google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 30, 2020

Hakuna Sababu Ya Wewe Kushindwa Kufanikiwa.

3 comments :

Hakuna sababu, kama umeshindwa kupata hicho unachotakiwa kukipata kwenye maisha yako. Watu wengi wanaposhindwa kupata yale wanayoyataka huwa wanakuja na sababu nyingi sana.

Nimekwambia tambua hakuna sababu, kama umeshindwa kupata ulichokipata, usijisumbue kuja na sababu, we kubali umeshindwa tum Unapokuwa na sababu, unazidi kutengeneza ulemavu wako wa kushindwa.

Ni kipi kinachokuzuia kufanikiwa. Je, ni ukosefu wa elimu au ni ulemavu wa viungo vya aina fulani. Chochote kile hakiwezi kukuzuia wewe kufanikiwa, bali kinaweza kikawa sababu ya wewe kufanikiwa sana.

Ngoja nikwambie,  dunia ina watu wengi sana ambao wamefanikiwa huku wakiwa hawajiwezi au walemavu wa aina fulani. Watu hao lakini wameza kufanikiwa  kwa sababu ya nia zao za kutaka kufanikiwa.

Ukitaka kuja na sababu kwa nini hufanikiwi, sababu zipo nyingi sana na ni nzuri. Kwa hiyo kama umeamua kweli kufanikiwa, weka visingizio pembeni we jali jambo moja tu, kutaka matokeo chanya ya wewe kufanikiwa tu.

Kama unapenda kujifunza zaidi juu ya mafanikio, tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER'S kwenda 0687449428 ili kuweza kujifunza zaidi kuhusu maisha na mafanikio.

Kila la kheri na karibu.