kwamba wamempenda mwingine kwa kumpenda tu, bila kutoa
maelezo. Kwa nini ni wachache? Ni kwa sababu, wanaopenda siyo wengi. Mtu
anayesema nimempenda fulani bila kujua ni kwa nini hasa, huyu ndiye ambaye
amependa. Huku ndiko tunakoita kupenda tunapopenda, kwa kawaida kuwa hatujui
sababu za kumpenda huyo fulani, bali tunampenda tu. Mtu anapotoa sababu ya
kumpenda mwingine, huyo hajapenda bado. Huu ndiyo ukweli!
Kwa bahati mbaya, kuna wengine wamependa na hawajui ni kwa nini wamependa. Lakini unapowauliza, wanaanza kujaribu kutafuta sababu za huko kupenda kwako. Kwa hiyo, mtu ataanza kusema, `nampendea upole`au `nampendea huruma zake` ama `nampenda kwa sabu ametulia.” Anasema haya kwa sababu anaamini kwamba, kupenda ni lazima kutolewe sababu, wakati kinyume chake ndiyo ukweli.
Unapovutwa na mtu na ukajikuta huna sababu unazoweza kuzitoa za kwa nini umevutwa naye, kuna uwezekano mkubwa kwamba uko kwenye upendo wa kweli na mtu huyo. Lakini pale ambapo unaziona sababu waziwazi za kumpenda kwako, hapo hakuna upendo wa kweli.
Kwa bahati mbaya, kuna wengine wamependa na hawajui ni kwa nini wamependa. Lakini unapowauliza, wanaanza kujaribu kutafuta sababu za huko kupenda kwako. Kwa hiyo, mtu ataanza kusema, `nampendea upole`au `nampendea huruma zake` ama `nampenda kwa sabu ametulia.” Anasema haya kwa sababu anaamini kwamba, kupenda ni lazima kutolewe sababu, wakati kinyume chake ndiyo ukweli.
Unapovutwa na mtu na ukajikuta huna sababu unazoweza kuzitoa za kwa nini umevutwa naye, kuna uwezekano mkubwa kwamba uko kwenye upendo wa kweli na mtu huyo. Lakini pale ambapo unaziona sababu waziwazi za kumpenda kwako, hapo hakuna upendo wa kweli.
Kumbuka kuwa sababu zote
unazoziona ni za muda, zinaweza kuondoka. Zinapoondoka, ina maana pia kwamba,
upendo haupo. Kama ulimpenda kwa sababu ya tabia ya upole na ukarimu, anapokuja
kubadilika na kuiacha tabia hiyo, itakuwa na maana pia kwamba, mapenzi
hayatakuwepo kwani ulichokipenda kitakuwa hakipo.
Lakini ukiona mwingine mwenye upole na ukarimu kuliko huyo, utampenda zaidi pia. Je, utaacha kumpenda yule wa kwanza au utawapanga kwa madaraja kiupendo?
Kama ulimpendea sura, mguu au jicho, ni wazi upendo wenu utakuwa ni wa muda kwani kwa kadiri siku zinavyopita, vitu hivyo havyo hupoteza nuru na mvuto. Mazoea nayo huingiza ukinaifu wa hisia. Lakini kuna wengine ambao wana miguu na macho mazuri zaidi ya hayo ya huyo. Hii ina maana kwamba, utahama kutoka mtu mmoja hadi mwingine ukifuata uzuri.
Kumpenda mtu bila kujua ni kwa nini umempenda, kuna maana ya kumkubali mtu huyo kama alivyo, kumpokea bila masharti. Kuna maelezo na nadharia nyingi zenye kuonyesha ni kwa nini siyo kila mtu anaweza kumpenda mwingine kwa njia hii.
Lakini bila shaka, nadharia na maelezo hayo hayana nafasi kubwa sana kwetu katika kujadili jambo hili. Chenye nafasi, ni kujua namna mtu anavyoweza kupima aina ya mapenzi aliyomo.
Lakini ukiona mwingine mwenye upole na ukarimu kuliko huyo, utampenda zaidi pia. Je, utaacha kumpenda yule wa kwanza au utawapanga kwa madaraja kiupendo?
Kama ulimpendea sura, mguu au jicho, ni wazi upendo wenu utakuwa ni wa muda kwani kwa kadiri siku zinavyopita, vitu hivyo havyo hupoteza nuru na mvuto. Mazoea nayo huingiza ukinaifu wa hisia. Lakini kuna wengine ambao wana miguu na macho mazuri zaidi ya hayo ya huyo. Hii ina maana kwamba, utahama kutoka mtu mmoja hadi mwingine ukifuata uzuri.
Kumpenda mtu bila kujua ni kwa nini umempenda, kuna maana ya kumkubali mtu huyo kama alivyo, kumpokea bila masharti. Kuna maelezo na nadharia nyingi zenye kuonyesha ni kwa nini siyo kila mtu anaweza kumpenda mwingine kwa njia hii.
Lakini bila shaka, nadharia na maelezo hayo hayana nafasi kubwa sana kwetu katika kujadili jambo hili. Chenye nafasi, ni kujua namna mtu anavyoweza kupima aina ya mapenzi aliyomo.
MAKALA HII ILIANDIKWA NA MWALIMU WANGU KIPENZI WA MAFANIKIO, HAYATI
MUNGA TEHENAN, ZAIDI YA MIAKA 18 ILIYOPITA. LAKINI LEO HII UMEJIFUNZA KITU
KIPYA, HII NDIO NGUVU ILIYOPO KATIKA MAANDISHI YANAYOISHI.
Mar 28, 2018
Usipoliangalia Jambo Hili Kwa Umakini Litakufanya Ushindwe Kufanikiwa.
Kati
ya kitu kimojawapo ambacho kitakupelekea wewe kuanguka kwenye maisha yako kama
usipokiangalia vizuri na kukijua jinsi ya kukabiliana nacho, ni kukatishwa tamaa. Usipokuwa
makini na kukatishwa tamaa kwa namna yoyote ile lazima ukwame.
Maisha
ya watu wengi yameishia kati na yamekuwa maisha ya ndoto na yale matumaini
makubwa waliyokuwa nao watu hao mwanzoni yamepotea kabisa, yote hiyo ni kwa
sababu ya kukatishwa tamaa iwe na wengine au wao wenyewe.
Inapifika
mahali kwenye maisha yako ukaona kabisa kwamba wewe ndio umekata tamaa, naomba
nikwambie kwamba wewe ndio basi tena kufanikiwa. Hutaweza kufanikiwa mpaka
urudi kwenye matumaini ya kuamini kwamba utafanikiwa tena.
Kukatishwa
tamaa kwa namna yoyote ile kunakupotezea sana nguvu zako ambazo ulikuwa
umejiandaa nazo kwa ajili ya kuchukua hatua. Kwa bahati mbaya kukatishwa tamaa
kwenyewe kunaweza kukawa kwa maneno tu, ambayo umeyasikia na hayana ukweli.
Ndipo
hapo ambapo unatakiwa ujiulize ni kwa jinsi gani maneno hayo yana nguvu au yana
ukweli na ule uhalisia. Kama una nia kweli ya kufanikiwa unayo, inatakiwa uzibe
masikio kabisa na usisikie kukatishwa tamaa kwa namna yoyote kukitokea kwako au
kwa wengine.
Ili uwe
mshindi wa mafanikio hutakiwi kuwa mtu wa kukata tamaa. Unatakiwa uwe mtu ambaye
una roho ngumu, lakini si roho ya kuwakomoa watu, bali ile roho ya kuamua
kutokatishwa tamaa na kitu chochote kile zaidi ya kutaka kuona ukifanikiwa.
Unapaswa
kuelewa, juhudi yoyote kwenye maisha yako iwe juhudi ya masomo, juhudi ya
kutaka kufikia mradi fulani au juhudi ya aina yoyote ambayo lengo lake ni
kukufanikisha, juhudi hiyo ni lazima huwa inakutana na kukatishwa na tamaa.
Utakuta
juhudi zako zinakatishwa tamaa na mazingira na kufika mahali unaona duu hakuna
kinachofanikiwa tena hapa. Pia wakati mwingine utakuta juhudi zako zinakatishwa
tamaa na wewe mwenyewe kutokana na mawazo yako au wale wote wanaokuzunguka.
Kitu
cha namna hii kinapokutokea si bahati mbaya, bali naweza nikasema kwamba unatakiwa
ujue juhudi yoyote ile kwa namna moja au nyingine upo muda wake utafika inakuwa
inatishwa tamaa na vitu vingi sana na kama usipokuwa makini utakwama.
Hata
hivyo unachotakiwa kuelewa hapa, huwezi kukwepa kwenye maisha yako kukatishwa
tamaa kwa namna yoyote ile. Kitu pekee ambacho unaweza kukifanya hasa pale
unapokatishwa tamaa je, unachukuliaje kukatishwa tamaa huko?
Fanya
kukatishwa tamaa kwako iwe sababu ya kujitoa zaidi mpaka kuona ndoto zako
zinatimia. Usikubali kuachia ndoto zako kirahisi eti kwa sababu umekatishwa tamaa.
Tumia kukatishwa tamaa kokote kule kunakokutokea kwako kwa faida.
Ukiwa
mwangalifu na ukajua jinsi ya kukabiliana na kukatishwa na tamaa, utaweza
kuzifikia ndoto zako, lakini usipojua vizuri jinsi ya kukabiliana na kukatishwa
tamaa, jambo hili litakusumbua sana na utashindwa kwenye maisha yako.
Je,
kukatishwa tamaa kwako unakuchukuliaje kwenye maisha yako, ni chanzo cha
kufanikiwa au kushindwa kabisa? Usisite kutoa maoni yako.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
MUHIMU ZAIDI, kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Mar 27, 2018
Njia Sahihi Za Kubana Matumizi Yako Ya Pesa Kwa Faida.
Katika safari ya kufikia uhuru wa kifedha, zipo njia ambazo unaweza ukatumia na zikakusadia sana katika kutunza pesa zako na pesa hizo zikakusaidia pia katika uwekezaji. Wengi wanapoteza sana pesa zao pasipo ya sababu za msingi.
Ni muhimu
sana kama unataka kufika mbali kiuchumi ukabana matumizi yako ili pesa zako
zikusaidie kuwekeza. Ni njia zipi ambazo unaweza kutumia katika kubana matumizi
yako na ikakusaidia sana?
Zifuatazo Ni Njia Sahihi Za Kubana
Matumizi Yako Ya Pesa.
1. Tengeneza
bajeti katika matumizi yako na uifatilie. Bajeti hiyo utakayoitengeneza ndiyo
iwe mwongozo wako, usitumie pesa nje ya bajeti hiyo.
2. Tambua
matumizi yako ya lazima na muhimu ni yapi. Yapo matumizi ambayo ni ya lazima
sana, na yapo ambayo si lazima unatakiwa kuyajua.
3. Matumizi
yako yasizidi kipato chako. Hakikisha unafanya kila linalowezekana matumizi
yako yasiwe makubwa kuliko kipato chako.
4.
Fanya matumizi yako, baada ya kuweka akiba. Kila wakati jizoeze kuweka akiba na
kisha ndio uanze kufana matumizi yako.
5.
Usifanye vitu kwa lengo la kutafuta sifa, kama kununua vitu vya gharama, fanya
vitu kulingana na uwezo wako.
6. Fahamu
faida na sababu za kila jambo ambalo unalolifanya. Usifanye jambo lolote kwa
hasara. Kila jambo unalolifanya lifanye ukijua faida zake hasa ni zipi.
7.
Ishi karibu na eneo lako la kazi au biashara. Kuishi mbali na eneo lako la kazi
nako huko ni kupoteza pesa zako ambazo hazikutakiwa kupotea.
8.
Badala ya kwenda kula hotelini nunua vitu upike nyumbani. Tafuta muda na kisha
pika mwenyewe, vinginevyo utakuwa unapoteza muda wako bure.
9.
Usiazime vitu hovyo vya watu , jitahidi ununue vyako. Kuna wakati vitu vya
kuazima vinaweza vikawa ni chanzo cha wewe kutozwa pesa kama vikipotea.
10.
Sio lazima kila mtu anayeomba msaada ni lazima apatiwe. Kujifanya wewe kila
anayeomba msaada unampatia basi utakuwa unapoteza sana pesa zako pia
11.
Nunua mahitaji yako kwa jumla badala ya rejareja. Kununua mahitaji yako kwa
jumla inakusaidia sana kuokoa pesa zako ambazo kama ungenunua kwa reja reja.
12.
Nunua mahali ambapo unaweza ukapunguziwa bei. Usiamue tu kununua vitu kila
sehemu, nunua eneo ambalo unaweza ukapata punguzo.
13.
Katika nyumba unayoishi hakikisha unazima taa, feni, redio au Tv, usiviache
vikiwa wazi kama havitumiki. Kila wakti angalia vitu hivyo kama havina matumizi
zima.
14. Mvua
ikinyesha kinga maji ili uokoe gharama zisizo za lazima za maji. Hakuna haja ya
kununua maji, kama maji ya bure yapo.
15.
Pika chakula kwa idadi ya watu na usitupe chakula kinachobakia huo utakuwa ni
uharibifu. Ukipika chakula kwa mahesabu hakitaharibika.
MAKALA HII IMEANDIKWA NA SHARIFF KISUDA
WA DAR ES SALAAM, TANZANIA.
Mar 26, 2018
Ukimudu Kufanya Jambo Hili Kwa Uhakika Na Mengine Mengi Utayaweza.
Unapopata kitu kizuri iwe ni mafanikio au kitu chochote kile, kitu hicho ni rahisi kuweza kukusaidia kuendelea kupata mambo mengine mazuri zaidi kwenye maisha yako. Hiyo ikiwa na maana mambo mazuri yanaweza kukuongoza kupata mambo mengine mazuri pia.
Kuboresha
eneo moja la maisha yako kwa uhakika inakusaidia sana kuweza kuboresha maeneo
mengine. Kama hujui ni wapi unatakiwa kuanzia, anzia hapo ulipo na kwa chochote
kile unachokifanya kwenye maisha.
Anza
leo kuwekeza kidogo, ukifanikiwa kuwekeza kwa hicho kidogo itakusaidia sana
kuweza kuwekeza kwa makubwa. Ni muhimu kujua kufanikiwa kwa jambo moja ni
rahisi kufanikiwa kwa mengine pia.
Ndio
maana kila wakati unatakiwa ujue namna ya kuweza kuthubu. Kama wewe ni mtu wa
kuthubu maanake unataka kufanikiwa na kufanikiwa kwako huko ndiko ambako
kunakokupelekea ufanikiwe kwa mambo mengi zaidi.
Huwezi
kupiga hatua kubwa au kama kila kitu hufanikishi. Unatakiwa kufanikisha mpango
wako hatakama ni kidogo sana, kwani kwa kufanikiwa huko hiyo inakuongoza kuweza
kufikia mafanikio makubwa.
Ninachotaka
kusema hapa ni kwamba, ushindi mdogo ni hatua
nzuri sana kwako ya kukusaidia kuweza kupata ushindi mkubwa. Kwa jinsi
unavyopata mshindi mdogo unakusaidia kukupa kujiamini na kusababisha kutenda
makubwa zaidi ya hayo.
Unatakiwa
sasa kuzingatia kwa chochote kile ukifanyacho unatakiwa ukifanye kwa ushindi.
Kwa jinsi unavyopata ushindi mwingi mdogo mdogo na ushindi huo unakusaidia
kukupa mafanikio makubwa uyatakayo maishani mwako.
Ikiwa
unataka kuwa miongoni mwa watu wenye mafanikio duniani, chukua hatua ya kufanya
hata kama kitu kidogo ila iwe kwa ushindi. Kama nilivyosema kwa ushindi huo
mdogo utakuwezesha kushinda na kupata ushindi mkubwa pia.
Ndio
maana nakwambia ukimudu kuweza kupata ushindi mdogo kila wakati, sina wasi wasi
na ushindi mkubwa utakuwa ni rahisi kuupata hivyo hivyo kwako. Anza kushinda
vitu vidogo vidogo kwanza kwenye maisha yako ili vikusaidie kushinda makubwa.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia
kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku
kujifunza maisha na mafanikio.
MUHIMU ZAIDI, kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Mar 25, 2018
Usipoteze Muda Na Nguvu Zako Kwa Kitu Hiki Kidogo.
Ni upotevu wa muda na nguvu nyingi sana kama kila wakati unaamua kuweka nguvu zako katika kulaumu watu wengine kwa kile ambacho kinatokea. Kama wewe ni mtu wa lawama, elewa kabisa unapoteza muda na nguvu zako bure.
Kwa jinsi
ilivyo unavyokuwa unalaumu, maanake unashugulika na tukio ambalo kiuhalisia
limeshapita. Kwa hiyo hapo unakuwa ni sawa na mtu ambaye unaelekeza nguvu zake
nje ya kitu ambacho hakisaidii sana.
Kitu
cha msingi kwako na ambacho kitakusaidia si wewe kundelea kuchukua lawama, kama
ni makosa ni tayari yameshatokea, unachotakiwa wewe ni kuweza kuchukua hatua za kusonga mbele na si lawama zako ambazo
hazina msingi.
Tafuta
namna gani utakavyo weza kundelea mbele na si kutafuta ni kwa namna gani
kulaumu udhaifu wa watu wengine kwa muda mrefu. Maisha ya mafanikio yanakuja
kwa kuwajibika na si kwa kulalamika au
kuishi kwa lawama.
Waangalie
kidogo watu ambao kila siku na kila wakati ni watu wa kuishi kwa lawama, mara
nyingi watu hao hata pia kwenye maisha yao, hawapigi hatua sana. Hiyo ikiwa na
maana kwamba lawama si nzuri katika kutafuta mafanikio.
Weka
nguvu zako katika kuweka juhudi za kutafuta mafanikio na si kuweka juhudi zako
katika kuwalaumu watu wengine kwamba hao ndio wameharibu maisha yako au mipango
yako mizuri ambayo ulikuwa umejiwekea.
Kitu
cha kufanya kwako wewe ni kuendelea kuweka nguvu zako za uzingativu kwa kitu kipi
kwamba ukirekebishe na kikusaidie kuweza kusonga mbele zaidi hapa kama ni kazi
ni lazima ujue namna ya kufanya kazi yako kwa upya kabisa.
Usikubali
kuchukua hatua kwa kutumia mdomo wako, usikubali kuchukua hatua kupitia maneno yako,
amua kuwajibika juu ya maisha yako kwa kuchukua hatua za kubadili maisha yako
na si kwa kulaumu ambako unakufanya.
Nikiwambie
tu ukweli huu, hutaweza kufika popote kwenye maisha yako ya mafanikio kama kila
siku utaendelea kulaumu wengine juu ya udhaifu wao na wewe kusahau udhaifu wako
ulionao, hilo unatakiwa kulielewa.
Kitu
cha kuelewa hapa ni kwamba, usipoteze muda na nguvu zako sana katika kulaumu,
badala yake wekeza nguvu zako hizo katika swala zima la kuwajibika na hapo
utakuwa na nafasi ya kujenga mafanikio yako sana.
Fanyia kazi haya na chukua
hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
MUHIMU ZAIDI, kama
unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana,
ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Mar 24, 2018
Kitu Ambacho Hutakiwi Kukisahau Wakati Unayatafuta Mafanikio.
Mafanikio yanawatenga watu wengi sana, kulingana na watu hao jinsi wanavyoyachukulia mafanikio yenyewe. Ukiangalia wengi wanayachukulia sana mafanikio kama pesa au umaarufu kwamba hayo ndiyo mafanikio halisi.
Ikiwa utakuwa
unayaangalia mafanikio tu kwa jicho la kuangalia vitu vya nje, basi utakuwa
unapishana sana na mafanikio yako. Hutakiwi kutazama mafanikio kwa jicho moja,
unatakiwa kuyatazama mafanikio bila kusahau kitu kimoja muhimu sana ambacho
nakwenda kukueleza.
Kitu ambacho
hutakiwi kukisahau wakati unayatafuta mafanikio au wakati unayatafsiri
mafanikio kwa jinsi unavyojua wewe ni kwamba mafanikio yanaletwa na thamani.
Hata uwe unatafuta mafanikio ya aina gani kwanza lazima uanze na kutoa thamani.
Kama unajua
mafanikio yanaletwa na thamani, basi kazana kutoa thamani sana. Na kila
unapotoa thamani, hata kwa nje kama sisi hatuoni mabadiliko makubwa lakini hayo
ndiyo mafanikio yenyewe na mafanikio ya nje itafika wakati yataonekana tu.
Unachotakiwa
kujiuliza kila wakati ni kwamba kitu gani ambacho unatakiwa kukikamilisha na
hujakikamilisha? Ukishakiona kitu hicho toa thamani zaidi ili kikupe mafanikio.
Kila wakati kazana kutoa thamani na utaishi maisha sawa na tajiri
yeyote yule duniani.
Huhitaji
pesa, huhitaji umaarufu au nguvu yoyote kubwa ili uweze kufanikiwa,
unachohitaji wewe ni kuweka thamani. Ukikazana na kuweka thamani na ukaipa
dunia kile inachotaka, itafika mahali utalipwa tu na hakuna
kitakachoshindikana kwako.
Kwa hiyo badala ya
kuanza kufikiria pesa utakazopata kwanza, badala ya kuanza kufikiria utajiri
kwanza utakaoupata, anza kujizoesha kufikiria kwanza ni thamani ipi ambayo wewe
utaitengenza na itakupa mafanikio.
Nasema hivyo kwa sababu
pasipo kutoa thamani, hata hayo mafanikio uyatake vipi hutaweza kuyapata kwenye
maisha yako zaidi utaishia kuyasikia kwenye redio au kwenye maisha ya wengine,
lakini sio kwako.
Dunia kwa jinsi ilivyo
inataka vitu vizuri, inataka kuona madiliko, dunia inatake kuonja radha
tofauti, sasa hivyo vyote vinapatikana kwa kutoa kitu cha thamani. Huhitaji kusubiri
kutoa thamani, anza kuweka juhudi wa kile unachokifanya sasa.
Katika mafanikio hakuna
hali ya ukawaida. Unapoona una ukawaida wowote ule ujue hakuna thamani inayozalishwa
hapo na mwisho wa siku utaishia kwenye kushindwa vibaya na hata usilaumu mtu
yeyote yule.
Kila siku ni nafasi kwako
wewe ya kuweza kutengeza thamani kubwa juu ya maisha yako. Usipoteze na wala
usiendelee kusubiri thamani hiyo ikapotea. Weka juhudi za kuhakikisha unabadili
maisha yako na ila kitu kitakaa sawa.
Fanyia
kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na
endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
Pia
rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio
zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma
neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S
kwenda 0713 048 035, hapo utapata
utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO
YAIMARIKE,
Ni
wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na
mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713
048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Mar 23, 2018
Usijidanganye, Hutaweza Kufanikiwa Kama Utakuwa Una Malengo Haya.
Ikiwa leo utakwenda kwa daktari na kumwambia kwamba unaumwa na kisha ukaamua kuisha hapo bila kuendelea kueleza zaidi ya unaumwa nini, daktari kwa kawaida hata weza kukupa dawa zaidi itabidi akuulize nini shida yako zaidi.
Daktari huyu atafanya hivi kutaka kujua
ugonjwa unaoumwa ni upi , na ugonjwa huo umeanza lini. Taarifa hizi ni muhimu
sana kwa daktari kwa sababu, taarifa hizo ndizo zitakazoweza kumwongoza yeye
ili aweze kukupa tiba sahihi.
Pia hata leo hii kama umeamua kusafiri kwa kutumia
basi la abiria na ukaenda kwa wakatisha tiketi ukamwambia nataka kusafiri, ujue
kabisa wauza tiketi za safari hawawezi kukupa tiketi au kukuuzia mpaka uulizwe
unataka kusafiri kwenda wapi.
Pia muuza tiketi taarifa hizi za wewe unaenda
wapi zinakuwa ni muhimu sana kwake ili aweze kukupa gari sahihi ambayo
inaenda kule unakotaka, kinyume cha hapo asipofanya hivyo atakupoteza na usifike
kule unakotaka kwenda kwenye safari yako.
Na katika maisha ya mafanikio mambo yako hivyo hivyo. Kama unataka
kufanikiwa kuwa na mawazo mazuri peke yake hiyo haitoshi na kusema kwamba hapo
ndio lazima utafanikiwa kwa sababu una mawazo mazuri.
Pia hata kule tu kusema kwamba nataka
kufanikiwa haitoshi, unatakiwa uwe na mawazo ya kujua unataka kufika wapi yaani
uwe na wazo maalumu ya kuelewa kwa ufasaha ni kitu kipi unachokitaka kwenye
maisha yako.
Unatakiwa ujue unataka kufanikiwa katika eneo
lipi, nini ambacho utakwenda kufanya kila siku ili kiweze kukusaidia kufanikiwa
katika hicho ambacho unataka kufanikiwa nacho. Kwa hiyo hapa unaona ni lazima
uwe na mawazo maalumu na yenye mwelekeo maalumu.
Kama tulivyoona hata kama unaumwa vipi,
huwezi kupona kwa kusema kwamba naumwa nahitaji dawa, hutapona kwa sababu
daktari hata jua unaumwa nini na ni dawa gani, kwa hiyo ni lazima ueleze
unaumwa nini, na mafanikio yako hivyo.
Muujiza wa mafanikio yako utaanza
kuonekana wakati ambapo utakuwa unajua ni nini unachokitaka, mwelekeo wako ni upi
na unataka kufanikiwa kwa kufanya kitu kipi yaani utafanikiwa kwa wewe kuwa ‘specific’ kwa kile ukifanyacho.
Usijidanganye, hutaweza kufanikiwa kama
utakuwa una malengo ya jumla ya kusema nataka kufanikiwa. Utafanikiwa kwa kuwa
na malengo maalumu ya kujua vizuri kile ambacho unataka kikufanikishe ni kitu
kipi hasa.
Acha kuchelewa, anza leo kuwa na malengo
maalumu, usiwe na malengo ya jumla ya kusema nataka kufanikiwa. Ifike mahali
ujue ni nini unachokitaka ili ufanikiwe na hayo mafanikio yako kwa makadirio
utayataka baada ya muda upi.
Ila kitendo cha kuwa tu na mawazo ya jumla ya
kimafanikio huko ni sawa na kuamua
kujidanganya, lakini ukweli wa wazi ni kwamba hata ufanyaje hutaweza
kufanikiwa kama utakuwa na malengo ya jumla ya kimafanikio.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha
ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea
kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na
mafanikio.
MUHIMU
ZAIDI, kama unapenda kujifunza
zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na
uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS
APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE
UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713
048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO
PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani
Ngwangwalu,
Mshauri
wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano;
+255 767 048 035, +255 713 048 035,
Email; dirayamafanikio@gmail.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)