google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

DIRA YA MAFANIKIO

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Apr 25, 2018

Elimu Ya Fedha Katika Biashara Inatakiwa Kuwa Hivi.

No comments :
Itakuwa ni bure kama unafanya biashara au unataka kufanya biashara kama utakuwa huifahamu elimu ya fedha.  Elimu ya fedha ndiyo msingi mkubwa wa maisha yako na biashara yako kiujumla.

Elimu ya fedha katika biashara yako inahusika na jinsi ya kupata fedha hizo na jinsi ya kufanya sizipotee.

Elimu ya fedha pia inahusisha masuala mazima kwa ajili ya kujua kile ambacho kinapatikana na kutumika.  Isipojua jinsi ya kupangalia mapato na matumizi yako katika biashara ni sawa bure.

Hivyo ili kuwa mtunza kumbukumbu mzuri katika biashara yako unatakiwa  kuwa na daftari la kumbukumbu ambalo litahusiana na kuweka kumbukumbu zako za kifedha na biashara yako.

Ijue vyema elimu ya fedha ikusaidie kufanikiwa katika biashara yako.

Kwani kuweka kumbukumbu katika daftari kunasaidia kwa kiwango kikubwa kujua kama unapata faida au unapata hasara. Pia kumbukumbu za kibiashara husaidia kuweza kupata taarifa kwa kile kinachoingia na kutoka katika biashara yako.

Lakini nitakuwa sijakutendea haki kama nitashindwa kukueleza ukweli kwamba katika elimu ya fedha lazima ujue ya kwamba fedha inahitaji nidhamu  hasa katika upande wa uwekaji akiba. 

Kama umeamua kuitenga fedha kwa ajili ya kuindeshea biashara yako basi jitahidi ubaki katika reli hiyo.

Lakini kama hiyo haitoshi tunashauriwa kwa katika suala la uwekaji akiba ni lazima uwe  kila baada ya muda fulani. Hii ikiwa na maana kama umeamua kutenga kila siku shilingi elfu kumi basi fanya hivyo kwani hii itakusaidia kuweza kuboresha biashara yako pale ambapo itakuwa haifanyi vizuri. 

Na wataalamu wa mambo wanasema asilimia 10 ndizo zinatumika kutenga katika uwekaji akiba,  hii inategemeana na kile unachokipata.

Lakini pia pesa yeyote ambayo unapata ni lazima uigawe katika mafungu matano ambayo ni:- 

Akiba.

Uwezekaji.

Matumizi ya lazima.
 
Matumizi yasiyo yalazima.

Fungu la kumi.

Endelea kusoma ukurasa huu kila wakati nitakuelezea kwa undani kuhusu ya ugawaji wa fedha ambazo unazipata,  ila kwa leo tu ni kwambie ya kwamba uhuru wa kifedha katika biashara unahitaji mambo yafutayo:

1. Kufanya kazi kwa bidii.
Kufanya kazi kwa bidii ni siri ambayo ipo katika kupata fedha ambazo unazihitaji.

2. Nidhamu.
Fedha inahitaji nidhamu katika kuipata na namna ambavyo unaweza kuitumia, maana fedha ina makelele mengi, hivyo inahitaji kufanya mambo ya msingi hasa pale inapopatikana.

Mpaka kufikia hapo sina la ziada naomba uyaweke yale niliyokueleza katika matendo maana usipofanya hivyo itakuwa ni sawa na kupika makande kwa mwanga wa mshumaa.

Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya,

Apr 24, 2018

Mambo Kumi Ya Kujikumbusha Katika Safari Ya Mafanikio Kila Wakati.

No comments :
Safari ya mafanikio ina mambo mengi ambayo unatakiwa uyajue na kuyafanyia kazi kila siku. Na unapoyafata mambo hayo ndio unazidi kujitengenezea msingi mkubwa wa kufanikiwa kwako kwa kile unachokifanya.
Leo katika makala haya nakukumbusha baadhi ya mambo ya msingi ya wewe kuyakumbuka kwenye safari yako ya mafanikio. Haya ni mambo ya msingi kwa sababu, ukiyatumia yatakutoa kutoka kwenye hatua moja na kukupeleka hatua nyingine.
Yafuatayo Ni Mambo Kumi Ya Kujikumbusha Katika Safari Ya Mafanikio Kila Wakati.
1. Unapowasaidia watu, ujue hiyo ni  sawa na kujisaidia wewe mwenyewe. Itafika wakati ule msaada unaoutoa kwa ajili ya watu wengine nao msaada huo utakurudia wewe kwa namna ya tofauti ambayo hujaijua bado.
2. Hakuna matokeo ya papo kwa papo ambayo unaweza kuyapata kwa chochote kile unachokifanya kwenye maisha yako. Unachotakiwa kufanya ni kuweka juhudi na kusubiri. Mafanikio ni matokeo ya kuwekeza juhudi na kuweza kusubiri. Kama hutaki kusubiri sahau kupata mafanikio yoyote makubwa maishani.

3. Ni muhimu kuboresha afya, ni muhimu kuboresha kipato, ni muhimu kuboresha mahusiano sahihi na wengine na muhimu pia kuwa na maarifa bora na sahihi. Unapokuwa unaboresha mambo hayo kila siku unajitengenezea uhakika mkubwa wa kuyafanya maisha yako kuwa bora sana karibu kila siku.
4. Kama kuna kitu unakihitaji kweli na kwa moyo wote, ni kweli lazima kitu hicho hata iweje ni lazima utaweza kukipata, Hautaweza kuweka sababu wala hutaweza kutoa visingizio kivile. Utakachokifanya ni kufanya kila linalowezekana mpaka kitu hicho uweze kukipata. Ni kipi ambacho unakitaka, usiweke sababu, kitu hicho utakipata.
5. Moja ya kitu ambacho unatakiwa kukisahau kabisa ni juu ya umri wako na kuendelea kuishi. Umri wako usikuzuie kufanya kitu chochote, bali wewe kama ni kuwekeza endelea kuwekeza sahau habari ya kwamba sasa hivi umri wako ni mkubwa. Kama unababaishwa na umri utapotea na maisha yanaendelea kusonga mbele.
6. Maisha ya kufanya makosa ni bora zaidi kuliko kuishi maisha ambayo hufanyi makosa kabisa. Ni bora uishi kwa kufanya makosa kabisa na hiyo itakusaidia kufika mbali kuliko ukae tu hufanyi kitu kisa eti unaogopa kukosea.
7. Mara nyingi kwenye maisha hatuoni vitu kama vilivyo kwa uhalisia wake, bali tunaona vitu kama tunavyoviona sisi kwa mitazamo yetu na sio kinyume cha hapo.
8. Hamna kitu cha maana kuwa nacho kama amani moyoni mwako. Unapokuwa na amani moyoni hiyo ndiyo inayokupa nguvu ya kufanya mambo makubwa kwa jinsi unavyotaka wewe. Anza leo kutengeneza amani moyoni ili ikupe faida kubwa kwako.
9. Unaweza kufurahia maisha yako popote na wakati wowote pasipo kujali mtu, kitu au hali ya aina fulani. Ni kitendo cha kuamua kuyafurahia maisha yako tu, na ukishaamua kuyafurahia maisha yako na kweli utayafurahia hayo maisha.
10. Kama unaweka nguvu za uzingativu, juhudi na mabadiliko chanya kwenye kila hatua unayofanya, hata kama huoni mabadiliko ya wazi, tambua kabisa, wakati utafika maisha yako yatabadilika kabisa.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Apr 23, 2018

Ukijifunza Kanuni Hizi Na Kuzifanyia Kazi, Utafanikiwa.

No comments :
Kila mtu anaweza akawa na mafanikio akiamua. Mafanikio si uchawi ni sayansi tu ya kujifunza kanuni za mafanikio na kuzifanyia kazi kila siku. Watu wenye mafanikio  wanajua kucheza na kuzitumia kanuni za mafanikio na kuweza kuwafanikisha.
Leo katika makala haya nataka tuzungumzie moja ya kanuni muhimu za mafanikio, ambazo ukizifanyia kazi na utafanikiwa. Nimesema kama utazifanyia kazi zitakusadidia kufanikiwa lakini kama usipozifanyia kazi utaendelea kubaki hapo ulipo kama ulivyo.

1. Picha unazoziweka kichwani mwako.
Kati ya kitu ambacho unatakiwa kukichunga sana ni picha ambazo unaweka kichwani mwako. Yapo matokeo makubwa sana kwa yale mambo ambayo unayoyaweka kichwani mwako kila wakati.
Jaribu kuangalia ni vitu gani ambavyo unaviweka akili mwako kila mara. Mambo hayo unayoyaweka akili mwako kila wakati, basi ujue mambo hayo ni rahisi kuweza kukutokea. Hii ni kanuni ambayo unatakiwa kuichunga na kuitumia.
2. Vitendo vyako.
Unaweza ukawa una ndoto zako nzuri sana, lakini kama huchukui hatua hiyo ni sawa na kazi bure. Unatakiwa kujua jinsi ya kuchukua hatua kwa yale mawazo ambayo unayo. Hatua ndizo zitakazo kusaidia kukufikisha kwenye ndoto ulizonazo.
Watu wengi wanaokwama kwenye maisha, ni watu  ambao wanakwama kwa sababu ya kushindwa kuchukua hatua zinazostahili kwenye maisha yao. Chukua hatua leo mapema kwa chochote kile unachotaka kukifanya na utaweza kufanikiwa.
3. Nidhamu.
Hutaweza kufanikiwa kwa chochote kwenye maisha yako kama huna nidhamu. Kila wakati nidhamu inahitajika kwenye ndoto zako, kwenye kazi na kila eneo ili uweze kufanikiwa. Ukikosa nidhamu upo kwenye wakati mgumu wa kushindwa.
Jenga nidhamu kwa chochote kile ambacho unakifanya na nidhamu hiyo itakuongoza kuweza kufanikiwa. Wanaoshindwa ni watu ambao kwa dhahiri naweza nikasema ni watu ambao hawana nidhamu kabisa maishani mwao.
4. Kujitoa.
Picha unazoziweka, vitendo vyako na nidhamu ni moja ya kanuni muhimu za kukusaidia kufanikiwa, lakini hivi haviwezi kukusaidia sana kama wewe mwenyewe hautaweza kujitoa. Ni muhimu sana kujitioa kwenye ndoto zako.
Toa kila kinachowezekana ikiwa ni pamoja na muda wako, nguvu zakio na kila kitu cha muhimu ili ikusaidie kufanikiwa. Usipojitoa kwenye ndoto zako ni ngumu sana kuweza kufanikiwa kwa sababu kuna changamoito na mambo mengi yanayotakiwa kukabiliana nayo.
Ukiweza kufanyia kazi kanuni hizi, zitakusaidia sana kuweza kufikia mafanikio yako.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
Pia kama wewe ni mfugaji wa kuku na unahitaji vifaranga bora, waone DM POULTRY FARM PROJECT kwa huduma ya uhakika. Hawa ni wauzaji wa vifaranga wa kuku aina ya KUROILER, SASSO, PURE KIENYEJI na KUCHI. Kwa mahitaji ya vifaranga wasiliana nao kwa 0767 048 035 au 0686 141097 na wote mnakaribishwa.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Apr 20, 2018

Hii Ndio Athari Ya Hatua Chanya Na Thamani Unayoitengeneza.

No comments :
Hatua chanya unazozichukua, haziishii kwako tu, bali hatua hizo huzidi kwenda zaidi na zaidi na kuweza kuwafikia watu wengine ambao hata hukuweza kufikiri kama hatua hizo chanya zinaweza kuwafikia.
Thamani unayotengeneza, pia thamani hiyo haiwezi kuishia kwako, thamani hiyo huweza kuenea na kusambaa na kuweza kuwasaidia watu ambao hata pia hukifikiri kwamba inaweza ikawasaidia watu hao ambao hata huwajui kwa sura.
Leo hii kuna sehemu, maisha ya watu ya watu yanakuwa bora kwa sababu ya hatua ambazo ulizichukua kipindi cha nyuma na hatua hizo zinawasaidia kuboresha maisha yao na kuonekana ni bora zaidi, lakini chanzo kikubwa ukiangalia ni wewe.
Huwezi kutawala na huwezi kujua hatua zako chanya zitafika wapi, kikubwa unachotakiwa kufanya ni kuzidi kuchukua hatua chanya na kutengeneza thamani iliyobora ambapo thamani hiyo itawasaidia wengine hata kama wewe hupo.

Kwa jinsi unavyowekeza nguvu zako katika hatua chanya na kutengeneza thamani, unatakiwa ujue kuna maisha ya mtu ambayo unayobadili hata kama maisha hayo huyaoni leo, lakini kuna mtu atasaidiwa na wewe pasipo kujua.
Kwa hiyo unachotakiwa kuelewa usiangaliae matokeo ya sasa kwa kile unachokipata na kukifanya, angalia nguvu zako jinsi ambavyo zitakavyosambaa na kuwasaidia watu wengine kuweza kupiga hatua za maisha yao pia.
Fanya kilichobora leo, tengeneza thamani iliyobora zaidi kwako kila siku na thamani hiyo itaenea karibu kila eneo kwa jinsi siku zinavyokwenda. Hakuna nguvu yako ambayo itapotea kama unaweka thamani na kutoa yale yaliyo mazuri kwako.
Angalia hata ulipo kuna mambo mazuri unayatumia ni kwa sababu ya hatua chanya na thamani kubwa ambazo kuna watu walizichukua na hiyo inakusaidia hata wewe kuweza kufaidi matunda yao.
Hilo ni fundisho kwako usiwe sehemu ya kutoa mambo hasi na hayo pia yanaweza yakasambaa na kuwaathiri watu wengine. Tengeneza thamani na kutoa mambo chanya ili uwe sehemu ya kuitengeneza dunia ikawa ni sehemu salama.
Ishi maisha yako kwa kutoa yaliyochanya na kutengeneza thamani inayotakiwa kila siku. Ukiwa utafanya hivyo utakuwa ni sehemu kubwa ya mabadiliko makubwa ya dunia. Hii ndio athari ya hatua chanya na thamani unayoitengeneza.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,





`


Apr 13, 2018

Nyuma Ya Pazia La Mafanikio.

No comments :
Mafanikio yoyote unayoyaona  kwa nje mara nyingi yanatengenezwa sana na hatua au vitu visivyoonekana, kile unachoona ni matokeo yake tu.
Kazi fulani inapokamilika na mafanikio yake kuonekana kwa nje, ni wazi dunia nzima inakuwa makini kushangaa kwa kuyaona mafanikio yale yaliyotokea.
Lakini kuna kuwa hakuna mtu ambaye anakuwa yupo tayari kufatilia mchakato wa nyuma ya pazia ni nini kilifanyika hadi kuibua mafanikio hayo.
Na kwa sababu hiyo ya kuangalia mafaniko au matokeo ya nje, yote hiyo hupelekea kuwaona watu wenye mafanikio ni kama watu wenye bahati sana.

Ikiwa utang’ang’ania kuangalia mafanikio ya nje ya watu na kuchanganyikiwa nayo na kusahau kwamba kuna nyuma ya pazia la mafanikio, umepotea.
Mchezaji wa mpira anaonekana anafanya vizuri uwanjani, ujue nyuma yake kuna mazoezi mengi sana ameyafanya tayari.
Mpiganaji bora wa ngumi duniani unayemwona anang’ara na kuchukua ushindi wa kila aina ujue kabisa huyo kafanya mazoezi mengi ya kutosha yaliyompa ushindi huo.
Biashara yoyote inayoonekana ina mafanikio makubwa haikuanzia pale, nyuma ya pazia la mafanikio, ilianzia mbali sana na pengine na mtaji mdogo na wa kawaida sana.
Hiyo yote inaonesha mafanikio yanajengwa na vitu vidogo sana, vitu ambavyo kuna wakati kama havionekani, lakini baadae huleta matokeo makubwa.
Utakata tamaa na kujiona mshindwaji kama utakuwa unaangalia mafaniko kwa kuona tu matokeo yaliyopo sasa na kusahau, kuna vitu vinatengenezwa nyuma ya pazia.
Ushindi na mafanikio hauendi kwa watu wenye bahati kama unavyofikiri wakati mwingine kwamba ndivyo ulivyo.
Ushindi na mafanikio unakwenda kwa kila mtu ambae ameamua kujenga nidhamu, kujituma, kuwa king’ang’anizi na kuwa chanya wakati wote.
Angalia nyuma ya pazia la watu wenye mafanikio, utajua na wewe ufanye nini, ujitume vipi na uweke juhudi gani zinazotakiwa.
Lakini ukiwa utakuwa unaangalia matokeo yao na kushindwa kuangalia nyuma ya pazia hutaweza kujifunza kitu cha kukusaidia.
Mafanikio yote makubwa yanatengenezwa nyuma ya pazia la mafanikio, huko ndiko mafanikio yanakopikwa na kuandaliwa haswaa, mengine unayoyaona ni matokeo.
Usiendelee kusubiri, tengeneza mafanikio yako nyuma ya pazia na hayo matokeo yatakuja kuonekana huko mbeleni, kama huoni matokeo kwa sasa usijali.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,








Apr 12, 2018

Inawezekana Kubadili Maisha Yako Sana…Ukiamua Kufanya Hivi.

No comments :
Kila wakati unapofikiria na kikiwaza kile kitu unachokita ili kikutokee, uwe na uhakika na ujue kabisa kitu hicho kitawezekana na kutokea.
Kila wakati unapojenga mategemeo chanya kwa kile ukifanyacho, tambua pia mategemeao hayo yatawezekana na kuwa kweli katika uhalisia.
Kila wakati unapoweka juhudi na kujitoa kikamilifu kwa kile ukifanyacho, uwe na uhakika inawezekana kufikia lile lengo lako ambalo umejiwekea.
Kila wakati unapokuwa upo tayari kuendelea kuchukua hatua na hata kama mbele yako kuna changamoto kubwa sana za kimaisha, tambua inawezekana kufanikiwa.

Kila wakati unapoamua kuwa king’ang’anizi na hadi kuhakikisha ndoto zako zinatimia, pia unatakiwa kujua kwamba hilo linawezeka na ndoto zako zitatimia.
Kila wakati unapojifunza kutokana na makosa unayofanya na ukachukua hatua za kujirekebisha kwenye makosa yako utafika wakati itawezekana kufanikiwa kwako.
Kila wakati unapoamua kuendelea mbele hata kama umekatishwa tamaa, itafika wakati pia ujue kufanikiwa kwako ni lazima utafanikiwa kwa sababu umeamua.
Kila wakati unapoamua kupambana na hali hatarishi, hali za kuogopesha zinakufanya uone ndoto zako hazitimii, ujue muda utafika itawezekana kufanikiwa kwako.
Unapaswa ujue kila hali unayotegemea, kila juhudi na kila kujitoa ambako unafanya kila siku, huko ndiko kutakapokupa mafanikio makubwa maishani mwako.
Hakuna ambaye anategemea kile kilichobora na halafu mwisho wa siku akabaki kama jinsi alivyokuwa mwanzoni.
Kitu cha kuzingatia ni kuwa mvumilivu na kujua kwamba mabadiliko katika maisha hayaji mara moja tu au ghafla, mabadiliko yanakuja wakati mwingine kidogo kidogo.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,







Apr 6, 2018

Ifanye Hii… Iwe Sababu Ya Kufanikiwa Kwako.

No comments :
Pale unapokuwa na kazi nyingi za kufanya na unaona kama hutaweza kukamilisha kazi hizo, hiyo sio sababu pekee ya kukufanya wewe ukate tamaa.
Pale unapoona njia ya kufikia mafanikio yako ni ndefu sana, na unaiona mafanikio yako kama yanachelewa vile, hiyo pia si sababu ya wewe kuweza kukata tamaa.
Kwa vyovyote vile unapoona ugumu wa kufanikiwa na kukatishwa tamaa na vitu kama hivyo, fanya sasa hiyo ndio iwe sababu ya kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa.
Usitishwe na njia ya mafanikio yako ni ndefu au usitishwe kwa kuona kwamba una majukumu mengi, hapo ndipo unapotakiwa wewe kukaza mwendo kuelekea mafanikio yako.
Unapokuwa na vitu vingi zaid vya kufanya na vinakutaka wewe, hapo ndipo ipo fursa pia ya kukusaidia wewe kuweza kufanikiwa.

Unapoona njia ya mafanikio ni ndefu, hapo ndipo huo wakati wa wewe kuweza kutafuta njia nyingine za kuweza kukusaidia kukufanikisha.
Unapaswa kujua mafanikio makubwa yanakuja katikati ya changamoto nyingi zaidi, na changamoto hizo ndizo unazotakiwa kukabiliana nazo na kuzishinda.
Matajiri unaowaona, walifanikiwa katika njia hizi hizi ambazo hata wewe kuna wakati unaona kwa njia hii kufanikiwa ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa tena.
Unapokutana na magumu, unapokutana na hali ya kuona kama njia yako ya mafanikio ni ndefu sana na haiwezi kufika hiyo isiwe sababu ya kufanya ukashindwa.
Kila wakati jaribu kutafuta sababu ya kufanikiwa pale unapokutana na ugumu au kuna njia ya mafanikio ni ndefu kwako.
Unapaswa kujua hakuna maisha pasipo changamoto na changamoto zipo ili tuweze kuzishinda na kutupa sisi mafanikio.
Ndio maana kuanzia leo unatakiwa kujua kwa uwazi kabisa, fanya sababu yoyote ile inayokupa ugumu wa kuweza kufanikiwa kiwe ndio chanzo cha mafanikio yako.
Kikubwa unatakiwa uwe mvumilivu na usiwe mtu wa kuweza kukata tamaa mapema kwani hautaweza kufika mbali kama utakuwa ni mkata tamaa mapema.
Unapokutana na magumu na unapoona njia ya mafanikio ni ndefu kwako huo ndiio wakati wa kutafuta kwako kung’aa kimafanikio.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kila siku kujifunza maisha na mafanikio.
Pia rafiki, kama unapenda kujifunza zaidi kuhusu mafanikio, fursa za mafanikio zinapopatikana, ajira pamoja na uwekezaji, karibu kwenye kundi la WHATS APP LA MAFANIKIO, kujiunga tuma neno THE UNIVERSITY OF WINNER’S kwenda 0713 048 035, hapo utapata utaratibu mzima wa kujiunga.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,
Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Apr 2, 2018

Andika Mawazo Yako na Ukae Kimya.

No comments :

Watu wengi wana mawazo mazuri, wana ndoto kubwa, lakini mojawapo ya sababu ya kwanini hakuna kinachofanyika ni kwamba wengi tunaongea sana. Utakuta mtu ndo kwanza amepata wazo la kufanya kitu fulani, lakini saa hiyo hiyo anaanza kuwashirikisha anaowaita marafiki zake. Na kuanzia hapo inakuwa kila siku ni...
kuongea ongea juu ya wazo hilo jipya.

Baada ya siku si nyingi, anapata wazo jingine na hapo lile la mwanzo linasahaulika na anaanza kuongelea wazo jipya. Mwisho wake ni kwamba unaendelea kujenga mazoea ya kufikiri wazo na kulitoa kwa marafiki na ndugu basi! Matokeo yake miaka inavyozidi kwenda unajikuta huna mradi wowote wa biashara ambao umeweza kuufanikisha.

Tabia hii ya kupenda kuwashirikisha wazo lako changa watu wengine, inakuingiza kwenye hatari kubwa sana. Kwasababu hao unaojaribu kuwashirikisha wazo lako, yawezekana ni watu ambao hawajawahi kuwazia wazo lako kwa kiwango ambacho wewe unafikiri juu ya wazo hilo. Lakini pia, hao wanaoitwa marafiki, unaweza ukakuta kuwa ni wale watu ambao hawana hamasa yoyote ya kufanikiwa, ni wavivu, wabinafsi na inawezekana hapo walipo wamefika mwisho, wamebakia kusubiri muujiza utokee ndipo watajirike—jaribu kuwa mwangalifu! 

Katika hali ya kawaida haiwezekani wewe upate kuwa na wazo zuri mwezi mzima halafu umshirikishe rafiki yako na yeye siku na saa hiyo hiyo akwambie “haiwezekani”. Ukiamua kumsikiliza kama wengi tunavyofanya nakuhakikishia kuwa itaendelea kuwa vigumu sana kwako kuweza kufanikisha mradi wowote wa maana. Ebu! Fikiria rafiki yako, anakwambia, hicho kitu unachotaka kufanya hakijawahi kufanywa na mtu yeyote na kwamba wewe utawezaje? Eti! unaambiwa husifanye jambo fulani kwasababu hakuna aliyewahi kufanya hivyo—ushauri wa namna hii utaendelea kuupata sana, kama utaendelea kuwa mtu wa kuongeaongea tu! 

Unapoamua kumwaga mawazo yako kwa wengine, ujue kuwa kwa namna moja au nyingine yatapokelewa kwa hisia na mtazamo tofauti kulingana na uelewa wa watu unaowambia. Mara nyingi watu wakiambiwa jambo ambalo liko nje ya fikra zao au uelewa wao, moja kwa moja upata hofu na baadae woga, kutegemea na ukubwa na upya wa wazo lako. Wakishapata hofu juu ya wazo lako, kinachofuata ni kutaka kujaribu kuhamishia hofu yao kwako. Hapo wataanza kukupa mifano ya watu waliowahi kujaribu na wakashindwa, watakueleza hatari zote zinazoweza kujitokeza endapo utendelea na mpango wa kutekeleza wazo lako hilo. Kwahiyo, wewe bila kujua, unashitukia umeambukizwa woga na hofu ambayo kimsingi hukuwanayo hapo awali.

Baadhi ya maneno yanayodhihirisha hofu ya marafiki zako juu ya wazo lako ni kama maneno ya “huwezi”, “haiwezekani”“ni ngumu sana kufanikiwa” n.k. Ndiyo maana ukiendelea kuhubiliwa maneno hayo mara kwa mara, utajikuta taratibu taratibu unaanza kuyaamini. Hali hii ndiyo mwisho wake ukusababishia kukosa ujasiri wa kuthubutu pindi zinapotokea fursa mbalimbali.

Kwa taarifa yako ni kwamba pale rafiki au ndugu yako akikwambia“huwezi” maana yake ni kwamba yeye ndiye “hawezi”. Mara zote usilichukulie jibu la “huwezi” kama ndiyo jibu lako. Pia, usijaribu kulitumia jibu la “huwezi” kama kisingizio au kikwazo cha kukuzuia wewe kutekeleza wazo lako kama ulivyolifikiria hapo awali.

Achana na kuongea ongea sana! Maneno ya nita……anza biashara, shule, kutafuta pesa, kufanya mazoezi mwaka huu hayasadii sana. Nataka nikwambie kwamba maneno yote ya “nita….nita…!” ni kuongea tu! Na ni sawa na “mvuke”—hakuna vitendo hapo.

Nitawezaje kuendeleza wazo langu bila kuongea? 
Sasa, ili kuepuka mawazo yako kuwa kama “mvuke”, inabidi kuanzia sasa kila ukipata wazo zuri, cha kwanza kufanya ni kuliandika na kisha kulifanyia kazi huku ukiwa kimya.
 
Unapoandika wazo lako, unapata fursa ya kutathimini kile ulichotakiwa kufanya kwa kulinganisha na kile ulichokifanya. Mfano; kama umeanza siku yako usiongee kwamba mimi leo nitafanya hili na lile; wewe unachotakiwa ni kuandika orodha ya mambo ambayo unatakiwa kuyafanya kwa siku hiyo basi! Kama yale uliyoyaandika kwenye orodha umekamilisha asilimia 40% basi ujue kuwa bado wewe ni walewale waongeaji tu! Lakini kama utakamilisha kuanzia asilimia 70-100%, basi ujue kuwa sasa umeanza kuwa mtu wa vitendo zaidi na siyo maneno.

Hapa nizidi kukusihi kuwa, kila wakati ujitahidi kuruhusu vitendo vikuongoze na siyo kuongozwa na maneno. Tumia muda wako mwingi kutenda na kila wakati “yape nafasi matendo yako yaongee kwa sauti”kuliko maneno.

Kila ukipata wazo zuri kumbuka kauli mbiu hii “andika mawazo yako na ukae kimya”. 

Makala hii imeandikwa na cypridion mushongi wa maarifashop.blogspot.com, unaweza kujifunza zaidi juu ya mafanikio kwa kutembelea blog yake.



Apr 1, 2018

UJUMBE WA PASAKA; Tenda Wema Kwa Faida Hizi Kwako.

No comments :

Habari za muda mpenzi mzomaji wa mtandao huu wa dira ya mafanikio bila shaka u mzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku.
Ikiwa leo ni tarehe 1/4/2018 ambapo wakristo wote duniani wanasherekea siku za kufufuka kwa bwana wetu Yesu Kristo yaani ni sikukuu ya pasaka.
Siku hii huenda sambamba na kipindi chenye tafakari kubwa yenye kuwataka wakristo wote duniani kote waweze kutafakari uwepo na uweza wa matendo makuu ya mwenyezi Mungu.

Kwa Misingi hiyo Uongozi mzima wa Mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO inapenda kukutakia sikukuu njema ya Pasaka, huku ujumbe wetu mkubwa kwako ikiwa ni  kwamba  hakikisha unaitumia siku hii katika kumshukuru Mwenyezi Mungu katika kuhakikisha unakuwa ni mtu Mwema na si kutenda dhambi.
Tunasiitiza juu ya hilo kwa sababu watu wengi hutumia siku hii katika kufanya maovu ambayo ni chukizo mbele ya Mungu wetu, yamkini yawezekana vipo vishawishi mbalimbali ambavyo vitajitokeza katika siku ya leo, unachopaswa kukifanya ni kujitenga mbali na vitu hivyo. Hata maandiko yanasema ya kwamba jicho lako likikukosea ling'oe.

Hivyo katika siku hii epuka sana marafiki ambao watakusababisha uingie katika kutenda maovu, kwani maovu ni dhambi na pia ni chukizo mbele za mwenyezi Mungu.
Tukutakie sikukuu njema ya Pasaka.
Imeandaliwa na uongozi mzima wa Blog hii ya dira ya mafanikio na kuletwa kwako nami Afisa Mipango Benson Chonya.